Wednesday 30 October 2019

PAPA FRANCIS KURUHUSU WANAUME WALIOOA KUWA MAPADRI....MAASKOFU WAMEPIGA KURA

Maaskofu wa kanisa katoliki wamepiga kura kuruhusu wanaume waliooa kuwa mapadri katika eneo moja la pembezoni ili kuweza kupata mwanya wa kuhubiri katika eneo la Amazon.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Papa Francis kutoa ombi kuwa ni vyema kutoa ruhusa kwa wanaume waliooa kuwa mapadri kwenye sehemu maalum katika eneo hilo la Amazon.

Eneo ambalo waumini wengi wanaotaka kushiriki misa na kupokea mkate wa komunio hawaonagi mapadri kwa zaidi ya miezi kadhaa na muda mwingine hata miaka.

Amesema yeye na washiriki wengine wanaojulikana kama 'synod' wapo wazi kwa mawazo ya kutafuta njia mpya itakayosaidia kusambaza imani hiyo.

Watahitajika kupata wanaume wanaoheshimika na kulingana na stakhabadhi hizo watafanya kazi katika jamii wanazotoka.

Maaskofu wa Marekani Kusini wamepigania juhudi hizo ili kukabiliana na upungufu wa mapadri katika eneo hilo.

Lakini wakosoaji wamedai kuwa papa anapaswa kuhamasisha mapadri wasioe, ingawaje katika karne ya kwanza ya kanisa, mapadri waliruhusiwa kuoa, na karibia mapapa wote wa mwanzo walikuwa wameoa.

Vilevile kuruhusu wanaume walioa katika sehemu za Amazon ambazo zinakabiliana na ukosefu wa mapadri, kutaenda kinyume na sheria za kikatoliki ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa sasa.

Kwa sasa papa anaruhusu wanaume walioa kuwa mapadri katika makanisa ya mashariki ya kati pekee.

Upigaji kura ukiwa unafikia ukingoni huko Vatican kutokana na uhaba wa mapadre ili mapendekezo hayo yaanze kufanya kazi rasmi.

Wengi wakiwa wanahofia mabadiliko hayo katika kanisa kwa kuanzisha utaratibu mpya katika kanisa.

Kura zimechukuliwa kwa kipindi cha wiki tatu,kwa maaskofu 180 wa mjini Rome.

Wakiwa wanaangalia majukumu ya wanawake katika kanisa na namna mazingira yatakavyoweza ruhusu.

Kanisa katoliki ni taasisi kongwe ya kidini ambayo imekuwa na historia kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita huku ikiwa na mabilioni ya waumini.

Huku inakadiriwa kuwa karibu 85% ya vijiji huko Amazon haviwezi kusherehekea Misa kila wiki kwa sababu ya uhaba huu na wengine huonana na makuhani mara moja tu kwa mwaka.
Chanzo - BBC
Share:

MAKONDA : UBUNGO HATUJAPATA VIONGOZI KWA AJILI YA MAENDELEO YA WANANCHI, TUMEPATA KWA AJILI YA MATUMBO YAO





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewaonea huruma wakazi wa Ubungo kwa kile alichokieleza kuwa hawakuchagua viongozi sahihi, ambao wangeweza kutatua kero zao hii ni baada ya kufika katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya, bila kuwaona wabunge,pamoja na Meya wa Halmashauri hiyo.

Hayo ameyabainisha Oktoba 29, 2019, alipotembelea eneo ambalo litajengwa hospitali hiyo inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu, ujenzi utakaosimamiwa na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.5.

''Kama nilivyosema juzi, Ubungo hatujapata viongozi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, tumepata kwa ajili ya matumbo yao na ndio maana nimefika hapa nikawa nawatafuta, Meya, Mbunge wa Kibamba na Ubungo yuko wapi, hayupo,sasa niwasihi wakati mwingine msiwaonee haya walafi na wanaonenepa kupitia pesa zenu, wakati wao wameshindwa hata kupaza sauti ili ninyi muweze kupata huduma bora, nafahamu kuna baadhi ya maeneo Ubungo yana changamoto ya barabara, lakini wabunge wenu wala Meya wenu hawana chochote cha kuongea lakini utawakuta wamehamia twitter'' amesema Makonda.

Kufuatia hali hiyo Makonda amewaomba wakazi wa Ubungo, katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wahakikishe wanachagua viongozi wanaojitambua na watakaoweza kuwasilisha vyema kero zao ngazi za juu.

Oktoba 26, 2019, wakati wa upokeaji wa ndege mpya Dreamline ya pili, Makonda aliwasilisha ombi la kutengewa fedha hizo, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, aliridhia ombi hilo na kuagiza zitengwe shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Share:

KUTOPANGA BAJETI YA FAMILIA CHANZO CHA LISHE DUNI KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA

Share:

Jobs Opportunities at SOS Children’s Village Tanzania

Jobs Opportunities at SOS Children’s Village Tanzania Deadline: 04 November, 2019 Mama Msaidizi SOS Children’s Villages Tanzania is a local non-government organization affiliated to SOS Children’s Villages International, a worldwide childcare organization that provides orphaned and destitute children with a permanent home and educational opportunities. Established 60 years ago, SOS Children’s Villages International the umbrella organization, currently has… Read More »

The post Jobs Opportunities at SOS Children’s Village Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Office Management Secretary Job Opportunity REPOA

Office Management Secretary Job Opportunity REPOA Deadline 11th November 2019 REPOA is an independent policy research institution established in 1994 to undertake research, capacity building, and policy engagement on various aspects of economic growth and human development. It is one of the leading research organization in Tanzania, and among the top Think Tanks in Sub-Saharan Africa. REPOA believes… Read More »

The post Office Management Secretary Job Opportunity REPOA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Internships Opportunities at International Organization for Migration (IOM) Dar es Salaam

Internships Opportunities at International Organization for Migration Dar es Salaam Deadline 06 November, 2019 Vacancy Announcement IOM/DAR/031/19 Position title CVAC Intern Position grade Ungraded – UG Duty station Dar es Salaam, Tanzania II. ORGANIZATIONAL CONTEXT AND SCOPE Under the general oversight of the Immigration & Border Management (IBM) Division’s Immigration & Visa Support Solutions (IVSS) Unit at HQ… Read More »

The post Internships Opportunities at International Organization for Migration (IOM) Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano October 30




Share:

Tuesday 29 October 2019

TGNP KUFANYA MAPITIO YA SERA NA ILANI ZA VYAMA VYA SIASA TANZANIA


Na Deogratius Temba
TGNP Mtandao imepanga kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa kwa mrengo wa kijinsia na kushauri kufanya marekebisho mapema kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukabidhi ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa chama cha ACT Wazalendo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, alisema kwamba baada ya kutembelea vyama kadhaa vya siasa nchini na kusikiliza jinsi wanavyotekeleza masuala ya kijinsia, ameona kuwa kuna haja ya TGNP na Mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na Usawa wa Jinsia, kufanya uchambuzi au mapitio ya sera na ilani za vyama kwa mrengo wa kijinsia na kuangalia mapengo ili kushauri marekebisho.

“Tunapoelekea uchaguzi wa seriali za Mitaa, na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2020, tunahitaji vyama hivi kuzingatia kwa kiasi kikbwa usawa wa kijinsia kwneye uteuzi wa wagombea. Kama chama hakina sera za ndani ambazo zina mrengo wa kijinsia, ni lazima mapendo yataendelea kuwepo. Tunashukuru kwamba vyama vya siasa vimejitahidi, lakini bado hatujafikia malengo”, alisema. 

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti w aTaifa wa ACT Wazalendo, Doroth Semu alisema pamoja na kwamba chama kinajitahidi kutoa fursa sawa kwa wanawake bado watajitahidi kuendelea kuteua wanawake kushiriki kwenye chaguzi.

“Mwaka huu tumejipanga kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, tutahakikisha kila mahali ambapo wanawake wamejitokeza wanapata nasi, lakini kwa sababu mmetuletea hii Ilani yenu, tutahakikisha tunaitumia ili wagombea watakao shinda wakatekeleze ilani husika”, alisema Semu.

Ilani ya Madai ya wanawake kwa uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Mtandao wa wanawake na Katiba, imewashirikia na kukusanya maoni ya wanawake kutoka katika makundi yote nchini hasa vijijini.

Asasi za kiraia zinazotetea haki na usawa wa Kijinsia zaidi ya 60 zimeshiriki.

Share:

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yakutana Na Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Viwanda, Biashara Na Mazingira.

Imebainika kuwa Sera ya Usimamizi wa Mazingira (1997) na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.20 ya mwaka 2004 (Sura ya 191) ndio muundo muhimu wa usimamizi wa mazingira nchini. 
 
Hayo yamesemwa hii leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano katika Sekta ya Mazingira mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira jijini Dodoma.
 
Naibu Waziri Sima amesema katika  kuhusisha masuala ya kuimarisha usimamizi wa rasilimali
Ofisi yake imeandaa Sera, Sheria na Mikakati inayohusiana na uhifadhi wa Rasilimali za  Misitu, vyanzo vya Maji, Ardhi oevu, Wanyamapori, Gesi asilia, Madini na Nishati.
 
Mambo mengine yaliyotekelezwa ni pamoja na kuongoa mifumo ikolojia ya majini iliyoharibika ili kuwepo kwa huduma bora kwa afya ya jamii na ikolojia; kuhifadhi rasilimali za bahari kwa maendeleo endelevu, Miradi na kampeni mbalimbali zimetekelezwa  zikilenga kupunguza uharibifu wa ardhi kwa maendeleo endelevu. 
 
Aidha katika kuimarisha mifumo ya kijamii ya usimamizi wa rasilimali, Naibu Waziri Sima amesema Ofisi yake imeimarisha usimamizi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi kupitia Mradi wa Bonde la Ziwa Nyasa, Mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika, Mradi wa usimamizi endelevu wa ardhi, ambayo yote inasimamiwa na Ofisi yake.
 
Katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa miradi mbalimbali na kukuza teknolojia za nishati jadidifu zinazoweza kurejereshwa (biogas, petroli gesi (LPG), nishati ya jua,pepo na joto la ardhi) pamoja na kusaidia programu za utafiti, kukuza teknolojia mpya, mbegu bora, udhibiti wa wadudu waharibifu, na mbinu bora za kilimo.
 
Wakichangia wasilisho hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Saddiq na Kanali Mstaafu Masoud Ali ameishauri Serikali kuwa na Mikakati thabiti ya kuzuia uharibifu wa Mazingira nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika kutunza rasilimali za misitu, ardhi na mazingira yanayowazunguka kwa kushirikiana na wakaguzi wa Mazingira.
 
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo imepokea taarifa  ya Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira kuhusu utekelezaji wa wa Mpango wa miaka mitano wa Maendeleo kwa Sekta ya Mazingira (Mafanikio na changamoto) pamoja na Ripoti ya hali ya mazingira Nchini.


Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Arejea Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, Ieo Oktoba 29, 2019 amerejea nchini akitoka Baku nchini, Azerbijan ambako alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi zisizofungamana na upande wowote.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Mkuu amepokelewa na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es salaam.

Awali, Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika na Urusi uliofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Fahamu Zaidi Kuhusu Ugonjwa Wa Mshipa Wa Ngiri (Hernia/Hydrocele)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Kwa Ushauri na Msaada  Wasaliana na 
0713785111


Share:

Bilioni 10 Za Rais Magufuli Zaanza Kazi Ruvuma

Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
Shilingi Bilioni 10 zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Askari wa Vyeo vya chini zimeanza kutumika mkoani Ruvuma huku jumla ya nyumba sita zikiwa zimejengwa katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Rais Magufuli aliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha wakati akizindua Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha mwezi April mwaka huu.

Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa nyumba hizo mkoani Ruvuma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alisema tayari nyumba hizo zimekamilika na tayari ujenzi unaendelea mikoa yote nchini ambako ilibainika kuna changamoto ya makazi ya askari

“Rais wetu aligundua changamoto ya askari wetu hawa hasa wa vyeo vya chini,akatoa kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa jeshi la polisi,leo nimefika hapa kuangalia matumizi ya fedha hizo na nimeridhishwa na hatua ya ujenzi ulikofikia kwani nyumba zimekamilika na tayari nimeona baadhi askari wetu washahamia,”alisema Masauni

“….tunatembea nchi nzima kuona nyumba hizo zimefikia hatua gani lengo ni kuona askari wetu wanahama katika makazi duni na kuhamia nyumba hizi mpya ambazo serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa hiyo changamoto.” Aliongeza Masauni

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Kamishna Msaidizi Simon Marwa alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kiasi hicho cha fedha ambapo wao walipata mgao wa Shilingi Milioni 150/=  huku akitaja idadi ya nyumba walizojenga.

“Nyumba zishakamilika na askari wa vyeo vya chini wameshahamia kama maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalivyosema, hapa kuna nyumba sita ambazo kuna vyumba viwili vya kulala, sebule na chumba cha kulala kwa kila nyumba,” alisema RPC Simon

Kamanda Simon alisema mkoa wa Ruvuma una wilaya tano za Songea, Tunduru, Mbinga, Namtumbo na Nyasa huku mapendekezo ya nyumba hizo kwa mkoa huo zikijengwa wilayani Namtumbo ambako changamoto ya makazi ilikua kubwa tofauti na wilaya zilizobakia.


Share:

Nafasi Mbalimbali za Kazi Zilizotangazwa na Coca Cola Tanzania, Tigo Tanzania, Vodacom Tanzania, Umoja wa Mataifa na Zingine Kibao

==>>Nafasi za Kazi za  Kujitolea SNV( Wanatakiwa watu 8)


👉Volunteers wanahitajika Dar,Moshi,Mbeya,Dodoma,Katavi, Songea
👉Deadline; November 3, 2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Coca Cola Tanzania Wametangaza Nafasi Mpya ya Kazi

👉Wanataka; Distribution Driver 
👉Deadline; November 5, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  
 
==>>Tigo Tanzania Wametangaza Nafasi Mpya ya Kazi

👉Wanataka;Commercial Execution Specialist 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  
 
==>>Vodacom Tanzania Wametangaza Nafasi Mpya ya Kazi

👉Wanataka; M-PESA Agents – MPESAN
👉Deadline; November 1,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Tangazo la Nafasi za Kazi Umoja wa Mataifa Katika Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)

👉Deadline ni; November 11, 2019
👉Kituo cha Kazi ni Kigoma,Tanzania

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

 ==>>Shirika la REPOA Limetangaza Nafasi Mpya za Kazi

👉Deadline ni; November 11, 2019
👉Wanawake Watapewa Kipaumbele zaidi

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Nafasi Mpya za kazi  Iringa katika shirika la Kimataifa FHI 360 Tanzania
👉Wanataka watu wa fani Mbalimbali
👉Deadline ni; November 23, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

==>>Nafasi Mpya za kazi  Zilizotangazwa na TANROADS - Mtwara.

👉Wanahitajika Watu wa fani Mbalimbali.
👉Elimu ni kuanzia kidato cha Nne
👉Deadline; 01 November 2019.

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>>
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

==>>Nafasi Mpya za  kazi Zilizotangazwa na Chuo Kikuu cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) - Mwanza.

👉Wanahitajika Watu wa Fani Mbalimbali
👉Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe; 01 November 2019.

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>>
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

==>>Nafasi 16  Za Kazi toka Mamlaka Ya Usafiri Wa Anga -TCAA

👉Wanahitajika Watu wa Fani Mbalimbali
👉Elimu: kuanzia ya Cerificate /Diploma
👉Deadline: November 06,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>>
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬


Share:

TIGO PESA MASTERCARD QR ZAWADI NJE NJE


Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, mapema leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha akionesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha(katikati), akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani)kulia kwake ni Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo- Mshana Mshana. 
Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha(katikati), akimuonyesha Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo- Mshana Mshana. 
Mkurungezi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na Mastercard mara baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, mapema leo Jijini Dar es salaam.

 Wateja wanaweza kujipatia fedha papo hapo baada ya kulipia kwa Tigo Pesa Matsercard QR.
Dar es Salaam. Oktoba 29, 2019.Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kushirikiana na Mastercard wamezindua kampeni kwaajili ya kuwazawadia wateja wanaofanya malipo kwa njia ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maduka na maeneo yanayoruhusu kulipa kwa Mastercard QR.
Kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wateja wanapata huduma rahisi na ya uhakika nchi nzima.
Akizungumza leo wakati wa hafla ya uzinduzi, Kaimu Mkuu wa huduma za fedha (MFS), Angelica Pesha alisema “Kama kampuni ya kidigitali siku zote tunalenga kuleta sulushisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi zaidi.Kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa njia mpya na salama ya malipo kwa wateja pale wanapotaka huduma na bidhaa kwenye maduka na maeneo mengine ya kibiashara yanayoruhusu mfumo wa Mastercard QR.”
Aliongeza, “Tigo Pesa Mastercard QR ni fursa ya kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwasababu Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha.Kwa kupitia Tigo Pesa Mastercard QR si tu tunapanua wigo wa utoaji wa huduma zenye usalama kwa wateja bali tunasogeza huduma zenye uharaka karibu na wateja wetu,” alisema Pesha.  
Mkurugenzi na Meneja wa  Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla alisema “Mastercard imejizatiti katika kutafuta njia mbadala ya kifedha kwa kuja na suluhisho linatoa nafasi kwa wateja kupata huduma za malipo zenye usalama na za uhakika.Shabaha hii ya kuleta mbadala wa fedha ni jambo la kujivunia hasa tunapoungana na Tigo.” 
Aliongeza “Kwa sasa biashara nyingi zinapokea malipo ya Mastercard QR ambapo wateja wanaweza kutumia njia hii ya kidigitali kujipatia zawadi ya fedha kwa malipo waliyofanya.”
Mteja wa Tigo anaweza kufanya malipo kwa njia ya Mastecard QR kupitia App ya Tigo Pesa kwa kuscani QR code au kwa kufuata hatua zifuatazo:
  1. Piga *150*01#, 
  2. Chagua namba 5, 
  3. Chagua 2, (Lipa kwa Mastercard QR). 
Baada ya malipo,mteja atapokea zawadi ya hadi asilimia 3 ya fedha kulingana na kiwango cha malipo aliyofanya.
Mastercard QR ni njia ya haraka na ya kidigitali yakufanya malipo ambayo kwa sasa inakubalika katika maeneo mbalimbali ya kibiashara kwa wateja wote wa Tigo Pesa.
Mteja anaweza kufurahia huduma ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maeneo maarufu kama vituo vya mafuta vya Puma, migahawa ya KFC, Pizza Hut na Samaki Samaki, Century Cinemax, Supermarket ya Shoppers, JD Phamacies pamoja na maduka ya GSM Mall.
Mwisho//
Share:

WANAFUNZI SHULE YA UGANGA WALIOKUMBWA NA MAPEPO WAMUUA MZEE WALIYEMTUHUMU KUWAROGA



Mzee Issa Pela anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka (70-80) enzi za uhai wake
Mzee Issa Pela anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka (70-80) aliyekuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa ushirikina wa kuwaangusha wanafunzi wa shule ya msingi Uganga iliyopo kata ya Luwumbu wilayani Makete mkoani Njombe ameuawa kwa kupigwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza na Mwandishi wetu Afisa mtendaji wa kijiji hicho Raphael Tweve amesema wanafunzi hao walianza kumkimbiza na kumpiga mzee huyo jana Oktoba 28, 2019, baada ya kuona hali hiyo aliwazuia lakini baadaye waliweza kumzunguka na kwenda kutekeleza kitendo hicho cha kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea umauti kwa mzee huyo.

“Mimi nikiwa ofisini nilisikia kelele nikatoka kwenda kuangalia kuna nini, kufika nawaona hao watoto akiwa na fimbo wanamtafuta mzee mwingine anayetuhumiwa kwa uchawi, na wakamweleza wameshampiga yule mzee waliyekatazwa wasimpige na alipokwenda eneo la tukio alimkuta mzee huyo amejeruhiwa kwa kipigo na baada ya muda mchache akafariki dunia” amesema Mtendaji huyo.

Amesema kwa sasa shughuli nyingi za maendeleo zimekwama kijijini hapo tangu Mei mwaka huu lilipoibuka suala la wanafunzi kudondoka ovyo shuleni hapo huku wakijaribu kutafuta muafaka bila mafanikio.

Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ambao majina yao tunayahifadhi wamesema kabla ya kutokea tukio hilo walimuona marehemu akionesha ishara za kishirikina kwenye nyumba za walimu shuleni hapo kwa kutumia kifimbo akiwa anachora ishara ya msalaba kwenye nyumba hizo huku akitoa maneno ya vitisho kuwa walimu hao watakufa.

Mmoja wa wanafunzi hao amesema kitendo hicho kiliwakasirisha na hata walipokuwa wakimuuliza alijibu kuwa hawamuwezi, huku wanafunzi wengine wakisema kuwa pia alichuma majani flani na akayaweka kwenye mfuko wa koti lake.

Wamesema walipoona hivyo ndipo walipolazimika kutafuta fimbo na kumfuata Mzee huyo kwa lengo la kumuadhibu ambapo alikiri kuhusika na vifo vya wananchi watatu kijijini hapo kwa njia za kishirikina.

“Sisi hatukuogopa kufa, kwani wamekufa wangapi, hata kama ni mchawi hatukuogopa kumpiga kwa kuogopa na sisi tungekufa”, amesema mwanafunzi mmoja.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Msigwa amezungumzia namna mazingira yalivyokuwa kwa wanafunzi wake, pamoja na kushangazwa na uamuzi wa wanafunzi hao na kwamba baada ya kutokea tukio hilo la mauaji bado wanafunzi wakaendelea kuanguka shuleni hapo huku wakitaja kuwa wanafunzi hao wamehusika na mauaji hayo kwa taswira tu lakini sio uhalisia.

“Wapo wanafunzi wamedondoka leo na wakawa wanataja mambo ya ajabu, wanasema wamemchukua mwenzao (huyo marehemu) kwenda kumuhifadhi tu na wamemchukua kupitia wanafunzi hao, sasa hatufahamu ukweli ni upi kwani walikuwa wakizungumza hayo wanafunzi hao waliodondoka na mapepo”, amesema Mwalimu Mkuu huyo.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Uganga Frank Gavana amethibitisha kutokea kifo hicho baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ambapo amesema majeraha ya sehemu za kichwa cha marehemu ni sababu kubwa iliyopelekea kifo chake.

Imeelezwa kuwa tangu mwezi wa tano mwaka huu kumekuwa na tabia ya kuanguka kwa wanafunzi katika shule ya msingi Uganga hali iliyopelekea watoto kushindwa kusoma kutokana na hali hiyo, pamoja na kuanguka watoto hao wamekuwa wakiwataja watu mbalimbali katika kijiji hicho kuwa ndiyo chanzo cha watoto kuanguka ambapo marehemu Mzee Issa Pila ni mmoja kati ya wanaotuhumiwa kufanya matukio hayo

Kwa upande wa serikali ya kijiji wakishirikiana na kata hiyo wameendesha vikao mbalimbali vya kutafutia ufumbuzi jambo hilo lakini hakuna mafanikio yoyote yaliyoweza kupatikana mpaka sasa.

Baadhi ya wanaotuhumiwa kutajwa na watoto hao pindi wanapodondoka wamekuwa wakiitwa kwenye vikao na kukiri kutafuta suluhu ya kumaliza tatizo hilo lakini hakuna mabadiliko mpaka sasa.

Jeshi la polisi wilaya ya Makete limefika eneo la tukio kwa hatua zaidi na kutoa elimu kwa wananchi hao na kuwataka kutochukua sheria mkononi huku pia wakiwaasa kuwa vitendo vya kishirikina kama hivyo vina madhara makubwa kwao kwa kuwa watumishi mbalimbali wanaopelekwa na serikali wataondoka kwa kuogopa ushirikina.

Juhudi za kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamisi Issa kuzungumzia tukio hilo zinaendelea baada ya Jana usiku kutafutwa bila mafanikio.
Share:

BABU ATOA DAWA YA KUKOMESHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME...VIBAMIA

Mzee James Makungu Sombi (85)

Vijana wameshauriwa kubadili mfumo wa maisha ili kukabiliana na changamoto ya kupungukiwa nguvu za kiume hali inayowaathiri kisaikolojia na kushindwa kutimiza majukumu yao ya kindoa. 

Ushauri huo umetolewa na Mzee James Makungu Sombi (85) ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utamaduni wakati akiongea na Malunde 1 blog leo Jumanne Oktoba 29,2019 nyumbani kwake Kisesa jijini Mwanza. 

Mzee Makungu amesema tatizo la vijana kupungukiwa nguvu za kiume limekuwa likiongezeka kila kukicha kutokana na vijana kupendelea kula vyakula vya kigeni ambavyo vingi vina kemikali zinazoathiri miili yao. 

“Tatizo kubwa ni lishe,tunakula kemikali nyingi sana,hizi bia,soda,mboga tunazokula mfano kabeji,mchicha,chinese,nyanya,nyanya chungu na vingine vyote vinapulizia dawa,unakuta ng’ombe,kuku wanachomwa sindano za dawa siku mbili tatu wanakua kisha mnakula. Sasa kama kila kitu kina kemikali,kina sumu utapataje nguvu za kiume?”,alihoji Mzee Sombi. 

“Jitahidini kula vyakula vya asili,muangalie vyakula ambavyo havijapuliziwa dawa,tumieni uji wa ulezi,mtama na kuleni kwa wingi karanga mbichi ni nzuri kwa afya,zilizokaangwa siyo nzuri sana”,alishauri Mzee Sombi. 

Katika hatua nyingine Mzee huyo alishauri wazazi kuachana na tabia ya kuwavalisha watoto nguo za kubana kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu maumbile ya watoto wao. 

“Nguo zinazobana pia zinachangia kukosa nguvu za kiume,misuli kuregea na kufanya maumbo kuwa madogo,nashauri pia vijana waache tabia ya kujichua ‘kupiga punyeto’ kwani inachangia kuregeza misuli yao matokeo yake wanakosa nguvu za kiume na kutengeneza vibamia bila kujua”,aliongeza Mzee Sombi. 

Mzee James Makungu Sombi ambaye ni mkazi wa Kisesa Mwanza Manju Mstaafu wa ngoma za Kisukuma na ni miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora yaliyopo Kisesa jijini Mwanza.

Mzee Sombi ni Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma,Wasiliana naye kwa namba 0755903972
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger