Wednesday, 30 July 2025

CCM YAMPITISHA JACKLINE ISARO KUGOMBEA UDIWANI KATA YA NGOKOLO


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kikao chake cha imepitia na kujadili majina ya wanachama waliowasilisha maombi ya kupitishwa kushiriki katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.

Miongoni mwa waliopitishwa ni Kada wa CCM, Jackline Isaro, ambaye sasa amepewa baraka za chama kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata ya Ngokolo, iliyopo katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia tiketi ya CCM.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 30,2025




Magazeti



Share:

SUZANA NUSSU AVUNJA UKUTA! CCM YAMPITISHA KUGOMBEA UBUNGE UKEREWE


Mwanasiasa machachari na mmoja wa wanawake wachache waliopenya katika mchujo wa CCM, Susana Kululelela Nussu, ameidhinishwa rasmi na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kushiriki kura za maoni kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Ukerewe.

Susana, ambaye anaungwa mkono na wafuasi wengi jimboni humo, anatarajiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kisiasa dhidi ya wagombea sita wa kiume, hatua inayoashiria pambano kali la ndani ya chama. Wagombea wengine waliopitishwa ni: Dk. Switbert Zacharia Mkama, Joseph Michael Mkundi, Dk. Laurian Salvatory Mganga, Joshua Bituro Manumbu, Leonard Mujola Babilasi na Japhet Mtyama Kasiri.

Jimbo la Ukerewe limekuwa likibadilika mara kwa mara katika uwakilishi wake bungeni. Hata hivyo, mchakato wa mwaka huu unaleta sura mpya na ushindani mkali kati ya viongozi wapya na wale waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini na ndani ya chama.

Kwa Susana, nafasi hii ni mwanzo wa safari kubwa kisiasa. Endapo atashinda kura za maoni na kuungwa mkono na wajumbe wa CCM, atavunja historia kwa kuwa miongoni mwa wanawake wachache waliowahi kupeperusha bendera ya CCM katika kisiwa cha Ukerewe, eneo lenye historia ndefu ya siasa na mvuto wa kipekee.

Share:

Tuesday, 29 July 2025

DKT. YONAZI AWAASA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU KUONGEZA BIDII NA UBUNIFU KATIKA UTENDAJI




Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, ametoa wito kwa watumishi wa ofisi hiyo kuongeza bidii, nidhamu na weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya Taifa.

Dkt. Yonazi alitoa rai hiyo Julai 29, 2025, wakati akifungua mkutano na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, akisisitiza umuhimu wa mshikamano, ubunifu na utendaji kazi kwa viwango vya juu, ukizingatia kuwa huduma wanazotoa zinagusa maisha ya mamilioni ya Watanzania.

“Tunaposhirikiana, tunajenga nguvu ya pamoja ambayo hakuna changamoto inayoweza kutuzuia. Nawaomba tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo mmoja. Kumbukeni kuwa kila mchango wenu una thamani kubwa katika kufanikisha malengo ya ofisi yetu na Taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Yonazi.

Aidha, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na kushughulikia changamoto zinazohusu maslahi ya wafanyakazi. Pia, italenga kukuza ubunifu, kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa maendeleo ya kazi na kuhakikisha kila mtumishi anawajibika ipasavyo.

Mkutano huo pia umewapa watumishi fursa ya kupata elimu kutoka kwa wataalam wa Mfuko wa Uwekezaji wa UTT kuhusu umuhimu wa kuwekeza. 

Vilevile, watumishi wanapewa mafunzo kuhusu uzingatiaji wa maadili ya utumishi wa umma, afya, hususan kinga dhidi ya homa ya ini na magonjwa yasiyoambukizwa.





Share:

MAJINA YA WAGOMBEA CCM BADO NI KITENDAWILI




Dotto Kwilasa, Dodoma

Mchakato wa kutangaza rasmi majina ya wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaoongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, umeendelea kusogezwa mara kadhaa huku waandishi wa habari wakilazimika kukesha katika Ukumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Awali, kikao hicho kilipangwa kufanyika jana, Julai 28, 2025, saa 11 jioni, lakini kikasogezwa hadi usiku wa manane kwa madai ya kukamilisha taratibu za ndani za chama. Waandishi wa habari waliokuwa wamefika mapema kwa ajili ya kufuatilia matangazo hayo walilazimika kusubiri hadi saa 10 alfajiri bila mafanikio ya kupata majina.

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, waandishi walipewa taarifa kwamba tangazo hilo lingefanyika tena leo, Julai 29, saa 4 asubuhi, jambo lililowalazimu kurejea kwenye maeneo ya mkutano kwa matarajio mapya. Hata hivyo, muda huo ulipofika, kikao kilisogezwa tena na kuahirishwa hadi saa 6 mchana.

Taarifa kutoka ndani ya chama zinaeleza kuwa kucheleweshwa kwa matangazo hayo kunatokana na mchakato wa kuhakikisha majina ya wagombea yanapitishwa kwa umakini, ikiwa ni pamoja na kupitia mapendekezo ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM yaliyokamilika usiku wa kuamkia leo.

CPA Amos Makalla anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo mchana mara baada ya vikao vya ndani kukamilika, na kuwatangaza wagombea wa Ubunge wa Majimbo, Viti Maalum vya Ubunge na Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Zanzibar.

Hali ya kusubiri kwa muda mrefu imezua taharuki miongoni mwa waandishi wa habari na wadau wa siasa huku wengi wakitaka kujua hatma ya wagombea waliopitishwa na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Pamoja na kucheleweshwa kwa hatua hiyo, viongozi wa CCM wameendelea kuwahakikishia wanachama na wananchi kwamba mchakato huo utazingatia misingi ya demokrasia ya chama na kuleta wagombea bora watakaoleta ushindi wa kishindo.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 29,2025

Magazeti
 

Share:

Monday, 28 July 2025

NILIPIGWA CHARACTER DEVELOPMENT, LAKINI MAOMBI MAALUM YALINIPA MPENZI WA KUDUMU


Kuna wakati katika maisha yangu nilihisi kama mapenzi yalikuwa laana tu juu yangu. Kila mara nikipenda, nateseka. Nikiwa chuoni nilikuwa na mpenzi ambaye nilimchukulia kama mchumba wangu wa baadaye. Nilimheshimu, nilimpenda, na nilimjengea ndoto za maisha mazuri pamoja.

Lakini baada ya miaka miwili ya mahusiano ya dhati, siku moja alipokea kazi nje ya jiji. Nilimpa baraka zangu zote. Ndani ya wiki mbili alinitumia ujumbe mfupi tu: “Nadhani huu ndio wakati wa kila mtu aendelee na maisha yake.” Soma zaidi
Share:

MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP - DKT. MATARAGIO


📌Yanahusisha ushiriki wa ajira kwa wazawa, mapato kwa nchi na utoaji huduma EACOP

📌 Atembelea ujenzi wa kiwanda cha kuweka mifumo ya upashaji na utunzaji joto kwenye mabomba ya EACOP kilichoko Sojo

📌 Apongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa utashi wake kutekeleza mradi wa EACOP

📌 Dola za kimarekani Bilioni 5.65 kutumika ujenzi wa bomba la EACOP hadi kukamilika

Na Neema Mbuja, Nzega

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Mafuta na Gesi Wizara ya Nishati, Dkt James Mataragio, amesema utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)  unazingatia maslahi mapana ya nchi ikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wazawa, kuongezeka kwa pato la Taifa na ushirikishwaji wa kampuni za wazawa kutoa huduma kwenye utekelezaji wa mradi wa EACOP.

Dkt.  Mataragio ameyasema hayo leo tarehe 28 Julai, 2025 wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kutembelea na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa EACOP hususani utekelezaji wa makubaliano kwenye mradi huo.

Akiwa kwenye kiwanda cha kuweka mifumo ya upashaji na utunzaji wa joto(Thermal Insulation System )Dkt.Mataragio alijionea namna mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga yanavyoandaliwa na kuwekwa teknolojia maalumu ya kudhibiti kutu eneo la Sojo wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora.

‘’ Wizara ya Nishati ndio mwenye dhamana ya kusimamia maslahi ya Serikali chini ya TPDC na tumeridhika na maendeleo ya utekelezaji wa mradi  kwa kuzingatia sheria na mikataba iliyopo, ambapo mpaka sasa fedha zote za mradi wa EACOP zimepatikana kwa asilimia mia moja’’ Amesema Dkt Mataragio

Ameongeza kuwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki unaendelea kwenye mikoa ya Kagera, Geita, Tabora,Singida,Dodoma,Manyara,na Tanga na utahusisha pia ujenzi wa vituo 4 vya kuongeza msukumo wa mafuta(Pump Stations) na vituo viwili vya kupunguza msukumo wa mafuta(Pressure reduction Stations) ambao umekamilika kwa asilimia 55

‘’ Ujenzi wa bomba la Mafuta ghafi la EACOP kwa sasa umefikia asilimia 65  na utagharimu kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 5.65 na jambo la kufurahisha ni kwamba ajira za wazawa takribani 9,194 zimezalishwa katika kipindi cha ujenzi wa mradi  na kati ya hizo asilimia 75 zimenufaisha wazawa’’ Amesistiza Dkt Mataragio

Amesema mpaka sasa jumla ya shilingi bilioni 60 zimepatikana kutokana na manufaa ya utekelezaji wa mradi wa EACOP ikiwemo 
Makusanyo ya pango la ardhi, ushuru wa huduma na usajili wa vibali mbalimbali kwenye halmashauri.

Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki unatekelezwa na nchi mbili za Tanzania na Uganda ambapo kila moja ina hisa asilimia 15, ambapo UNOOC ya China asilimia 8 na Total Energies asilimia 62 ambapo mradi unatarajia kukamilika mwezi Julai, 2026.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger