Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa
mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT
kwa Mujibu wa Sheria.
Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kwa
kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye
makontena.
Wanafunzi wa kidato cha sita waliohitimu mwaka huu May 2017 takribani
14,747 sawa na asilimia 23.2%, wamepangiwa katika vituo mbalimbali vya
Jeshi kati ya wahitimu 63,623, wanatakiwa kufika kambini kuanzia 25-30
May. Taarifa imetolewa na Mkuu wa JKT Akiongea na ITV amesema Orodha ya waliochaguliwa katika kambi mbalimbali yanapatikana katika tovuti yao ya JKT. www.jkt.go.tz Source: ITV (Habari)
Ni hivi Majina yametoka na leo nlimsikia msemaji pale JKT akiongea
Kwenye Habari ITV, na idadi ya wanafunzi waliochaguliwa imepungua sana
ndo maana leo Mbunge wa Newala akauliza Swali kwa Waziri wa Ulinzi ni
kwanini Idadi hiyo imeshuka sana?
Habari zenu, Maswayetu blog tunafanya usajili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo mbalimbali katika kozi za afya,kilimo etc mwaka wa masomo 2017/2018. Pia tunatoa ushauri kabla ya kufanya application kulingana na matokeo yako uliyopata. Gharama zetu ni nafuu sana. Kama unataka ushauri unaweza ukauliza swali lako kwa kutuma na maksi zako ulizopata,kwa kutuma kwenda namba 0652740927
Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inawatangazia wanafunzi wote
wanaohitaji kujiendeleza katika fani mbalimbali za Elimu ya Juu kuwa
fomu za maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18
zitaanza kutolewa kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 02/05/2017 hadi tarehe
31/07/2017.
Mikopo itatolewa kwa waombaji waliotimiza sifa za kujiunga na masomo ya juu katika ngazi za:
Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree),
Shahada ya Pili (Master Degree)
Shahada ya Tatu (PhD).
Walengwa wa maombi ya mikopo ni:
Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
Wahitimu wa Diploma wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
Wahitimu wa Shahada ya Kwanza wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Pili.
Wahitimu wa Shahada ya Pili wenye sifa za kujiunga na Shahada ya Tatu.
Kuanzia
mwaka wa masomo 2017/18 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar
haitatoa mikopo kwa waombaji ambao ni watumishi wa Taasisi za Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (SMT). Mkazo umewekwa kwa vijana wapya waliomaliza masomo na
ambao hawajapata ajira.
Waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia
Fani za Vipaumbele vya Serikali ambazo zinapatikana katika tovuti za
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz).
Fomu za maombi zitalipiwa shilingi 10,000 ambazo zitalipwa moja kwa moja na muombaji kwenye akaunti namba 021108001357 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Wanaohitaji
fomu za maombi wanaombwa kufika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu
ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Amali, Chakechake Pemba na wanatakiwa kuchukua:
Kitambulisho cha Mzanzibari
Fomu ya malipo (Pay Slip) kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
Vivuli vya vyeti na matokeo ya masomo kwa ngazi aliyohitimu.
SIFA ZA KUPATA MKOPO
Sifa za waombaji wa mikopo ambao maombi yao yanaweza kuzingatiwa wakati wa uteuzi zimetajwa kwenye kifungu cha 20 zikiwemo:
Mwombaji awe Mzanzibari
Awe ameomba mkopo kwa kujaza Fomu Namba 1 au
kupitia njia nyengine yoyote ile ambayo BMEJZ itaona inafaa. Maombi
yawe yamewasilishwa ndani ya muda maalum uliowekwa na BMEJZ unaoanzia
Mei 2 hadi Julai 31 ya kila mwaka.
Awe amepata udahili kwenye chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka husika nchini.
Awe amepata alama nzuri za ufaulu.
Mwombaji wa shahada ya kwanza (Bachelor/First Degree) aliyehitimu kidato cha sita anapaswa awe amefaulu angalau masomo mawili (Principal subjects) kwa alama za ufaulu zinazoanzia:
alama 4.0 kwa wahitimu wa masomo ya sayansi au ufundi;
alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya biashara;
alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya sanaa au sayansi jamii.
Mwombaji wa shahada ya kwanza aliyehitimu stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma)
katika masomo ya sayansi au ufundi anatakiwa awe na ufaulu wa alama
(GPA) 3.0 au B; wahitimu wa stashahada za masomo ya biashara, sayansi
jamii au Sanaa wapate alama kuanzia 3.5 au B+.
Mwombaji wa shahada ya uzamili (Master/Second Degree) katika
masomo ya sanaa au sayansi jamii awe amehitimu shahada ya kwanza na
kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la juu (upper second class). Waombaji
wa shahada ya uzamili katika nasomo ya sayansi, ufundi, tiba, uchumi,
mipango na biashara wawe na alama za ufaulu za kuanzia daraja la pili la
chini (lower second class). Wahitimu wa stashahada ya uzamili wanapaswa kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la chini (lower second class)
Mwombaji wa shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy - PhD) awe
amehitimu shahada ya uzamili na kupata alama za kuanzia daraja la pili
la juu kwa waombaji wa masomo ya sanaa na sayansi jamii. Waombaji wa
shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi, ufundi, udaktari na uchumi,
mipango na takwimu wapate alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la
chini.
Waombaji
wanaoendelea na masomo vyuoni pia wanaweza kuomba kwa kuzingatia sifa
za kitaaluma zilizotajwa hapo juu [d(i) –(iv)]. Aidha mwombaji awe
amefaulu mitihani yake ya chuo kwa kiwango kitakachomwezesha kuendelea
na masomo kwa mwaka unaofuatia katika ngazi ya masomo anayoombea mkopo.
Awe ameomba fani inayolingana na vipaumbele vya SMZ katika mwaka husika.
Asiwe na mkopo au udhamini wa masomo kutoka taasisi nyengine.
Mwombaji
wa shahada ya kwanza asizidi umri wa miaka 40 kuanzia tarehe ya kutuma
maombi na mwombaji wa shahada ya uzamili asizidi miaka 45 kuanzia tarehe
ya kutuma maombi. Ukomo wa umri wa mwombaji wa shahada ya uzamivu ni
miaka 47 kuanzia tarehe ya kutuma maombi.
Mwombaji aliyeajiriwa kwenye utumishi wa umma awasilishe barua ya ruhusa kutoka kwa mwajiri wake.
Mwombaji
anayedaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar awe ameshaanza
kulipa deni lake kwa angalau asilimia 25 ya deni lote bila ya kusita kwa
malipo ya deni ya kila mwezi.
Mwombaji
aliyesoma kwa mkopo kutoka BMEJZ awe ameshafanya kazi kwa angalau miaka
miwili baada ya kuhitimu masomo yake ya awali kabla ya kuomba mkopo
mwengine kutoka BMEJZ.
Angalizo:
Waombaji
wanaotumia sifa za masomo ya kidato cha nne kuomba udahili katika vyuo
vikuu vya nje ya nchi ili kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza,
maombi yao ya mkopo hayatozingatiwa.
Waombaji
wa mikopo waliohitimu masomo ya Diploma pasi na kuwa na elimu ya kidato
cha sita au sifa za kujiunga na kidato cha sita, wanatakiwa wawe
wamefaulu angalau masomo matano ya Kidato cha Nne kwa kiwango cha alama D
na kuhitimu ngazi ya cheti (Certificate) kabla ya kujiunga na masomo ya Diploma.
Waajiriwa hawahusiki na utaratibu wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka huu wa masomo
FANI ZA VIPAUMBELE WA KIPINDI CHA 2016 - 2020
Tume
ya Mipango ya SMZ imetoa taarifa kuhusu utafiti uliofanywa juu ya hali
ya utumishi nchini ambayo imeonesha uwepo wa mahitaji makubwa ya
wataalamu. Taarifa hiyo imeibua maeneo ya Vipaumbele vya SMZ juu ya
mahitaji ya wataalamu na imeagizwa kuwa taarifa hiyo itumike kama kigezo
muhimu kwa utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu nchini ili kufikia
utekelezaji wa mipango na maendeleo ya rasilimali watu iliyo bora na
itakayowaandaa watu wenye ujuzi sahihi, taaluma, tabia na silka zenye
tija zinazoendana na mabadiliko ya mfumo wa ushindani wa soko la ajira
na kufikia viwango vya juu vya uzalishaji na utoaji huduma.
Ili
kurahisisha utekelezaji wa Vipaumbele vya SMZ katika utoaji wa mafunzo
ya elimu ya juu kuanzia mwaka wa masomo 2016/17 hadi 2019/20, Tume ya
Mipango imevigawa vipaumbele hivyo katika madaraja matatu tofauti
kulingana na umuhimu wa kila kada kama inavyoonekana katika jedwali la
hapo chini.
Hivyo, kwa mwaka huu wa masomo, BMEJZ itazingatia
kikamilifu taarifa ya Tume ya Mipango wakati wa upokeaji wa maombi ya
mikopo na uteuzi wa waombaji katika mwaka wa masomo 2017/18.
Shambulizi
la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika
kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri
mashirika tofauti duniani.
Kampuni
ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000
za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.
Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.
Programu
hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola
300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku
nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
==> Hii ni Tahadhari Iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu Kirusi hicho
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria
ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na
kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii
inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya
kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla
haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo
yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE).
Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni,
isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu.
Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.
Udahili
wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara
ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE).
Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.
Aidha
vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya
watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya
na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.
Baraza
linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili
wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017.
Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo
kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25
Septemba, 2017.