Sunday 4 September 2016

List of Students MIST:Selected for Various Ordinary Diploma Programmes Offered by MUST for Academic Year 2016/2017 (Batch One) Dat

Share:

Rais Magufuli Azungumzia Tukio la Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein

Rais John Magufuli amemshangaa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwa kuidhinisha fedha za matibabu ya mpinzani wake wa kisiasa, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi wiki mbili zilizopita. 
“Mtu mmekutana kwenye msiba, mahali kwenye majonzi, mnamsindikiza marehemu. Kwa unyenyekevu wako Dk Dhein ukatoa mkono wako kumsalimia mtu fulani. Huyu mtu akakatalia mikono yake na bado asubuhi yake ukasaini fomu zake za kwenda kutibiwa nje ya nchi?” alisema Magufuli. 
“Haya ni mapenzi makubwa sana. Amekataa mkono wako. Huyohuyo akiugua unampeleka hospitali. Akitaka kusafiri nje, unasaini na unampa na fedha na posho za kwenda nje. Mimi nisingeweza.” 
Rais ametoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani Unguja ambako amekwenda kushukuru wananchi kwa kumchagua kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita. 
Visiwani Zanzibar, uchaguzi wa Rais, wawakilishi na madiwani uliingia dosari siku ya mwisho ya kutangaza matokeo. Mwenyekiti wa Tume ya Ucha- guzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani Oktoba 28 mwaka jana, siku ambayo alitarajiwa kutangaza mshindi wa mbio za urais. 
Alifuta wakati matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa na kubakia tisa ambayo yalishahakikiwa na kusubiri kutangazwa huku baadhi ya washindi wa viti vya uwakilishi wakiwa wameshatangazwa na kupewa vyeti. 
Jecha alisema kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi na kutangaza uchaguzi mpya Machi 20, lakini chama kikuu cha upinzani visiwani humo, CUF kikasusia na tangu wakati huo uhusiano baina ya wafuasi wa vyama hivyo umeharibika. 
Uhasama huo ulifikia kiwango cha juu wakati Maalim Seif alipokataa kumpa mkono Dk Shein walipokutana kwenye mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kitendo kilichomfanya Rais Magufuli aeleze yake ya moyoni jana. 
Akishangiliwa na wananchi, ambao wengi walivalia fulana za rangi za njano na kijani ambazo hutumiwa na CCM, Rais Magufuli alisema Dk Shein ni mpole na kama angekuwa na moyo kama wake, hali ingekuwa tofauti baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha Maalim Seif. 

“Niutoe mkono wangu, uukatae halafu kesho niende ofisini kukusainia wewe (akaongea kilugha). Ndiyo maana nasema wewe ni special. Nafikiri wanapotoka malaika wewe ndiyo unafuata. Kama mtu anaukataa mkono wako, na wewe kataa kufanya mambo yake, ajifunze kwamba na wewe mkono wako una thamani.” 
Alisema anaomba Mungu amsaidie kumpa angalau nusu ya moyo wa Dk Shein na kuomba Mungu ampe Dk Shein nusu ya roho na mawazo yake ili Zanzibar iende bila kelele za aina yoyote. 
“Jana nilikwambia angalau uongeze kaukali kidogo. Umefanya mambo makubwa sana katika nchi hii. Tulishazungumza na wewe umezungumza kwamba kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi umekwisha, ukisharudiwa umekwisha. Utarudiwa tena mwaka 2020, wazunguke waimbe lakini wewe ndiye rais,” alisema. 
Magufuli alisema upendo na unyenyekevu alionao Dk Shein ni wa hali ya juu kwani licha ya mikikimikiki aliyoipata kutoka kwa wapinzani, ameendelea kuwaingiza katika Serikali yake, jambo ambalo yeye hawezi kulifanya. 

“Mimi nilipata ushindi kwa asilimia 58, lakini hakuna mtu kutoka chama kingine atakayekanyaga mguu kwenye Serikali yangu. 

"Mzee huyu ana moyo wa tofauti, namuomba Mungu apate hata robo ya moyo wangu maana amekuwa mpole mno,” alisema Dk Magufuli. 

Rais Magufuli alisema licha ya maendeleo yaliyopo, bado wapo Wazanzibari (hakuwataja majina) wanaokwenda nje ya nchi na kuwazuia wageni na watalii kuacha kutembelea visiwa hivyo. 

“Mwenyeji anakuja na kuwaambia wageni wasije hapa na wao wamempuuza. Bado wageni wanakuja. Ukigombea mwaka wa kwanza ukashindwa, mwingine ukashindwa, mwingine ukashindwa, huwezi kujifunza hata kwenda kuuza nyanya sokoni kwamba biashara hii imekataa kwako,” alisema na kuongeza:

“Kwani hakuna wengine ambao wanakuja? Kuna mtu alitegemea kwamba nitakuwa Rais, hata kuota.Lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20 sikujaribu hata siku moja kugombea (urais). 

“Unajua vyeo hivi vinaletwa na Mungu, hata uzunguke namna gani, hata ufuge ndevu namna gani hata unyoe. Kama kasema hapana ni hapana tu, ndiyo maana nasema watu, ni shetani kama sivyo, basi ana moyo wa kishetani na mtu anayefarakanisha mke na mume kwa itikadi za vyama vyao pia ni shetani.
Share:

Rais Magufuli aahidi kulinda Muungano na kudumisha amani.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atasimamia kwa nguvu zote masuala yote yanayohusu maendeleo, kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar na kudumisha amani kwa faida ya wananchi.

Rais Magufuli amesema hayo jana tarehe 03 Septemba, 2016 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja.

Dkt. Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alisema ili mambo hayo yafanikiwe Wananchi wa Zanzibar hawana budi kukataa kujihusisha na vitendo vya vurugu na kuvunja amani na amewaonya watu wanaochochea vitendo hivyo kuacha mara moja.

Aliwataka wananchi wa Zanzibar kujihadhari dhidi ya wanasiasa ambao wanapandikiza chuki, ubaguzi na fitina, kwani watu hao wanataka kubomoa misingi mizuri ya umoja, upendo na mshikamano wa Taifa uliojengwa na waasisi wa Taifa hili.

Rais Magufuli alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyehudhuria mkutano huo, kwa hatua mbalimbali anazozichukua kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar huku akibainisha kuwa tatizo la maji linalovikabili visiwa vya Zanzibar litakwisha baada ya kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa maji utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 92, na mradi mwingine utakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 21.

Aidha, Rais Magufuli alivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri vinayofanya katika kusimamia amani visiwani humo huku akivihakikishia kuwa yeye akiwa kiongozi wao anawaunga mkono.

Pamoja na Rais Shein Mkutano huo ulihudhuriwa na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Mawaziri na Viongozi wa Siasa na Dini.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEP 4 2016

Share:

Saturday 3 September 2016

HVI HAPA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA KUTOKA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA -TFDA

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 3.9.2016



Share:

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumuita Rais Magufuli ni Kilaza


ELIZABETH Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App.

Akisomewa mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho kilicho kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Wakili Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa huyo aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;

“….Rais kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… f****l** lile, kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”

Hata hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Mtuhumiwa alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.

Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.
Share:

Waziri Mkuu aitaka Wizara ya Elimu kuongeza wataalamu wa Afya nchini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha wataalam hao nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo Ijumaa, Septemba 2, 2016  wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila.

Amesema Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.

“Wafanyakazi waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,” amesisitiza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.

Amesema hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ujenzi wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.

Prof. Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Share:

Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima .........Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe

RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana  jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama kuna  tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.

Rai Magufuli pia alimtaka Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni  na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger