Sunday 1 December 2019

Kampeni Ya Elimu Kwa Mlipakodi Kuanza Kesho Dar

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatarajia kuanzisha Kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Mkoa wa Dar es Salaam itakayodumu kwa siku 13 kuanzia kesho tarehe 2 hadi 14 Desemba, 2019.

Akizungumzia kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema kuwa lengo ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na kupokea maoni kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

"Kampeni hii ni mwendelezo wa kampeni ambayo imemalizika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani na sasa tunaingia katika Mkoa wa Dar es Salaam tukiwa na lengo la kuwaelimisha walipakodi na wananchi masuala yanayohusu kodi, kupokea maoni yao, kusikiliza changamoto na malalamiko ili tuweze kuyatafutia ufumbuzi", alisema Kayombo.

Kayombo ameongeza kuwa kampeni hiyo itaambatana na huduma ya usajili wa wafanyabiashara wapya wasiokuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi yaani TIN.

"Pamoja na kutoa elimu ya kodi, kupokea maoni na kusikiliza changamoto za walipakodi pia tutatoa huduma ya usajili wa walipakodi wapya ambapo tutawapatia cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi tukiwa na dhumuni la kupanua wigo wa walipakodi hapa nchini", aliongeza Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo amebainisha maeneo ambayo yatafikiwa katika kampeni hiyo kuwa ni Ilala, Kinondoni, Temeke na Kariakoo na itafanyika kwa njia ya semina katika vituo vilivyopangwa kwenye maeneo hayo pamoja na kuwatembelea walipakodi katika biashara zao yaani duka kwa duka.

MWISHO.


Share:

WENYEVITI WAPYA WA VIJIJI NA VITONGOJI JIMBO LA KISESA MKOA WA SIMIYU WAAPISHWA, MBUNGE MH. LUHAGA MPINA AWATAKA WAKATAMBUE MAHITAJI YA WANANCHI, KUTANGAZA MAFANIKIO YA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

 Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wao kutoka Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu wakila kiapo cha utii  kwenye hafla iliyofanyika Mwandoya Makao Makuu ya Jimbo la Kisesa.
 Wenyeviti wote wa Vijiji vya Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuapishwa.
 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ikigijo Kata ya Mwabusalu Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Itinje Kata ya Itinje Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo

  Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Lingeka  Kata ya Lingeka Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha  Matale Kata ya Tindabuligi Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha  Mbugayabahnya Kata ya  Mbugayabahnya Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo

 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mwashata  Kata ya  Mwabuma Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
 Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ntobo  Kata ya Kisesa  Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
  Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Nyanza  Kata ya Mwakisandu  Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Semu  Kata ya Isengwa  Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo

Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha  Ming’ongwa Kata ya Sakasaka  Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili December 1















Share:

Saturday 30 November 2019

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA KUPANDIKIZA FARU WEUPE NCHINI KWA MARA YA KWANZA


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala  akiwa na baadhi ya wasanii wa muziki na filamu katika hifadhi ya Burigi Chato

Na Ashura Jumapili - Malunde 1 blog 

WIZARA ya Maliasili na Utalii ipo katika mchakato wa kupandikiza Wanyama zaidi wa aina mbalimbali katika hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi Chato wakiwemo Faru weupe ili iweze kuwa kivutio kwa watalii mbalimbali ambao wameanza kutembelea hifadhi hiyo.

Akiongoza zoezi la utalii wa kutembea kwa miguu akiwa amefuatana na wasanii wa muziki na filamu katika hifadhi hiyo, mpya iliyopo katika mikoa ya Kagera na Chato Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala amesema kwa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania imeamua kupandikiza Faru weupe katika hifadhi ya Burigi Chato.

Alisema utatifi bado unaendelea wa kuangalia namna ambavyo Faru hao weupe wataweza kuishi katika hifadhi hiyo kwa sababu hawakuwahi kuwepo kabisa hapa nchini.

Alisema ,Asili ya Faru weupe wanazaliana kwa wingi na kwa haraka hivyo wakipandikizwa katika hifadhi hiyo watasaidia sana kukuza idadi ya Faru weupe katika nchi na pia kuendelea kuwahifadhi kwa faida ya dunia nzima.

Pia alisema utafiti wa kupandikiza Faru weusi katika hifadhi hiyo umekamilika na malisho yapo ya kutosha na kudai kuwa asili ya hifadhi ya Burigi Chato ni nchi ya Faru historia inaonyesha kulikuwa na Faru wengi.

Alisema pia wamesha peleka familia moja ya Simba kutoka hifadhi ya Serengeti Mkoani Mara na kudai kuwa bado wapo kwenye uzio na wataachiwa rasmi baada ya wiki mbili.

 Msanii wa filamu Steven Mengele maarufu kama (Steve Nyerere) alisema hifadhi ya Burigi Chato ilichelewa sana lakini awamu ya tano imewekezekana chini ya msimamizi wake Khamis Kigwangala na wizara nzima ya maliasili na utalii.

Mengele,alisema Burigi Chato ndio mbuga ya kwanza yenye Twiga warefu na weusi pia ina kila vivutio alivyowahi kuviona.

Single Mtamabile,maarufu kama (Rich )alisema kutembelea hifadhi unapata uzoefu mkubwa sana katika mambo ya uhifadhi wa mazingira na utalii.

“Sisi wenyewe tulikuwa tunaona ni kawaida lakini tulipofika katika hifadhi hii ya Burigi Chato tumeona na kujifunza vitu vingi katika masuala ya Utalii”,alisema Mtambalike.

Alisema kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za Taifa unakuwa unalinda asili yako na rasiliamali za nchi kwa kufika kujifunza na kuelewa namna ya kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira.
Share:

Picha : SHIRIKA LA FIKRA MPYA LAENDESHA KONGAMANO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA




Shirika lisilo la kiserikali liitawalo Fikra Mpya la Mkoani Shinyanga, linalofanya shughuli ya kutoa elimu ya kujitambua kwa mtoto wa kike, limeendesha Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike kutoka Shule za Sekondari Nane Mjini Shinyanga.


Kongamano hilo limefanyika leo Novemba 30, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu mjini Shinyanga (Shycom), na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakiwemo maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la jinsia kutoka polisi, walimu, pamoja na wazazi.

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, amesema wameendesha Kongamano hilo kwa wanafunzi wa kike, ili kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni, ambalo limekuwa likizima ndoto za wanafunzi walio wengi.

Amesema wameendesha Kongamano hilo kama sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia, ambayo ilianza kuadhimishwa Novemba 25 mwaka huu na itahitimishwa Desemba 10, kwa kufanya mijadala mbalimbali ya kujadili namna ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.

“Shirika letu tumeamua kuendesha Kongamano hili la kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambapo tunajadili kwa pamoja na wanafunzi ili kupata suluhu ya kutokomeza ukatili na wanafunzi wapate kutimiza ndoto zao,” amesema Josiah.

“Mkoa wetu wa Shinyanga na Kanda ya ziwa inatajwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake, ambapo takwimu zinaonyesha kuanzia Januari hadi Juni 2019 kanda ya ziwa inaongoza kwa asilimia 38, ikifuatiwa na mikoa ya nyanda juu kusini asilimia 32, Pwani asilimia Tisa (9),

“Kanda ya kaskazini asilimia Tisa (9), Kanda ya Kati asilimia Saba (7), pamoja na Kanda ya Magharibi asilimia Tano (5),”ameeleza Josiah.

Naye mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda, akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wanafunzi wanapokuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wasikae kimya, bali watoe taarifa ili wahusika wapate kuchukuliwa hatua na kukomesha vitendo hivyo.

Nao baadhi ya wanafunzi akiwemo Mariamu Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele, wameshukuru kuendeshwa kwa Kongamano hilo, ambalo wamedai limewasaidia kuwapatia upeo namna ya kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia, pamoja na wapi pa kwenda kutoa taarifa hizo.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia leo Jumamosi Novemba 30,2019. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Kongamano la Kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mratibu kutoka Shirika la Women Fund Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia, akifungua mjadala wa kujadili juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutafuta suluhu ya kuvitokomeza.

Mwenyekiti wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga Rose Matiku akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia.

Afisa wa Jeshi la Polisi kutoka dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga Joseph Christopher, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah.

Mzazi Aida Luben akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwandishi wa habari Isack Edward kutoka Radio Faraja, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia namna vyombo vya habari vinavyosaidia kutoa elimu ya kutokomeza matukio hayo.

Mwanafunzi Verynice Busanga kutoka Shule ya Sekondari Mwasele, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwanafunzi Mariam Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia.

Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa Kijinsia.

Mgeni Rasmi afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akipokea maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa wakiwa na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa, wanafunzi pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya ,wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Share:

SIMBA SC YAMTIMUA KOCHA PATRICK AUSSEMS

Share:

Mbowe Arejesha Fomu yake ya Kugombea Uenyeki CHADEMA, Tundu Lissu Kuwa Makamu Mwenyekiti

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema atagombea Makamu Mwenyekiti wa chama hicho katika Uchaguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa ndani ya chama hicho.
 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe wakati akirejesha fomu yake ya kuwania Uenyekiti wa chama hicho kwa Katibu wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini.

Mbowe amesema kuwa "Sisi viongozi tunafahamiana historia zetu na umadhubuti wetu, baada ya mashauriano tumemuelekeza Tundu Lissu ajaze fomu ya kuomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti, na amefanya hivyo japo hatuzuii mwingine yoyote kujaza nafasi hiyo"

"Kwa sababu Prof. Abdallah Safari (Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara) anaondoka, wamejitokeza Watanzania kadhaa kujaribu kugombea nafasi hiyo, kwa kuwa tunahitaji viongozi" amesema Mbowe


Mbowe alichukuliwa fomu hiyo na wanachama waliochanga Sh1 milioni kulipia gharama na kumkabidhi. Baada ya kuipokea mbunge huyo wa Hai aliikabidhi kwa katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.

Mara baada ya kukabidhi fomu hiyo, wanachama waliofurika katika ukumbi unakofanyika mkutano huo walishangilia

Kwa sasa chama hicho kimeingia kwenye Uchaguzi wake wa ndani ngazi ya Kikanda ambapo Desemba 18, ndiyo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti utafanyika.


Share:

NHIF Yatoa Ufafanuzi Juu ya Taarifa za Ongezeko la Michango ya Wanachama Kutoka 18,000 Hadi 40,000

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema hakuna mabadiliko ya michango kwa watumishi kama ambavyo taarifa zinazosambazwa mitandao zinadai kuwa kuna ongezeko la uchangiaji kutoka TZS 18,000 hadi TZS 40,000.


Share:

Madiwani Watano CHADEMA Jijini Arusha Wajiuzulu na Kutimkia CCM

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni amethibitisha amepokea barua za madiwani watano kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka ndani ya jii hilo kujiuzulu nyadhifa zao.

Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho.

Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala.




Share:

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila aagiza mawakala mashine za EFD kukamatwa

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameagiza mawakala wa mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD) mkoani humo, kukamatwa na kuwekwa ndani kutokana na kutohudhuria mkutano wa wafanyabiashara soko la Sido, jijini Mbeya leo Novemba 30, 2019.

Chalamila ametoa agizo hilo leo Jumamosi  katika mkutano wake na wafanyabiashara wa soko hilo kwa ajili ya kusikiliza kero zao.

"RPC  watafute leo Jumamosi wapumzike mahali tutakutana nao Jumatatu, haiwezekani huu ni upuuzi tunawahitaji wao hawapo hata sisi tumeacha usingizi," amesema.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Mbeya (TRA),  Jiji la Mbeya lina mawakala wanne kwa sasa ambao walitakiwa kuhudhuria mkutano huo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger