Saturday, 22 November 2025
WITO KWA WATANZANIA KUTUMIA FIKRA CHANYA KULINDA AMANI

Viongozi, wachambuzi wa kijamii, na wadau wameungana kutoa wito kwa Watanzania wote kudumisha amani na umoja wa nchi, huku wakitahadharisha dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayolenga kuleta vurugu, hususan kuelekea mwezi wa Desemba. Kauli za wadau zinabainisha wazi kuwa, bila amani, hakuna mustakabali wa maendeleo, hasa kwa vijana.
Akizungumza kwa hisia, Bwana Shamte Mkali, alipongeza jitihada za uongozi wa nchi katika kuimarisha utulivu.
"Napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais ,Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwani wakati ule hali ilipokuwa ngumu, wananchi wapo ndani wanasikilizia, Rais akasema neno, neno lile likatoa faraja nchi nzima. Kuanzia siku hiyo hali imekwenda vyema hadi leo," alisema Bwana Mkali, akisisitiza umuhimu wa kauli za kiongozi mkuu wa nchi.
Bwana Mkali pia alisisitiza umuhimu wa maridhiano kama msingi bora wa kutafuta amani na si vinginevyo.
"Nchi hii ni yetu sote, ni lazima tuwe katika mshikamano... watu wakae wafanye mazungumzo, kwani shida ni nini? Taifa linaendelea na si kufanya fujo... vurugu hizo madhara sio kwa serikali tu, bali hata kwa wananchi na wale wanaoingia kuzifanya," alionya.
Wakati kukiwa na taarifa za uchochezi zikizunguka mitandaoni zikilenga kuleta vurugu Desemba 9, wadau wameonya umuhimu wa kuwa na fikra chanya na kukataa waziwazi wachochezi wanaojificha nyuma ya skrini.
Amani ni Tunu: "Amani tuliyonayo ni tunu na alama ya taifa letu maana mataifa mengine yamekosa hii sifa na wanakuja kwetu," alisema mdau mmoja katika mijadala ya kijamii, akitaka Watanzania kudumisha sifa hiyo.
Amani ni Ngao: Mdau mwingine alibainisha kuwa, "Amani ni ngao ya taifam,ikipotea kila mmoja huwa dhaifu. Vurugu huharibu utulivu wa taifa, biashara husimama, shule hufungwa na jamii hupoteza mwelekeo."
Katika mitandao imeoneshwa na taswira mbalimbali za uvunjifu wa amani ambao ndio adui mkubwa wa maendeleo ya vijana. Wakati amani ikivunjika na serikali inapambana na kuirejesha mara zote biashara na wawekezaji huondoka, ajira hupungua,elimu husimama: Shule hufungwa na vijana hukosa msingi wa kupata maarifa na badala ya kufanyakazi za maendeleo jamii huishi kwa wasiwasi.
"Hatuwezi kufurahia matunda ya maisha bila mbegu ya amani. Tupande mbegu hiyo leo," ni kauli inayotolewa kama ujumbe wa kuamsha Watanzania kuchukua hatua chanya.
4, 826 WAHITIMU MAFUNZO YA POLISI MOSHI, IGP AKIONYA KUHUSU UGAIDI NA DAWA ZA KULEVYA
BODI YA TANAPA YATEMBELEA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
TBS WATOA WITO USALAMA WA CHAKULA
Friday, 21 November 2025
WATANZANIA KATAENI KUVURUGWA DESEMBA 9 – AMANI NDIO RIZIKI YETU!
Katika hali inayoonyesha wasiwasi wa baadhi ya wananchi kuhusu mipango ya uvunjifu wa amani, inayosambazwa mitandaoni hasa ile inayoelezwa kulenga Desemba 9, wito umetolewa kwa Watanzania wote kusimama imara na kukataa ushawishi wa wale wanaotaka kuingiza taifa kwenye machafuko.Wananchi wamesema amani ni msingi mkuu wa maisha yao ya kila siku, huku wakisisitiza kwamba hakuna kazi wala maendeleo yanayoweza kupatikana bila utulivu.
Amani Huratibu Kazi, Huzima Vurugu
Malugu Nkwabi mkazi wa Bariadi ambaye ni Afisa Usafirishaji, alitoa msisitizo mkubwa kwa umuhimu wa amani katika ufanisi wake wa kazi.
"Ni lazima Watanzania tushikane kuhakikisha amani ndiyo kila kitu. Amani ndiyo kitu cha muhimu sana kwenye taifa. Maisha yote yanategemea kuwepo kwa amani. Ukiangalia kuanzia saa 12:00 jioni ukifika ni lazima nifanye kazi ili niweze kurudi nyumbani na maisha yangu kuendelea. Huwezi kufanya kazi pasipo kuwepo amani.."
Kauli hii inalenga moja kwa moja wale wanaofikiria kuandamana au kufanya vurugu, ikiwakumbusha kwamba uvunjifu wa amani kwanza unakwenda kuathiri shughuli zao za kujipatia riziki.
Kwa upande wake, Bwana Marco Mahega,kutoka mkoani Simiyu , alieleza masikitiko yake kwa jinsi Watanzania wanavyotaka kuichoma nchi yao na kukumbusha nchi zenye migogoro, akisisitiza kuwa amani inalinda hata viwango vya chini vya jamii.
"Sisi wenye familia zetu tukikuta nchi haina amani hatuna kwa kuikimbilia... Tunashukuru Mwenyezi Mungu, tumepewa amani. Naomba tuendelee kuihifadhi. Ukiona nchi haina amani maana yake haina amani hata kwenye familia yako. Tunaangalia nchi nyingi ambazo hazina amani wanatumia muda wao mwingi kuendelea kwenye migogoro. Sisi amani ndiyo kila kitu. Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kudumisha amani."
Wakati wakikataa vurugu, wananchi pia wanatoa wito kwa viongozi kuwajibika. Bwana Paul Mboyi,alielekeza wito wake kwa viongozi waliochaguliwa hivi karibuni, akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi badala ya kuendeleza siasa.
"Kila mtu atimize wajibu wake... Naomba viongozi ambao kwanza wamechaguliwa waanze kufanya yale mambo waliyoahidi. Tusiishie tu kwenye siasa. Tunaomba viongozi kuwafuata wananchi, wasikae ofisini tu. Mkutano wa mkoa tulinde kwanza kauli ya amani. Kusiwe na makundi."
Wito wa Bwana Mboyi unaonesha kuwa wananchi wanataka kuona uongozi unajikita katika maendeleo, lakini wanakiri kwamba amani lazima ilindwe kwanza kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi.














