MSANII maarufu wa sinema za Kibongo,
Rose Ndauka amesema kuwa watu wasiwe na wasiwasi kwani kwa mipango ya
Mungu atafunga ndoa na mzazi mwenzake Maliki Bandawe hivi karibuni.
“Si
muda mrefu mambo yatakuwa mazuri tulikuwa tunaendelea kujuana, nadhani
sasa tunafahamiana vizuri hivyo watu wasiwe na shaka, tutafunga ndoa
soon,” alisema.
Rose ambaye hivi karibuni alihamasisha zoezi la
usafi na kuungwa mkono na wasanii mbalimbali akiwamo Meya wa Ilala Jerry
Slaa, alisema watu wasihofu kuhusu ndoa hiyo kwani ipo njiani.
“Hatujui
labda kuchelewa kwetu kuna kitu Mungu amekiepusha, siku zote haraka
haraka haina Baraka,” alisisitiza Ndauka ambaye amepanga kutembea
Tanzania nzima kuwahamasisha wananchi kuzingatia usafi.
STAA
wa muziki wa bongo fleva nchini, Abdul Nassib "Diamond"
ametakiwa kutokanyaga kabisa nchini China na kwamba akitokeza
pua yake nchini humo asahau kabisa kurudi uraiani...
Hiyo
inafuatia kijana mmoja mtanzania kukamatwa wiki iliyopita
uwanja wa ndege wa Macau China na kudai kuwa yeye ni
mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....
Habari
kutoka Macau China zinadai kuwa kijana huyo aliyejulikana kwa
jina moja la Manyota alikamatwa akiwa kwenye harakati za
kuingiza mzigo huo wa dawa za kulevya kwa kupitia uwanja wa
ndege wa Macau....
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, inaarifiwa kuwa Manyota
alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita katika uwanja uleule
aliokamatwa mtanzania mwingine Jackline Patrick, anayesotea
rumande mpaka hii leo huko huko Macau China.....
Kijana
mmoja wa kitanzania anayefanya shughuli zake huko China amedai
kuwa Manyota alikamatwa na maofisa wa usalama wa uwanja wa
ndege na katika utetezi wake alidai kuwa yeye ni mwanamuziki
toka Afrika Mashariki...
Mtanzania
huyo aliendelea kudai kuwa, Manyota baada ya kukamatwa alianza
kubabaika kwa kujifanya mwanamuziki na baadae akadai kuwa yeye
ni mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....
"Alijifanya
yeye ni mwanamuziki, baadae akabadilika na kudai yeye ni
mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania na kwamba
ndani ya ule mzigo alikuwa hajui kuna nini zaidi ya kuombwa
na jamaa zake wa Dar awapelekee nchini China"...Alisema
mtanzania huyo
Inasemekana
kuwa, ili kujiridhisha, maofisa hao wa usalama wa uwanja wa
ndege walimtaka kijana huyo aoneshe moja ya kazi zake na
yeye akaishia kuwaonesha moja ya video za Diamond kupitia
mtandaoni na kumuonesha mmoja wa wacheza shoo wa mwanamuziki
huyo kuwa ndo yeye Manyota...
Inasemekana
kuwa, pamoja na utetezi wake huo ambao unaweza kumuingiza
matatani Diamond,maofisa hao wa usalama walishndwa kumuelewa na
kumtupa ndani.....
Mtanzania
huyo alihitimisha kwa kudai kuwa, kutokana na mazingira
yalivyo,ni vyema mwanamuzi Diamond akawa makini sana kama
atakuwa na safari za kwenda China kwani kwa namna moja ama
nyingine jina lake limewekwa kwenye orodha ya majina machafu
na wanaweza kumkamata kwa lengo la kuujua ukweli....
MWANADAFADA mkali wa Bongo Movies,
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza
nusu utupu kwa sinema za nje ya nchi.
Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akipiga stori mbili-tatu na kona hii,
Batuli alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa
maadili na kwamba kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini
hizo, atakuwa tayari.
“Zamani
nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu utupu. Wenzetu Nigeria wameendelea na
ndiyo maana wanaigiza hata nusu utupu, kama itatokea nafasi ya kuigiza
huko (nje ya Bongo) nusu utupu, nipo tayari,” alisema Batuli.
KIMENUKA! RB namba
KT/RB/1178/2014-KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO inamsaka staa wa Ngoma
ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa tuhuma ya
kutishia kumuua mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Amani Shija, Ijumaa
Wikienda limeinyaka.
Staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano nyumbani kwake, Manzese jijini Dar.
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na
Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni
walikuwa maeneo ya Kijitonyama, Dar, wakipata chakula cha usiku na
marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo akajichanganya na kujikuta
akiropoka neno lililomuudhi Nay, akapaniki.
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki,
Nay alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua, ambaye alishindwa
kujizuia na kujikuta akimwaga chozi.
Akaendelea
kueleza kuwa hata baada ya siku hiyo, Nay aliendelea kumtumia SMS za
kutishia kumuua ambazo bado anazo kama ushahidi Baada ya kudaka mchongo
huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia ni msanii wa Bongo
Fleva na kumuuliza juu ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na kaka
yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay amekuwa akiendelea kumtishia kumuua jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema
ili kujilinda ndipo alipoamua kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha
Polisi Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha kufunguliwa jalada la kesi
namba KT/RB/1178/2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila
mafanikio lakini kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, baada ya kujua msala
huo ametorokea nchini China.
PASUA jipu! awili wenye majina
makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma
Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada
ya kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’atwa sikio.
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Juma Nature’.
Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga
kutomaindi lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa
Temeke amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la
biashara ya ndala au kandambili.
Kabla ya madai haya mapya, Nature
aliwahi kunukuliwa redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma
Ulete kuwa yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni. Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake la biashara.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa bila mafanikio. “Nature
amekuwa akimpigia simu Jokate lakini haipokelewi,” kilidai chanzo hicho
kwa sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu wa bastola.
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika
kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa
mrembo huyo kamuibia.
NATURE AFUNGUKA Alifunguka:
“Hadi sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu
wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.
“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya. “Kweli
sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate)
ila hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.“Nitakuja kuzitoa tu
hizo kandambili zenye picha na jina langu.”
Kandambili zilizosababisha mtifuano.
BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE Baada
ya kusikia upande mmoja wa Juma Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa
habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na kumsomea mashitaka yake
hayo ya kuiba wazo la biashara la Juma Nature. Bila kupepesa macho
wala kuchezesha masikio, Jokate alifunguka kwamba kwa upande wake
anasikitishwa na mtu kama Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu
anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake. “Wewe
siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo kutoka kwa Nature, niliamini baada
ya mimi kutoa hizo ndala, atanisapoti kwani mimi niko katika kuendeleza
na kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu letu la
maisha.
MASIKITIKO “Kweli Nature amenisikitisha sana kwa kitendo chake cha kunitangazia ubaya. “Hata
hivyo, siwezi nikaacha kutoa bidhaa zangu, nitaendelea kutoa ‘so’
itabidi tu anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za kwake,” alisema Jokate,
mmiliki wa lebo ya mavazi ya Kidoti.
MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA HILO? Wanahabari
wetu walizungumza na baadhi ya mastaa ambao walionesha kushangazwa na
sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na Nature kuhitilafiana wakati
kazi zao zinategemeana. “Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo
tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni watu ambao muda wowote wanaweza
kukutana kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema mmoja wa wanamuziki
wakubwa wa Bongo Fleva.
NATURE KAMGEUKA JOKATE? Kwa
mujibu wa mastaa hao, awali Nature aliposikia Jokate ana ‘aidia’ kama
hiyo alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii mwenzake hivyo kipato
atakachopata kitamsaidia maishani lakini kumbe inawezekana kimoyomoyo
ilimuuma ndiyo maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA Ni
vyema Jokate na Nature wakakaa na kukubaliana waifanye biashara hiyo
kwa pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa zaidi, ni kiasi cha kuona
SOME OF THESE CODES MIGHT NOT WORK FOR YOUR PHONE CUZ SOME WORK WITH S60 PHONES ONLY AND SOME FOR S60V3.
On the main screen type in *#06# for checking the IMEI (International Mobile Equipment Identity). *#7780# reset to factory settings. *#67705646# This will clear the LCD display(operator logo). *#0000# To view software version. *#2820# Bluetooth device address. *#746025625# Sim clock allowed status. #pw+1234567890+1# Shows if sim have restrictions. *#92702689# - takes you to a secret menu where you may find some of the information below: 1. Displays Serial Number. 2. Displays the Month and Year of Manufacture 3. Displays (if there) the date where the phone was purchased (MMYY) 4. Displays the date of the last repair - if found (0000) 5. Shows life timer of phone (time passes since last start)
*#3370#
- Enhanced Full Rate Codec (EFR) activation. Increase signal strength,
better signal reception. It also help if u want to use GPRS and the
service is not responding or too slow. Phone battery will drain faster
though. *#3370* - (EFR) deactivation. Phone will automatically
restart. Increase battery life by 30% because phone receives less signal
from network. *#4720# - Half Rate Codec activation. *#4720* - Half Rate Codec deactivation. The phone will automatically restart If you forgot wallet code for Nokia S60 phone, use this code reset: *#7370925538# Note, your data in the wallet will be erased. Phone will ask you the lock code. Default lock code is: 12345 Press *#3925538# to delete the contents and code of wallet.
[Answer] What does a hard reset really means? it means to reset your phone to the settings and features
which were accompanied from the company or at firmware update instant.
There are actually two codes you can use to reset the password and phone setting.
Below are these codes. Type them in the phone and this should solve your problem.
*2767*3855#
and
*2767*2878#
The security code will be reset to 0000.
This will allow you to format the phone easily.
================================================
Here some tutotial how unlock phone, this work on many models:
Follow those steps:
1.)*2767*3855#
2.)*7465625*638*00000000*00000000#
3.)#7465625*638*00000000#
Warning :by performing the hard reset will erase all fo personal data in internal storage, e.g. contact, message, reminder etc. Please do full backup first. To perform the hard reset on Samsung Galaxy Pocket GT-S5300, there's two methodes :
- First, input secret code methode : Go to dial pad and type *2767*3855#
- Use recovery mode methode :
Turn off the phone
Press & hold volume up + home button simultaneously, then power on the phone
Release volume up + home button if recovery menu appear
Scroll down to factory data reset menu, use volume down to navigate and home button to confirm.
Phone will automatically restart and now the phone is on factory state.
or
our device freezes or has fatal errors
If your device freezes or hangs, you may need to close programs or reset the device to regain functionality. If your device
is frozen and unresponsive, press and hold [POWER] for 8-10 seconds,
the device will reboot automatically or pull out the battery and then
reinsert it. Replace the back cover and power on the device.
If this does not solve the problem, perform a factory data reset. In Idle mode, open the application list and select Settings → Privacy → Factory data reset → Reset phone → Erase everything.
or Factory Format by entering S5300 RESET CODE
Use
this method to hard reset your Samsung Galaxy Pocket S5300 phone: Enter
*2767*3855#. Warning! All your data including contacts, messages etc.
will be lost! Copy all your necessary data/Contacts/Messages etc. to SIM
or make backup to your PC before full reset! Take out SIM card before
full reset. When disposing of your device, back up all data and then reset your device to prevent misuse of your personal information.
SIKU
moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (UKAWA) warudi bungeni akidai hawana sababu ya kwenda
kushitaki kwa wananchi kwa sababu watawacheka na kuwasikitikia, umoja
huo umemjibu wakisema wapo tayari kuchekwa.
Akihutubia
vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi, siku moja kabla ya sherehe za
miaka 50 ya muungano, Rais Kikwete alisema kuwa huko nje wanakotaka
kwenda UKAWA siko na siku yake sio sasa, hivyo akawaomba wasipoteze
fursa hiyo muhimu ya kutoa mawazo yao bungeni ili yafanyiwe kazi.
Alisema wananchi hawahusiki wala hawana namna ya kuwasaidia kwani mengi ya hayo yanayowakasirisha ni matatizo waliyoyazusha wao.
Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa kama
Kikwete anafikiri kwamba watarudi bungeni kwenye mijadala ya dharau,
ubaguzi na matusi inayofanywa na wajumbe wa CCM, basi hajui chimbuko la
tatizo.
"Kadiri
anavyoendelea kuliacha Bunge liendelee na mijadala ya kibaguzi na
matusi, taifa linazidi kupasuka na washauri wake hawamwelezi tatizo
hilo," alisema.
Mbowe
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini atalitumbukiza
taifa kwenye machafuko ingawa yeye anafanya utani kwa kuipasua nchi na
kushangilia kauli za kibaguzi, kejeli na matusi zinazotolewa na baadhi
ya wajumbe wa CCM.
"Rais
na wasaidizi wake inaelekea hawajasikiliza hata kauli zinazotolewa na
viongozi wa dini kuhusu rasimu ya Warioba, atuache twende kwa wananchi,
wao ndio wataamua. Tumevumilia kwa kiwango fulani, lakini itafika mahali
uvumilivu utaisha, kwani hatuwezi kuendelea kuzuiliwa kufanya mikutano
na jeshi la polisi wakati mikutano ya CCM inafanyika kote nchini
kutuchafua," alisema Mbowe. CHANZO: TANZANIA DAIMA
RAIS
Jakaya Kikwete amehujumiwa na viongozi wakuu wastaafu waliomlazimisha
kuachana na msimamo wa muundo wa muungano wa serikali tatu na kukumbatia
serikali mbili zilizopendekezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa
kutoka kwa baadhi ya vyanzo vya habari vilivyo karibu na rais, Ikulu na
makao makuu ya CCM, zimelithibitishia kwamba hadi Bunge Maalumu la
Katiba linaanza, Rais Kikwete alikuwa na msimamo ule ule wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi
ya viongozi wastaafu, wakiwamo marais na viongozi waandamizi wa CCM,
walishinikiza rais aachane na serikali tatu, kwa vitisho kwamba zitaua
muungano.
Baadhi
ya wastaafu hao walimficha Rais Kikwete kwamba kwa kuwa yeye aliingia
madarakani akiwa rais wa muungano wa serikali mbili, halikuwa jambo la
busara kwake kujiingiza kwenye historia ya kuwa rais aliyevunja
muungano.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu, shinikizo hilo liliambatana na jingine la
kumtaka asizindue Bunge kabla ya rasimu ya pili ya katiba mpya
kuwasilishwa bungeni, ili apate fursa ya kudhoofisha hoja ya serikali
tatu.
Mara
baada ya Rais Kikwete kukubaliana na "washauri wake", serikali
ililazimika kuingilia kati ili Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta atengue
kanuni, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba awasilishe rasimu kabla
ya rais kuzindua Bunge, jambo ambalo limesababisha mvurugano unaotishia
kuvuruga kabisa mchakato wa katiba mpya.
Hata
hivyo, hali hiyo inasemekana kumnyima amani Rais Kikwete ambaye ndiye
aliyepokea na kusaini rasimu hiyo, kwa maana kwamba aliridhia.
Uamuzi huo umefanya rais aonekane kiongozi asiye na msimamo thabiti katika masuala muhimu.
Baadhi
ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai hatua hii imemfanya
ashindwe kuacha urithi makini na muhimu katika utawala wake wa miaka 10,
kama ambavyo alikuwa amedhamiria.
Wadadisi
wanasema wastaafu walimzuia rais kutekeleza azima yake kwa sababu ya
hofu tu, wakidhani kwamba katiba mpya yenye mfumo mpya inaweza kufumua
mambo yaliyofichika na kuwaingiza matatani.
Wanadai
kwamba muungano wenye mfumo mpya una kila dalili za kuiondoa CCM
madarakani, na kuhatarisha maslahi ya watawala waliopo na waliopita.
Hoja hii, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, ndiyo ilimkuna Rais Kikwete hata akabadili msimamo.
Kwa hali halisi ilivyo, na mchakato unavyoendelea, ahadi ya Rais Kikwete kuwapa Watanzania katiba mpya mwezi huu imeshindikana.
Alipohutubia
taifa na kutangaza kuanzisha mchakato wa katiba mpya miaka mitatu
iliyopita, alisema kwamba lengo lake lilikuwa kuzindua katiba mpya
katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya muungano iliyofanyika jana.
Hadi
Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa juzi, zilikuwa zimepita siku 68
kati ya 70 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, huku kukiwapo
mgawanyiko mkubwa wa wajumbe na kutishia uhai wa muungano, hasa baada ya
wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia Bunge
baada ya kukerwa na hujuma na matusi kutoka kwa wajumbe wenzao wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Hadi
sasa Bunge la Katiba limefanikiwa kujadili sura mbili za rasimu bila ya
kuzipigia kura. CCM imekataa maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
yanayopendekeza mfumo wa muungano wa serikali tatu, wakatetea mfumo wa
serikali mbili.
Mapendekezo
hayo ni kinyume kabisa cha yaliyomo kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba iliyowasilishwa ili ijadiliwe na wajumbe hao na kisha kutunga
katiba mpya.
UKAWA
wanadai kuchoshwa na vitisho na matusi kutoka kwa wajumbe wa CCM na
viongozi wa serikali, wakisema kuwa kwa hali ilivyo katiba bora ya
wananchi haiwezi kupatikana kwa shinikizo la muundo wa serikali mbili.
Katika
hili, Rais Kikwete analalamikiwa kuwa ndiye mvurugaji wa kwanza wa
mchakato ambao aliuasisi na kuahidi kuwapatia wananchi katiba bora kabla
ya kuondoka madarakani.
Wakati
akilihutubia Bunge la Katiba na kulizindua rasmi Machi mwaka huu, Rais
Kikwete aliibeza rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, akisema takwimu zao
kuhusu watu waliotoa maoni ya muundo wa muungano zinatiliwa shaka.
Alisema
kuwa muundo wa serikali tatu unaopendekezwa hautekelezeki kwani rais wa
dola hiyo hatakuwa na mamlaka kwa vile hana ardhi, rasilimali na hivyo
hataweza kukopa.
Kwa
mujibu wa Rais Kikwete, katika hali kama hiyo, jeshi linaweza kupindua
serikali na hivyo ukawa mwanzo wa kuvunjika kwa muungano, huku
akisisitiza kwamba wao kama CCM muundo ambao unaweza kutatua kero
zilizopo ni ule wa sasa wa serikali mbili.
Kauli
hiyo ya rais iliibua mjadala mkubwa, na hivyo kufifisha ndoto za
kupatikana kwa katiba bora kwani ilionyesha wazi kwamba mapendekezo ya
wananchi ya serikali tatu yaliyomo kwenye rasimu hayatazingatiwa.
Hali
hiyo imeendelea kujitokeza kwenye Bunge Maalumu la Katiba baada ya
wajumbe wote wa CCM kuendeleza msimamo wa rais wa serikali mbili na
kumshambulia Jaji Warioba binafsi kwa matusi mazito wakidai ana ajenda
ya kuvunja muungano kwa kupendekeza serikali tatu.
Hatua
ya Rais Kikwete kubadilika na kuvuruga mchakato aliyouasisi na
kuusimamia kwa mafanikio makubwa, imeelezwa kusababishwa na mambo
makubwa mawili, likiwemo hilo la kuburuzwa na viongozi wastaafu.
Duru
nyingine za kisiasa katika suala hilo la kukwama kwa mchakato wa
katiba, zinahusisha na rasilimali ya gesi na mafuta zilizopatikana
nchini, ambapo inadaiwa mataifa makubwa yanayotaka kuwekeza ndiyo
yanaishinikiza serikali isibadili muundo wa muungano uliopo.
Vyanzo
vyetu vya habari vinaeleza kwamba mataifa hayo tayari yameweka msimamo
wa kuisaidia CCM kifedha ili kuhakikisha inapigana kufa au kupona
kutobadili muundo wa muungano katika katiba mpya.
Inaelezwa
kuwa muundo wa shirikisho la serikali tatu unaopendekezwa kwenye rasimu
ya katiba mpya, unatoa fursa ya wazi kwa wananchi wa serikali washirika
kusimamia rasilimali zao tofauti na ilivyo katika muundo wa sasa ambapo
mambo mengi yamefanywa siri na serikali.
Hadi
sasa majaliwa ya kupatikana kwa katiba mpya yametoweka baada ya UKAWA
kujiondoa, na hivyo kulifanya Bunge la Katiba kushindwa kufanya maamuzi
ya kupitisha ibara na sura za rasimu kutokana na theluthi mbili ya
wajumbe kutoka Zanzibar kushindikana. Chanzo Tanzania Daima.
(CCM) kimepanga mkakati wa kuengua wataka urais wanaume.
Na Hudugu Ng'amilo
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais
wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti
aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena
nafasi hiyo mwaka 2010.
Wachunguzi
wa masuala ya kisiasa wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa mkakati
huo unalenga zaidi kumng'oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye
anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais.
Kwa
mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete,
wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee
urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
Kisingizio wanachotumia katika kampeni yao ya siri, ni kusaka kura za wanawake.
Katika
mkakati huo, wanamwandaa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kuwa
Waziri Mkuu. Tayari Membe ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge mwaka
2015.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu, Membe ndiye alikuwa akipigiwa chapuo zaidi
miongoni mwa makada wa CCM ili kurithi mikoba ya Rais Kikwete, lakini
kutokana na uhusiano wa kifamilia uliopo baina ya wawili hao, sasa
ameshawishiwa kuwa atakuwa waziri mkuu endapo Dk. Migiro atashinda.
Wiki
hii, gazeti dada la Tanzania Daima Jumatano liliripoti mkakati wa
kumzima Lowassa asigombee urais, ambao unaendeshwa na mtoto wa kigogo
akishirikiana na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Dk.
Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, na pia Mkurugenzi
wa Idara ya Mahusiano ya Nje wa CCM, tayari ameanza kuzungushwa mikoani
ili kumjengea uwezo na uzoefu wa kisiasa.
Miongoni
mwa wana CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015 mbali na Lowassa na Membe,
ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Mahusiano), Stephen Wasira, William Ngeleja na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
"Ukiwalinganisha
Membe na Lowassa kwa nguvu na umaarufu ndani ya CCM, hata vigogo
wengine wanaotajwa kuutaka urais, utaona hakuna wa kumshinda Lowassa,
sasa ndani ya chama wameamua kumchezea rafu.
"Kwa
vile ana mtandao mrefu ndani ya CCM, wanafahamu wakikata jina lake
itakuwa balaa, hivyo wameona waibuke na hoja ya zamu ya wanawake kama
walivyomzima Samuel Sitta asigombee uspika wakampa Anne Makinda,"
alisema mtoa habari wetu.
Chanzo
hicho kinaongeza kuwa mlengwa ni mtoto wa kigogo ambaye anaendesha
mkakati wa kumchafua Lowassa ili 2025 ndiye awe mgombea urais baada ya
Dk. Migiro kumaliza uongozi wake endapo atachaguliwa kwa vipindi viwili.
Pamoja
na mkakati huo, kundi la Membe limeshauriwa kuendelea na harakati za
kujiimarisha ili kuhadaa makundi mengine ndani ya chama yaamini kwamba
naye ni miongoni mwa watakaochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania
urais.
Hata
hivyo, wakati CCM ikiendesha mkakati huo dhidi ya Dk. Migiro ambaye
amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, baadhi ya wasomi wamemchambua mwanamama huyo wakisema hana
uwezo huo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod
Slaa, alisema kuwa Dk. Migiro haonekani kubadilika licha ya kuwa na
elimu kubwa.
"Nilimtembelea
ofisini kwake akiwa UN kama Naibu Katibu Mkuu, nilikuwa na kazi za
kitaifa kabisa kwa masuala yaliyoshirikisha mabalozi wa Ulaya, lakini
aliponiona aliniuliza kwanini sitaki kurejea CCM.
"Huyu
hawezi hata kubaini hapa tunazungumzia masuala ya kitaifa au kimataifa,
yeye akili yake inawaza CCM tu kila wakati, hajaonyesha kutofautisha
u-CCM wake na taaluma ili aweze kusaidia katika nyanja za kitaifa na
kimataifa," alisema.
Dk.
Slaa aliongeza kuwa aliposikia kuwa Dk. Migiro ndiye aliyeandaa rasimu
ya kwanza na ya pili ya katiba kwa upande CCM ambazo zinaleta shida kwa
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba zikikinzana na rasimu ya Tume ya Jaji
Warioba, amedhihirisha kabisa udhaifu wake.
"Ukiangalia
rekodi zake akiwa UN, huwezi ukaona matokeo yoyote, ndiyo maana Ban Ki
moon hakutaka tena asaini mkataba kwa awamu nyingine kwani hakuwa na
msaada kwake," alisema Dk. Slaa.
Dk.
Azavery Lwaitama ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bukoba ambaye alisema
kuwa Dk. Migiro sio mtu mwenye umaarufu wowote ambao unaweza kumfanya
amweke katika orodha ya watu wanaoweza kuwa viongozi wa nchi hii.
"Aliteuliwa
kuwa Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, akafanya kazi kipindi kifupi na
baadaye akafanywa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa awamu ya Rais
Kikwete.
"Kutokana
na kunong'onezana kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon
na Rais Kikwete, Dk. Migiro aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa na baadaye kwa utaratibu huo huo wa kunong'onezana
akarejeshwa tena nchini," alisema.
Dk.
Lwaitama aliongeza kuwa vyombo vya habari vya nje viliandika vizuri
kuhusu uwezo wa Dk. Migiro wakati akiwa Umoja wa Mataifa, lakini
Watanzania hawakujishughulisha kuangalia yaliyoandikwa.
"Nilitarajia
kuwa yeye atakuwa na mawazo tofauti katika mjadala wa rasimu iliyopo
bungeni, lakini amerudi kwa wana CCM wenzake, anafikiri kama wao,
analeta ushabiki wa makundi ya kisiasa, kwa utaratibu huo hawezi kuwa
kiongozi anayefaa," alisema.
Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye ni mwanafunzi wa Dk.
Migiro, alisema haoni dalili au uwezo wowote wa yeye kuwa kiongozi
katika wadhifa huo mkubwa wa urais.
"Huyu hajawahi kushiriki uchaguzi wowote akashinda, ukiwemo hata ubunge, isipokuwa nafasi za kuteuliwa ambazo hupewa na marais.
"Angalia
kwa mfano katika Bunge hili la katiba ametoa mchango gani wa kukumbukwa
na wananchi licha ya kuchangia na kubaki katika Bunge linalotoa matusi
na kuacha kujadili rasimu?" alisema Lissu.
Waziri mkuu nchini Korea Kusini
amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la
ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita. Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake. Bwana Chung alizomwa alipozitembelea
familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya
kuzama katika hali ya kutatanisha. Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji
katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani
waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika
ziara ya shule. Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama. Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.