Sunday, 7 September 2025

BODI YA TAIFA GROUP YAZIDI KUWEKA WAZI MCHAKATO WA UNUNUZI WA HISA ZA MAKAMPUNI YAKE YA TANCOAL NA WDL


Wanaochafua taswira ya kampuni kuchukuliwa hatua za kisheria








Share:

JUMLA YA MIRADI YA MAENDELEO 58 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 23.8 ITAZINDULIWA,KUKAGULIWA,KUTEMBELEWA PAMOJA NA KUWEKEWA MAWE YA MSINGI NA MWENGE WA UHURU MKOANI KAGERA



Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa(aliyeshikiwa maiki) Akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya muleba Dkt Abel Nyamahanga kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge huo katika wilaya ya Muleba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa ( aliyeko upande wa Kulia ) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na mkuu wa mkoa wa Geita .

Na Mariam Kaagenda
Jumla ya Miradi ya Maendeleo 58  yenye thamani ya shilingi bilioni 23.8 itazinduliwa , Kukaguliwa , kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Kagera ambao umeanza kukimbizwa leo Septemba 7 ambapo mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika katika kata ya Nyakabango wilaya ya Muleba ukitokea mkoani Geita.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema kuwa kwa mwaka 2024 Mwenge wa Uhuru ulitembelea, kukagua,Kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye Jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi bilioni 53.9

Hajjat Mwassa amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Kagera utakimbizwa katika halmashauri zote 8 za mkoa huo kwa umbali wa kilometa elfu 1 na 40 na kuishukuru  Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan kwa kuwezesha fedha nyingi  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo katika Sekta mbalimbali  mkoani   Kagera kwani miradi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali, Wananchi pamoja na wadau wa maendeleo .

Ameongeza  kuwa kwa kuzingatia  Ujumbe wa mbio za  mwenge wa Uhuru Kitaifa  mwaka 2025 usemao Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu mkoa wa Kagera umetekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu pia  umeendelea kuweka utayali kwa kuhamasisha vyama vya siasa pamoja na wananchi wa makundi yote wakiwemo Vijana, Wazee na watu wenye mahitaji maalum  kushiriki uchaguzi mkuu  utakao fanyika October 2025 ili kutimiza haki yao ya kikatiba 

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa  mwaka 2025  Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi wa Barabara ya Katembe _Mwaloni yenye urefu wa Kilometa 0.56 kwa kiwango cha Lami amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni kutokana na dhamila na maono ya Rais Samia ya kuhakikisha maendeleo hayo yanafanyika ni kwasababu ya kuendelea kuienzi farsafa ya Mwenge wa Uhuru .

Aidha ameongeza kuwa Tanzania inayo Tunu ya Taifa ambayo Mwananchi  yoyote akiiona anajua kuwa mahali hapo Tunu inaenda kuweka matumaini , Upendo na heshima katika maeneo hayo kwani ipo miradi ambayo watu walidhani haiwezi kutekelezwa lakini Mwenge wa Uhuru umeizindua na  kuweza kuwasaidia wananchi huku akiwaomba wananchi kuitunza miradi hiyo ikiwemo Barabara na kuendelea kuithamini kwa dhati .




 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 7,2025





Magazeti


Share:

Saturday, 6 September 2025

TCRA YASITISHA LESENI YA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI JAMIIFORUMS

 


Share:

Video Mpya : NG'WANA SAMAKA - NG'WITOGWIONE



Share:

Video : MAHOJIANO MAALUM NA ROSTAM AZIZ

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 6,2025


Magazeti
 
 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger