Monday, 4 August 2025

BARRICK BUZWAGI YAFADHILI MRADI WA UJENZI WA CHUJIO LA MAJI YA MVUA WILAYANI KAHAMA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa , Ismail Ali Ussi (Mbele mwanzo kushoto) akikata utepe na uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa chujio wa maji ya mvua , mradi unaofadhiliwa na Barrick Buzwagi na serikali ya Tanzania eneo la mwendakulima Wilaya ya Kahama katika upokeaji wa mbio za mwenge mjini Kahama
Sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji ya mvua mwendakulima , Kahama Shinyanga ndani ya mgodi wa Buzwagi Barrick
Kiongozi wa Mbio wa Mwenge , Ismail Ali Ussi akihutubia hadhara na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji ya mvua eneo la Mwendakulima wilayani Kahama
Sehemu ya jiwe la msingi wa mradi wa ujenzi wa chujio wa maji ya mvua mjini Kahama , Shinyanga

Kiongozi wa mbio za mwenge, Ismail Ali Ussi (Katikati) akisikiliza maelezo ya mradi kutoka kwa msimamizi wa mradi huo , Mhandisi Magige Marwa (wa kwanza kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usimamizi wa Mazingira, , Mamlaka ya Maji Safi wa Mazingira Kahama (KUWASA) wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama , Frank Nkinda

Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi , Zonnastraal Mumbi wa pili kulia kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali


-Utagharimu takribani shilingi Bilioni 4.8 za kitanzania

Na Mwandishi Wetu, Kahama Shinyanga

Mgodi wa Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa umefadhili mradi wa ujenzi wa chujio la maji ya mvua eneo la mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga unaoghalimu takribani shilingi Bilioni 4.8 kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa mji wa kahama maji safi na salama.

Akiongea wakati wa hafla ya kupokea mwenge ulioambatana na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo wa mradi wa maji, Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi ,Zonnastraal Mumbi amesema mgodi katika hatua zake za mwisho za ufungaji umeamua kufadhili mradi huo ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye Wilaya ya Kahama.

“Haya ni matokeo ya ufungaji wa mgodi wa Buzwagi kwa kuamua kufadhili mradi mkubwa kabisa wa maji ya mvua kwa kutengeneza miundombinu ya uvunaji , ukusanyaji na usambazaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi wa wananchi wa mji ya Kahama,” amesema Mumbi.

Ameongeza kwamba moja ya dhamira ya kampuni ya Barrick inayoendeha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

“Mgodi wa Buzwagi umefadhili mradi huu wa maji ya mvua kwa 62% kwa ajili ya kuhakikisha kwamba miundombinu ya kisasa na bora inajengwa kwenye mradi huu kama sehemu za kuleta matokeo Chanya kwa wananchi wa mji wa kahama,” amesisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usimamizi wa Mazingira, , Mamlaka ya Maji Safi wa Mazingira Kahama (KUWASA)Mhandisi , Magige Marwa , ametoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kufadhili mradi huo mkubwa ambao ukikamilika utaondoa changamoto ya upatikanaji maji safi na salama wilayani Kahama,

Ameongeza kwamba mradi wa ujenzi wa chujio la maji mwendakulima unatazamiwa kuhudumia zaidi ya 66% ya wakazi waishio manispaa ya Kahama na una uwezo wa kuzalisha lita milioni 10 kwa siku.

“Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu na mpaka sasa 78% ya mradi mzima umeshakamilika kutokana na kasi ya ujenzi wa mradi huu mkubwa kwenye mji huu wa Kahama,” amesisitiza

Mhandisi Marwa amefafanua kwamba mradi huo wa chujio la maji ya mvua 62% imefadhiliwa na mgodi wa Barrick- Buzwagi na 38% ni KUWASA kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wake , kiongozi wa mbio za mwenge , Ismail Ali Ussi amesema wizara ya maji inaendelea kufanya vizuri na kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kupeleka huduma ya maji mijini na vijijini.

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa wizara na mamlaka za maji hapa kahama kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama,” amesema.

Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda amesisitiza kwamba umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya huduma za wananchi kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 4,2025

 
Magazeti ya leo



 

Share:

ALIJIKUTA KATIKA KESI YA UNYANG’ANYI LAKINI USHAHIDI WA VIDEO ULIMNUSURU


Nilijikuta nikiketi kwenye benchi la mahabusu, machozi yakiwa yamenikauka, akili ikiwa haielewi kilichotokea. Mimi? Miongoni mwa washukiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia nguvu? Nilihisi kama ndoto mbaya iliyojificha kwenye mchana wa jua kali. 

Nilikuwa najiuliza, “Nani angeniamini? Nani angenisaidia kuondoa doa hili kwenye jina langu?”
Share:

Sunday, 3 August 2025

Video Mpya : NG'WANA SIPE - TIKTOK

Share:

Saturday, 2 August 2025

MWILI WA MWANAUME ASIYEJULIKANA WAKUTWA KWENYE DIMBWI LA MAJI KAHAMA

 Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mwili wa mwanaume mwenye umri unaokadiriwa (25-30)  ambaye hajafahamika jina wala Makazi amekutwa amefariki dunia katika dimbwi la Maji linalotumiwa kwaajili ya shughuli za Bustani katika mtaa wa Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Malunde 1 blog  imezungumza na baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Maria Frank mkazi wa mtaa wa Malunga amesema aliubaini mwili huo alipokwenda kuchota maji katika dimbwi hilo ndipo akatoa taarifa kwa waendesha pikipiki waliokuwa karibu na eneo hilo.

"Nimechota maji awamu ya kwanza sikuona kitu ila niliporudi kwa awamu ya pili ndio nikaona Mguu unaelea kwanye dimbwi hilo ambalo linatumiwa kwaajili ya kumwagilia bustani katika eneo hili ambalo lipo jirani karibu na shule ya Msingi Malunga,"amesema Frank.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa Marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwaajili ya Uchunguzi wa madaktari.

"Bado hajajulikana jina wala Makazi,ila nitoe rai kwa Wananchi ambapo kuna madimbwi hatarishi ili kuzuia vifo visivyokuwa na tija,kwani eneo hilo lipo karibu na shule ya Msingi Malunga hivyo ni hatari kwa Maisha ya Wanafunzi,"amesema Magomi.


Share:

MJUE BONDA WILLIAM NKINGA – MGOMBEA UBUNGE KISHAPU 2025



"Kazi na Utu, Kishapu Mpya ya Kimataifa"

Bonda William Nkinga ni kiongozi makini, mzalendo wa kweli na mchapa kazi anayeamini katika maendeleo ya vitendo. Akiwa na historia ndefu ya kulitumikia taifa na jamii, Bonda amejipambanua kama kiongozi anayeweza kuibadilisha Kishapu kuwa kitovu cha maendeleo ya kisasa.


🔰 ASILI NA MAISHA YA AWALI

Bonda alizaliwa mwaka 1969 katika Kata ya Ukenyenge, Wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga. Kutoka katika mazingira ya kijijini, alijifunza thamani ya bidii, nidhamu, na mshikamano wa kijamii – misingi inayomfanya leo kuwa kiongozi wa mfano.


🎓 ELIMU NA UMAHIRI KITAALUMA

Bonda ni msomi aliyebobea katika uhasibu na biashara:

👉MBA – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

👉CPA (T)

👉B.COM – Biashara na Uongozi

Mafanikio haya yamemuwezesha kusimamia kwa ufanisi rasilimali za umma na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa uadilifu.


💼 UZOEFU WA KITAALUMA NA KAZI SERIKALINI

Kwa zaidi ya miongo miwili, Bonda amehudumu katika Wizara ya Kilimo kama Mhasibu Mwandamizi akisimamia miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo:

👉Tanzania Agricultural Inputs Support Project (TAISP)

👉Agricultural Sector Development Programme (ASDP)

Amekuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa fedha za Serikali na michango ya wahisani wa kimataifa kama Benki ya Dunia, AfDB, na JICA, akihakikisha kila shilingi inaleta matokeo kwa wananchi.


🏛 UONGOZI NDANI YA CCM

Bonda si mgeni kwenye siasa za CCM. Kwa miaka mingi amekuwa nguzo muhimu ya chama katika mkoa wa Shinyanga:

  1. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (2012–2022)

  2. Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Kishapu

  3. Naibu Kamanda wa UVCCM – Kishapu (2007–2017)

Kupitia nafasi hizi, amekuwa daraja la kuunganisha chama, serikali na wananchi.


🌍 UONGOZI KATIKA JAMII

Zaidi ya siasa, Bonda ni kiongozi wa kijamii mwenye historia ya kupigania haki na maendeleo ya watu:

👉Mwakilishi wa wafanyakazi – Wizara ya Kilimo

👉Rais wa Serikali ya Wanafunzi SHYCOM (1991–1993)

👉Kilanja Mkuu – Mwadui Sekondari (1989–1990)

👉Mwakilishi wa Wanafunzi – UDSM (1995–1998)

Aidha, alihudumu JKT Kikosi 842 KJ Oparesheni, ambapo alijifunza nidhamu, uzalendo na misingi ya uongozi wa kweli.


🚀 MALENGO YA KISIASA NA KIJAMII

Bonda William Nkinga ana dira ya kulifanya Kishapu kuwa kitovu cha maendeleo:

👉Kuweka msukumo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo.

👉Kuchochea mapinduzi ya kilimo kwa kutumia uzoefu wake wa kitaalamu.

👉Kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.

👉Kusimamia rasilimali za umma kwa uwazi na uwajibikaji.

👉Kukuza viwanda na sekta za uzalishaji ili kuchangia uchumi wa taifa.

👉Kuwaunganisha wananchi na serikali kwa ushirikiano wa dhati.


🌟 BONDA – KIONGOZI WA VITENDO

Bonda Nkinga anaamini kuwa maendeleo ya kweli yanahitaji kiongozi mwenye maono ya mbali, moyo wa kujitolea, na mshikamano na wananchi. Kwa falsafa yake ya “Kazi na Utu”, anataka kuijenga Kishapu mpya yenye maendeleo ya kimataifa.


📧 Email: bonda.nkinga@kilimo.go.tz

🗳 KISHAPU MPYA YA KIMATAIFA – TWENDE NA BONDA NKINGA!


Share:

Friday, 1 August 2025

KAMISHENI YA COSTECH YATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA STU LA COSTECH JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa John Kondolo, ameongoza ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) la COSTECH jijini Dodoma, ambapo amepongeza hatua kubwa iliyofikiwa na mkandarasi anayejenga jengo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Julai 31, 2025 Jijini Dodoma Profesa Kondolo amesema kuwa wamejiridhisha na maendeleo ya ujenzi ambao umeendana na masharti ya mkataba unaotakiwa kukamilika ifikapo Machi 2026.

“Kiwango na ubora wa kazi tulivyoshuhudia vinatupa matumaini makubwa kwamba jengo hili jipya la STU litakuwa na hadhi ya kitaifa na kimataifa katika kuendeleza sekta za sayansi na teknolojia,” amesema Profesa Kondolo.

Ameeleza kuwa jengo hilo linajengwa kwa umadhubuti na heshima inayostahili taasisi muhimu ya COSTECH, hivyo linaonesha kukidhi viwango vya usanifu wa kisasa na matumizi ya muda mrefu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa kutumia fedha za Serikali takriban shilingi bilioni nane za Kitanzania kupitia mradi wa HEET, ukiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuboresha miundombinu ya utafiti na ubunifu nchini.

Dkt. Nungu amefafanua kuwa jengo hilo litakuwa na kumbi za bunifu, kumbi za mikutano ya wanasayansi, na maabara za kisasa zitakazowezesha wabunifu kuwndeleza bunifu zao kwa ufanisi zaidi.

“Tunategemea pia kuwa na nafasi maalum kwa ajili ya wabunifu kupata huduma za Atamizi (incubation) ili kukuza mawazo na ubunifu mpya,baada ya makao makuu kuhamia Dodoma, nafasi iliyokuwa ikitumika Dar es Salaam itatumika kikamilifu kwa ajili ya huduma hizo,” ameeleza Dkt. Nungu.

Aidha, Dkt. Nungu amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutarahisisha uratibu wa shughuli za kitaifa za utafiti na teknolojia kutokana na uwepo wa miundombinu ya kisasa na mazingira bora ya kazi kwa wataalamu na wabunifu.

Kwa upande wake, Msanifu Majengo wa mradi huo, Benedict Martin, ameeleza kuwa usanifu wa jengo hilo umezingatia vigezo vya kisayansi na kiteknolojia kwa kuhakikisha linaendana na mahitaji ya utafiti na ubunifu wa kisasa.

Martin alisema usanifu huo umejumuisha ofisi za kisasa, kumbi za mafunzo, maeneo ya maonyesho ya teknolojia, na mifumo ya kidigitali itakayorahisisha mawasiliano ya kitaifa na kimataifa kwa COSTECH.

“Tumepanga kila kipengele kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha kuwa linaweza kubeba shughuli zote za COSTECH kwa miongo kadhaa ijayo bila kuhitaji mabadiliko makubwa,” alisema Martin.

Kukamilika kwa jengo la STU kunatarajiwa kuimarisha zaidi nafasi ya Tanzania katika utafiti na maendeleo ya kisayansi, ikileta urahisi kwa wanasayansi, wabunifu na sekta binafsi kushirikiana katika kukuza teknolojia na ubunifu nchini.
Share:

FEMINERGY – NGUVU YA MWANAMKE

 

 

💗 FEMINERGY – NGUVU YA MWANAMKE! 💗

Unajisikia kuchoka haraka? Huna hamu ya tendo la ndoa? Maumivu ya hedhi au homoni hazipo sawa?

FEMINERGY kutoka BF Suma ni suluhisho bora kwa wanawake wote wanaopitia changamoto za kiafya na uzazi!
🔥 Inasaidia kwa:

✅ Kuboresha nguvu za mwili na hisia za kimapenzi
✅ Kuimarisha mfumo wa homoni kwa wanawake
✅ Kupunguza maumivu ya hedhi na kuimarisha mzunguko wa kawaida
✅ Kuongeza uzalishaji wa yai (ovulation) kwa wanaotafuta ujauzito
✅ Kurejesha hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

💯 Asilia, salama na imethibitishwa na wataalamu!

📍Inapatikana Kahama – Shinyanga
📦 Tunatuma popote Tanzania 🇹🇿
📲 Wasiliana na Neema Nkumbi:
📞 +255 755 448 022

Feminergy ni zaidi ya virutubisho – ni maisha mapya kwa mwanamke! 🌺

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger