Friday, 25 July 2025
Thursday, 24 July 2025
LUKUVI AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA, ATAKA KUKAMILISHA KABLA YA OKTOBA
Na Dotto Kwilasa,Dodoma
Katika juhudi za kuimarisha utoaji wa huduma serikalini na kutekeleza ndoto ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhamisha ofisi za wizara na taasisi katika Mji wa Serikali Mtumba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, amezitaka taasisi zote husika kuongeza kasi ya usimamizi na kuhakikisha kazi za ujenzi wa majengo yanakamilika kwa wakati.
Akizungumza jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo 34 ya wizara na taasisi katika Mtumba, Lukuvi amesisitiza kuwa licha ya fedha zote muhimu kutolewa, kuna baadhi ya wakandarasi ambao bado wanachelewesha kukamilisha miradi yao, jambo ambalo linapaswa kusitishwa haraka.
“Ujenzi huu ni kipaumbele cha serikali yetu ya Awamu ya Sita, na tunataka uendelee kwa kasi. Tunatakiwa kuhakikisha majengo yote yanakamilika kabla ya Oktoba 2025 ili kufanikisha malengo ya kuwahamisha watumishi na kuleta mabadiliko ya kiutendaji serikalini,” amesema Lukuvi.
Mradi huu una gharama ya jumla ya shilingi bilioni 738, na hadi sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 92.2. Mratibu wa Kikosi cha Kuhamishia Serikali Mtumba, Noeli Mlindwa, ameongeza kuwa serikali imeshatoa shilingi bilioni 544.7 kwa ajili ya ujenzi na tayari majengo 10 yamekamilika na yanatumika kwa huduma kwa wananchi.
Lukuvi pia alisisitiza umuhimu wa kuzingatia matumizi ya samani na vifaa vinavyotengenezwa ndani ya nchi, akitoa mfano wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo tayari imehamia Mtumba kwa kutumia fanicha za mbao za ndani.
Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Mhandisi Benjamini Maziku, aliripoti kuwa ujenzi wa barabara kilomita 51 ndani ya mji huo umekamilika, pamoja na ufungaji wa taa za barabarani na kamera za usalama.
Aidha, serikali imepanga kupanda miti zaidi ya 253,000 katika mji mzima ili kuufanya Mtumba kuwa mji wa kijani na rafiki kwa mazingira.
Ziara ya Waziri Lukuvi ni sehemu ya mikakati ya serikali kuhakikisha mji wa Mtumba unakuwa kituo cha kiutendaji chenye miundombinu imara na huduma bora kwa wananchi, kulingana na malengo ya serikali ya sasa.
Wednesday, 23 July 2025
WATUHUMIWA 125 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI MKOANI SHINYANGA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watu 125 wanaotuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni hadi Julai 22, 2025.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 23, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema operesheni hizo zimehusisha ukamataji wa watuhumiwa wa makosa ya kutumia na kusambaza dawa za kulevya pamoja na wizi wa mali mbalimbali.
Katika operesheni hizo, dawa za kulevya zilizokamatwa ni pamoja na bhangi gramu 2,261, mirungi kilo 29, pamoja na pombe ya moshi lita 142.
Aidha, vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 22, mabati 16, nondo vipande 17, vitanda 4, redio 08, runinga 07 na bajaji 01 ambazo ni mali za wizi na nyingine hazina usajili.
Kamanda Magomi amesema kuwa operesheni hizo zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa salama dhidi ya vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo viovu vinavyofanyika katika maeneo yao.
Tuesday, 22 July 2025
DKT. BITEKO AHANI MSIBA WA MZEE MGANGA NGELEJA
NILIKUWA KIBARUA, SASA NIMEAJIRI WENYE DEGREE

Miaka miwili iliyopita nilikuwa najitahidi tu kuishi. Nilikuwa kibarua wa kubeba mizigo sokoni kazi za kuchafuka mikono, kulala njaa mara kwa mara, na kuamka mapema sana nikisaka riziki ambayo haikuwa na uhakika. Siku moja kuna kazi, kesho hakuna. Nilikuwa na ndoto kubwa sana, lakini sikuwa na mtaji, msaada wala mtu wa kuniinua.
Wakati wenzangu walikuwa wakijipanga na mipango ya maisha kununua pikipiki, kuanzisha biashara ndogo ndogo, hata kusomesha watoto wao mimi nilikuwa nikiishi kwa mkono wa mdomo. Ukipata kazi ya siku hiyo, unakula. Ukikosa, unalala na njaa.Soma zaidi











aa

















