Wednesday, 26 November 2025

WAZIRI KAPINGA AITAKA SIDO KUONGEZA UBUNIFU NA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kuongeza ubunifu na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa majukumu yake, ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kuongeza tija katika sekta ya viwanda.

Waziri Kapinga alitoa maagizo hayo Novemba 26, 2025, alipotembelea makao makuu ya SIDO jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Bodi pamoja na Menejimenti ya shirika hilo. 

Amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuwezesha viwanda vidogo na biashara ndogo kukua, kuimarika na kuongeza ajira kwa vijana.

Amesisitiza kwamba mifumo ya kidijitali itaiwezesha SIDO kuwa na takwimu sahihi za viwanda vidogo nchini, hatua itakayosaidia Serikali kupanga mikakati ya maendeleo kwa usahihi na ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, amesema SIDO ni uti wa mgongo wa maendeleo ya viwanda vidogo na mshirika muhimu wa Serikali katika kutekeleza ajenda ya uchumi wa viwanda.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya SIDO, Prof. Mussa Nyamsingwa, ameihakikishia Serikali kuwa Bodi na Menejimenti ya shirika hilo wako tayari kutekeleza maelekezo yote kwa ufanisi, ili kuhakikisha sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo inaendelea kukua na kuchangia ajira kwa vijana nchini.
Share:

NI MPANGO MCHAFU; NIA NI KUHUJUMU UCHUMI NA MAISHA YA WATANZANIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefichua kwamba vurugu za Oktoba 29 hazikuwa tu uharibifu wa mali, bali zilikuwa ni jaribio lililopangwa la kuhujumu na kuua uchumi wa nchi na kudhoofisha maisha ya Watanzania mmojammoja.

Akizungumza kwa hisia, na wahariri na waandishi wa habari waandamizi jijini Dar es salaam,Dkt. Mwigulu alieleza jinsi wahuni hao walivyolenga miundombinu muhimu.

"Mpango uliwekwa pasiwe na miundombinu ya hawa watu kusafiri. Walipanga kuchoma stendi ya mabasi ya Magufuli, kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi na reli ya SGR. Hizi siyo mali za Serikali, ni mali za umma," alisema.

Alisisitiza kuwa uharibifu huo uliathiri maisha ya kila siku ya Mtanzania: "Maisha ya Mtanzania mmojammoja yanahusisha mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kujipatia riziki zao. Hawa watu wasipotoka unataka wale nini?"

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kusisitiza kwamba fedha zinazotekeleza miradi mikubwa—kama vituo vya DAWASCO, barabara, na zahanati—si za Serikali, bali ni za Watanzania.

"Ukinunua shati kuna sehemu unapeleka kujenga barabara, unakuwa umetenga sehemu ya kutumia na sehemu umejinyima ili kuchangia maendeleo ya nchi. Hivyo unapochoma kituo cha DAWASCO kinachowapa maji safi na salama, unataka hawa watu waishije?" alihoji Waziri Mkuu, akionyesha jinsi hujuma inavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja.

Aliwataka watanzania kuelewa njama za makusudi zinavyopangwa ili kuvuruga mfumo wa maisha na kudidimiza maendeleo yaliyopatikana nchini.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 26, 2025

Share:

Tuesday, 25 November 2025

SIMBA SC YAKUBALI KIPIGO NYUMBANI DHIDI YA PETRO ATLETICO DE LUANDA



Klabu ya Simba SC imepoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo, Novemba 23, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 78 na kiungo Benardo Oliveira Dias, maarufu kama “Benny”, akiipatia Petro Atletico ushindi muhimu ugenini.

Simba ilijitahidi kusaka bao la kusawazisha katika dakika za mwisho, lakini ukuta wa Petro ulibaki imara huku kipa wao akifanya kazi ya ziada kuzuia jaribio la mwisho la Moses Phiri.

Kwa matokeo haya, Wekundu wa Msimbazi wanalazimika kusaka ushindi katika michezo yao ijayo ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 25, 2025


 














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger