Wednesday, 15 February 2017

AUDIO | YAMOTO BAND - KICHECHE | Download


Share:

NECTA: ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION MAY 2017


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 
Ref. ACSEE 2017 
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL 
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION MAY 2017
Share:

AUDIO | Diamomd Platnumz Ft. Sporah - Kosa Langu | Download [Extended]

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEB 15 2017

Share:

Monday, 13 February 2017

Zitto Kabwe Amtaka Rais Magufuli Avunje Bunge

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amemshauri Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo analiona ni kikwazo kwake.

Ushauri huo ameutoa jana ikiwa ni saa chache baada ya Rais Magufuli kukosoa uamuzi wa Bunge kumuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kujieleza mbele ya Kamati ya Bunge, kutokana na kilichodaiwa na wabunge kuwa ni kauli ya kulidhalilisha Bunge.

Katika hotuba yake aliyoitoa jana wakati wa kuapishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rais Magufuli aliwataka viongozi wengine kumuunga mkono mtu anayejitokeza kupiga vita dawa za kulevya badala ya kumdhalilisha.

"Tunapomuona mtu anajitokeza kupambana na haya madawa ya kulevya, badala ya kumdhalilisha tumuombee na kumtia moyo, hawa wanaweza hata kubadilisha maneno uliyoyazungumza wakabadilisha wakatengeneza kwenye clip wakatupa, na wakajitokeza wengine wakasema wameingilia mamlaka yao, wakati wao wanaingilia mamlaka ya kuwaita wengine, hii ni vita". Alisema Magufuli

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonesha kushangazwa na kile alichodai  kuwa Rais hakujua kuwa sheria ya kuundwa kwa mamlaka hiyo, ilitungwa, na kwamba anashangaa kuona Rais hakuwa akijua kuwa alipaswa kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo

Ujumbe wa Zitto unasema
"Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.

"Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi.

"Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?

Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje".

Share:

Yusuf Manji Alivyochukuliwa na Gari la Wagonjwa Polisi na Kisha Kupelekwa Hospital

Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.

Jana jioni Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na  alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.

Baada ya gari hilo kumchukua msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
Gari la wagonjwa lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi katika viunga vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Share:

Masaa 72 ya Askofu Gwajima Mahabusu ya Polisi

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati sakata la kutangaza na kushikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Pia alieleza kushangazwa kwake na baadhi ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa nchini kuingizwa katika sakata hilo hata kabla uchunguzi kufanyika.

Gwajima ambaye alikuwa ameshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam alikokwenda baada ya kutangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, alisema hana mpango wa kumshtaki mkuu huyo wa mkoa.

Askofu Gwajima alisema badala yake anakata rufaa kwa Rais Magufuli akimtaka kufuatilia tuhuma hizo kwa undani kwa watu wanaoendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi ili waweze kupata haki.

Akizungumza kanisani kwake Dar es Salaam jana, Gwajima alisema alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kwenda kuitikia mwito uliotolewa na Makonda kwa ajili ya kutoa ushirikiano kuhusu tuhuma za dawa za kulevya

Alisema baada ya kufika kituoni hapo na kufanyiwa mahojiano alikutana na mfanyabishara na Diwani wa Mbagala Kuu, Yusuph Manji ambaye naye alikuwa amefika kituoni hapo kwa ajili ya kuitika mwito huo wa Makonda.

"Kwenye chumba changu tulikuwa mimi na Yusuph Manji, huyu ana kampuni zaidi ya 23 ameajiri Watanzania zaidi ya 5,000, sasa mtu kama huyo imeshindikanaje kumuita kwa kumpelekea hati ya kuitwa kuhojiwa, badala yake anatangazwa?"

"Imeshindikanaje mtu kama Manji kumuita kwa kumuandikia barua ili aende ahojiwe na ikigundulika achukuliwe hatua, kwa nini atangazwe kabla ya kuchukuliwa hatua?  Ilipaswa aandikiwe barua ya wito kisha uchunguzi ufanyike na kama akibainika ndiyo achukuliwe hatua, ila kwa sababu mkuu wa mkoa hakuwa na nia nzuri hata kwa Manji ndiyo maana hakufanya hivyo," alisema Gwajima.

Alisema hadi alipoachiwa katika kituo hicho bado Manji alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi, ambapo alihoji sababu ya Manji na wengine wanaoendelea kushikiliwa kituoni hapo kutofanyiwa uchunguzi na ukaguzi kama aliofanyiwa yeye ili waachiwe kama yeye au kuchukuliwa hatua kama wakibainika kujihusisha na biashara hiyo.

"Sioni sababu ya kuendelea kuwashikilia watu wale bila kuchukuliwa hatua. Kama mimi nilituhumiwa tena kwa kutangazwa lakini mwishowe ikabainika hakuna ukweli, nitaamini vipi kama wale waliobaki ndani mikononi mwa Polisi nao wanahusika?"Alihoji Gwajima.

Gwajima alisema mbali na Manji na wafanyabishara wengine waliotajwa kuhusika na biashara hiyo, wamo pia askari wa Polisi ambao nao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara hiyo na wameendelea kushikiliwa kwa amri ya mkuu wa mkoa.

Kutokana na hali hiyo, Gwajima alisema ameamua kukata rufaa kwa Rais ili aweze kuwaangalia watu hao kwa jicho la tatu na tuhuma dhidi yao ziweze kuchunguzwa na ukweli ujulikane.

"Mheshimiwa Rais ninakuomba sana, kuna wale watu wengine ambao nilikuwa nao, ambao ni wafanyabishara na walitangazwa kama mimi, naomba uwatazame kwa macho ya huruma ili tuhuma zao zishughulikiwe, kuliko kuendelea kukaa kwenye giza chini mule, kwa niaba yao ninakata rufaa kwako naomba uwahurumie.

"Kuna askari Polisi wapo ndani kwa wiki ya pili sasa kwa amri ya Makonda, mimi naomba niwasemee leo, kama mimi imeonekana kuwa sina makosa, vipi kuhusu wao? Nampongeza mheshimiwa Rais kwa kuingia katika vita ya dawa za kulevya naomba atazame jambo hili, "alisisitiza Askofu Gwajima.

Alisema kuwa alichogundua ni kuwa Rais anahitaji msaada wake hivyo anaingia katika kazi ya kumsaidia Rais kwa maelezo kuwa inawezekana anapata taarifa zisizo za ukweli.

Gwajima alisema kuwa leo amepanga kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa wengine ambao wanaendelea kushikiliwa.

Aeleza alivyokaguliwa
Katika hatua nyingine, Gwajima alisimulia waumini wa kanisa lake namna shughuli ya ukaguzi dhidi yake ilivyoendeshwa na Jeshi la Polisi, huku akidai amechiwa baada ya kubainika tuhuma dhidi yake hazikuwa na ukweli.

Alisema baada ya kuhojiwa alielezwa anatakiwa kwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ili kubaini kama anajihusisha na  utumiaji wa dawa za kulevya ama la, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alieleza kuwa licha ya kufanyiwa yote hayo Polisi walifikia pia hatua ya kukagua akaunti zake za fedha.

"Kwa sababu mimi tangu kuzaliwa sijawahi kuonja mambo hayo, lakini walivyopima wakakuta hamna chochote na wakanipa fomu kuonesha hawajakuta kitu.

"Niliwaambia kwangu mkikuta hata kipisi cha sigara andikeni dawa za kulevya, tulifika kwangu nyumba yangu ina ghorofa tatu wakakagua zote na hawakukuta kitu walichotaka," alisema

Aliongeza kuwa,"wakaona haitoshi, wakahamia kwenye akaunti zangu za benki na mimi nikawaruhusu waendelee walipofanya uchunguzi wao wakabaini hakuna kitu cha kuweza kunikamatia, hawakupata kitu wakaamua kuniachia,". 

Gwajima alisema hana mpango wa kumshtaki Makonda ama kumfungulia kesi bali anajua cha kumfanya.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEB 13 2017

Share:

Dkt. Slaa amtumia ujumbe Gwajima kuhusu Dawa za Kulevya

Vita ya kupambana na dawa za kulevya nchini iliyopamba moto zaidi na kuzua mijadala tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipoanza kutaja majina ya watuhumiwa imemuibua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa.
Share:

Sunday, 12 February 2017

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO BAADA YA KUKATA RUFAA BODI YA MIKOPO 2016/2017



Bodi ya Mikopo imetangaza majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo baada ya kukata rufaa,kiukweli ni wanafunzi wengi waliopata mkopo awamu hii ukilinganisha na miaka iliyopita.
Maswayetu blog tumekuwekea hapa taaarifa hiyo,

Ukitaka kuangaliziwa jina lako ,au la mwanao au ndugu yako kama limepata mkopo baada ya kukata rufaa, fanya yafuatayo;

1.TUMA JINA LAKO KAMILI,MFANO (JUMA PAUL-HESLB 2017)
2.HUDUMA HII UTALIPIA TSHS 1000 TU AMBAYO UTAITUMA KWENDA NAMBA 0652740927

3.KAMA UNATUMIA AIRTEL,TIGOPESA AU MPESA  TUMA KWENDA NAMBA 0652740927

4.UTAJIBIWA BAADA YA DK MOJA

5.TAFADHALI TUMA KWANZA PESA NDIO UJIBIWE.

Share:

Askofu Gwajima Kaachiwa Huru na Jeshi la Polisi


Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ameachiwa na Polisi leo jioni baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi mchana kwenye kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya.

Baada ya kuachiwa Askofu huyo aliandika yafuatayo kwenye mitandao yake ya kijamii “FREE AT LAST: Mungu awabariki wote mlioomba kwa ajili ya jambo hili, kesho nitakuwepo kwa ajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam. Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya hili”
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEB TAREHE 12.2.2017

Share:

Saturday, 11 February 2017

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEB TAREHE 11.2.2017

Share:

Friday, 10 February 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Ya February 10

Share:

Agizo wa Rais Magufuli uwanja wa ndege Dar laanza kutekelezwa

Shughuli za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017 zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08 Februari, 2017.

Wafanyakazi 850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.

Pia, timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.

Mkandarasi ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za ujenzi kuendelea.

Katika ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa dosari na kuahidi kuchukua hatua.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa ujenzi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Share:

Thursday, 9 February 2017

TANGAZO:TUNAFANYA USAJILI WA VYUO VYA NACTE KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA FORM 4 NA 6

Habari zenu,
Je,wewe ni mhitimu wa kidato cha nne 2016 na kurudi nyuma?

Nacte imefungua application kujiunga na vyuo katika ngazi ya cheti na diploma mwaka wa masomo 2017/2018 March intake.

Maswayetu blog tutakusaidia kuomba kozi unayoipenda pamoja na kukupa ushauri kuhusu kozi ya kusoma nzuri yenye soko kwa sasa.

Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

KAMA UNAHITAJI HUDUMA YETU TAFADHALI TUPIGIE/AU TUTUMIE SMS KWENYE SIMU NAMBA 0652740927

 KUMBUKA KUWA NAMBA YAKO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE.

MPE TAARIFA NA MWENZAKO
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA FEBRUARI 9,2017

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger