Sunday, 29 September 2024
KATAMBI ATOA MATUMAINI KWA WALEMAVU (VIZIWI), AHIMIZA MATUMIZI YA LUGHA YA ALAMA KILA KONA
Na. Mwandishi wetu: Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa kuwa na lugha moja ya alama ili kuwezesha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo.
“Serikali imeendelea kuimarisha matumizi ya Lugha ya Alama kwa kuchukua hatua za muda mfupi, kati na mrefu. Hatua za muda mfupi ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watoa huduma katika Sekta mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa mafunzo kwa watoa huduma za Afya, Maafisia Ustawi wa Jamii, Walimu wa Shule ya Msingi na sekondari“ amesema.
Mhe. Katambi amebainisha hayo Septemba 28, 2024 katika Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye Uwanja wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga, ambayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo “TUMIA LUGHA YA ALAMA KUTIMIZA HAKI YA LUGHA YA ALAMA.”
Aidha, amelitaka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ikamilishe mwongozo wa Wakalimani wa Lugha ya Alama ambao utachangia kukua na kuenea kwa lugha ya alama pamoja na tasnia ya ukalimani.
Vile vile, ametoa rai kwa vyombo vya habari vya kitaifa vinapotangaza matukio ya kitaifa na taarifa za habari kuhakikisha Wanakuwa na Wakalimani wa lugha ya alama, Wizara na Taasisi kuchukue hatua ya kuwapeleka Watumishi kwenda kupata mafunzo ya muda mfupi ya Lugha ya Alama.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Selina Mlemba ameipongeza serikali kwa kuendelea kutambua umuhimu wa lugha ya alama na hivyo kutenga siku maalumu kwa ajili ya siku hiyo Pamoja na kutenga fungu kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu.
Naye, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP) Ghati Horombe, amesema Shirika hilo linathamini na kutambua juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu na serikali kwa ujumla katika kuhakikisha ujumuishwaji kijamii, kisiasa, kiuchumi na upatikanaji wa haki, kwa Watu wenye Ulemavu.
MZEE WA UBWABWA ATETEA NAFASI YAKE YA UENYEKITI CHAUMMA
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashimu Rungwe amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa chama hicho taifa kura 118 kati 120 katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar Essalam.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Mohamed Masoud amesema nafasi ya mwenyekiti mgombea alie jitokeza ni mmoja na amepigiwa kura ya ndiyo au hapana
Hashimu Rungwe ametetea nafasi hiyo kwa muhura wa tatu tangu chama hicho kianzishwe.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine Rungwe ameshukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuendelea kumuamini na kuwa atandelea kuisimamia sera yake ya Ubwabwa mashuleni na hosptalini huku pia akisisitiza kuwa mpango wa chama kupeleka bahari Dodoma ukiwa palepale.
Naibu msajili kutoka ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa Sist Nyahoza amekipongeza chama hicho kwa kufanya siasa za ustarabu na kusimamia tunu za taifa ikiwemo amani.
BILIONI 15 KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI 105 MKOA WA ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda,akizungumza na wananchi wakati mara baada ya kumkabidhi Mkandarasi tenda atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda,akizungumza na wananchi wakati mara baada ya kumkabidhi Mkandarasi tenda atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
SEHEMU ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda (hayupo pichani) ,akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkandarasi tenda atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
SEHEMU ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda (hayupo pichani) ,akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkandarasi tenda atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
SEHEMU ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda (hayupo pichani) ,akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkandarasi tenda atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
Na.Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri ya kutekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini.
Mhe.Makonda ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa kumtambulisha na kumkabidhi Mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vya mkoa wa Arusha
Amesema kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini imewezesha wananchi kuunganishiwa umeme kwa gaharama nafuu na imeondoa dhana kuwa umeme ni wa matajiri.
Aidha amemtaka Mkandarasi aliyetambulishwa kutekeleza mradi huo kwa weledi na kwa kuzingatia muda wa mkataba aliopewa.
"Tunamtaka Mkandarasi kutekeleza mradi huo kwa uaminifu na hatutasita kuchukulia hatua pindi atakavyoshindwa kutekeleza kwa wakati na pia tunamtaka Mkandarasi kutumia vijana wetu waliopo katika mkoa wa Arusha kutekeleza mradi huo.
Naye Mkurugenzi wa umeme Vijijini REA, Mhandisi Jones Olotu,amesema kuwa jumla ya vitongoji 1,039 vitapatiwa umeme kupitia mradi huu.
"Vitongoji 105 kati ya 1,039 vilivyobaki vitapata huduma ya umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji vyote nchini (HEP Densification project)."
Mhandisi Olotu alimtambulisha Mkandarasi anayetekeleza mradi huo ni kampuni ya CEYLEX ENGINEERING (Pvt) LTD na gharama ya mradi huo ni takribani shilingi bilioni 15 na utanufaisha wateja wapatao 3,465.
Saturday, 28 September 2024
“DAWASA SHUHULIKIENI UPOTEVU WA MAJI KATA YA MAKUBURI” DC BOMBOKO
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh.Hassan Bomboko ameelekeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kumaliza changamoto ya upotevu wa maji katika kata ya Makuburi, Wilaya ya Ubungo ila wananchi waweze kupata huduma ya maji kwa uhakika.
Mheshimiwa Bomboko ameeleza hayo katika siku ya pili ya ziara ya Mtaa kwa mtaa aliyoifanya katika Kata ya Makuburi kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
"Maji ni huduma muhimu, tumepata changamoto kuwa maji yanapotea na muda mwingine kupelekea barabara kuharibika na kujaa maji, DAWASA mtatue changamoto hii na nitafatilia kuona imekwisha ili wananchi waendelee kupata huduma ya uhakika" ameeleza Mh.Bomboko
Bomboko ameongeza kuwa maeneo yote yanayopata huduma ya maji kwa mgao, yasimamiwe vyema na wananchi waweze kupata maji kupitia mgao husika na zaidi maji yatoke muda wa mchana ambapo kila mwananchi atakua na uwezo wa kutumia huduma hiyo.
Kwa upande wake Mhandisi wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Tabata, Daniel Sabuni ameeleza kuwa wameyapokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na kazi inaanza mara moja kutatua changamoto hiyo, lakini zaidi kutoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa pindi wanapopata changamoto yeyote ya huduma ya maji katika Ofisi za Kihuduma DAWASA
Picha : RAIS SAMIA AFUNGA KIKAO MAALUM CHA BARAZA KUU LA JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE TANZANI 'UWT' TAIFA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Ndugu Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, tarehe 28 Septemba 2024
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Ndugu Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Parokia ya Bombambili Wilayani Songea Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kufunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, tarehe 28 Septemba 2024