Thursday, 4 December 2025

WABEBA ZEGE WAYAKATAA MAANDAMANO YA DISEMBA 09, "TUMECHOKA"



Na mwandishi wetu,Dar

WAKATI joto la maandamano ya Disemba 09 likizidi kupanda, mjadala wa kuyapinga na kuyakataa maandamano hayo umeendelea Kila Kona, huku vijana, wazee na wanawake wakieleza kuwa wasingependa kilichotokea Oktoba 29 kijirudie tena.

Hawa hapa ni Vijana waliokuwa katika Shughuli zao za Kujitafutia mkate wa kila siku kama ambavyo inaonekana kwenye Video hii maongezi yao yaliyonaswa hapa ni kuhusu kupinga vikali kujihusisha na masuala ya maandamano huku wakilinganisha athari ambazo wamezipata Oktoba 29.

"Tumechoka na maandamano tumekaa ndani siku tatu tunachokula chamaana hakuna hiyo Tarehe 09 hatuyawezi tumechoka maandamano " Mwananchi wa Dar es Salaam.


Share:

MWIGULU AMALIZA UTATA: “WAMETENGEWA FEDHA ZA KUCHAFUA NCHI”, KAULI YAZUA HISIA KALI


Kauli ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni mbili (sawa na takribani Shilingi Bilioni 4.5) zimetolewa kwa ajili ya kuchochea chokochoko na vurugu nchini, limezua mjadala mkali mtandaoni. 

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamejikita katika kuchambua chanzo cha vurugu, maslahi ya mataifa ya kigeni, na umuhimu wa busara katika kushughulikia masuala ya kitaifa.

Waziri Mkuu alisema kuwa wachochezi wamelenga kuharibu uchumi wa nchi na kurudisha nyuma maendeleo, huku lengo kuu likiwa ni kunyakua rasilimali adimu za Tanzania kama vile madini ya Uranium na maendeleo ya miradi ya gesi asilia.

Baada ya ufichuzi huo, maoni yamegawanyika kati ya wale wanaosisitiza umuhimu wa kufahamu maslahi ya Taifa na wale wanaotilia mkazo umakini wa vijana kujitambua.

Mchangiaji Oliver Kibua alikaribisha ufichuzi wa Serikali, akisisitiza umuhimu wa wananchi kujua chanzo na sababu ya vurugu hizo:"Afadhali kama inaweza kuwaambia wananchi sababu na chanzo cha yote wajue kipindi watu wanatumika na kuhadaika kuwa wapiganie haki kumbe wenzao wana wanachokitaka, na vurugu ikiwepo waumiao ni wananchi waliopo nchini na sio nje ya nchi."

Kibua pia alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kufahamu kuwa hakuna taifa linaloingilia kati masuala ya nchi nyingine bila maslahi yao binafsi. Alihimiza, "Hao wanaojitambua waamke maana wanajitambua wao hawatambui ukweli wa mambo... think before you act."

Mchangiaji mwingine alitumia nafasi hiyo kukosoa matumizi ya lugha ya matusi na mihemko katika mijadala ya kitaifa, hasa kwa wale waliowahi kushika nyadhifa za uongozi.

"...Nikuona watu waliowahi kuwa madarakani mahali fulani wakakosana na waliowaweka madarakani wanavyokuwa hawajui kutumia lugha ya ushawishi na badala yake wanatukana... Si suala tu la kuamsha hisia bali ni suala la kusoma, kutafakari na kuona kweli katika muda sahihi na mazingira sahihi." alisema mmoja wa wachangiaji hao.

Mchangiaji huyo alitumia fumbo la kijadi kuhusu njiwa waliokosa ushauri na kufa ufukweni, akisisitiza kuwa nguvu (mihemko) bila maarifa (busara na ushauri) haisaidii. Alihimiza Watanzania kuchanganya maarifa ya kimagharibi na hekima za zamani ili kupata majibu sahihi.

Hata hivyo Rafael Valency Kwembe alionyesha imani kwa vijana wa Afrika, akisema:"Uzuri waafrika wa sasa tunajitambua sana, nyie pigeni ngonjera ila ukweli tunaujua na tunaufanyia kazi. Tunajua nani anazingua na nani yupo sahihi."

Mchangiaji mwingine aliunga mkono msimamo wa Serikali kwamba vurugu hizo zinaletwa na wanaharakati wanaolipwa na kuwahimiza Watanzania kuamka na kuchukua tahadhari, akisisitiza: "Ajira na uondoaji wa umaskini utapatikana tu nchi ikiwa na amani."

Kauli ya Waziri Mkuu inahimiza Watanzania kujiuliza maswali kuhusu maslahi na ajenda ya watu wanaotoa malipo hayo. Alionya kuwa mbinu hizi zimetumika katika nchi zingine barani Afrika, ambapo chokochoko huanzishwa ili kuruhusu uvurugaji na uchukuaji wa rasilimali, kabla ya wachochezi kuondoka baada ya rasilimali kuisha.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 4,2025





Magazeti



Share:

Wednesday, 3 December 2025

SERIKALI YASEMA HAITAAMRISHWA, WALA KUVUMILIA UCHOCHEZI

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza msimamo thabiti wa Serikali ya Awamu ya Sita kulinda amani, umoja na utulivu wa Taifa, huku akionya dhidi ya matamko yanayoashiria uchochezi.

Akizungumza kwenye mkutano maalum na Wazee wa Dar es Salaam, Rais Samia alitoa kauli kali akijibu mfululizo wa matamko yanayotolewa na baadhi ya taasisi za kidini, hususan Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

“Tupo tayari kukaa, kuzungumza na kuondoa mapungufu yaliyopo, lakini Serikali hii si ya kuamrishwa wala kupewa maelekezo,” alisema Dkt. Samia.

Rais Samia alifichua kuwa tangu aingie madarakani, TEC imetoa matamko takribani nane. Hata hivyo, alibainisha kuwa ndani ya Kanisa Katoliki lenyewe kuna tofauti za kimtazamo kuhusu uhalali na malengo ya baadhi ya kauli hizo.

Alisema baadhi ya viongozi na waumini wa Kanisa wanahoji kuwa matamko hayo hayajengwi katika misingi ya haki na ukweli, na hivyo kuchochea migawanyiko isiyo ya lazima katika jamii.

Rais alisisitiza kuwa Serikali haitavumilia kauli zozote zinazoashiria uchochezi ama zinazoweza kuvuruga misingi imara ya Taifa.

“Tanzania yetu ni nchi ya umoja, mshikamano, amani na utulivu, na hizo ndizo ngao zetu. Tusivurugwe ndugu zangu kupitia mirengo ya dini, siasa au mingineyo,” alihimiza Rais Samia.

Dkt. Samia alieleza masikitiko yake kuwa tuhuma dhidi ya Serikali ya Awamu ya Sita mara nyingi zimekosa msingi, akitaja mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali.

Aliuliza, "Kosa la Serikali ya awamu ya sita ni nini? Kueneza huduma bora za afya? Kupeleka elimu bora hadi vijijini? Kukuza uchumi hadi kutambuliwa duniani? Kuiweka Tanzania salama? Kosa letu ni lipi?"

Alisisitiza kuwa misingi ya kidemokrasia inaruhusu kukosoa, lakini sio kuhatarisha utulivu wa nchi.

Alitoa wito kwa wananchi kuvumilia na kutokubali vurugu kwa sababu za tofauti za kidini, asili, au mtazamo binafsi kuhusu kiongozi. 

“Kama humpendi anayeongoza, stahimili. Mioyo yetu imeundwa kwa stahimilivu. Demokrasia ipo, ataongoza na ataondoka. Hakuna sababu ya kuvuruga nchi,” aliongeza.

Rais Samia alitoa wito mkali kwa viongozi wa dini kutojificha nyuma ya majoho na kujaribu kuongoza nchi.

 Alisema, Tanzania itaendelea kuongozwa kwa mujibu wa Katiba na sheria, si kwa hisia ama matamanio ya mtu binafsi.

Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu, lakini inatarajia taasisi za dini kubaki kuwa chachu ya maadili na sio jukwaa la mijadala inayoweza kupandikiza migawanyiko.

Rais aliwahimiza wananchi kutumia busara dhidi ya misimamo mikali na "sumu" wanayopewa, akibainisha kuwa dini mara nyingi hutumiwa kuwashawishi watu bila uchambuzi wa kina.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 3, 2025




 
















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger