Thursday, 21 August 2025

TPA YACHUKUA HATUA MBALIMBALI UBORESHAJI MIUNDOMBINU,KUONGEZA UFANISI BANDARINI.


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imechukua hatua mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa Miundombinu, kusimika mifumo bora ya TEHAMA na kushirikisha Wadau wa Sekta Binafsi wakiwemo waendeshaji wa Bandari, ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia Shehena za ndani na nje ya nchi kupitia katika bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa wakati akifungua kikao cha Wadau wa Usafirishaji wa Shehena kupitia Ushoroba wa kati, Agosti 21, 2025 Kilichofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mha. Dkt. Baraka Mdima amesema, hatua hizi madhubuti zilichukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa na TPA kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha tija Bandarini, ziende sambamba na kujenga utamaduni wa Uadilifu na Uwajibikaji kwa Wafanyakazi wake, wateja na wadau ili kurahisisha ufanyaji biashara kupitia ushoroba wa kati.

Mha. Dkt. Mdima amesisitiza kuwa ni vyema, Wadau wanaoshiriki kikao hicho, wakajadiliana changamoto zinazokabili Sekta ya usafirishaji na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kurahisisha biashara kupitia ushoroba wa kati.

Aidha, amewahakikishia Wadau wa Usafirishaji kuwa TPA inaendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Wadau wake ili kuhakikisha kuwa Ushoroba wa Kati unakuwa wa kisasa, wenye ufanisi, na wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na nchi zote zinazohudumiwa na ushoroba huo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Martin Masunga, amesema maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao, yamepokelewa na yatafanyiwa kazi na Serikali ili kurahisisha ufanyaji wa Biashara na kuondoa ucheleweshaji kupitia Ushoroba wa kati.

Kikao hiki cha Wadau wa Usafirishaji kimeandaliwa na TPA chini ya Usimamizi wa Wizara ya Uchukuzi na kimehudhuriwa na Wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha Mawakala wa Meli ( TASAA), Chama cha Mawakala wa Forodha ( TACAS) Baraza la Wasafirishaji ( TSC) Wamiliki wa Bandari Kavu ( CIDAT) Chama cha Wasafirishaji Tanzania ( TAT) na Chama cha Wamiliki wa Malori madogo na ya kati ( TAMSTOA).







Share:

MPENZI WANGU ALIANZA KUNITENGA KWA SABABU YA KUFIKA HARAKA, SASA ANAOMBA TUFUNGE HARUSI



Kwa muda mrefu nilijiona sifai, duni, na kama mwanaume nusu. Nilikuwa kijana wa miaka 29 kutoka Chamwino, Dodoma, mwenye kazi ya mhasibu katika shirika moja la fedha, maisha mazuri kwa mtazamo wa nje lakini ndani yangu nilibeba aibu isiyoelezeka.

Nilikuwa nikisumbuliwa na tatizo la kufika kileleni mapema, yaani kukosa udhibiti wa msisimko wa nguvu za kiume, hali iliyoharibu kabisa uhusiano wangu wa kimapenzi na kunifanya nijitenge kijamii.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 21,2025



 

                     

 

 




  




Share:

Wednesday, 20 August 2025

KILIMANI YALIPUKA KWA VIFIJO: MUSSA MKUNDA RASMI MGOMBEA WA CCM



Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Shangwe, nderemo na vifijo vilitawala leo katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kilimani Jijini Dodoma baada ya Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Mussa Mkunda, kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Wanachama wa CCM, wananchi pamoja na viongozi wa chama walijitokeza kwa wingi kumsindikiza Mhe. Mkunda katika hatua hiyo muhimu ya kisiasa. Tukio hilo limeonyesha mshikamano mkubwa wa wana CCM wa kata hiyo, ishara ya umoja kuelekea ushindi wa chama hicho katika uchaguzi ujao.

Akizungumza katika ofisi ya Mtendaji wa Kata mara baada ya Mgombea kuchukua fomu, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilimani, Comrade Nathan Chibeye, alisema kuwa chama hicho kina utaratibu wa kidemokrasia wa kupitia mchakato wa ndani na kuteua mgombea mmoja wa nafasi ya Udiwani, ambaye sasa ni Mhe. Mussa Mkunda.

“Sisi kama chama, tukimaliza uchaguzi wa ndani, tunavunja makundi yote yaliyokuwepo na sasa tunakuwa kitu kimoja – chama kimoja na kundi moja la wana CCM – kwa lengo la kuhakikisha wagombea wetu walioteuliwa wanashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu,” alieleza Chibeye.

Akikabidhi fomu za kugombea kwa Mhe. Mkunda, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata ya Kilimani, Bi. Neema Simanjilo, alimwelekeza kuzisoma kwa umakini na kuzijaza kikamilifu kama inavyoelekezwa kabla ya kuzirejesha kwa wakati.

Baada ya kupokea fomu, Mhe. Mussa Mkunda alitoa shukrani kwa chama chake kwa imani waliyoionyesha kwake, pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi kwa kurahisisha mchakato wa kuchukua fomu hiyo.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu, chama changu, pamoja na wana Kilimani wote kwa kuniunga mkono. Nashukuru tume kwa ufanisi wa mchakato huu – hakuna changamoto yoyote nimekutana nayo,” alisema Mkunda.

Akiwahutubia wananchi na wanachama waliomsindikiza, Mkunda aliwaahidi kuendeleza miradi yote iliyoanzishwa na aliyekuwa Diwani mstaafu na kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Alitaja mfano wa shule yenye vyumba vinne vya madarasa ambavyo bado havijakamilika – akiahidi kuvimalizia na kuongeza miundombinu mingine ya elimu.

Mkunda alitaja vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, hasa katika Mtaa wa Chinyoyo,kujenga kituo cha afya, shule ya sekondari, kituo cha polisi, na ofisi za viongozi wa serikali za mitaa yote minne.

Vipaumbele vingine ni kuanzisha soko la kisasa la kata ya Kilimani,kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kusimamia na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa ushirikiano na wananchi wote wa kata hiyo.

Amehitimisha kwa kuahidi kuwa uongozi wake utakuwa wa ushirikiano, uwazi na kushirikisha wananchi wote bila ubaguzi, ili kwa pamoja kuijenga Kilimani mpya yenye maendeleo endelevu.








Share:

MASHIRIKA YA WANAWAKE YAKOSHWA NA KASI YA WANAWAKE KUGOMBEA URAIS NA MAKAMU WA RAIS






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger