Saturday 22 February 2020

Walimu Mkoani Tabora Watakiwa Kuwafundisha Wanafunzi Umuhimu Wa Uzalendo

...
NA TIGANYA VINCENT
WALIMU Mkoani Tabora wametakiwa kuwalea kimaadili wanafunzi na wanavyuo ili waweze kukua katika uadilifu na uzalendo ambao utakaowawezesha kushiriki ujenzi wa Tanzania mpya msingi mkuu ni viwanda.

Kauli hiyo imetolewa leo  na katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa mafunzo na maelekezo  kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo.

Alisema kuwa katika kukuza uchumi Tanzania mpya ipo haja ya kuwa na vijana ambao wamekuzwa katika msingi ya uadilifu na uzalendo ambao utaweka mbele maslahi ya Taifa na sio masalahi binafisi.

“Maslahi ya Taifa yatadumu daima …lakini maslahi ya mtu binafsi ni ya muda baada ya kufa basi nayo yamekwisha” alisema.

Makungu alisema mafunzo hayo ni muhimu sana katika kujenga jamii yenye maadili mema ambayo yatasaidia kuzalisha Viongozi wazalenda na waadilifu.

Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza  walimu kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kukuza maadili mkoani Tabora na kuongeza kuwa uanzishwaji wa Klabu  za Maadili utaleta mabadiliko chanya na  kuongeza ufaulu kwa vijana mashuleni na vyuoni.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Gerald Mwaitebele alisema Ofisi hiyo imeamua kuanzishia Klabu hizo ili kuwajenga vijana tangu awali ili kuwajenga kukua kimaadili na uzalendo wakiwa wadogo.

Alisema ni kazi kubwa kufundisha umuhimu wa maadili kwa mtu mzima kuliko kufundisha akiwa mdogo kwa kuwa atajengeka katika hali ya uadilifu na kuipenda nchi yake.

 Mafunzo hayo ya siku moja yameshirikisha walimu wa shule za Msingi, sekondari na Vyuo vya Elimu vilivyopo Manispaa ya Tabora na yalikuwa na mada za Sheria  ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mgongano wa Masilahi na Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Klabu za Maadili

mwisho


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger