Friday 1 November 2019

Serikali Yawatoa Hofu Wananchi Wa Handeni Mkoani Tanga

Serikali imewahakikishia wakazi wa Handeni, Mkoani Tanga uendelevu wa huduma ya maji licha ya kuharibika kwa miundombinu ya maji kulikosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa kauli hiyo hapo juzi wilayani hapa wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua athari ya mvua kwenye miundombinu ya maji sambamba na kupata ufumbuzi wa haraka kufuatia hali ya mvua zilizonyesha kwa takribani wiki mbili mfululizo.

Mara baada ya kujionea hali halisi, Mhandisi Sanga aliwatoa hofu wananchi wa Handeni ambapo aliwataka kuwa watulivu na aliahidi kuwa Serikali itahakikisha huduma ya maji inarejea haraka iwezekanavyo.

"Ninawasihi wananchi kufanya subira na kuwa watulivu na kuzingatia maelekezo ya Serikali," alisisitiza Naibu Katibu Mkuu Sanga.

Mhandisi Sanga alibainisha kuwa zoezi la tathmini ya athari ya mvua hizo kwenye miundombinu ya maji wanaloendelea nalo halitochukua zaidi ya siku tatu kama ilivyoagizwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa.

"Waziri wa Maji ametuagiza kuharakisha kukamilisha zoezi hili, nasi tutahakikisha linafanyika kwa kasi ikiwa ni pamoja na kutazama njia mbadala ili wananchi wapate huduma ya maji kwa haraka," alisema Mhandisi Sanga.

Aliongeza kuwa Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli haipo tayari kuona wananchi wake wanataabika na kwamba hatua madhubuti na za haraka zinachukuliwa ili kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akielezea kwa ujumla athari za mvua hizo kwenye Mkoa wa Tanga, alisema kuwa zimeleta madhara kwenye miundombinu ya barabara na madaraja na kusababisha huduma ya usafiri katika maeneo mbalimbali kuathirika.

“Tulichokibaini katika mvua hizi zilizonyesha ni kuwa zimeharibu mabwawa ya maji na kusababisha maji yaliyotoka katika mabwawa hayo kuathiri miundondombinu mbalimbali ikiwemo ya maji na barabara,” alieleza Shigela.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akielezea athari za mvua hizo alisema ni pamoja na kuharibika kwa mabwawa 11 ya maji yanayotumiwa na wakazi wa Handeni na maeneo jirani na kati ya hayo yapo mabwawa makubwa matano ambayo aliyataja kuwa ni Kwenkambara, Mandera, Suwa, Msomera na Mkomba.

Aidha, Gondwe alipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna inavyotekeleza majukumu yake kwa wakati na kwa hatua mbalimbali za haraka zinazoendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kurejesha mawasiliano ya miundombinu ya barabara na maji iliyoathirika.

Sambamba na hilo, Gondwe alimpongeza Mhandisi Sanga na timu ya wataalam aliyoambatana nayo kutoka Wizara ya Maji na taasisi zake kwa kufika Wilayani hapa mapema ili kufanya tathmini ya uharibifu wa miundombinu ya mabwawa ya maji ili kupata ufumbuzi.

“Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Handeni tunatoa shukrani nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais kwa kutujali na kuwatuma watendaji wa Serikali kufika hapa Handeni ili kutatua matatizo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha,” alisema Gondwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo ambaye ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Sanga alisema kuwa wanaendelea na tathmini ila kwa mabwawa yaliyopasuka wamebaini yalijengwa chini ya kiwango na pia hayakuwa yakitunzwa inavyostahili na hivyo kupelekea kuharibika wakati mvua hizo zilizonyesha.


Share:

Kundi la IS latangaza kiongozi mpya Atakayemrithi Abu Bakr al-Baghdadi

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS limemtangaza kiongozi wake mpya baada ya kuthibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi katika shambulizi lililofanywa na Marekani nchini Syria. 

Taarifa iliyotolewa kwenye chombo cha habari cha IS, al-Furqan imeeleza kuwa nafasi ya al-Baghdadi itazibwa na Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi. 

Kundi la IS halikutoa taarifa zaidi kuhusu al-Qurayshi. Kiongozi huyo mpya anatambuliwa kama msomi, shujaa mashuhuri na kiongozi wa kivita ambaye amepambana na majeshi ya Marekani na ana ufahamu kuhusu vita hivyo. 

Taarifa hiyo pia imethibitisha kifo cha Abu Hassan al-Muhajir, msaidizi wa karibu wa al-Baghdadi ambaye alikuwa pia msemaji wa IS tangu mwaka 2016.

 Vifo hivyo ni pigo kubwa kwa kundi la Dola la Kiislamu karibu miezi saba tangu lilipofurumushwa kutoka kwenye ngome yake ya mwisho nchini Syria.


Share:

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro asimamia Zoezi la wanafunzi Watoro kuchapwa viboko mbele ya wazazi wao

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro jana Alhamisi  alisimamia zoezi la  kucharazwa viboko wanafunzi 3 ambao ni watoro sugu katika Shule ya Msingi Ligoma iliyoko wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni Tunduru.

Mkuu huyo wa wilaya  alimtaka mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwachapa viboko vinne wanafunzi hao na kuagiza  wapewe adhabu nyingine zisizohusiana na viboko, ikiwa ni pamoja na kuchimba visiki.

Baada ya viboko hivyo, aliwauliza wanafunzi hao lini wataanza kwenda shule na mmoja alijibu kuwa ataripoti Jumatatu,hata hivyo, mkuu huyo wa Wilaya alisema wote wanapaswa kuripoti leo.


Share:

Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Kwa Kumbaka na Kumpa Mimba Mtoto wake wa Kumzaa

Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani  Katavi  imemuhukumu  Lazaro  Charles (35)  Mkazi    wa Mtaa wa  Mji   Mwema katika  Manispaa ya   Mpanda Mkoa wa  Katavi kutumikia jela kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mtoto wake wa kumzaa  mwenye (14) ambaye ni, mwanafunzi wa  darasa la  saba shule ya msingi  Majengo Manispaa ya  Mpanda.

Hukumu  hiyo iliyovuta hisia za wakazi  wengi  wa  Manispaa ya Mpanda, ilitolewa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gosper Luoga baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani na upande wa mashtaka.

Awali katika kesi hiyo Mwanasheria wa Serikali Gregory  Muhangwa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti hapo Januari 1 mwaka 2017 na April 29, 2019.

Mshtakiwa huyo alikuwa akitenda kosa hilo huko nyumbani kwake wakati mke wake ambaye ni mama  mzazi wa mtoto huyo alipokuwa amesafiri ndipo alipokuwa akiingia kwenye chumba alichokuwa akilala mtoto wake huyo na kumbaka kwa nguvu.

Mwendesha mashtaka huyo alieleza kuwa baada ya kuwa anambaka  alikuwa akimwekea majani kwenye sehemu zake za siri kama dawa ya kienyeji  ya  kumwondolea maumivu.

Hakimu Luoga amemtaka mshtakiwa kama atakuwa na sababu yoyote ile ya msingi ambayo inaweza kuifanya mahakama iweze kushawishika ili kumpunguzia adhabu basi inatoa nafasi kujijitetea.

Lazaro Charles ameiomba mahakama  impatie nakala ya hukumu ya mwenendo wa kesi hiyo tu kwani hana utetezi wowote ule.

Baada ya ombi hilo la mshtakiwa mwanasheria wa Serikali Gregory Muhangwa aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia kama hiyo.

Hakimu Luoga baada ya kusikiliza pande hizo mbili alisoma hukumu na kuiambia Mahakama kuwa mshtakiwa amepatikana na kosa la kifungu cha sheria Namba 158 (1) (a ) SURA YA 16 ya marejeo 2002, hivyo Mahakama inamuhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela kuanzia leo Novemba 1, 2019.


Share:

Idris Sultan Aripoti Tena Polisi

Msanii wa vichekesho, Idris Sultan leo Ijumaa Novemba 1, 2019 saa 2 asubuhi ameripoti Kituo cha Polisi ‘Central’ jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana aliyopatiwa jana October 31, 2019.

Idriss alitakiwa kwenda polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa na kuambiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuripoti kituo chochote cha Polisi.


Share:

Twitter yapiga marufuku matangazo ya kisiasa

Jukwaa la mtandao wa kijamii Twitter limetangaza kwamba halitatangaza tena matangazo yenye muelekeo wa kisiasa.

Kiongozi mkuu ( CEO) wa Twitter, Jack Dorsey amearifu kwamba shirika hilo halitatoa tena matangazo yenye muelekeo wa kisiasa.

Dorsey amearifu kwamba uamuzi huo mpya utaanza kutumika mwishoni mwa mwezi Novemba.

Washindani wa mtandao wa kijamii wa Facebook hivi karibuni walifutilia mbali mpango wa kupiga marufuku matangazo ya siasa ya kibiashara.

Taarifa ya marufuku hiyo imeibua mgawanyiko katika kambi za kisiasa nchini Marekani zinapojiandaa katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Brad Parscale,meneja wa kampeni ya Raisi Donald Trump, kugombea muhula wa pili, amesema marufuku hiyo ni jaribio jingine la kumnyamazisha Trump


Share:

WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO KUELEKEA UCHAGUZI

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo kuripoti kwa weledi habari kuhusu ujenzi wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 31, 2019 Holmand Hotel jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko akitoa salamu kwenye ufunguzi wa warsha hiyo.
 Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Rose Mwanga akitoa neno la shukurani wakati wa kuahirisha mafunzo hayo.
Wanahabari wakimsikiliza na kunasa habari kwenye warsha hiyo. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo yenye Tija kwa Watu wote (PCD), Prof. Francis Matambalya akitoa utambulisho kuhusu Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) kwenye warsha hiyo. PCD ni idara ndani ya MNF.
 Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wanahabari mkoani Mwanza kuandika habari kwa weledi kabla, wakati na baada ya chaguzi.
Tazama Video hapa chini


Share:

Idris Sultan Aachiwa kwa Dhamana.....Kuripoti tena Polisi Leo

Msanii  Idris Sultan aliyehojiwa na polisi  jana Alhamisi Oktoba 31, 2019 kwa saa tano na kupekuliwa nyumbani kwake ameachiwa kwa dhamana usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kuhojiwa, mchekeshaji huyo ambaye jana alitakiwa kuripoti polisi na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikwenda na polisi nyumbani kwake.
 
Wakili wake, Benedict Ishabakaki amesema licha ya kwamba Msanii huyo ameachiwa kwa dhamana usiku, atatakiwa kuripoti tena Kituo cha Polisi leo saa mbili asubuhi ili Polisi waendelee na upelelezi wao.

Idris alitakiwa kwenda polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa.

Pia, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa November 1























Share:

Thursday 31 October 2019

Bashe:Serikali Imeamua Kuheshimu Na Kuweka Kipaumbele Sekta Ya Kilimo

Na.Faustine Galafoni,Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kilimo,Husein Bashe amesema Serikali imeamua kuheshimu na kutoa kipaumbele mazao ya kilimo kama sekta zingine zinavyothaminiwa kwa kujenga miundo mbinu rafiki kwa mkulima hususani pembejeo bora.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa kwenye mkutano wa kitaifa wa wakulima wadogo Tanzania uliofanyika jijini Dodoma kujadili changamoto wanazokumbana nazo ulioandaliwa na Shirika la ANSAF.

Waziri Bashe amesema kuwa sekta ya kilimo imekuwa msaada katika kuinua uchumi wa nchi kutokana na kaya ,jamii kwa ujumla kutumia malighafi nyingi zinazotokana na kilimo mbali na changamoto zinazowakabili wakulima .

Amebainisha tarari serikali imeweka mikakati ya kuboresha miundo mbinu kwa wakulima wadogo katika suala zima la kuongeza maafisa ugani vijijini huku wakishirikana na maafsa watendaji kutembelea wakulima,pembejeo zilizo bora na bei rahisi,upatikanaji wa mbegu nzuri,sheria ya kulinda wakulima,kuwapatia Bima ya mazao ,pamoja na kuongea na taasisi za kifedha kupata mikopo yenye riba nafuu jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo.

"Kama Wizara itaendelea kutangaza  na kuhamasisha wakulima wadogo kuboresha miundo mbinu ili kuwe na kilimo chenye tija  kwani wamekuwa wachangiaji wazuri uchumi wa nchi na jamii imategemea chakula kutoka kwa wakulima wadogo"alisema Waziri Bashe.

Hata hivyo amepiga marufuku kwa viongozi wa Ushirika ambao sio wakulima kuongoza wakulima kutokana na malalamiko yanayotolewa ambapo wao kazi kubwa ni kujinufaisha badala ya kuwasaidia wakulima hao.
"Kuanzia leo kiongozi ambaye sio mkulima hapaswi kuongoza wakulima haiwezekani wewe sio dhehebu ya kiislamu halafu eti uwaongoze waislamu"amesema.

Mbali na hayo amesema wizara imeanzisha Dawati la masoko ambalo litashughulikia wakulima ambao ufanyiwa ukiritimba na TBS huku akisema kutakuwa na huduma bure ya mawasiliano ambayo itawala fursa wakulima kupiga simu kueleza changamoto zao na kutatuliwa hapo hapo.

Nae mwenyekiti kamati ya Bunge kilimo,mifugo na maji Mahamoud Mgimwa amesema wabunge wako tayari kuendelea kuwatetea wakulima ili serikali iweze kutatua changamoto zao lengo ni kufikia asilimia kumi .

Kwa upande wake  Mwenyekiti jukwaa la wakulima wadogo wanawake ,Janeth Nyamayahasi amesema wanakumbana na changamoto ya upungufu wa maafisa ugani vijijini kwenye sekta ya mifugo,kilimo na uvuvi na kwamba baadhi ya wataalamu hao hawatoi ushirikiano na mara utoa ushauri mbovu unaopelekea mazao yao kuharibika.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Atarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi Wiki Ya Azaki.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya asasi za Kiraia Tanzania  [AZAKI]itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Novemba 4-8,2019.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Oktoba 31,2019,Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Civil Society  [FCS]BW.Francis Kimwanga amesema wiki ya asasi za kiraia nchini itakutanisha zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka nchi nzima Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi mtendaji huyo wa  FCS]  amefafanua kuwa Wiki ya Asasi za Kiraia [AZAKI]itajumuiya Maonesho  ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo huku lengo likiwa ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali  katika kutimiza azma ya kuiletea Tanzania Maendeleo.
 
"Lengo la kongamano hilo nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kutimiza azma ya kuileteaTanzanaia maendeleo," amesema .

Hata hivyo amesema "Kupitia  kongamano  hili asasi  za  kiraia  zitafanya majadilianao juu ya kazi  zao, kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na wananchi, serikali, bunge, wabia  wa  Maendeleo na sekta binafsi," amesema.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti  maalum mkoa  wa Dodoma  Fatma Taufiq ambaye  pia  ni  Mkurugenzi wa shirika  la  WOWAP  amesema wiki hiyo  ni  Wiki  ya kipekee  kwa  mwaka  huu washiriki  mbalimbali  wanatarajiwa kuwepo bila  kuwasahau viongozi  wakubwa kutoka serikalini huku pia akitoa rai kwa vyombo vya Habari kuhabarisha jamii umuhimu wa makundi maalum katika jamii.
 
“Asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika jamii,AZAKI inatekeleza Malengo 17 ya maendeleo endelevu hivyo nitoe rai kwa asasi ambazo zimekuwa zikienda kinyume na matakwa ya serikali na asasi sio adui zinashirikiana  na serikali .Pia nitoe rai kwa Vyombo vya Habari kuhabarisha umma juu ya Umuhimu wa Asasi hizi.amesema.

Hata hivyo  aliwataka  wananchi  wote kufika  katika viwanja  vya Jamhuri Novemba 4 Hadi 8 ili  kuweza  kuona  na  kujifunza  asasi  za  kiraia zinafanyaje  kazi zao n'a kuachana na  kusikiliza  habari  potofu kuwa  asasi za kiraia zinakula  hela na hazileti Maendeleo yoyote huo ni upotoshaji.

Msajili wa  asasi za kiraia kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia Wazee na Watoto,Charles Komba amesema asasi za kiraia zimekuwa chachu kubwa ya Maendeleo  na katika kuisaidia serikali.
 
“Asasi za kiraia ni Wadau wetu,ni wadau  wetu wakubwa   sana katika maendeleo ya kijamii,serikali haiwezi kufanya kwa kila jambo lakini sasi za kiraia zmekuwa mstari wa mbele kutusaidia.
 
Aidha,ameongeza kwa kusema ,Mpaka  mwaka 2017 serikali ilishasajili asasi za kiraia zaidi ya 10,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Haki,Rasilimali ,Mafuta ,Madini na gesi Rachel Chaganda amesema  taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na madini,Mafuta na gesi ambapo ni mchango mkubwa kwa serikali  Ya Tanzania.

Naye mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Ulemavu Tanzania[SHIVYAWATA] Ummy Nderiananga amesema katika wiki hiyo ya AZAKI,Kutakuwa na elimu pamoja na miradi mbalimbali  inayofanywa na watu wenye ulemavu huku afisa Uhusiano wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu,Legal Human Rights   Centre[LHRC] Michael Malya akisema katika wiki hiyo kituo hicho kitajihusisha na utoaji wa huduma za kisheria.
 
Ikumbukwe kuwa FCS itatoa tuzo za Umahiri wa asasi za kiraia  ili kusheherekea na kutambua ufanisi na michango   za taasisi na watu binafisi  katika uchocheaji na uimarishaji wa sera ya maendeleo ya nchi.
 
Zaidi ya asasi za kiraia 15  zikishirikiana na FCS   Kuandaa wiki ya AZAKI ni LHRC,LSF,Save the children, Wajibu Institute,UN Women,Oxfam,Twaweza,Policy Forum,msichana Initiative,Hakirasilimali, UNA Tanzania, Acountability Tanzania,Sikika,TLS,SHIVYAWATA,na TANGO.
Kaulimbiu  wiki  ya asasi za Kiraia [AZAKI] Mwaka ,2019 ni ubia kwa Maendeleo ,Ushirikiano kama chachu ya Maendeleo.







Share:

Watu 70 wafariki Pakistan kufuatia moto kwenye treni

Watu wasiopungua 70 wameuwawa na dazeni kadhaa kujeruhiwa baada ya jiko la gesi kuripuka ndani ya treni iliyokuwa ikiwasafirisha waumini waliokuwa njiani kwenda kufanya ziara ya kidini nchini Pakistan.

Picha za televisheni zinaonyesha moto unaofuka ndani ya mabehewa matatu ya treni huku vilio vikisikia ndani ya treni hiyo katika eneo la vijijini la mkoa wa kati wa Punjab.

Baadhi ya abiria-wengi wao wakiwa waumini waliokuwa njiani kwenda katika ziara ya kidini katika mji wa mashariki wa Lahore, walikuwa wakipika chakula cha asubuhi pale majiko yao mawili ya gesi yaliporipuka-Ali Nawaz, afisa wa ngazi ya juu wa shirika la safari za reli la Pakistan ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wapakistan wengi wanabeba vyakula wanapokuwa katika safari ndefu lakini majiko ya gesi yamepigwa marufuku. Ali Nawaz anasema uchunguzi unafanywa kuhusu ajali hiyo.

Televisaheni za Pakistan zimeonyesha jinsi dazeni za watu walivyokusanyika njiani kuangalia jinsi moto unavyofuka ndani ya mabehewa  ambayo yaliachana na sehemu nyengine ya treni.

Waziri Mkuu Imran Khan ameamuru uchunguzi juu yakisa hicho kufanywa mara  moja
 
Vikosi vya  zimamoto vimefika haraka katika eneo hilo karibu na wilaya ya Rahim Yar Khan. Watumishi wa mashirika ya uokozi na wanajeshi pia wameonekana wakisaidia. Miili ya wahanga wa ajali hiyo iliyofunikwa shuka nyeupe imekuwa ikiondolewa.
 
-DW

Share:

TIGO YAINGIZA SOKONI ‘KITOCHI 4G SMART’ ’ YENYE UWEZO WA 4G KWA BEI NAFUU

Share:

TRENI YASHIKA MOTO NA KUUA WATU 65

Takriban abiria 65 wamefariki dunia wakati treni iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Karachi Pakistan kuelekea Rawalpindi iliposhika moto.

Waziri wa reli, Sheikh Ahmed, alisema kwamba moto huo ulisababishwa na kulipuka kwa mtungi wa gesi uliokuwa ukitumiwa na abiria kupikia kiamsha kinywa mwendo wa asubuhi.

Moto huo unadaiwa kusambaa hadi katika mabehewa matatu, kulingana na maafisa walionukuliwa katika vyombo vya habari vya eneo hilo.

Waathiriwa wengi walifariki walipojaribu kuruka kutoka kwa treni hiyo iliokuwa ikichomeka.

Watu wengine 30 wameripotiwa kujeruhiwa na maafisa wanasema kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

"Majiko mawili aina ya stove yalilipuka. Walikuwa wakipika , walikuwa na mafuta ya kupikia ambayo yalichochea moto huo kuongezeka'', Sheikh Rashid Ahmed alisema.

Abiria wanaoingia na stove katika treni ili kupika chakula wakati wa safari ndefu ni swala la kawaida waziri huyo aliongezea.

Aliongezea kwamba abiria wengi walikuwa wakielekea katika kongamano lililoandaliwa na vuguvu la dhehebu la Kisuni Tablighi Jamaat.

Ajali hiyo ilitokea karibu na Rahim Yar Khan kusini mwa mkoa wa Punjab. Treni hiyo iliokuwa ikisafiri kutoka Karachi kupitia maeneo mengi ya Pakistan hadi Rawalpindi inaitwa Tezgam mojawapo ya treni za zamani ambayo ni maarufu sana.

Inahudumu kila siku na inachukua saa 25 na nusu.

Pakistan ina historia ya ajali za gari moshi zinazosababisha maafa mengi. Waathiriwa huwa wengi kwa kuwa treni hizo hubeba watu wengi zaidi ya viwango vyao.

Tarehe 11 mwezi Julai , watu walifariki katika ajali , huku wengine wanne wakifariki katika ajali nyengine mwezi Septemba.

Mwaka 2007, takriban watu 56 waliuawa na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa katika ajali karibu na eneo la Mehrabpur.

Mwaka 2005, zaidi ya watu 130 waliuawa wakati treni tatu zilipogongana katika mkoa wa Sindh katika kile kilichotajwa kuwa ajali mbaya zaidi inayohusisha treni kuwahi kutokea.
CHANZO - BBC
Share:

Job Opportunity at Coca Cola – Kwanza Limited, Warehouse Team Leader

WAREHOUSE TEAM LEADER (CCB191030-8) Closing date: 2019/11/12 Job Title WAREHOUSE TEAM LEADER Function Logistics, Warehouse & Distribution Company: Coca-Cola Kwanza (Tanzania) Job Type Permanent Location – Country Tanzania Location – Province Not Applicable Location – Town / City Dar es Salaam Job Description  Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Logistics Department. We are looking for a… Read More »

The post Job Opportunity at Coca Cola – Kwanza Limited, Warehouse Team Leader appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Business Performance Lead Job at Diageo Tanzania

Position: Business Performance Lead Location: Dar es Salaam, Tanzania Job Description : Are you looking to grow and develop as your role rapidly increases the value it brings to the organization? The finance functions within Diageo both at the headquarters and in markets has a mission to be great business partners driving great business performance‟. As business partners,… Read More »

The post Business Performance Lead Job at Diageo Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MWANAFUNZI APIGWA VIBOKO MPAKA KUFA DARASANI

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 huko nchini Burundi amefariki baada ya kupigwa na mwalimu wake, baba wa mtoto huyo ameiambia BBC.

Mtoto huyo, Chadia Nishimwe alipigwa viboko kwenye maeneo ya shingo na miguuni , kipigo ambacho kilimpelekea kutokwa damu puani na masikioni, alisema Jean-Marie Misago.

"Alikufa darasani mara baada ya kupigwa na mwalimu wake, na wakaenda kumtelekeza katika ofisi ya mwalimu mkuu," Bwana Misago alisema.

Mkuu wa shule alijaribu kumuwahisha hospitalini mtoto huyo wakati mtoto ameshakufa tayari, aliongeza baba huyo.

BBC imejaribu kutafuta taarifa zaidi katika sekta ya elimu bila mafanikio.

Mtoto huyo aliuwawa siku ya jumanne na kuzikwa siku hiyo hiyo .

Nchini Burundi, adhabu ya kuchapwa kwa mwanafunzi ni kinyume na sheria ingawa bado wanafunzi wanachapwa.
Chanzo - BBC
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger