SERIKALI imepanga kununua ndege za kisasa ili kuimarisha ulinzi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha
TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa
(TBC1).
Meja
Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika kulinda
hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza
katika hifadhi mbalimbali nchini.
“Sekta
ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5
na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali
ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika
kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.
Aidha,
alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria
watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya
magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.
Aidha
Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa
kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira
na hifadhi za taifa.
Mbali
na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi
zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka
wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa
ili kuzudi kuvutia watalii nchini.