Tuesday, 3 February 2026

WADAU WA HABARI WAISHAURI MAMLAKA KUZINGATIA MAPENDEKEZO KUHUSU MSWADA WA HUDUMA ZA HABARI ZANZIBAR




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 3,2026

Magazeti
 
Share:

Monday, 2 February 2026

JENERALI MKUNDA AWATAKA ASKARI WAPYA KUTII KIAPO CHA UTUMISHI

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Jacob John Mkunda, amewataka askari wapya waliohitimu mafunzo yao kukiishi kiapo cha utii wakati wote watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ). 

Aidha Jenerali Mkunda ametoa onyo kali kuwa jeshi halitasita kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya askari yeyote atakayekwenda kinyume na kiapo hicho cha uaminifu kwa nchi na jeshi.

Wito huo ameutoa mkoani Pwani wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kundi la 44 la mwaka 2025, yaliyofanyika katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi, RTS Kihangaiko, iliyopo wilayani Bagamoyo. Katika hotuba yake, Jenerali Mkunda amewasisitiza wahitimu hao kuwa nidhamu na utii ndio msingi mkuu wa kazi ya kijeshi na bila hivyo hakuna usalama wa taifa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Majeshi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Daktari Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuliwezesha jeshi kupata rasilimali na vifaa vinavyohitajika katika kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi. Jenerali Mkunda amebainisha kuwa msaada wa Amiri Jeshi Mkuu umekuwa chachu ya mafanikio makubwa katika utendaji wa JWTZ.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko, Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala, amewapongeza askari hao kwa uvumilivu na jitihada walizozionyesha kipindi chote cha mafunzo. 

Brigedia Jenerali Myala ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewajengea vijana hao uzalendo wa hali ya juu na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu ya jeshi kwa ufanisi, huku akibainisha kuwa wako tayari kuitumikia nchi kwa weledi.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa shamrashamra na maonesho mbalimbali ya kijeshi ikiwemo michezo ya kareti inayolenga kuimarisha ukakamavu, pamoja na burudani za muziki na ngoma za asili zilizowavutia waliohudhuria tukio hilo muhimu la kutaifisha askari hao wapya.



Share:

NILIHAMISHWA KAZI MARA TATU MPAKA NILIPOTUMIA NJIA ILIYOBADILI HATIMA YANGU



Kwa miaka kadhaa, maisha yangu ya kikazi yalikuwa kama mzunguko wa mateso. Nilifanya kazi kwa bidii, nikatimiza majukumu yangu, lakini bado nilijikuta nikihamishwa kutoka idara moja hadi nyingine bila sababu ya wazi. Mara ya kwanza nilijipa moyo kuwa labda ni kawaida ya kazi.

Mara ya pili nikaanza kuwa na wasiwasi. Ilipofika mara ya tatu, nilijua kuna kitu hakikuwa sawa kabisa. Kila uhamisho uliambatana na fedheha ya kimyakimya. Niliona heshima yangu ikipungua, wenzangu wakinichukulia kama mtu asiyeaminika, na wasimamizi wakinitazama kwa shaka.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 2,2026



















Share:

Sunday, 1 February 2026

Video Mpya : SHILEKA NGANO - SIRI

 

Share:

UTALII INJINI INAYOCHOCHEA AJIRA NA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIJAMII

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka wazi kuwa nguvu ya sekta ya utalii nchini haipaswi kupimwa kwa wingi wa fedha zinazoingia kwenye mfuko wa serikali pekee, bali kwa namna inavyogusa maisha ya mwananchi mmoja mmoja kupitia mnyororo mpana wa thamani.

Akizungumza jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha Tuzo za Kitaifa za Uhifadhi na Mazingira (The Serengeti Awards), Dkt. Mwigulu amesema uhifadhi ni injini inayochochea ajira na kuimarisha huduma za kijamii.

"Faida ya utalii haiishii kwenye mapato pekee. Inajumuisha manufaa mapana yanayoifikia jamii pamoja na mnyororo mzima wa thamani unaotokana na uhifadhi. Serikali itaendelea kuhakikisha faida hizi zinamfikia mwananchi wa kawaida," alisema Dkt. Mwigulu.

Katika uchambuzi wake, Waziri Mkuu alibainisha kuwa sekta ya utalii inategemea mazingira yaliyohifadhiwa vyema. Alisisitiza kuwa bila jitihada za makusudi za kutunza rasilimali asilia, uchumi wa maeneo yanayozunguka hifadhi utatetereka.

Sekta hiyo imetajwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza biashara ndogo kama za mama lishe, wauza vinyago, na wasafirishaji .Aidha mapato ya utalii yanasaidia ujenzi wa zahanati na shule katika vijiji vya jirani na hifadhi huku maelfu ya vijana wakiwa wameajiriwa kama waongoza watalii, madereva, na wahudumu wa hoteli.

Sauti za Wananchi

Wakizungumza nje ya ukumbi wa tuzo hizo, baadhi ya wakazi wa Arusha na wadau wa utalii wamepongeza kauli hiyo ya serikali, wakisema inatoa picha ya uhalisia wa maisha yao ya kila siku.

Bwana Juma Bakari, ambaye ni dereva wa magari ya watalii kwa zaidi ya miaka kumi, alisema: "Ni kweli kabisa, watalii wasipokuja, siyo serikali tu inayokosa kodi, bali hata sisi mtaani hatuna kitu. Akija mtalii mmoja, mimi napata mshahara, mama ntilie anauza chakula, na kijana wa kuosha gari anapata riziki yake."

Naye Bi. Rehema Mollel, mfanyabiashara wa vinyago na ushanga, aliongeza: "Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kutangaza utalii (Royal Tour). Sisi tunaoishi karibu na hifadhi tunaona faida moja kwa moja, kwani soko letu linategemea wageni hawa."

Dkt. Mwigulu ambaye alihitimisha kwa kutoa rai kwa wadau wa mazingira kuendelea kushirikiana na serikali amesisitiza kuwa tuzo hizo za Serengeti  ni kielelezo cha kutambua mchango wa wale wanaopambana kulinda urithi wa nchi kwa ajili ya vizazi vijavyo na uchumi wa sasa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger