Friday 21 February 2020

China Yakanusha Vikali Kwamba Virusi vya Coroni ni Vya Kutengeneza Maabara ( Silaha za Kemikali)

China imekanusha vikali madai ya Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilivyodai kwamba Virusi vya COVID -19 vinavyoendelea kuitikisa Dunia ni vya kutengenezwa Maabara.

Kauli hiyo imetolewa na  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang  ambapo amesema   China inatumai kuwa wakati jumuiya ya kimataifa inapopambana kwa pamoja kukabiliana na ugonjwa huo mpya wa COVID-19, itaendelea kupambana na kuzuia kwa pamoja "virusi vya njama mbalimbali za kisiasa".

Hivi karibuni, baadhi ya watu na vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilidai kuwa virusi vipya vya COVID-19 ni "silaha za kikemikali" ambavyo vilitoka kwenye maabara moja nchini China. 

Bw. Geng amesema, hivi sasa watu wa China wanapambana na virusi hivyo kwa nguvu zote, hali ambayo inajiwajibika na pia inawajibika na usalama wa afya ya umma duniani. 

Amesema kitendo cha baadhi ya watu na vyombo vya habari kutoa kauli kama hizo zinazochochea hofu kina nia mbaya ama kukosa elimu ya kimsingi.

Bw. Geng amesema, hivi karibuni maofisa wa Shirika la Afya Duniani WHO wametangaza mara kwa mara kuwa, hakuna ushahidi wowote kuwa virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara au kusababishwa kutokana na utengenezaji wa silaha za kikemikali.


Share:

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane kushtakiwa kwa mauaji ya mkewe

Jeshi la Polisi Nchini Lesotho limesema litamshitaki Waziri Mkuu Thomas Thabane, 80 kwa mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane

Thabane ametangaza kuwa atajiuzulu mwezi Julai kutokana na umri wake, lakini Chama chake kilimtaka ajizulu kabla ya Jana Alhamisi.

Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa kwa mauaji hayo..

Thabane atakuwa kiongozi wa kwanza kusini mwa Afrika kushtakiwa kwa mauaji akiwa madarakani, katika kesi ambayo imeishitua nchi hiyo.


Mkewe wa zamani Lipoleo Thabane alipigwa risasi na kufariki nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Maseru siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu 2017.

Wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na kabla ya mauaji hayo walikuwa katika mchakato wa kupeana talaka.

Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana , lakini stakahabadhi zilizowasilishwa mahakamani hivi karibuni na kamishana wa polisi ,zinawatuhumu Waziri Mkuu na Mkewe wa sasa kwamba walihusika na mauaji hayo.


Share:

Rwanda Yapinga Uchunguzi Huru Wa Kifo Cha Msanii Kizito Mihigo

Rwanda imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kutaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu kifo cha msanii maarufu wa muziki wa kiinjili Kizito Mihigo, ambaye alifariki katika kituo cha polisi Jumatatu asubuhi.

Alifariki siku tatu baaada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kwa jaribio la kutaka kutoroka nchi na kujiunga na la waasi linalopigana dhidi ya serikali ya Rwanda.

Bw. Mihigo alipigwa marufuku kuondoka nchini Rwanda kutokana na mashitaka yaliyopita dhidi yake.

Msemaji wa shirika la upelelezi la Rwanda, Marie Michelle Umuhoza, ameiambia BBC kwamba "Rwanda ni nchi huru inayojitawala na ambayo ina uwezo wa kuchunguza kitu chochote".

Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch, Amnesty International na Commonwealth Human Rights Initiative yamekuwa yakishinikiza kufanyika kwa uchunguzi huru wa kubaini mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanamuziki huyo aliyekuwa na miaka 38- amabaye alizoa umaarufu kutokana na ujumbe wake wa amani na maridhiano.

Siku ya Jumatatu, polisi ya Rwanda ilitangaza kuwa alijinyonga akiwa kizuizini.

Afisa wa Human Rights Watch ameiambia BBC kwamba uchunguzi huru utaangalia kamera za siri katika eneo ambalo msanii huyo alikuwa anazuiliwa.

Lakini Umuhoza amesema Rwanda tayari inafanya uchunguzi kuhusu kifo chake.

"Sioni haja ya kufanyika kwa uchunguzi huru, katika nchi huru", alisema


Share:

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu
pamoja na ajali za barabarani.

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia kijana DAVID MUSA [20] Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya kwa tuhuma ya kupatikana na mali zidhaniwazo kuwa za wizi.

Tukio hilo limetokea tarehe 18.02.2020 majira ya saa 16:10 jioni huko Mtaa wa Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika msako uliofanywa na Jeshi la Polisi mkoani hapa na kumkuta mtuhumiwa akiwa na Kamera moja [01] aina ya Cannon 7D, Lens mbili [02] ndogo aina ya Canon 7D, simu ndogo nne [04] aina ya Tecno mbili, Itel moja na Samsung moja na laini tatu [03] za Tigo, Vodacom na Halotel mali zidhaniwazo kuwa za wizi.

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI TOKA NDANI YA GARI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa watano 1. JOSEPH MOHAMED [38] Mkazi wa Airport ya Zamani, 2. PASCHAL JOHN [57] Dereva Hiace na Mkazi wa Mwambene, 3. MAWAZO SAMWEL [28] Dereva na Mkazi wa
Mafiati, 4. IBRAHIM MAKOKULA [25] Mkazi wa Ilomba na 5. ZAWADI RICHARD [25] Mkazi wa Makunguru kwa tuhuma za wizi toka ndani ya gari.

Tukio hili limetokea tarehe 15.02.2020 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Stendi ya Mabasi Nanenane Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kupata taarifa za kuwepo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi toka ndani ya magari hasa kwa abiria ndipo ulifanyika msako kwa kushirikiana na viongozi wa Stendi ya Mabasi Nanenane na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na matukio hayo.

Aidha katika msako huo, yamekamatwa magari mawili yenye namba za usajili T.632 BQQ aina ya Toyota Hiace na T.780 CZT aina ya Toyota Hiace ambayo hufanya safari kati ya Stendi Kuu – Uyole ambayo yanatuhumiwa kwamba vitendo vya wezi kwa abiria hutokea.

Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa watuhumiwa wengine pamoja na gari moja ambalo limetajwa kuhusika katika matukio hayo.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI.
Jeshi la polisi mkoani mbeya linawashikiliae watuhumiwa wanne [04] 1. MASIKITIKO PATSON @ MBUZI [34] Mkazi wa Mtakuja 2. HURUMA MWASILE [36] 3. AMANI MSWIMA [21] Mkazi wa Mlima reli na 4. EZEKIA SINKALA [26] Mkazi wa Mtakuja kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio ya unyang’anyi, uporaji wa Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12/02/2020 baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanyika msako maalum maeneo mbalimbali ya Mbalizi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao. Watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kutenda matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-

1. Mnamo tarehe 20/12/2019 majira ya usiku huko Mtakuja mtu aitwaye ZACHARIA JACKSON [30] dereva bodaboda aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina ya T- BETTER
yenye namba za usajili MC 149 CFJ.

2. Mnamo tarehe 10/02/2020 huko MtakujaUtengule Usongwe mtu aitwaye SHUKURU JUMA [26] aliuawa kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina
King lion.

3. Mnamo tarehe 29/01/2020 huko ZZK Mbalizi majira ya usiku mtu aitwaye SADOCK NIMROD [21] dereva bodaboda alivamiwa na kisha kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kisha kunyang’anywa Pikipiki.

Upelelezi wa mashauri haya unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WAHALIFU SUGU WA MATUKIO YA UVUNJAJI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili 1 .MAJALIWA CHARLES [18] Mkazi wa DDC Mbalizi na 2. ANDWELE ANDIGENIE MWAKAOISON [26] Mkazi wa DDC.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 19/02/2020 majira ya saa 17:00 alfajiri katika msako maalumu uliofanyika huko maeneo ya DDC Mbalizi, Kata na Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa na baada ya kuwapekua wamekutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-

1. Televisheni mbili inchi 52 aina ya hitech na inchi 32 aina ya samsung
2. CPU mbili aina ya dell
3. Monitor mbili [2] aina ya samsung na dell
4. Laptop moja aina ya hp Watuhumiwa wamekiri kuhusika kwenye matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba. baadhi ya mali zimetambuliwa na wahusika.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa February 21





















Share:

Thursday 20 February 2020

NEC yaongeza siku za uandikishaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura Dar

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza muda wa uandikishaji katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa ya Dar es Salaam.

Muda uliongezwa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura ni siku tatu ambapo zoezi hilo litaitimishwa Februari 23, 2020.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchanguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles amesema kuwa kusogezwa kwa zoezi hilo kumetokana na maombi mbalimbali katika vituo vya uandikishaji.

Dkt.Charles amesema baada ya maombi hayo walifanya kikao cha Februari 19 kwa ajili ya kutathmini zoezi hilo na kuamua kuongeza muda wa kujiandikisha. Amesema vituo vyote vitafunguliwa kama kawaida kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.



Share:

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MADAKTARI KITAIFA MWAKA 2020 JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaktari Kitaifa Mwaka 2020 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataiafa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 20, 2020 PICHA NA IKULU
Share:

Land Surveyor at TANROADS

LAND SURVEYOR  Ref.No.:TNR/RM/KG/A.20/2/VOL.XI/7 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania entered into a contract for the Upgrading of NDUTA JCT-KIBONDO TOWN-KIBONDO-JCT(25.9KM) to Bitumen Standard, The Rigional Manager’s Office TANROADS – Kigoma, on behalf of the Chief Executive, TANROADS, intends to recruit qualified and competent Staff to fill the… Read More »

The post Land Surveyor at TANROADS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Works Inspector Drainage and structure at TANROADS

Ref.No.:TNR/RM/KG/A.20/2/VOL.XI/7 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania entered into a contract for the Upgrading of NDUTA JCT-KIBONDO TOWN-KIBONDO-JCT(25.9KM) to Bitumen Standard, The Rigional Manager’s Office TANROADS – Kigoma, on behalf of the Chief Executive, TANROADS, intends to recruit qualified and competent Staff to fill the following vacant… Read More »

The post Works Inspector Drainage and structure at TANROADS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Material Technician at TANROADS

MATERIAL TECHNICIAN  Ref.No.:TNR/RM/KG/A.20/2/VOL.XI/7 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania entered into a contract for the Upgrading of NDUTA JCT-KIBONDO TOWN-KIBONDO-JCT(25.9KM) to Bitumen Standard, The Rigional Manager’s Office TANROADS – Kigoma, on behalf of the Chief Executive, TANROADS, intends to recruit qualified and competent Staff to fill the… Read More »

The post Material Technician at TANROADS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BINTI ALIYEVUNJA NDOA YA WAZAZI ASOME ASIMULIA ALIVYOFANIKIWA KUWA KIONGOZI MWANAMKE KIJIJINI

Share:

Programme Assistant (M&E)SC (G5 equivalent) at United Nations World Food Programme

WFP seeks candidates of the highest integrity and professionalism who share our humanitarian principles. Selection of staff is made on a competitive basis, and we are committed to promoting diversity and gender balance. ABOUT WFP The United Nations World Food Programme is the world’s largest humanitarian agency fighting hunger worldwide.  The mission of WFP is to help the… Read More »

The post Programme Assistant (M&E)SC (G5 equivalent) at United Nations World Food Programme appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MEAL Officer – Zanzibar – Save the Children

Job Description  MEAL Officer – Zanzibar–(2000016A) Monitoring, Evaluation, Accountability & Learning (MEAL)  Officer TEAM/PROGRAMME: Operation LOCATION:  Zanzibar GRADE:  4 POST TYPE: National Child Safeguarding: Level 3 – the responsibilities of the post may require the post holder to have regular contact with or access to children or young people ROLE PURPOSE: Under direct supervision of the CP/CRG MEAL Coordinator, the… Read More »

The post MEAL Officer – Zanzibar – Save the Children appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Protection Manager at Danish Refugee Council (DRC) (Re-Advertisement)

Background The Danish Refugee Council (DRC) established operations in Tanzania in October 2015 to provide emergency assistance to Burundi refugees who were fleeing violence that ensued following the disputed presidential election in April 2015. From the onset, DRC’s operations in Tanzania have been based in Nduta and Mtendeli refugee camps. Responsibilities The Protection Manager will be responsible for… Read More »

The post Protection Manager at Danish Refugee Council (DRC) (Re-Advertisement) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

AWESO AMWEKA NDANI MKANDARASI WA MAJI MKINGA KUSHINDWA KUSIMAMIA MRADI WA MAJI MBUTA

 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakati wa ziara yake ya siku moja
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark wakati wa ziara yake katika ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura
 MBUNGE wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dastan Kitandula akizungumza wakati wa ziara hiyo
 MKUU wa wilaya ya Mkinga Mark Yona kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye hayupo pichani
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisistiza jambo wakati wa ziara hiyo kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona


 Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Mkinga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso
 NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso katika akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula kulia na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona wakitoka kukagua moja  ya miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akiteta jamboi na Diwani wa Kata Mwakijembe kushoto kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna
 Mhandisi wa Wakala wa Maji Vijiji (Ruwasa) wilaya ya Mkinga Castory Keneth katika akiwa chini ya ulinzi wa askari kufuatia Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuamuru akamatwe kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa maji wilayani humo

 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akimsaidia kufunga madumu ya maji kwenye baiskeli mtoto aliyemkuta akichota maji kwenye bwawa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona


NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso ameliamuru Jeshi la Polisi wilayani Mkinga kumkatama Mhandisi wa Wakala wa Maji Vijiji (Ruwasa) wilaya ya Mkinga Castory Keneth kutokana na kushindwa kusimamia mradi wa maji wa Mbuta na kupelekea kushindwa kukamilika kwa wakati huku wananchi wakiendelea kutekeseka kupata huduma hiyo muhimu.

Mradi huo ulianza 2013 ambapo serikali ilitoa kiasi cha zaidi ya milioni 400 lakini utekelezaji wake ulishindwa kukamilika na kupeleke tatizo la maji kwenye eneo hilo ambalo kupata shida ya maji.

Hatua hiyo ilichukuliwa na Naibu Waziri huo mara baada ya kuutembelea mradi huo ambao ulikuwa ukitekelezwa na mkandarasi White City ya Jijini Dar es Salaam na serikali ilikuwa imekwisha kulipa zaidi y a sh.milioni 400 lakini hakuna kitu ambacho kimefanyika na mkandarasi huyo huku ameutelekeza.

Alisema wizara hiyo imebaba dhamana kubwa hivyo wataalamu msipokuwa makini mnaweza kuungiza kwenye matatizo na kuchukiwa na wananchi hivyo kuna haja ya pamoja kufanya mageuzi ya uzalishaji wa maji vijijini lakini lazima watipie wataalamu husika.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba lazima Mkurugenzi Ruwasa ajiridhishe kwani wengine hawana sifa na kazi zao huku akimueleza kwamba mhandisi huyo hatoshi kwenye nafasi hiyo na hana uwezo ikiwemo kuwa na maslahi kwenye mradi huo.

“Hivyo Mimi kama Naibu Waziri nimeona kuna ubadhirifu mkubwa hapa hivyo nitatuma timu ya kuhakikisha ya mabwawa kuja kufanya tathimini kuona namna wanaweza kufanya kazi hii”Alisema

“Lakini wewe unatetea na kabisa inaonekana zahiri kuna fedha zimeliwa hapa sasa kabla hatujaenda huko nimuombe ODC akuchukua ukatusaidia kwenye jambo hilo”Alisema Naibu Waziri huyo.

Awali kabla ya kutoa maamuzi huyo Naibu Waziri huyo alimpa nafasi Mhandisi huyo wa Ruwasa kueleza kuhusiana na mradi huo na namna ulivyotekeleza ambapo alimueleza majibu yasiyoridhisha na kuamua kuchukua maamuzi hayo.

Hata hivyo serikali imesema kwamba n kuhakikisha wannahi mkinga wanapata huduma ya maji kwa kuanzisha mamlaka ya maji pamoja na kupata mradi mkubwa utakaotoa maji Mabayani hadi Horohoro.

Awali akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Aweso, Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula alisema kwamba bwawa moja la mbuta lilishazolewa huku akikabidhiwa mkandarasi aanze kazi upya.

Alisema ilifikia mahali wakatumia ujanja ujanja kupasua tuta ili maji yasipasue tena tuta lakini eneo la Mwakijembe umejaa maji kwa hali hii yanaweza kutokea balaa wakati mwengine hivyo wanahitaji fedha haraka ili mkandarasi akamilishe mradi kwa sababu kazi ni ndogo.

Aidha alisema lakini wilaya ya Mkinga hawana mradi mkubwa wa maji hasa kwenye ukanda wa bahari eneo la mkinga mkoa wa Tanga ambapo ndio lina eneo kubwa kuliko sehemu nyengine na upozungumzia uwekezaji unaongeleo huku kuwepo mahoteli makubwa lakini hakuna wekezaji unauofanyika kutokana na ukosefu wa maji.

Hata hivyo alisema kwamba ule mradi wa mabayani ungeweza kutengewa fedha ufanyika kutoka Tanga mpaka horohro kilomita 65 na kinachoumiza maji wanayokunywa watu wa Jiji la Tanga chanzo chake ni Mkinga kata ya Bosha na Mhinduro wanatunza vyanzo vya maji lakini wao wanabaki watazamaji.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark alisema kwamba wakazi wa wilaya hiyo wanapata maji bomba, visima na mabwawa kwa asilimia 56 ongezeko hilo ni asilimia mbili toka asilimia 54 2015/2016.

Alisema kwamba asilimia hiyo inatokana na kwamba wametengeneza mabwawa lakini hawajatengeneza miundombinu ya kuwapelekea wananchi maji kwenye maeneo yao .

Alisema wizara ya maji imewapelekea bilioni 2.9 ili kutekeleza miradi ya maji vijiji vya mapato,Makao Makuu ya wilaya ya Mkinga Parungu Kasera,Kilulu,Doda,Bwagamacho,Bamba Mavenegro,Mwarongo,Mbuta na Mwakijembe.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba ujenzi wa miradi ya maji vijijini walifanikiwa kupata vyanzo vya maji tisa badala ya kumi lakini vijiji saba vimekamilisha ujenzi huku miradi ya miwili ni ule wa Mbuta na Mwakijembe huku akieleza ule wa mbuta changamoto mkandarasi alikatisha mkataba kwa sababu kutokulipwa. Mwisho.
Share:

Director of Finance & Operations

Overview Management Sciences for Health (MSH) is seeking a Director, Finance and Operations for a potential 5-year US Centers for Disease Control (CDC)-funded, Sustained Health Systems Strengthening (SHSS) Project in Tanzania. This project will provide technical assistance (TA) to the Government of Tanzania (GOT) in the form of capacity building of Public Health Institutions (PHIs) to implement and… Read More »

The post Director of Finance & Operations appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

External Relations, INTERN, I (Temporary Job Opening) – International Residual Mechanism for Criminal Tribunals

Job Opening Posting Title: External Relations, INTERN, I (Temporary Job Opening) Job Code Title: INTERN – ADMINISTRATION Department/Office: International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Duty Station: ARUSHA Posting Period: 22 May 2019 – 24 May 2020 Job Opening Number: 19-Administration-RMT-117024-J-Arusha (A) Staffing Exercise N/A   United Nations Core Values: Integrity, Professionalism, Respect for Diversity Apply Now Org. Setting… Read More »

The post External Relations, INTERN, I (Temporary Job Opening) – International Residual Mechanism for Criminal Tribunals appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger