Tuesday 2 April 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne April 2

































Share:

Monday 1 April 2019

Waziri Biteko Awasimamisha Kazi Maafisa Madini Ofisi Ya Madini Chunya

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wote ofisi ya madini Wilayani Chunya na kuagiza  kuwafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa madini.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya , wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika ukumbi wa halmashauri ya Chunya.

Amesema, baada ya serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inadhibiti mapato yake, utafiti umebaini kwamba Wilaya ya Chunya inashika namba moja kwa wizi na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu ikifuatiwa na Kahama.

“Baada ya kufanya utafiti tumeabaini kunawizi mkubwa na usio na aibu ambapo unakuta mtu amepata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikali inapata  gramu 208, lakini kuna mahali mtu anapata kilo nne anawasilisha taarifa za gramu 155,sasa wizi namna hii tukiendelea kunyamaza nchi haiwezi kuwa na afya.,”alisema.

Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko  amewataka watendaji na viongozi husika kubadilika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

“Ukiangalia sasa, wazalishaji wengi wanakimbilia Chunya na hii ni kwa sababu ya utaratibu wa eneo husika kushindwa kubaini wizi huu unaofanyika kupitia taarifa za kiwango cha uzalishaji ambacho ndicho kinachohalalisha mapato kwa serikali kupitia mrahaba wa Madini “Amesema Waziri Biteko

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alimueleza Biteko kuwa Wilaya ya Chunya inahitaji msaada hasa wa kielimu na utaalamu wa madini na kuomba watendaji wasafi wapatikane kwenye sekta hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa sasa wanataka kuzungumza na uongozi wa Mkoa  wa Songwe  ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuimalisha Ulinzi katika maeneo hayo ili kuepusha wizi wa Madini.


Share:

PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Godbless Lema Katika Msiba wa Dada yake Mchungaji Msigwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshma za mwisho kwenye msiba  wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.



Share:

Maandalizi Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa Yaanza

Na.Alex Sonna/ Fullshangwe
Wakati  uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, ukitarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) leo imekutana na wadau wa vyama vya siasa kwa ajili ya kupitia rasimu za kanuni za uchaguzi huo.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo wakati wa kufungua kikao cha kupitia rasimu ambapo ametaja  rasimu tatu ambazo wadau hao watazijadili kuwa ni pamoja na Rasimu ya kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za mwaka 2019.

Waziri Jafo ametaja rasimu zingine kuwa ni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za mwaka 2019 na Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji midogo za mwaka 2019.

Aidha Jafo amewaomba wadau hao kutoa maoni na mapendekezo yatakayokuza demokrasia na utawala bora huku akiahidi kuwa serikali itazingatia maoni yao ili kanuni hizo ziweze kuleta tija na ufanisi kwenye uchaguzi.

Hata hivyo Jafo amesema utii wa Sheria za Nchi, Kanuni na Taratibu za Uchaguzi ndio msingi wa uchaguzi ulio wa haki na wenye kuzingatia ushiriki wa makundi yote ya jamii.

“Vyama vya siasa vinaowajibu wa kuwaelimisha na kuwaelekeza wagombea, wafuasi na wanachama wao kuzingatia matakwa ya Sheria za Nchi na kanuni hizi za uchaguzi wa serikali za mitaa,”amesema Jafo

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa John Shibuda  ametoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe ameshukuru kwa fursa hiyo waliyoipata na kuwataka wajumbe kuvumiliana na kutumia vizuri nafasi waliyoipata kwa maslahi mapana ya wananchi.


Share:

Rais Magufuli Atoa Pole Kwa Mbunge Wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa Aliyefiwa Na Dada Yake Jijini Dar Es Salaam

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mbunge wa Iringa Mjini Mch Peter Msigwa ambaye amefiwa na Dada yake Tryphosa Simon Sanga aliyefariki dunia tarehe 30 Machi, 2019 kwa ajali ya gari Jijini Dar es Salaam.

Wakiwa nyumbani kwa Marehemu Kimara Stopover, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wameungana na wanafamilia kumuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.



Share:

Rais Magufuli ataka TRA iache kuwa kamua walipa kodi wachache

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango atakayeshughulikia sera Adolf Hyasinth Ndunguru na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Akizungumza baada ya kuwaapisha, Rais Magufuli ameitaka TRA na Wizara ya Fedha na Mipango kupanua uwigo wa kodi kwa kuongeza idadi ya walipa kodi na kuibua vyanzo vipya vya mapato, pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa watu wengi zaidi kulipa kodi ili kuongeza makusanyo ya kodi.

Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na utendaji wa TRA ambayo mpaka sasa inakusanyaji kodi kwa walipa kodi Milioni 2 na Laki 7 tu kati ya Watanzania wote zaidi ya Milioni 55, na amesema kwa mtindo huo TRA itakuwa inazidi kuwakamua walipa kodi wachache wakati ingeweza kupanua uwigo wa kodi na kuweka viwango vya kodi vinavyolipika na vitakavyowavutia watu wengi zaidi kulipa kodi.

“Ukienda mipakani wafanyabiashara wanafungua maduka upande nchi za wenzetu na sio upande wa Tanzania, na sababu ni kwamba wakifungua upande wa Tanzania wanasumbuliwa na TRA, wekeni viwango vya kodi vinavyolipika ili watu wengi waweze kulipa kodi badala ya kukwepa” Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na mrundikano wa kesi za kodi mahakamani na ametaka tatizo hilo lifanyiwe kazi kwa kuwa linasababisha kodi nyingi kutolipwa kwa kusubiri mivutano ya kesi.

Amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwa ufuatiliaji mzuri wa fedha za bajeti zinazoelekezwa katika miradi mbalimbali na kuchukua hatua zinazostahili ikiwemo kuzirejesha hazina na kuzielekeza mahali pengine zinapohitajika.

Aidha, Rais Magufuli amemtaka Naibu Katibu wa Fedha na Mipango Mkuu Ndunguru na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mbibo kwenda kurekebisha dosari zote zilizopo katika ofisi zao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watumishi wanaoonekana kuwa kikwazo cha kutekeleza mipango ya Serikali.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema viongozi hao wanatarajiwa kufanya vizuri zaidi katika nafasi walizopewa hivi sasa hasa ikizingatiwa kuwa wanakwenda kufanya kazi katika ofisi zenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.

Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere wamemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi wa viongozi hao na wameahidi kwenda kusimamia kwa ukaribu zaidi utekelezaji wa fedha za bajeti na kufanyia kazi changamoto ya kupanua uwigo wa kodi na kuongeza idadi ya walipa kodi.



Share:

Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 form five selection

Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 selection

How to change form five Combination – Students who wish to join Form Five and Colleges for 2019/2020

The Government has provided opportunities for students who passed the Form four exam in 2018 and who are expecting to joining Form Five and varous colleges in 2019 to change their Combination.

“For the first time students will be able to change options or choose from Form Five to College or College to Form Five as per their requirements and how they passed their examinations” said Jafo.

How to change form five Combination – Students who wish to join Form Five and Central Colleges for 2019/2020

Monday 1st, April 2019 @Tanzania entire Date Released for Students who are hoping to join Form Five and Central Colleges, this date has been announced by the Minister of State OR-TAMISEMI.

Download and read the Guide for details….. Selform _ Student Manual.pdf

You can Log in to the System via the following Address After reading the Manual http://selform.tamisemi.go.tz/Account/Login

Click here to change your combination

This modification process will take place from 01/04/2019 to 15/04/2019.

The post Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 form five selection appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Ukaguzi Wa Maduka Ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni

Dodoma, 1 Aprili, 2019: Katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Fedha inachangia ipasavyo utulivu na ukuaji wa uchumi nchini, Benki Kuu ya Tanzania ilibaini uwepo wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalikuwa yakiendeshwa pasipo kuzingatia Sheria ya Foreign Exchange Act 1992, Kanuni za The Foreign Exchange (Bureau de Change) Regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017 na Taratibu za utoaji wa huduma za ubadilishaji wa fedha za kigeni. Kufuatia hali hiyo, zoezi maalum la ukaguzi wa kina kwa maduka hayo lilifanyika Arusha Novemba 2018 na kwa Dar es Salaam siku ya tarehe 27 Februari 2019, 1 na 8 Machi 2019 kwa kuhusisha vyombo vya Dola na kubaini ukwepaji mkubwa wa kodi na uvunjaji wa Sheria.

Zoezi hili limebaini pia uondoshwaji wa fedha katika mfumo rasmi wa fedha na kuelekezwa kwenye mifumo ya utakasishaji wa fedha haramu, kupokea Amana kutoka kwa wafanyabiashara kinyume cha matakwa ya leseni za biashara husika, kudhoofisha thamani ya shilingi, pamoja na mambo mengine ambayo yalianza kuathiri usalama wa nchi kwa ujumla. Kwa mfano, baadhi ya maduka yaligundulika kutumia fedha nyingi za Tanzania kununua fedha za kigeni lakini fedha kidogo za kigeni ziliuzwa na hakuna taarifa ya matumizi ya fedha za kigeni zilizobaki.

Ni vizuri ieleweke kuwa,  zoezi la ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni lilitekelezwa kwa kuzingatia Sheria za nchi tofauti na malalamiko na tuhuma mbalimbali zilizotolewa za kudai uwepo wa ukiukwaji wa Sheria na haki kwa wamiliki wa maduka hayo. Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mmiliki yeyote wa duka aliyewasilisha malalamiko kuhusiana na zoezi hili kwenye mamlaka husika. Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania na Mamlaka nyingine za Serikali zinafuatilia kwa umakini ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zinazotolewa.

Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza majukumu yake kwa umakini. Hivyo, Serikali inauthibitishia umma wa Watanzania kuwa katika zoezi la ukaguzi wa Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni hakuna fedha au mali yeyote iliyotaifishwa. Taratibu za kisheria zilifuatwa wakati wa kuchukua vielelezo mbalimbali zikiwemo fedha, kompyuta, simu za viganjani, mashine maalum za kuhifadhi taarifa na taarifa mbalimbali ili kusaidia uchunguzi. 

Aidha, lengo la zoezi hili sio kufuta biashara ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa watu binafsi, bali ni kudhibiti ukiukwaji wa sheria uliokithiri, ukwepaji wa kodi na utakatishaji wa fedha haramu. Maduka machache ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalizingatia Sheria na Kanuni za Foreign Exchange na masharti ya biashara hiyo yaliachwa kuendelea na utoaji wa huduma hiyo.

Hivi sasa Serikali imeandaa Kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisi yeyote na masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.

Kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo hayatatoa athari kwa sekta ya fedha na uchumi jumla, na inakuwa yenye manufaa kwa nchi. 

Kwa kuzingatia maduka mengi yaliyokaguliwa yamefungwa, Benki Kuu ya Tanzania imechukua tahadhari ya kuhakikisha huduma ya ubadilishaji fedha za kigeni inaendelea nchini kwa kutolewa na benki zote pamoja na Shirika la Posta. 

Benki Kuu ya Tanzania itakuwa inatoa taarifa kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo na kuzihimiza benki za biashara na Shirika la Posta kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na huduma katika maduka yaliyofunguliwa na benki hizo na Ofisi ya Posta.

Kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni, thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri. 

Kabla ya zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha ya kigeni dola ya Marekani ilikuwa inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hivi sasa dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,300. 

Aidha, Benki za biashara kwa wastani hivi sasa zinakusanya jumla ya dola za Marekani milioni 15 kwa siku. Ni matarajio ya Serikali kuwa udhibiti huu utaziwezesha Benki za biashara na taasisi nyingine kuuza fedha za kigeni kwa wingi kwenye soko la fedha za kigeni na hatimaye kuongeza akiba ya fedha za kigeni.

Serikali inatoa tahadhari kwa wananchi kutoshiriki kwenye biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia zisizo halali. Hivi sasa kuna taarifa kwa baadhi ya maeneo ya mipakani na majiji ya Dar es Salaam na Arusha wamejitokeza watu wanaofanya biashara haramu ya kubadilisha fedha za kigeni ambao wamewaathiri baadhi ya wananchi kwa wizi. 

Vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi vimeongeza nguvu katika kuhakikisha biashara hii haramu (Black Market) inatokomezwa na hivi sasa wahalifu saba wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Serikali inapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa inayo akiba ya fedha za kigeni ya kutosha zipatazo dola za Marekani bilioni 4.67 hadi tarehe 30 Machi 2019 zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisicho pungua miezi 4.8. 

Hivyo, wasiwasi kuwa Serikali imechukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si ya kweli hata kidogo. 

Aidha, hofu kwamba nchi inarejea katika kipindi cha nyuma ambapo fedha za kigeni zilikuwa zinatolewa kwa vibali (rationing) ili kukidhi mahitaji ya fedha hizo kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, nazo hazina msingi.

Mapato ya Nchi yanayotokana na vyanzo vya fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi yalikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 8,554.5 kwa mwaka unaishia Februari 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.4 ikilinganishwa na fedha za kigeni zilizopatika mwaka unaishia Februari 2018. 

Ongezeko hilo la mapato ya fedha za kigeni kwa Nchi yamechangiwa zaidi na uuzaji wa bidhaa zisizo asilia nje ya nchi zikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 3,878.5 sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. 

Vile vile, huduma zilizotolewa nje ya nchi kama vile usafiri na usafirishaji na utalii ziliingiza jumla ya dola za Marekani milioni 4,074.1 sawa na ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa kiasi kilichopatikana mwaka ulitangulia.

 Aidha, Serikali inachukua fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa nchi yetu ina akiba ya chakula cha kutosha ambacho kina utoshelevu wa asilimia 124 kwa mwaka huu wa fedha 2018/19.  Hivyo, Serikali haitarajii kutumia  fedha za kigeni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi isipokuwa tu kama ikitokea hali ya ukame ikawa mbaya katika siku zijazo.

Serikali, kupitia Benki Kuu ya Tanzania, inawataka wafanyabiashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kuzingatia na kutii Sheria ya Foreign Exchange 1992, Kanuni ya Foreign Exchange (Bureau de Change) Regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017, Masharti ya biashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni na Maelekezo ya Msimamizi (BOT) wa Sekta ya Fedha Nchi. Mwisho Serikali inawapongeza wananchi wa Tanzania kwa kuwa waelewa na watulivu wakati wote zoezi la ukaguzi likiendelea, licha ya kujitokeza kwa taarifa za upotoshwaji wa zoezi hili.

IMETOLEWA NA:
DKT. PHILIP ISDOR MPANGO
WAZIRI YA FEDHA NA MIPANGO


Share:

ASASI 65 ZA KIRAIA ZAMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AACHE KUINGILIA MIGOGORO YA NDANI YA VYAMA VYA SIASA

Asasi 65 za Kiraia zimemtaka Msajili wa vyama vya Siasa Nchini aache kuvitisha na kuingilia migogoro ya ndani ya vyama vya siasa.

Aidha, badala yake wamemtaka aongozwe zaidi na hekima katika kusimamia misingi ya demokrasia na haki za wananchi kujiunga na vyama wanavyovitaka bila kuwekewa vikwazo visivyotambulika na sheria za nchi.

Wito huo umetolewa leo na Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI katika ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC), ambapo pia zimewataka viongozi waheshimu sheria za nchi na katiba kwa kuacha kuzuia mikutano ya siasa ya ndani na nje.

Akitoa tamko kwa niaba ya Azaki hizo, kuhusu hali ya demokrasia, haki ya kujumuika na kujiunga na vyama vya siasa, Onesmo Olengurumwa kutoka THRDC, amesema kumekuwa na matukio yanayoashiria ukiukwaji wa haki za kidemokrasia haki ya uhuru wa kukifanyika na kujiunga na vyama vya siasa.

“Kama Watanzania wenye jukumu kikatiba kulinda mshikamano, umoja,haki na amani ya nchi tumeona ni vyema kuzungumza na kuwashauri viongozi wetu wa kisiasa kufuata sheria za nchi.

“Tumeshuhudia ukiukwaji wa haki hizo za kisheria na Katiba ya nchi ya mwaka 1977 na kwa kuwa asasi tumekuwa washauri na wakosoaji na wasaidizi wakubwa wa mambo mengi yakitaifa ni busara zaidi kulisemea hili ili kuhakikidha ukiukwaji wa haki hizi tajwa haziwezi kuwa sababu ya kupelekea kupoteza amani na umoja wa kitaifa,” amesema Olengurumwa.

Amesema mwenendo wa muda mrefu wa Msajili wa vyama vya Siasa kuonekana kuchukua upande katika mgogoro wa ndani wa Chama cha Wananchi (CUF) na kusahau yeye ni mlezi wa vyama alipaswa kutokuwa sehemu ya mgogoro ndani ya vyama.

Naye mwakilishi kutoka LHRC, Felister Mauya, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha uhuru wa kujumuika ikiwa ni pamoja na uhuru wa kufanya maandamanao ya amani unaheshimiwa na kulindwa na vyombo vya usalama kama sheria zinavyoelekeza.

Share:

MWANAMKE ALIYEKANA KUWA 'SIYO MJAMZITO' AJIFUNGUA AKIWA CHOONI

Mwanamke wa miaka 23 amejifungua mtoto akiwa kwenye choo licha ya kukana mara kadhaa kwamba hakuwa mjamzito. 

Emmanuella Osei ambaye anaishi Pennsylvania, Marekani alijifungua akiwa kazini Jumamosi Machi 30,2019.

 Kulingana na jarida la Daily Mail, mtoto huyo alinusurika kifo baada ya maafisa wa polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa.

 Emmanuella tayari yuko na mtoto mwingine wa miaka miwili nyumbani kwao nchini Ghana na hakuwahi kuwwambia jamaa yake kwamba alikuwa mjamzito.

 Alipozidiwa na uchungu wa kujifungua, Emmanuela alimwambia meneja wake apige nambari ya dharura 911 ila hakumwelezea kwamba alikuwa amejifungua. 

Polisi waliikuta damu ikiwa imejaa kwenye sakafu huku akiwa na muimivu mengi na mwanawe pia akiwa ameachwa sakafuni bila hata kufunikwa chochote. 

Inaelezwa kuwa Emmanuela alitaka mtoto huyo afe kwani alikuwa amemuacha ndani ya maji kwa zaidi ya dakika 10. 

Mtoto huyo alikimbizwa hospitalini akiwa hali mahututi ila alipata nafuu baada ya kutibiwa.

 Emmanuela alikamatwa na maafisa wa polisi na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha miaka 10. 
Share:

MVULANA WA MIAKA 16 AWAPACHIKA MIMBA WASICHANA WATATU

Mvulana mwenye umri we miaka 16 kutoka Kibera, Nairobi anadaiwa kuwapachika mimba wasichana watatu. 

Wasichana hao wa umri mdogo kutoka mtaa wa Kibera, Nairobi huenda wakakosa masomo yao kwa muda baada ya mvulana rafiki yao mwenye umri wa miaka 16 kuwatunga mimba katika kipindi cha miezi sita.

 Urafiki wa wasichana hao wa kati ya umri wa miaka 13 na 15 na mvulana huyo ulianza mwishoni mwa 2018 na mapema 2019 na baada ya muda mfupi walipachikwa mimba.



 Katika mahojiano na NTV, Jumamosi, Machi 30, mmoja wa wasichana hao alisema alikutana na baba ya mtoto wake wakati wa kupigwa picha na hatimaye wakaanza urafiki. 

"Baada ya kukutana naye tulianza kupendana. Baada ya mwezi mmoja na nusu niligundua mimi ni mjamzito. Baadaye alikana kuhusika nilipomuuliza," alisimulia. 

Kwa mshtuko mkubwa, msichana huyo we Kidato cha Kwanza aligundua mvulana huyo alikuwa na wasichana wengine wawili ambao tayari nao walikuwa wajawazito. 

Kwa msichana mwingine mwenye umri wa miaka 13, kisa chake kilikuwa tofauti kwani zawadi za mara kwa mara zilimfanya kupumbazwa kimapenzi ingawa hakumpenda mvulana huyo mwanzoni.

Kulingana na takwimu za punde kuhusu visa vya mimba za mapemba miongoni mwa wasichana vi vya juu zaidi Kaunti ya Narok huku ikiongoza kaunti zingine kwa 40%.

 Homa Bay inafuatia kwa 33%, Pokot Magharibi kwa (29%), Mto Tana na Nyamira (28%) kisha nambari sita ni Samburu kwa 26%. 
Share:

CHADEMA WAMPOTEZEA JOSHUA NASSARI


Joshua Nassari

Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, umesema kuwa msimamo wao ni ule ule kwamba hautashiriki uchaguzi kwenye jimbo la aliyekuwa Mbunge wake Joshua Nassari, kutokana na sababu zao za awali kuwa hakuna uwanja sawa wa ushindani.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vincent Mashinji ambaye maamuzi ya kikao chao kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam kikiongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo.

"Hatujabadili msimamo wa chama kutoshiriki chaguzi hizi, kwa sasa mtazamo wetu ni Uchaguzi Mkuu, na chama ndicho kinachoamua, kuhusu Nassari mwenyewe kama alikuwa ndani ya chama kwa ajili ya madaraka anaweza kuondoka”, amesema Dkt. Vicent Maashinji.
Share:

DUDU BAYA AIOMBA RADHI FAMILIA YA RUGE MUTAHABA

Share:

KILIMANJARO SAR WATIMIZA MWAKA MMOJA,WATANGAZA KUTOA BURE HUDUMA YA UOKOAJI KWA WAONGOZA WATALII MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA HELKOPTA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Shrika la Kilimanjaro SAR,Ivan Brown akitoa taarifa za shirika hilo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu shughuli mbalimbali za uokoaji ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu katika shirika la Kilimanjaro SAR,Amour Abdalah akizungumza na wanahabari (hawapo pichani kuhusu mwaka mmoja wa operesheni ya shirika hilo. 
Kikosi cha uokoaji kwa kutumia Helkopita kikiwa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa msaada kwa wageni. 
Ndege aina ya Helkopta inayotumiwa na Shirika la Kilimanjaro SAR katika kufanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. 


Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo yenye muinuko ikiwemo Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa waongoza watalii pamoja na wapagazi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato cha uhakika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.

“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia katika uokoaji”alisema Brown.

“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha ,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi ,uhai ndio kipaumbele cha kwanza”aliongeza Brown.

Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya ,umbali wa Mita 5000.

“Tayari tumetoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita 4800 ,katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”,alisema Borown.

“Tumeokoa waongoza watalii na wapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughuli za uokoaji maisha kwa urahisi.

Mbali na shughuli ya utafutaji na uokoaji ,Kampuni ya Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha Kliniki ya kisasa “Kilimanjaro SAR High Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa yatokanayo na muinuko.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu.

“Magonjwa ya mlimani yanahitaji ,matibabu maalumu ,na ndio sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu na kupatiwa matibabu”,alisema Abdalah.

Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013 baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.

Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.

“Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro”, alisema Amour.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika” ,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “ ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo iliyotolewa na ATE .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger