Sunday, 26 October 2025

MRADI WA WLER WAIBUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU GONGO LA MBOTO



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANAWAKE wa Kata ya Gongo la Mboto wamehamasishwa kushiriki katika nafasi za uongozi na kujiimarisha kiuchumi kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) baada ya kufanya tathimini ya mradi wa Women’s Leadership and Economic Rights (WLER) unaoratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNWOMEN

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2025 Jijini Dar es Salaam, Muweka Hazina wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa cha kata hiyo, Bi. Hajra Mbwambo amesema kufanya tathimini kumewapa nguvu ya kuibua na kuwaandaa wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii badala ya kubaki nyuma kwa hofu au utegemezi.

“Wanawake wengi tulikuwa tunajiona hatuwezi. Kufanya tathimini imetusaidia kujitambua na sasa wengi wameingia kwenye biashara, licha ya kuwa mitaji ni midogo,” amesema.

Hata hivyo, alitaja urusimu katika upatikanaji wa mikopo kama kikwazo kinachowakatisha tamaa wanawake wanaotaka kujitegemea kiuchumi.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa kituo hicho, Bw. Humphrey Mgeta, amesema waliendesha uhamasishaji kupitia makundi ya bodaboda, wanafunzi na akinamama ili kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki katika nafasi za maamuzi.

“Awali wanawake walikuwa waoga kugombea au hata kupiga kura kwa maamuzi yao, lakini sasa tunayaona matokeo. Ushawishi umeanza kuzaa viongozi wanawake katika ngazi ya jamii,” amesisitiza.

Licha ya mafanikio yaliyopatikana nchini Tanzania yakiwemo kuchaguliwa kwa Rais mwanamke kwa mara ya kwanza wanawake wengi bado wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na mfumo dume, umaskini, na ubaguzi wa kijinsia.

Ukatili wa kijinsia kama ndoa za utotoni na mimba za utotoni zinaendelea kuwa kikwazo kwa elimu ya wasichana, jambo linalowazuia wanawake kupata fursa za kiuchumi na nafasi za uongozi katika jamii.

Wanawake, hasa wanaoishi vijijini, wanakumbwa na changamoto za kumiliki ardhi, kupata mikopo, mafunzo ya ujuzi na teknolojia, huku majukumu ya kazi zisizolipwa za malezi yakipunguza ushiriki wao katika maisha ya kijamii na kisiasa.

Katika kukabiliana na changamoto hizi, Mradi wa WLER umejikita katika kuimarisha ushiriki, uongozi, na haki za kiuchumi za wanawake na wasichana katika ngazi za jamii kwa kubadilisha mitazamo na desturi kandamizi za kijinsia.

Nae Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka TGNP Mtandao, Bi. Clara Godson amesema mradi wa WLER umejengwa juu ya mafanikio ya miradi ya awali na tayari umechangia mabadiliko kwenye jamii.

“Tunaona serikali za mitaa zikipanga bajeti zinazoangalia masuala ya kijinsia, huduma kwa watu wenye ulemavu zimeongezeka, na ajenda za usawa wa kijinsia sasa zinajadiliwa kwenye mipango ya maendeleo,” amesema.

Mradi wa WLER unatekelezwa kwa kushirikiana na UN Women na LGTI, ambapo zaidi ya watu 40,000 wamenufaika moja kwa moja kupitia mafunzo, uhamasishaji na mikakati ya usawa wa kijinsia tangu mwaka 2023.
Share:

ELIMU, HAMASA NA UWEZESHWAJI WA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA WASHIKA KASI MTWARA


-Wananchi waipokea kwa kishindo

-Klabu za Nishati Safi ya Kupikia zaanzishwa mashuleni

-Walimu na Wanafunzi waipongeza REA waahidi kuwa mabalozi

-Lengo ifikapo 2034; 80% ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika kila kona ya Nchi ili kuhakikisha ustawi wa wananchi kupitia matumizi endelevu na salama ya nishati safi ya kupikia.

Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Daniel Mwandupe wakati wa kampeni ya uelimishaji na uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Shule ya Sekondari Mbawala Wilayani Mtwara Mkoa wa Mtwara.

“Leo hii tumefika hapa kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuleta mabadiliko ya fikra na tabia katika jamii kwa ujumla; REA imedhamiria kuona wananchi wanaongeza uelewa wa faida zinazopatikana kwa kutumia nishati safi,” alifafanua Mha. Mwandupe.

Mha. Mwandupe alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni ya nishati safi ya kupikia hasa ikizingatiwa kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta hiyo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Jaina Msuya alisema dhamira ya kuanzisha Klabu ya Nishati Safi ya Kupikia shuleni hapo ni kuongeza hamasa kwa wanafunzi ili waweze kutambua umuhimu wake sambamba na kuongeza ushiriki wao katika kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Leo hii tumezindua rasmi Klabu ya Nishati Safi ya Kupikia hapa shuleni na tumetoa zawadi ya jiko banifu kwa Klabu na pia tumejadili masuala mbalimbali na tumeona namna ambavyo wanafunzi wamehamasika na hii ni dalili njema kwamba tutafanikiwa kwa kishindo kufikisha lengo la Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia,” alisisitiza Jaina.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbawala, Amina Mtuvenge aliishukuru na kupongeza REA kwa kufika shuleni hapo kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo.

“Tumeelezwa uwepo wa mpango maalum unaoandaliwa na REA wa uwezeshwaji kwa taasisi zinazoandaa chakula na kulisha zaidi ya watu 100 kwa siku kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, taarifa hii tumeipokea vyema na tumehamasika kuchangamkia fursa hii mapema iwezekanavyo ili tubadilishe aina ya nishati tunayotumia kupikia hapa shuleni,” alisisitiza Mwalimu Mtuvenge.

Aidha, kwa nyakati tofauti wanafunzi waliipongeza REA kwa ubunifu inaoufanya na waliahidi kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia majumbani mwao na kwa jamii zinazowazunguka.
Share:

CCM KINAKWENDA KUIFUNGUA RUFIJI KWA KUKAMILISHA BARABARA, MADARAJA- MCHENGERWA


Na Yohana Kidaga- Ngorongo, Rufiji

Mgombea wa Ubunge jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kumchagua tena katika kipindi atahakikisha anaiomba Serikali iweze kukamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Mkongo, Ngorongo hadi Ikwiriri kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya CCM ili kuifungua Wilaya ya Rufiji na mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kukiombea kura Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu kwa ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika Kijiji cha Kilimani kata ya Ngorongo jimboni Rufiji, ambapo pia aliwapokea wanachama kadhaa kutoka upinzani, Mhe. Mchengerwa amesema pamoja na kwamba tayari CCM kimefanya mambo makubwa kwenye ujenzi wa miundombinu ambao umehusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na taa za umeme, madaraja makubwa ya kisasa, stendi na masoko lakini bado atahakikisha wananchi wa kata Ngorongo wanajengewa barabara ya kisasa ya kiwango cha lami.


"Ndugu zangu naomba niendelee kuwahakikishia kuwa kama mgombea Urais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi Oktoba 20, kwenye mkutano wake wa kampeni pale Ikwiriri kwamba atahakikisha Serikali inakamilisha kazi nzuri iliyoanza ya ujenzi wa barabara basi mimi kama Mbunge na mtumishi wenu nitahakikisha nasimamia utekelezaji wa ahadi za Mhe. Rais kwa masilahi mapana ya Wanarufiji na watanzania kwa ujumla". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Amefafanua kuwa katika kipindi chake alipokea jimbo likiwa hakuna hata nusu kilomita ya barabara ya kiwango cha lami lakini sasa mitaa yote ya Ikwiriri na barabara za kila kona za Wilaya ya Rufiji zimeanza kutengeneza kilichobaki ni kumaliziwa tu.
Kuhusu madai ya kunyang'anywa ardhi ya Kijiji cha Kilimani, Mhe. Mchengerwa amewahakikishia wananchi wa kata ya Ngorongo kuwa hakuna mtu anayeweza kutwaa ardhi ya Kijiji hicho bila taratibu za kisheria na kwamba tayari jambo hilo lilishajadiliwa na vikao vya madiwani na kupatiwa ufumbuzi hivyo hakuna sababu ya kuwa na mashaka kwani tayari limeshafanyiwa kazi.

Aidha, amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Ngorongo kwa kuendelea kukiamini CCM na yeye binafsi kutoa kura nyingi bila kutaka kupewa rushwa ili wakipigie kura.
"Kwa dhati ya moyo wangu ninawashukuru wana Ngorongo kwa heshima mnayoendelea kutoa kwa CCM na kwangu binafsi kwa kupiga kura nyingi kwenye kila uchaguzi kwa kuzingatia kazi kubwa tuliyoifanya ni matumaini yangu pia kwenye uchaguzi huu mtapiga kura nyingi za heshima kwa CCM, ahsante sana". Ameshukuru Mhe. Mchengerwa

Amewaomba watu kujitokeza siku ya kupiga kura bila hofu yoyote na kuitumia haki yao ya kikatiba kupiga kura kwa amani na kusuburi matokeo majumbani.

Mhe. Mchengerwa anaendelea na mikutano ya hadhara katika kata nyingine za Jimbo hilo kuomba kura kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa madiwani na kwake mwenyewe ili apewe ridhaa ya kuwaongoza tena katika kipindi hiki.

Mhe. Mchengerwa ni Mbunge wa tisa wa kuchaguliwa katika jimbo hilo la Rufiji toka lianzishwe na kuongozwa na wabunge kadhaa kuanzia Mhe. Bibi Titi Mohamed ambapo anaelezewa kuwa ni miongoni mwa wabunge walioliletea maendeleo makubwa Jimbo hilo ukilinganisha na wabunge waliotangulia.

Licha ya kuwa Mbunge wa tisa wa Jimbo hilo, Mhe. Mchengerwa ni miongoni mwa wanasiasa wachache nchini ambao wamehudumu kwenye mihimili yote katika nafasi za juu za uandamizi.

Akiwa kwenye mkutano wa kampeni zake alioufanya Ikwiriri, Mgombea wa Urais, mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alimwelezea Mhe Mchengerwa kuwa amefanya kazi nzuri katika Wizara zote nne alizomteua kuhudumu kwenye kipindi chake cha uongozi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 26,2025

 

Magazeti 

     

 


Share:

Saturday, 25 October 2025

HAMZA TANDIKO AENDELEA KUWASHA MOTO WA KAMPENI... AOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI 'KUTIKI' KWA WAGOMBEA WA CCM OKTOBA 29

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 24,2025


Magazeti
   

 

  

   

 







  
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger