Thursday 30 May 2019

Serikali yakanusha kuwalazimisha wafanyakazi wake kuwa na laini ya TTCL

Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema hakuna agizo la Serikali linalolazimisha mfanyakazi wa Serikali kuwa na laini ya TTCL isipokuwa viongozi wanaowekewa vocha za Serikali kwamba ni muhimu kuwa na laini hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo amesema taarifa inayosambaa kwenye mitandao kuhusu hilo ni ya upotoshaji na kuwataka wananchi kuipuuza.


Share:

Rais Magufuli arejea nchini akitokea Zimbabwe

Rais John Magufuli amerejea nchini kutoka Zimbabwe ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen.  Venance Mabeyo.

Rais  Magufuli kwa takribani wiki moja sasa amekuwa ziarani katika nchi kadhaa za Afrika, ziara hizi za wanachama wa SADC zilikuwa muhimu kwa sababu ya uhusiano wa kipekee na kihistoria wa Tanzania na nchi hizo 


Share:

ATCL yamvuruga Nape, ahoji kucheleweshwa kwa ndege

ATCL yamvuruga Nape, ahoji kucheleweshwa kwa ndege


Share:

ACHAPWA VIBOKO 40 KISA KULA EMBE OVYO OVYO HADHARANI MWEZI WA RAMADHAN

 Ibrahim Ismail, jamaa mwenye umri wa miaka 20 amepatikana na hatia ya kula embe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kupokea mijeledi 40 kwa kosa hilo.

 Ismail ambaye alituhumiwa kula wakati Waislamu wengine wakifunga, amepatikana na hatia hiyo na mahakama inayoongozwa na sheria za Shariah katika eneo la Ringim, mjini Jigawa, nchini Nigeria. 

Ibrahim Ismail alipokea mijeledi 40 kwa kula embe wakati wa mfungo wa Ramadhan   katika soko la Ringim baada ya afisa wa mahakama kumsomea mashtaka

Jaji Safiyanu Ya’u, alitoa amri kwamba jamaa huyo acharazwe mijeledi 40 hadharani ili iwe funzo kwake na kwa wengine ambao walikaidi sheria za mwezi mtukufu. 

Kushiriki mlo kwa wakati usiofaa inakinzana na sheria za kifungu cha 370 za mji wa Jigawa, Nigeria. 

 Awali, Nabahani Usman ambaye ni kamanda wa polisi wa Kano Hisbah, alionya kwamba yeyote atakayepatikana akila ovyo ovyo hadharani atachukuliwa hatua kali kwa kukaidi sheria za mfungo wa Ramadhan. 

Aliongeza kuwa, wale watakaonaswa wataachiliwa huru iwapo watatoa ushahidi wa ripoti ya daktari kwamba walikuwa wanaruhusiwa kula kwa sababu za kiafya. 
Chanzo - Tuko
Share:

Video Mpya: Rich Mavoko - Usizuge

Video Mpya: Rich Mavoko - Usizuge


Share:

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUJIKATA UUME KWA WEMBE

Jamaa kutoka kijiji cha Bula, kaunti ya Isiolo  nchini Kenya aliripotiwa Jumatano kujikata uume wake, akitumia wembe baada ya kuzidiwa na dawa za kulevya. 

Kwa mujibu wa ripoti ya eDaily, mamake jamaa huyo alifichua kwamba kisa hicho kilitokea wakati mwanawe huyo wa miaka 27, Abshiro Abdi, alikuwa akizikata kucha zake. 

 Kwa sasa, abdi anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Isiolo. 

Msimamizi wa hospitali hiyo Daktari Hussain Abdi Mohamud adokeza kwamba, mwathiriwa alikuwa amepoteza fahamu alipowasilishwa katika kituo hicho cha afya na kuwa alikuwa ametumia dawa za kulevya kupita kiasi.

 "Alivuja damu nyingi...lakini atakapopata nafuu bado atakuwa na uwezo wa kujisaidia kama kawaida. Nguvu zake za kiume hazitaathirika lakini iwapo kutakuwepo na uwezekano basi madaktari wa upasuaji watamshughulikia kwa njia nyingine ile," Daktari Mahamud alisema. 

Wakati uo huo, alitoa wito kwa vijana kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya akisema kuwa wanahatarisha maisha yao. 

"Vijana wanapaswa kujiepusha na dawa za kulevya za aina yoyote ile, la si hivyo, watazidi kuhatarisha maisha yao, afya yao na mawazo yao pia yataathirika," aliongeza.

Chanzo - Tuko
Share:

MKE,HAWARA MTOTO WAUA MUME MOROGORO

Boniface Agustino (46) mkazi wa Chamwino Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kuuawa na mke, mpenzi wake na mtoto wake kwa kupigwa kwa kitu kizito kichwani kwa kile kinachodaiwa kuwa wivu wa kimapenzi.


Majirani walioshuhudia tukio hilo, akiwamo Mariam Mohamed, walidai kuwa juzi majira ya saa 8:00 mchana, walisikia vishindo na kelele kutoka kwa mwanamume huyo akiomba msaada na kudai kuwa mke wake anataka kumuua huku wakiwa chumbani kwao.

Mohamed alisema, awali mwanaume huyo alikuwa na ugomvi na mke wake, jambo ambalo lilisababisha ndugu kulisuluhisha, lakini wanashangazwa kuona mwanamke huyo akishirikiana na mtoto wake, wamefikia hatua ya kufanya mauaji hayo.

Alidai kuwa mwanamke huyo, Neema Godfrey, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume aliyefahamika kwa jina moja la Salum ambaye alikuwa mpangaji wake katika nyumba waliyokuwa wakiishi na mume wake, huku pia mwanamume huyo akiwa na uhusiano wa kimapenzi na binti yake, Alphonsina Boniface.

Pia Nipashe ilizungumza na ndugu wa marehemu, Revina Makundi, ambaye alisema kaka yake huyo na mkewe walikuwa na ugomvi kila mara ambao yeye alikuwa akiusuluhisha kuhusu Boniface kumbaka binti yake wakati akiwa mdogo kwa imani za kishirikina.

Aidha, Makundi alisema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kimapenzi baada ya mpangaji wao kutembea na Godfrey na binti yake, hatua iliyosababisha mpangaji huyo kufukuzwa, lakini baadaye alirudi.

Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Bright Sospeter, alisema majira ya 10:00 jioni alisikia watu wakieleza tukio hilo huku wakiwa na hisia za kutokea mauaji ndipo walijumuika na viongozi wengine.

Alisema walipofika eneo la tukio walimhoji mwanamke ambaye ni mke wa marehemu na kusema mumewe alirukwa na akili mchana na ndiyo maana alisema anauawa na muda huo wakati anaulizwa hakuwapo.

Sospeter alisema walipoingia ndani, walimkuta na kumkuta binti na kumuuliza ndipo akasema baba yake alienda kwa Ustaadhi kuombewa, hivyo hayupo jambo lililowafanya walazimike kupekua nyumba nzima na ndipo walipokuta akiwa tayari amefariki dunia akiwa chooni, huku pembeni yake kukiwa na mchi na damu sakafuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema wanawashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi.

Aliwataja watu hao kuwa ni Neema Godfrey (41) mkazi wa Chamwino, Alponcina Boniface (19) na mtu mwingine ambaye hakumtaja kwa sababu za kiuchunguzi.

Mutafungwa alisema inadaiwa kuwa mpangaji aliyekuwa amehamishwa alihusika baada ya kuingia ndani akiwa amevaa vazi aina ya dela hadi usoni na baadaye kutoroka. Aliwataka wananchi wa mkoa wa Morogoro hususan wakazi wa Chamwino, kushirikiana na polisi kufanikisha mtuhumiwa mwingine wa mauaji kupatikana.
Share:

BABA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MTOTO WAKE

Said Rashid (36), mkazi wa Mbezi Juu jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kumbaka mwanaye mwenye umri wa miaka 13.

Akisoma hati ya mashtaka jana Jumatano Mei 29, 2019 mbele ya hakimu, Anifa Mwingira, wakili wa Serikali, Matarasa Hamisi amedai kati ya mwaka 2016 na 2019 mshtakiwa alimbaka mtoto wake huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Matarasa amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakati mshtakiwa huyo akikana kufanya kitendo hicho Hakimu Mwingira alieleza kuwa dhamana ipo wazi, akimtaka kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaosaini bondi ya Sh1 milioni kila mmoja.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa rumande hadi Juni 10, 2019.

Na  Pamela Chilongola, Mwananchi 
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 30,2019


Share:

Wednesday 29 May 2019

RAIS MAGUFULI ATAKA JUMUIYA ZA KIMATAIFA KUONDOA VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwa hatua madhubuti za kufanya mageuzi ya kiuchumi katika nchi hiyo na ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe.


Rais Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Mnangagwa kwa heshima yake na kufanyika Ikulu Jijini Harare.

Rais Magufuli amesema katika kipindi kifupi cha tangu Rais Mnangagwa aingie madarakani hali ya uchumi imeanza kuimarika ambapo kwa sasa uchumi wa Zimbabwe unakua kwa wastani wa asilimia 3.5, mwaka ujao unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 4.2 na mwaka unaofuata kuongeza hadi wastani wa asilimi 4.4.

Kufuatia hali hiyo ameisihi Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe kwa kuwa vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Zimbabwe wakiwemo watoto na wanawake.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli kwa mara nyingine amewapa pole Rais na wananchi wote wa Zimbabwe kwa kupoteza watu takribani 400 waliofariki dunia katika mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai kilichoikumba Zimbabwe Machi 2019. Amesema Watanzania wanaungana na ndugu zao Wazimbabwe katika majonzi ya kuondokewa na jamaa zao na wanawaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi, Amina.

Kuhusu uhusiano wa Tanzania na Zimbabwe ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mzee Robert Mugabe, Rais Magufuli amesema Tanzania inatambua na inathamini uhusiano huu wa kihistoria na kidugu na amebainisha kuwa jukumu lililopo sasa ni kuelekeza nguvu nyingi zaidi katika uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi utakaoziwezesha Tanzania na Zimbabwe kuongeza biashara na uwekezaji.

Rais Magufuli amebainisha kuwa katika mazungumzo yake ya faragha na Rais Mnangagwa leo mchana wamekubaliana kusimamia ipasavyo makubaliano yaliyopo katika Kamati ya Pamoja ya Kudumu (Joint Permanent Commission – JPC) kwa manufaa ya nchi zote mbili.

“Rais Mnangagwa ujio wangu hapa Zimbabwe ni kuthibitisha kuwa urafiki wetu bado upo imara na sisi Tanzania tumejipanga kuuimarisha zaidi, tunataka tufanye biashara zaidi na nyinyi ndugu zetu wa Zimbabwe ili tukuze uchumi wa nchi zetu na kuongeza kipato cha wananchi wetu” amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Rais Mnangagwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake, na amemthibitishia kuwa yeye na wananchi wa Zimbabwe wanatambua kuwa Watanzania ni ndugu zao waliojitolea kwa dhati katika ukombozi wao wakiongozwa na dhamira ya dhati ya Hayati Mwl. Nyerere.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwa kiongozi wa kwanza katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa msaada wa chakula, dawa na vifaa vya kujihifadhi wakati Zimbabwe alipokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Idai mwezi Machi 2019.

Rais Mnangagwa amesema msaada huo uliwagusa Wazimbabwe wengi na kuwakumbusha umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesisitiza kuwa daima Zimbabwe itabaki kuwa rafiki na ndugu wa kweli wa Tanzania na hivyo amemhakikishia Rais Magufuli kuwa nchi hiyo ipo tayari kukuza zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa kuongeza biashara na uwekezaji pamoja na kushirikiana katika usafiri wa anga.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kumpa mbinu mbalimbali za kiuongozi ikiwemo kuondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo mkubwa kwa Serikali na ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya chama chake ZANU-PF na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Share:

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB): STAND UNITED IMESHUKA DARAJA...KAGERA SUGAR IMEBAKI

Utata uliojitokeza wa timu ipi itaungana na African Lyon kushuka daraja baada ya msimu kumalizika, umehitimishwa rasmi leo baada ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kutangaza rasmi kuwa Stand United ya Shinyanga imetereka daraja baada ya kumaliza nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi.

Sintofahamu hiyo iliibuka baada ya msimamo wa mwisho wa ligi uliotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuonyesha kuwa Kagera Sugar ndio inapaswa kushuka daraja ikizidiwa idadi ya mabao ya kufunga na Stand United.

Msimamo huo ulionyesha kuwa timu hizo zote zina idadi sawa ya pointi ambazo ni 44, huku kigezo cha pili cha kuamua mshindi baina yao ambacho ni kutazama utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa pia wakiwa sawa kwa maana ya timu zote mbili kuwa na mabao -11.

Kwa mujibu wa msimamo huo uliotolewa na TFF, Stand iliwekwa juu ya Kagera Sugar kwa kutazama kigezo cha tatu ambacho ni uwingi wa mabao ya kufunga ambapo wao walikuwa na mabao 38 huku Kagera wakiwa nayo 33.

Hata hivyo msimamo huo wa ligi uliotolewa na TFF ulionekana kuwa na makosa kwani kwa mujibu wa matokeo halisi ya timu hizo, Kagera walimaliza wakiwa na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa -10 huku Stand United wakiwa na -12 na ndio walipaswa kushuka.

Akizungumza jijini leo, Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura alisema baada ya bodi na TFF kupitia upya takwimu za ligi, Stand United ndio timu itakayoshuka daraja.

Na Charles Abel - Mwanaspoti
Share:

SERIKALI YATOA TAMKO KWA WATU WENYE VITAMBI TANZANIA


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema uwepo wa vitambi ni mojawapo ya dalili za mtu ananyemelewa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza na kuwataka watu wenye vitambi kuzingatia suala la mlo bora.

Naibu Waziri Ulega ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali kwa niaba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambapo amesema si dalili nzuri.

Akizungumza kwenye kikao hicho Naibu Waziri Ulega amesema kuwa "kitambi ni dalili mojawapo ya uzito kupita kiasi hii si dalili njema, hupelekea magonjwa yasiyoambukiza"

Aidha Naibu Waziri Ulega amesema kuwa "katika kupambana na kitambi nikujikinga kupunguza chakula cha wanga, sukari, chumvi, mafuta kwenye chakula, kunywa maji lita 1 na nusu na kupunguza unywaji wa pombe uliopitiliza"

Kwa sasa Bunge linaendelea Bungeni jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Share:

MUFTI WA TANZANIA ASHIRIKI FUTARI ILIYOANDALIWA NA KIBADA GARDENS KIGAMBONI,ATOA NENO KWA WAGENI WAALIKWA

   Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wageni wakibadilishana mawazo kabla ya kufuturu.
     Muda wa Kufuturu (Iftar)
Maulid Kitenge (MC) akifurahia jambo pamoja na Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir.
Mufti akitoa mawaidha kwa watu mbalimbali waliofika Kibada Gardens kwa ajili ya Iftar maalum  iliyoandaliwa siku hiyo,Mufti amewataka Waislamu waendelee kumcha Mungu na kuendelea kufanya matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu,na kwa si kwa wakati huu tu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani,lakini pia wakati wote.
Sheikh wa msikiti wa Kibada akikabidhiwa baadhi ya vitu kwa ajili ya Futari kwa wakazi wa Kibada.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mr. Ali Davutoglu akipeana mkono na Sheikh wa wilaya ya Kigamboni, Mr. Sharrif Hassan wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Kibada Gardens Dar es Salaam. Pili kushoto ni Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally
    Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally akitoa maneno ya hekima kwa baadhi ya watu waliofika katika Iftar maalum iliyoandaliwa na Kibada Gardens, Kigamboni Dar es salaam.
    Mufti wa Tanzania pamoja na baadhi ya masheikh wa bakwata wakiwasili Kibada Gardens kwa ajili ya Iftar iliyoandaliwa maalum katika mfungo wa Ramadhan unaoendelea.
1.      Kibada Gardens imeandaa Iftar maalum ambayo ilihudhuriwa na Mh. Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh.  Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania.
Share:

Simbachawene Aitaka Serikali Ipunguze Gharama za Umeme

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM), amesema gharama za uzalishaji wa umeme kwa sasa ziko juu, hivyo Serikali inatakiwa kuliangalia jambo hilo wakati ikielekea katika uchumi wa kati.

Kauli hiyo ameitoa bungeni leo Jumatano Mei 28, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20.

Aidha, mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, amesema umeme utakuwa na tija kama utaenda katika huduma za kijamii na shughuli za uzalishaji.


Share:

Makonda atangaza vita na Wamachinga wasio na vitambulisho Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuanzia June 3 mwaka 2019 ni marufuku kwa Wamachinga wote wasio na vitambulisho kufanya biashara katika maeneo yote jijini Dar.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 29, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mwitikio wa wafanyabiashara kuchukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli kwa wakuu wote wa Mikoa nchini.

Makonda amesema Jiji hilo lilipatiwa vitambulisho 175,000 lakini wapo ambao hawajachukua hadi sasa.

Amesema kuwa atafanya msako mkali kuwatafuta wamachinga wote wasio na vitambulisho hivyo


Share:

Serikali Kuajiri Watumishi Wapya 44,800 kwa kipindi cha 2019/20

Watumishi 44,800 wataajiriwa katika taasisi za Serikali kwa kipindi cha 2019/20

Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Dk Mary Mwanjelwa jana Jumanne Mei 28, 2019. na kubainisha kuwa ajira hizo zitawalenga Watanzania wenye sifa.

Dk Mwanjelwa alisema kuwa si Serikali pekee ndio inayotakiwa kutoa ajira, hata watu binafsi wanaweza kutoa ajira kwa vijana.

Naibu Waziri huyo alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Aida Khenan aliyehoji kama kuna utaratibu wowote wa kuajiri watu waliohitimu vyuo na kukidhi vigezo vya kuajiriwa.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo amehoji kwa nini Serikali inaendelea kuweka vigezo vya uzoefu kazini wakati inajua hakuna vijana wenye uzoefu.

Katika majibu yake, Dk Mwanjelwa alisema duniani kote Serikali si mwajiri pekee, akitolea mfano waajiri wengine ambao ni sekta binafsi, mashirika, asasi za kiraia na maeneo mengine.

Kuhusu uzoefu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama alisema wameondoa uzoefu badala yake Serikali imeanzisha kozi maalum kwa wahitimu ambazo husaidia kuwapa ujuzi.


Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH ....Anauwezo wa wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Mohamedi Buruhani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Mohamedi Buruhani  Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger