Friday 28 June 2019

Iran Yakutana Na Mataifa Yenye Nguvu Duniani Kuokoa Makubaliano Ya Nyuklia

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka mataifa matano yaliyo na nguvu duniani wanakutana na wenzao wa Iran mjini Vienna Austria, katika juhudi za kuishawishi Tehran kutoachana na makubaliano ya pamoja ya nyukilia. 

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqhchi amewaeleza waandishi wa habari mjini Vienna kuwa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa wanapaswa kuwasilisha mipango thabiti ili kupunguza athari za vikwazo vya Marekani. 

Mataifa hayo ya Ulaya yanatarajia hii leo kuwasilisha mpango wa biashara baina yake na Iran unaojulikana kama Instex, ili kuepuka vikwazo vya Marekani. 

Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa mpango huo huenda usifufue mauzo ya mafuta ya Iran kwasababu makampuni na wafanyabiashara wana hofu kuwa mkataba wowote na Iran utawafanya walengwe na Marekani katika hatua zake. 

Marekani ilijiondoa katika makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa mwaka 2015 na kuiweka vikwazo vipya Iran vinavyolenga sekta ya mafuta ya taifa hilo la Kiislamu.


Share:

Fahamu Chanzo Halisi cha Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Unafahamu kwa kina tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na  maumbile ya kiume kusinyaa?

Wanaume wengi kwa sasa wanasumbuliwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile  kuwa mafupi na wengi wao huamua kutafuta tiba ili waweze kujilejeshea nguvu zao za asili bila kujua ni nini chazo cha hilo tatizo 

Tambua kuwa hakuna dawa ya kuongeza maumbile ya kiume  kama  ulikuwa mdogo  tangu unazaliwa, labda kama tatizo limeazia ukubwani kwa kujichua ( kupiga punyeto)  au kutokana na magonjwa 

Pia hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume kama tatizo umezaliwa nalo bali zipo tiba za kutibu na ukapona matatizo hayo kama yameanzia  ukubwani kutokana na sababu zifatazo ;
1,Unene kupita kiasi 
2.Kuvaa nguo za kubana 
3.Magonjwa ya moyo,kisukar,presha,vidonda vya tumbo,ngiri,tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kupiga punyeto,Msongo wa mawazo.

Haya ndo mambo makuu yanayosababisha tatizo hilo. kwa ushauri zaidi , piga simu 0683645920


Share:

Rais Magufuli akutana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la SADC, Ikulu Jijini Dar es Salaam




Share:

ATCL yazindua safari za Tanzania kwenda Afrika Kusini

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), leo limeanza rasmi safari yake ya kwanza kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kwa kutumia ndege aina ya Airbus. 

Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhandisi Ladslaus Matindi amesema kwa wiki kutakuwa na safari nne. 

Ndege hiyo  aina ya Airbus 220-300 imeondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam Tanzania (JNIA)  saa 4:30 asubuhi ikitarajia kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa OR Tambo, Afrika Kusini saa 6:45 mchana.


Share:

AOLEWA NA BABA YAKE ILI KUMKOMESHA DADA YAKE


HASSAN DAUDI NA MITANDAO

UKIAMBIWA duniani kuna mambo, basi kubaliana na hilo. Kuna mengi ya kustaajabisha ila huenda usiamini utakaposikia kwa kuwa tu hujawahi kuyashuhudia kwa macho.

Katika hayo, leo hii makala haya yanakukutanisha na familia ya Travis Fieldgrove, mkazi wa Jimbo la Nebraska nchini Marekani.

Fieldgrove mwenye umri wa miaka 39, alimuoa msichana aitwaye Samantha Kershner (21), ambaye katika kile kinachoweza kukushangaza, ni binti yake kabisa.

Hapo unaweza kujiuliza, ilikuwaje jamaa akaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kisha kufunga ndoa kabisa na mtoto yake huyo? Hii hapa simulizi yao.

Inasemekana kuwa chanzo cha Fieldgrove na Samantha kuwa wapenzi ni binti mwingine wa mwanamume huyo.

Eti watoto hao wa kike walianza kama utani na kisha kujikuta katika upinzani mkali, kila mmoja akitamba kuwa angekuwa wa kwanza kupumzika faragha na baba yao huyo.

Huku Fieldgrove akiwa hajui kinachoendelea, aliingia mtegoni, asijue mabinti zake walikuwa kwenye vita kali ya kulinasa penzi lake.

Bahati kwake, mitego ya Samantha ndiyo iliyomnasa mzee wao huyo na rasmi uhusiano wa kimapenzi ulianza Septemba, mwaka jana.

Hawakutaka kuchelewa, mwezi mmoja baadaye, wawili hao waliamua kuingia kwenye ndoa ili waweze kulifaidi penzi lao vizuri.

Hata hivyo, Fieldgrove na Samantha walikutana na mkono wa sheria Januari, mwaka huu, wakishutumiwa kwa uamuzi wao huo wa kuingia katika uhusiano wakati wakifahamu fika kuwa ni baba na mtoto.
Fieldgrove akiwa na mabinti zake

“Kesi hii inawahusisha watu wawili walioingia katika uhusiano wa kimapenzi, wakijua wazi kuwa ni ndugu wa damu. Kabla ya hapo, walikuwa wakifahamiana kabisa kuwa ni baba na mtoto.

“Fieldgrove hakutajwa katika cheti cha kuzaliwa cha Kershner na kule walikokwenda kufunga ndoa huwa hawapimi damu kabla ya kutoa leseni ya ndoa,” inasomeka taarifa ya polisi baada ya uchunguzi wake.

Sheria ya Marekani inaitaja ndoa ya aina hiyo kuwa ni laana, hivyo ilikuwa ni lazima wahusika wakumbane na adhabu kali kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wengine.

“… inaonekana kwamba waliamua kufunga ndoa haraka iwezekanavyo baada ya kugundua kuwa kulikuwa na uchunguzi dhidi yao,” inaongeza taarifa hiyo.

Mbele ya maofisa wa polisi, msichana huyo hakuficha, alikiri wazi kuwa ni kweli huyo ni mzee wake na alifanya hivyo ili kumshikisha adabu dada yake, ambaye pia alikuwa akimtaka.

Samantha anasema alimjua baba yake akiwa na umri wa miaka 17 kwa kuwa kwa muda mrefu alikuwa akiishi na mama yake.

Kwa utetezi wake huo, bibiye huyo aliepuka kutupwa gerezani na badala yake alikumbana na kifungo cha nje atakachokitumikia kwa kipindi cha miezi tisa. Kesi yake itasikilizwa Julai 16, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, mambo yalikuwa mabaya kwa baba yake wakati wa usikilizaji wa kesi yao mwezi uliopita, kwani kwa kosa lake la kudanganya katika kiapo cha ndoa, akijua wazi kuwa yeye ni baba mzazi wa msichana huyo, alihukumiwa kwenda jela miaka miwili.

Licha ya kujitetea, akisema haamini kwamba msichana huyo ni mtoto wake, vipimo vya DNA ndivyo vilivyomuumbua baada ya kuonesha kuwa wana uhusiano huo wa damu kwa asilimia zaidi ya 99.

“Siamini kuwa mimi ni baba wa Samantha kwa sababu hakuna jina langu katika cheti chake cha kuzaliwa,” anasema Fieldgrove katika mahojiano yake na polisi.

Nayo taarifa ya chombo cha dola hicho ilikinzana naye, ikisomeka: “Samantha ni binti wa Fieldgrove kwa asilimia 99.999.”
Fieldgrove na Samantha

Lakini sasa, wakati Fieldgrove akisikiliza kesi yake mahakamani, mwanasheria wake, Jeff Loeffler, alisema mteja wake alijisikia vibaya na alitamani jambo hilo lisingetokea.

“Pia ana jeraha ndani ya ubongo. Huwa hafanyi kazi nyingi,” anasema mwanasheria Loeffler na kuutupia lawama uamuzi wa mahakama kumwacha nje bibiye Samantha.

Loeffler anaamini wote, kwa maana ya Fieldgrove na Samantha, ni watu wazima. Hivyo, kilichotokea ni makubaliano ya pande mbili na si kama ilivyo sasa ambapo binti huyo anaonekana kutokuwa na makosa.

Fieldgrove hatakiwi kuwasiliana na binti yake huyo kwa sasa na baada ya mwaka mmoja gerezani, ataimalizia miezi mingine 12 akiwa uraiani, japo atakuwa chini ya uangalizi mkali.
Chanzo - Mtanzania
Share:

Bunge Lapitisha Muswada Wa Sheria Ya Marekebisho Ya Sheria Na.3 Mwaka 2019

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge Limepitisha Muswada Wa Sheria Ya Marekebisho Ya Sheria Mbalimbali Namba 3 Wa Mwaka 2019 Unaofanyia Marekebisho Sheria 8 Ambazo Ni Sheria Za Makampuni, Hakimiliki, Filamu Na Michezo Ya Kuigiza, Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali, Takwimu, Vyama Vya Kijamii, Uwakala Wa Meli Na Miunganisho Ya Wadhamini.

Akisoma mapendekezo hayo bungeni mwanasheria mkuu wa serikali Prof. Adelardus Kilangi amesema  Madhumuni ya marekebisho ya  kila sheria ni kuondoa migongano   kwa sheria ya makampuni juu ya msajili na msimamizi wa asasi,kuweka namna bora ya usimamizi,kuweka mipaka ya usimamizi ,usimamizi wa asasi pamoja na kuongeza kiwango cha adhabu na kuongeza mapato katika sekta ya Filamu.
 
Mkatika sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali imeweka wigo wa mashirika yatakayoruhusiwa kusajiliwa kama NGO’s kuwa ni yale yanayolenga kunufaisha jamii na sio wanachama wake.

Katika hatua  nyingine,Prof. Kilangi amesema katika sheria ya takwimu muswada huo unapendekeza kuanzisha kamati ya kitaalam itakayokuwa na jukumu la kupokea na kujadili malalamiko yanayotokana na wadau kuhusu usahihi wa takwimu zilizotolewa kwa umma.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge katiba na sheria Najma Giga  akiwasilisha maoni ya kamati hiyo amesema  Wakati umefika sheria zinazoratibu na kusimamia sekta ya sanaa zioanishwe na masharti ya sheria na ulinzi kwa maendeleo ya wadau husika wa sanaa na Taifa kwa Ujumla.

Aidha, kamati inapendekeza msajili kutoa onyo kwa notisi ya muda wa siku 30 itakayoitaka taasisi husika kurekebisha kasoro au makosa iliyoyafanya kabla ya kuchukua hatua ya kusimamisha shughuli zake.

Katika Mapendekezo ya kamati ilibaini ibara  19 zenye Dosari mbalimbali za kimaandishi  ambazo zinahitaji marekebisho na  zimekubaliwa na serikali katika marekebisho .
 
Ibarahizo ni Ibara ya 4,Ibara 6,Ibara ya 10,Ibara ya 16,ibara ya 17,Ibara ya 18,ibara ya 20,ibara ya 25 ,ibara ya 27,ibara ya 35,ibara ya 36,ibara ya 42,ibara ya 47,ibara ya 50,ibara ya  50,ibara ya 52,ibara ya 55,ibara ya 61,ibara  ya 62 na Ibara ya 73.

Mapendekezo mengine ya Kamati ya bunge,katiba na sheria ni kuwepo kwa maboresho kwa sheria mahususi kwa Tasnia ya Filamu  ,Sanaa,Ubunifu na utalii nchini kwani  wasanii  wengi wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kutokuwepo kwa sheria madhubuti hivyo serikali ni  vyema kukamilisha mchakato wa sheria  .


Share:

Wimbo Mpya: Jux Ft. Vanessa Mdee - Sumaku

Wimbo Mpya: Jux Ft. Vanessa Mdee - Sumaku


Share:

Benki ya Azania yazindua Kampeni Ya ‘AMSHA NDOTO’ kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania  Charles Itembe Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Amsha Ndoto ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.Kulia kwake ni Mkurungezi wa Biashara wa Benki ya Azania Rhimo Nyansaho na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo mapema leo Jijini Dar es salaam.

 ***
Benki ya Azania (ABL)  imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS 1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3 watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti, ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni Tatu

Akiongelea kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000 watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho itakayowapata washindi.

 “Tunawahamasisha watanzania wote, wateja wetu wa sasa na wapya,wazazi na walezi kufungua akaunti hizi ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuongeza mitaji, kulipia kodi za pango na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye”, alisema Itembe, akigusia pia kuwa akaunti hizi zitakuwa fursa ya kuwahimiza kuweka akiba kwa ajili ya .

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule’, itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.

Masharti na vigezo kuzingatiwa


Share:

Jeshi la Wananchi (JWTZ) Latoa Onyo Kali....Latangaza Msako Mkali

Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetangaza kuwachukulia hatua viongozi wa ndani na nje ya jeshi hilo na vijana waliohusika katika vitendo vya udanganyifu katika uandikishaji wa majina ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Udanganyifu huo ulihusisha ukiukaji wa taratibu na kughushi nyaraka na vyeti vilivyotumika katika uandikishaji huo.

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, alisema licha ya taratibu za uombaji kuwa wazi, baadhi ya viongozi wamebainika kutumia nafasi walizonazo kupenyeza majina ya ndugu, jamaa na rafiki ili wasajiliwe.

“Napenda kuwataarifu kuwa baada ya kubaini kuwako kwa udanganyifu huu, JWTZ/ JKT tutafanya uhakiki wa vyeti na nyaraka zote husika kwa vijana walioandikishwa tutashirikiana na ofisi ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa), Baraza la Taifa la Mitihani, Takukuru na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuwabaini waliofanya udanganyifu,” alisema Kanali Ilonda.

Ilonda bila kutaja uhakiki huo utafanyika lini na wakati gani, alisema utahusisha kuhakiki wa vyeti, nyaraka mbalimbali zilizokuwa zikihitajika kwenye uandikishaji huo pamoja na vyeti vya kuzaliwa na vipimo vya afya.

"Kwa kuweka usawa tutafanya uhakiki huu kwa kushirikiana na JKT, Nida, Wizara ya Elimu, taasisi zinazohusika na masuala ya rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama, ili tuweze kuwachuja, tunataka kujiridhisha je, ni Watanzania kweli, wana afya njema, wana akili timamu, ametoka eneo husika na ana sifa stahiki, wale wenye sifa watachukuliwa, hata kama idadi yao itakuwa ndogo tofauti na matarajio yetu," alisema.

Ilonda alisema wale ambao watabainika kughushi watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

“Hakuna atakayesalimika labda wahame nchi, aliyeghushi vyeti na nyaraka mbalimbali kiwe cha kuzaliwa au daktari aliyetoa majibu ya uongo atakamatwa, waliowashawishi kughushi watakamatwa, waliotengeneza vyeti bandia, waliohusika kuwaandikisha vijana hao bila kuwa na vigezo, viongozi wote waliohusika kupenyeza majina wa ndani na nje ya jeshi nao watachukuliwa hatua kupitia mamlaka zao husika,” alisema.

Alisema hatua zitakazochukuliwa hazitaangalia wadhifa au cheo cha mtu kwa sababu lengo ni kusafisha nchi iwe na viongozi waadilifu na wanaofuata sheria na taratibu.


Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA


Manchester United inafikiria kumnunua beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 23, anasalia kuwa mchezaji anayelengwa sana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich msimu huu licha ya mpango huo kusita hapo awali. (Sky Sports)

Mkufunzi wa klabu ya Sporting Marcel Keizer anaamini kwamba nafasi ya kumzuia kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandez katika klabu hiyo ni ndogo, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zimevutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Record, via Manchester Evening News)
Mkufunzi wa Celtic Neil Lennon ameambia Arsenal watahitajika kulipa zaidi iwapo watamsajili beki wa kushoto wa Uskochi Kieran Tierney, 22. (Telegraph)

Arsenal inamlenga mshambuliaji wa Monaco Keita Balde, 24, baada ya inter Milan kujiondoa katika harakati za kumsajili mchezaji huyo wa Senegal . (Le 10 Sport, via Metro)

Beki wa Borussia Dortmund na Ufaransa,20 Dan-Axel Zagadou, anataka kuondoka katika klabu hiyo na ananyatiwa na Arsenal. (Bild, via Mirror)

Babake mshambuliaji wa Juventus Moise Kean, 19, ametangaza kwamba raia huyo wa Itali anataka kuhamia Inter Milan". (Mirror)

Atletico Madrid inafikiria kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombian James Rodriguez, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ahitajiki tena Real . (Cadena SER, via AS)

Tottenham iko tayari kumnunua mchezaji anayelengwa na Arsenal William Saliba, huku klabu ya St-Etienne ikisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ana thamani ya £20m. (RMC, via Star)

Bayern Munich ilijaribu kuteka uhamisho wa beki wa klabu ya PEC Zwolle Sepp van den Berg kuelekea Liverpool wakati ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 kutoka Uholanzi alikuwa akifanyiwa ukaguzi wa matibabu. (Times)

Naibu mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola ataondoka Chelsea wikendi hii wakati ambapo kandarasi yake itakuwa inakamilika baada ya kukataa ofa ya kuwa balozi wa klabu hiyo. (Guardian)

Manchester United itafanya uamuzi wa iwapo itamsaini beki wa katikati kufikia mwisho wa wiki hii.. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, anayelengwa na Manchester United, anaonekana kukaribia kuondoka katika klabu ya PSG baada mamake kufichua kwamba hakuna klabu iliowasilisha ofa yoyote kwa mwanawe(Daily Mail)

Mchezaji wa Real Madrid na Norway Martin Odegaard, 20, anatarajiwa kuondoka kwa mkopo kwa kipindi cha misimu mingine miwili (AS)

Kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 21, anatarajiwa kuripoti kwa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu kama kawaida wiki ijayo licha ya kulengwa na Man United. (Chronicle)

Beki wa Arsenal na Poland Krystian Bielik anataka kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu . (Sun)

Mshambuliaji wa Ujerumani Bassala Sambou, 21, amekataa kandarasi mpya na klabu ya Everton na anatarajiwa kuhamia Ujerumani ama Eredivisie. (Liverpool Echo)

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

Korea Kaskazini Yaitaka Korea Kusini kuacha kuwa mpatanishi katika mazungumzo yao na Marekani

Korea Kaskazini imeitaka Korea Kusini kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mazungumzo yake na Marekani. 

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae In mjini Seoul Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka Japan. 

Moon amesema Korea Kaskazini na Marekani wanatafakari kuandaa mkutano wa kilele kwa mara ya tatu. 

Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim huko Hanoi mwezi Februari uliishia bila makubaliano kuhusiana na Korea Kaskazini kuharibu silaha zake za nyuklia ili ipunguziwe vikwazo. 

Lakini sasa mkurugenzi mkuu katika idara inayohusika na masuala kuhusu Marekani katika Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini Kwon Jong Gun amesema uongozi wa Korea Kusini ni bora ukashughulika na mambo yake ya ndani.


Share:

Habari Zilizopo katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 28 June




















Share:

Thursday 27 June 2019

Picha : VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP ,MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR

Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga wanaoshiriki Kambi ya Ariel 2019 leo Juni 27,2019 wametembelea Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na Kampuni ya IPP Media ambavyo ni ITV,Radio One, Capital Radio,Capital Tv,East Africa Tv ili kujifunza namna wanavyoendesha vipindi na kurusha matangazo.

Vijana na watoto hao pia wametembelea Makumbusho ya taifa ili kujifunza historia ya mwanadamu na nchi ya Tanzania hali kadhalika wametembelea kiwanda cha kutengeneza juisi kinachomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa ili kujionea namna uzalishaji unavyofanyika.

Ziara hiyo inakuja baada ya watoto hao wanaoshiriki kambi ya Ariel 2019 ya wiki moja iliyoanza Juni 23,2019 jijini Dar es salaam, kujifunza darasani masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia,ujasiriamali na kujengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao.

Kambi ya Ariel 'Ariel Camp' inasimamiwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ambayo inafanya shughuli zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara.

ANGALIA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA VIJANA NA WATOTO 

Kulia ni Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio ,Deogratius Rweyunga akiwaelezea vijana na watoto kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara wanaoshiri Ariel Camp 2019 namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio,Deogratius Rweyunga akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Wa pili kulia ni  Naibu Mkurugenzi wa Radio One Stereo Bahati Alex akifuatiwa na Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary.
Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary akiendelea na kipindi wakati vijana na watoto wa Ariel Camp 2019 walipotembelea studio ya Radio One.
Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akielezea 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo ' lengo la ziara ya vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019.
Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akizungumza 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. Kabigi alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kukaa na watoto na kuwaeleza kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'.
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'.
Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Capital Radio, Abdallah Mwaipaya akitoa ufafanuzi namna wanavyoendesha vipindi vya radio.
Hapa ni Control Room ITV: Kulia Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyoandaa vipindi vya Televisheni.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyofanya mawasiliano wakati wa kuandaa vipindi vya Televisheni.
Ndani ya chumba cha kurushia matangazo ITV na East Africa Tv: Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyorusha vipindi vya Televisheni.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akielezea namna wanavyofanya vipindi vya mahojiano ya vipindi mbalimbali.
Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akionesha namna kamera za studio zinavyofanya kazi.
Hapa ni chumba cha kusomea taarifa ya habari ITV: Kulia ni Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaonesha vijana na watoto  namna wanavyoendesha vipindi vya habari.
 Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaelezea vijana na watoto  namna wanavyoendesha vipindi vya habari.
Vijana na watoto wakipiga picha na Mtangazaji wa Kipindi cha Habari za saa, Richard Stephen.
Mtangazaji wa ITV ,Isaack Mpayo akielezea namna wanavyoendesha kipindi cha habari za saa.
Washiriki wa Ariel Camp 2019 wakiwasili katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya historia ya mwanadamu na historia ya nchi ya Tanzania.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940. Alisema katika Makumbusho hayo kuna maeneo matano ya kujifunza ambayo ni Chimbuko la Mwanadamu,jumba la maonesho ya kihistoria,jumba la michoro ya mapangoni na miamba,jumba la sanaa za kisasa,jumba la kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani na Jumba la Baiolojia.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940.
Kushoto aliyenyoosha mkono ni Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana akionesha gari (la kijani) la kwanza kutumiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana akionesha moja ya nyumba za kihistoria.
Vijana na watoto wakipiga picha ya pamoja nje ya jumba la makumbusho lililojengwa mwaka 1940 na Waingereza.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana simba aliyekaushwa.
Vijana na watoto wakiwa katika jumba la makumbusho ya kihistoria.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro mbalimbali katika jumba la sanaa za kisasa.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro iliyochorwa mapangoni.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha vinyago.
Vijana na watoto wakiendelea kutembelea jumba la sanaa za kisasa.
Vijana na watoto wakifurahia kinyago cha mwanamke anayetwanga vitu huku kabeba mtoto na kashikilia mtoto.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha vitu mbalimbali vya asili.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha nyayo za binadamu wa kale.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha picha ya binadamu aliyejitambua.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Happiness Lema akitoa ufafanuzi kwa vijana na watoto kuhusu nyumba za historia.
Watoto wakisoma vitabu na kuangalia katuni kwenye vifaa vya kisasa katika Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa.
Watoto wakisoma vitabu kwenye Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa.
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa.
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa.
Kijana akikata nyama kwa kutumia jiwe.
Zoezi la kufuma mkeka likiendelea.
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi akipiga picha ya kumbukumbu na washiriki wa Ariel Camp 2019 baada ya kutembelea Makumbusho ya taifa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger