Wednesday, 21 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 23, 2025






















Share:

WIZARA YA KILIMO YAOMBA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 1.24



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imewasilisha mpango wake wa makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ukilenga kuimarisha ajira staha kwa vijana na wanawake kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo na miundombinu ya umwagiliaji.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Wizara yake imepanga kukusanya jumla ya Shilingi 12.26 bilioni kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ambapo Shilingi 8.66 bilioni zitatokana na ukaguzi wa mazao, kodi za majengo na uuzaji wa nyaraka za zabuni, huku Shilingi 3.6 bilioni zikipatikana kupitia ada za umwagiliaji na ukodishaji wa mitambo.

Akizungumza Bungeni leo Mei 21,2025 Jijini Dodoma, Waziri Bashe ameomba Bunge liidhinishe matumizi ya jumla ya Shilingi trilioni 1.24 kwa mwaka huo wa fedha.

Kuhusu miradi ya Maendeleo na Matumizi ya Kawaida, Wizara imeomba Shilingi bilioni 838.26, ambapo Shilingi bilioni 702.28 zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, zikiwemo Shilingi bilioni 424.33 kutoka vyanzo vya ndani na Shilingi bilioni 277.95 kutoka nje.

Fedha nyingine ni Shilingi bilioni 135.98 zitatumika kwa matumizi ya kawaida, ikiwa ni pamoja na Shilingi bilioni 81.45 kwa mishahara ya watumishi na Shilingi bilioni 54.54 kwa matumizi mengine ya wizara, bodi na taasisi zake.

Waziri Bashe amesema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaomba kuidhinishiwa Shilingi bilioni 382.14, kati ya hizo Shilingi bilioni 308.72 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo (zikiwemo Shilingi bilioni 259.62 kutoka ndani na Shilingi bilioni 49.10 kutoka nje), na Shilingi bilioni 73.42 kwa matumizi ya kawaida ambapo Shilingi bilioni 8.27 ni kwa ajili ya mishahara na Shilingi bilioni 65.15 kwa matumizi mengineyo.

Kuhusu Tume ya Maendeleo ya Ushirika, jumla ya Shilingi bilioni 22.58 zinaombwa, ambapo Shilingi bilioni 21.88 ni kwa matumizi ya kawaida (mishahara Shilingi bilioni 12.85, matumizi mengineyo Shilingi bilioni 9.03) na Shilingi milioni 697.18 kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani.

Kwa upande mwingine Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo amesema Ajira kwa Vijana na Wanawake Kwenye Mashamba Makubwa

Mbali na makadirio ya fedha, Serikali imeeleza maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya BBT inayolenga kuimarisha ajira za vijana na wanawake kupitia miradi mitano.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mashamba ya pamoja, mitaji, huduma za ugani, uongezaji thamani wa mazao, na umwagiliaji,Shamba la Chinangali (ekari 1,772) limekabidhiwa kwa vijana 261 na linaendelea kuzalisha mazao mbalimbali.

Aidha, shamba la Ndogowe (ekari 11,453) limekabidhiwa kwa vijana 342, huku miundombinu muhimu ikiwa tayari imejengwa.

Aidha ameutaja mradi mwingine mkubwa ni Shamba la Mapogoro mkoani Mbeya ambalo litafadhiliwa kwa Dola milioni 129 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, ikiwa ni hatua ya kukuza kilimo kikubwa chenye tija nchini.





Share:

MAKAMANDA WA POLISI WAFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya polisi CP Awadhi Juma Haji
Fred Mfikwa Mkuu wa kitengo cha usalama GASCO

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, CP Awadhi Juma Haji, ameongoza Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara—mikoa inayopitiwa na miundombinu ya gesi asilia na kufanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu hiyo inayotoka Msimbati, Madimba hadi Kinyerezi kupitia Somanga.

,Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya GASCO inayosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, CP Awadhi amebainisha kuwa Jeshi la Polisi lina wajibu wa kuhakikisha miundombinu ya gesi asilia inakuwa katika hali ya usalama wa kutosha, kwa kuwa rasilimali hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

“Jeshi la Polisi lina makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya GASCO kupitia TPDC kwa ajili ya kutoa ulinzi kwenye miundombinu ya gesi asilia. Ziara hii ni utekelezaji wa takwa la makubaliano hayo, ambapo kila mwaka tunatakiwa kufanya ukaguzi ili kutathmini hali ya kiusalama,” amesema CP Awadhi.

Amesema ukaguzi huo unaangazia tathmini ya hali ya usalama katika kipindi kilichopita, kutambua changamoto zilizojitokeza na namna zilivyoshughulikiwa, pamoja na kupanga mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi wa miundombinu hiyo.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru wenzetu wa GASCO na TPDC kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kuandaa ziara hii. Ushirikiano huu unatupa nafasi ya kufanya tathmini ya pamoja ya hali ya kiusalama kwenye maeneo yote ya miundombinu ya gesi asilia,” ameongeza.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usalama GASCO,Fred Mfikwa ameeleza kuwa mbali na vyombo vya dola, GASCO pia imeingia mikataba na vijiji vinavyopitiwa na miundombinu hiyo, ambapo wananchi hushiriki katika shughuli za ulinzi na usafi wa maeneo yanayopitiwa na miundombinu ya gesi asilia. 

Mfikwa amesema hatua hii imeongeza urafiki kati ya TPDC na jamii, hali inayowasaidia kupokea taarifa muhimu za kiusalama na kutambua mapema hitilafu zinazoweza kutokea.

Aidha, ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa namna lilivyo mstari wa mbele katika kushughulikia changamoto za kiusalama.

 “Kwa kipindi chote tangu tuingie makubaliano na Jeshi la Polisi, hatujakumbwa na changamoto yoyote kubwa. Polisi wamekuwa wakijitokeza haraka tunapohitaji msaada, na hatua za kisheria huchukuliwa kwa wanaoharibu au kuingilia miundombinu yetu,” amesema.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 21, 2025



Magazetini leo

Magazeti
Share:

Monday, 19 May 2025

DUNIA IMEISHA: MAMA APAGAWA NA KIJANA!



Kuna siku kulijitokeza kisa cha kushangaza mtandaoni baada ya kijana mmoja, Moses, 19, kudai kuwa mama yake bado anamchukulia kama mtoto mdogo, anasema kutokana na kuwa mtoto pekee na wa kiume analizimika kukubaliana na jambo hilo.

Moses anadai kuwa mama yake bado anataka kumnyonyesha angali tayari ni mtu mzima, mama yake hukasirika anapomkataa kila anapomvuta karibu ili kumpa titi zake laini.

Anafichua kwamba mama yake, mwanamke wa makamo katikati ya miaka 49 hivi anaendelea kuvuka mipaka yake, mara nyingi humuomba kulala naye kitandani.
Share:

WATU WOTE WAMEOKOLEWA KWENYE AJALI YA MGODI MWAKITOLYO ...WAPUUZENI WANAOZUA TAHARUKI– DC MTATIRO


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius S. Mtatiro
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius S. Mtatiro, ametoa taarifa rasmi kuhusu ajali ya mgodi iliyotokea katika Mgodi wa Dhahabu wa Mwakitolyo, unaomilikiwa na Kikundi cha Wachimbaji cha "HAPA KAZI TU!", Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, akithibitisha kuwa watu wote waliokuwa kifusini wamepatikana.

Katika taarifa hiyo, Mtatiro amesema kuwa baada ya tukio hilo, alifika eneo la ajali mara moja akiwa na timu za uokozi, na kwa kushirikiana na wananchi, waliendesha zoezi la uokoaji kwa kutumia mashine za kisasa za migodini. 

Mashine zaidi ya 10 zilikuwepo, lakini ni mashine 4 pekee zilizohitajika kukamilisha kazi hiyo.

"Tumefanikiwa kuwaokoa watu 11 wakiwa hai, na watu 6 tumewatoa wakiwa wamefariki. Ukiwa pale eneo la ajali utaona tulihamisha kifusi chote kilichowaangukia watu na kukichambua kwa mashine na mikono, hakukuwa na mtu mwingine yeyote aliyebakia ndani ya kifusi," amesema Mtatiro.

Ameeleza kuwa eneo la ajali ni wazi na pana kiasi kwamba hata mashine 20 za kuchimba zinaweza kuingia kwa wakati mmoja, hivyo wananchi walishuhudia moja kwa moja hatua zote za uokoaji.

Aidha, Mtatiro amesema hakuna mtu yeyote anayekosekana katika eneo la Mwakitolyo na Shinyanga, na familia zote zimethibitisha kuwa watu waliokosekana ghafla ni wale waliopatikana—yaani, 6 waliofariki na 11 wanaoendelea na matibabu.

"Ukiwa pale eneo la ajali utaona tulihamisha kifusi chote kilichowaangukia watu na kukichambua kwa mashine na mikono, hakukuwa na mtu mwingine yeyote aliyebakia ndani ya kifusi, na zoezi la uokoaji lilifanyika wananchi wote wakiwa wanaangalia kwa sababu lile ni eneo la wazi na ni eneo pana ambalo zinaweza kuingia excavators hata 20 kwa wakati mmoja, siyo kwamba ni eneo finyu lisilo na nafasi. 

Pia, na bahati nzuri, eneo la Mwakitolyo na Shinyanga halina mtu yeyote ambaye labda anakosekana "missing person", majirani, ndugu, jamaa, marafiki, wapangaji, wenye nyumba na familia zote za Mwakitolyo na Shinyanga, zinakiri kuwa watu waliokosekana ghafla walikuwa wale 6 waliofariki na wale 11 wanaotibiwa",ameeleza. 

"Kwa hiyo siyo tu kwamba tumekamilisha uokoaji huu kwa uzito wa kipekee, lakini pia tumeongoza kufuatilia ikiwa kuna mtu hapatikani, watu wote wa eneo la ajali wameridhishwa kuwa hakuna mwenzao aliyebakia kwenye kifusi",ameongeza Mkuu huyo wa wilaya.

Mtatiro amesema kuwa majeruhi walioko hospitalini walithibitisha kuwa wakati ajali inatokea, walikuwa watu takribani 17 mgodini na walikuwa wanajuana. 

Aidha, mashine zilifanikiwa kuhamisha kifusi chote, na watu wote walipatikana kutoka humo.

"Kifusi chote kilitolewa eneo la ajali na kuhamishiwa upande mwingine kabisa na ndipo tukapata hao watu 17 kwa mchanganuo huo.  Kama hiyo haitoshi, hata majeruhi walioko hospitalini walitueleza waziwazi siku ya ajali kuwa wakati ajali inatokea mgodini kulikuwa na watu takribani 17 ,wanajuana",amefafanua.

Amesisitiza kuwa taarifa zinazodai kuwepo kwa watu waliobaki chini ya kifusi si sahihi na zinapaswa kupuuzwa.

"Naomba tupuuze taarifa zozote zinazoeleza eti kuna watu, wenzetu, wameachwa chini ya kifusi. Taarifa hizo siyo sahihi, ni potofu, zinalenga kuzua taharuki na zenye malengo yasiyo sahihi - tuzipuuze", amesema Wakili Mtatiro.

Share:

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATAJA MAFANIKIO YAKE KUMI IKIWEMO MAPATO KUONGEZEKA



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetaja mafanikio yake 10 iliyopata katika kipindi cha miaka minne ikiwemo kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii ambapo Serikali imeingiza Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa.

Mafanikio hayo yametajwa leo Mei 19,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo,Dk Pindi Chana wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri Chana amesema Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa.

Aidha, mapato yatokanayo na utalii wa ndani yameongezeka kutoka Shilingi 11 bilioni 46.3 Mwaka 2021 hadi Shilingi bilioni 209.8 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 353.1.

“Hatua hii imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya tisa (9) duniani na kushika nafasi ya tatu (3) Barani Afrika kwa ongezeko la mapato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya UVIKO-19,”amesema Waziri Chana.

Ameyataja mafanikio mengine ni Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali, Tanzania Imeendelea Kutambulika na Kung’ara Kimataifa, Kuimarika kwa Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori, Kuimarika kwa Biashara ya Mazao ya Misitu na Nyuki, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Kurejeshewa Hadhi ya Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (UNESCO Global Geopark).

Mafanikio mengine ni Mafanikio ya 4R za Rais Samia Katika Kukuza Biashara ya Utalii kwa Kuiwezesha Sekta Binafsi, Kuandaa Tuzo za Kwanza za Uhifadhi na Utali, Mafanikio ya Mikakati Mahsusi ya Kutangaza Utalii.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger