Thursday, 15 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 15,2025





Magazeti ya leo



Share:

Tuesday, 13 May 2025

AENDEKEZA ANASA CHUO KIKUU NA KUSAHAU MASOMO, MZAZI AFUNGUKA


Mtoto wangu alijiunga na chuo miezi michache iliyopita na kama unavyojua ni furaha ya kila mzazi kuona mtoto wake akifaulu na kupanda ngazi za juu kimasomo, mafanikio yake yamekuwa ya kusisimua sana kwangu.

Hata hivyo, miezi mitatu baada ya kujiunga na chuo kikuu, nilianza kupigiwa simu na marafiki zake kwamba alikuwa anafanya umalaya na kutumia dawa za kulevya na hata kujihusisha na magenge hatari.

Nilidhani ni uvumi lakini baada ya kupigiwa simu uongozi wa chuo kuwa mwanangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nilijua hali ni mbaya huko tena sana.
Share:

NAIBU WAZIRI UMMY AZINDUA MIRADI YA KIUCHUMI YA WENYE ULEMAVU



Na Mwandishi wetu- Dar es salaam

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amezindua miradi ya kiuchumi ambayo iko chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Strategic Alternative Learning Technique (SALT), inayohudumiwa na vijana wenye changamoto za ufahamu.

Mhe. Nderiananga alifanya uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam kwa miradi ambayo ni pamoja na Salt Special Supermarket, Mgahawa na Bakery itakayohudumiwa na vijana wenye ulemavu wa ufahamu huku akisema jumla ya vijana na Watoto 83 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwa wananchi hatua itakayowasaidia kujipatia kipato chao na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Aidha, Mhe. Nderiananga aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu, kujiwezesha kiuchumi na kusaidia mashirika yanayoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya Awamu ya Sita imeendelea kutoa fedha kwa watu wenye ulemavu ili wafanye kazi zao vizuri. Nimefurahi kuona Shirika hili la SALT linafanya kazi zake kwa ubunifu kwa kuwafundisha stadi za kazi na ubunifu wa mavazi,” alisema Mhe. Nderiananga.

Vilevile, amefafanua kwamba ikiwa kila mmoja atafanya kwa nafasi yake katika kuwawezesha watu wenye ulemavu itaongeza chachu kwao kujituma kufanya kazi kwani vipaji na uwezo wao utatambulika na kuungwa mkono hali itakayoongeza uzalishaji katika Nchi.

“Nitoe wito tuendelee kuliunga mkono Shirika hili na mengine yanayowasaidia watu wenye ulemavu wa aina zote kwani yanafanya kazi kubwa hivyo viongozi wetu wa Serikali za Mitaa tuyapokee mashirika haya na kuwapa ushirikiano kwa manufaa ya Taifa letu.

Aidha alibainisha kwamba watu wenye ulemavu wanahitaji fursa bila kunyanyapaliwa huku akiwataka wazazi na walezi kutosikiliza maneno ya kukatisha tamaa na badala yake wawaamini watoto wao kuwa wana uwezo wa kipekee.

Aliwahimiza wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa katika taasisi mbalimbali ili kuwajengea Watoto kujiamini kuwa wanaweza na wanamchango katika jamii.

“Baadhi ya mafunzo yanayotolewa na SALT ni pamoja na uokaji, mapishi, mitindo ya mavazi na wahudumu katika migahawa hatua inayowajengea ujuzi wa kujipatia kipato ili kuendesha maisha hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Strategic Alternative Learning Technique (SALT), Bi. Rebeca Lebi alieleza kuwa Shirika hilo lilianza mwaka 2019 kwa lengo la kuwasaidia watoto na vijana wenye changamoto za ufahamu ambazo ni Usonji (Autistic Spectrum Disoder), Down syndrome, Mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy ), Ulemavu wa akili (Intellectual Impairment) , Kifafa kikali (Severe epilepsy) na changamoto zote zinazohusiana na ulemavu wa ubongo na ufahamu.

Awali akisoma risala Meneja wa Operesheni kutoka Shirika la SALT, Bi. Jasmine Omary Iddy alisema SALT, ilianzisha chuo cha ufundi na uzalishaji (Vocational training and production) ikiwa na malengo ya kumuandaa kijana mwenye changamoto za ulemavu wa ufahamu kuweza kuwa mzalishaji kupitia mpango wa Viwanda 10 ambavyo vitazalisha bidhaa tofauti, kama vile sabuni za kuogea, shampoo, mafuta ya kupaka, vitambaa vya batiki, mikate na ufugaji wa samaki, kuku pamoja na bustani za mbogamboga.

“Kituo hiki kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana wenye changamoto za kiakili na ufahamu kupata stadi za kazi, stadi za maisha na mazingira salama ya kujifunza na kushiriki katika shughuli za kiuchumi. Lengo letu kuu ni kuwapatia fursa ya kujitegemea, kuongeza thamani katika maisha yao na kupunguza utegemezi kwa familia au jamii,” ameeleza Meneja huyo.



Share:

SERIKALI KUTEKELEZA MFUKO WA UBUNIFU WA SAMIA “SAMIA INNOVATION FUND” WENYE THAMANI YA BIL 2.3

Serikali inatarajia kuanza utekelezaji wa mfuko wa Ubunifu wa Samia “SAMIA Innovation Fund” wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3 utakaotoa mikopo nafuu kwa wabunifu kwa lengo la kuendeleza na kubiasharisha ubunifu pamoja na kutoa fursa za ajira kwa watanzania kupitia kazi za ubunifu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) amebainisha hayo leo tarehe 12 Mei 2025 wakati akiwasilisha bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.

Amesema kuwa lengo la mfuko huo itakuwa ni kuimarisha ubora wa kazi za watafiti na kukuza ushindani wa kitaaluma.

Pia amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa tuzo yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kwa utafiti utakaochapishwa katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa ili kuwahamasisha watafiti na wabunifu kuchapisha na kusambaza matokeo ya kazi zao na kuweza kutumika na wananchi.

Vilevile, Waziri Mkenda amesema kuwa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na ubunifu kikanda na kimataifa, Serikali itaendelea na mapitio ya Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (1996) ili kuwa na sera inayoakisi hali halisi na mahitaji ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Waziri Mkenda amesema, serikali itafanya tathmini ya Sera ya Taifa ya Utafiti na Maendeleo 2010, Sera ya Taifa ya Bioteknolojia 2010 na Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia 2013 ili kubaini hali halisi ya utekelezaji wa sera hizo.

Wabunifu na kazi za ubunifu ni chachu katika kuzalisha teknolojia mpya, kutatua changamoto za kijamii na kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Share:

Monday, 12 May 2025

SERIKALI INABORESHA MIUNDOMBINU YA UMEME KIBITI KUONDOA CHANGAMOTO YA UMEME- KAPINGA

 

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inatekeleza miradi mbalimbali ya matengenezo na ukarabati wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibiti ili kuondokana na tatizo la kukatika kwa umeme kunakotokana na uchakavu wa miundombinu hiyo.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Mhe. Twaha Mpembenwe aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali kutatua tatizo la kukatika kwa umeme Jimbo la Kibiti. 

Ameitaja Mikakati hiyo ni kubadili nyanya za umeme kwa kuweka zenye uwezo mkubwa, kubadili nguzo za umeme na kuweka za zege, kubadili Pin insulators na kuweka mpya, na kufunga vidhibiti matatizo (fault auto recloser) kwenye line zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 50.

Share:

PROF MKENDA ATINGA BUNGENI, LEO NI BAJETI YA HISTORIA

Waziri wa Elimu Mhe Prof Adolf Mkenda akiwasili bungeni leo tarehe 12 Mei 2025 kwa ajili ya kuwasilisha Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2025/2026

Share:

WACHIMBAJI GEITA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA YA SEKTA YA MADINI

▪️Wachimbaji Madini wapongeza upatikanaji wa Leseni na mazingira rafiki ya biashara

▪️Waziri Mavunde aainisha mafanikio 16 ya Rais Samia kwenye sekta ya Madini

▪️Aagiza uanzishwaji wa Soko la Dhahabu Katoro

▪️RC Shigela aja na mikakati mizito ya kupaisha sekta ya madini Geita


Katoro,Geita

Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini wa Mkoa wa Geita wamempongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia sekta ya madini katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.


Hayo yamesemwa Mei 11,2025 kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wachimbaji hao katika eneo la mnada wa zamani Katoro,Geita kwa lengo la kumpongeza Rais Samia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia sekta ya madini.

Akitoa maelezo ya awali,Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Geita(GEREMA) Ndg. Titus Kabuo amesema dhumuni kubwa la kusanyiko hilo ni kumpongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuiboresha sekta ya madini na kuweka mazingira rafiki ya uchimbaji na ufanyaji biashara hali inayopelekea kukua kwa shughuli za uchimbaji na kuathiri chanya maendeleo ya wachimbaji na uchumi wa nchi.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania(FEMATA) Ndg. John Bina amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia sekta ya madini imeshuhudia mabadilko makubwa hasa katika upatikanaji wa Leseni kwa wachimbaji na hatua iliyoanzwa na serikali ya kufanya utafiti wa kina ili kuwaongoza vyema wachimbaji madini nchini.

Akiwasilisha hotuba yake,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ameyataja mafanikio 16 ya Rais Samia S. Hassan katika kuipaisha sekta ya madini kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kufikia 10.1%,ununuzi wa Dhahabu kupitia Benki Kuu,Kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kuelekea lengo la kukusanya Shilingi Trilioni moja na upatikanaji wa mitambo ya kuchoronga 15 kwa ajili yaa wachimbaji wadogo.

Aidha, Waziri Mavunde ametumia fursa hiyo kukipandisha hadhi kituo cha ununuzi wa dhahabu cha Katoro na kuwa soko kamili la Dhahabu la Katoro.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge Joseph Msukuma na Tumaini Magesa wamempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira rafiki ya biashara ambayo yamesaidia kupatikana kwa maendeleo makubwa na kukuza uchumi wa watu wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Martin R. Shigela amesema Mkoa wa Geita umejipanga kuchochea shughuli za madini kwa kuboresha mazingira ya uchimbaji ili kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa wa Geita kupitia upatikanaji wa Leseni zaidi ya 5308 na mitambo ya Uchorongaji ambayo Mhe. Rais ameitoa kwa kwa wachimbaji wadogo.
Share:

Sunday, 11 May 2025

UNESCO - ALWALEED PHILANTHROPIES KICKS OFF ITS SECOND COHORT OF GRANTEES IN TANZANIA



Michel Toto

 By a correspondent in Dar es Salaam

UNESCO in collaboration with the Alwaleed Philanthropies has kicked off the second cohort of grantees, a move meant to support arts and culture education, capacity building, and sustainable community development.

UNESCO Head of Office Michel Toto made the revelations in Dar es Salaam recently during the Kick-Off Meeting for the Second Cohort of Grantees and Knowledge Sharing Session.

The move comes with testimonies indicating that the support to the first cohort grantees has helped to create a positive impact to communities where it was implemented.
Speaking during the session Rose Ngunangwa, Tanzania Media for Community Development (TAMCODE) Executive Director, a grantee from the first cohort thanked UNESCO and Alwaleed Philanthropies saying through the support, her organization in collaboration with community radios and digital platform journalists had been able to publicize the various economic opportunities in Katavi and Rukwa regions and to promote forest conservation, cultural tourism as well as use of clean energy.

“The support helped TAMCODE to also engage with local policy makers in Mpanda and Sumbawanga districts where we came with guidelines for the enactment of the by law on Intangible Cultural Heritage. We are grateful to district authorities, mayors and councilors in the two districts for their commitment to support us,” said Ngunangwa.

The UNESCO–Alwaleed Philanthropies Programme supports community-based development in Tanzania by enhancing the role of culture and arts through Technical and Vocational Education and Training (TVET).

The initiative contributes to unlocking the economic and social potential of cultural heritage and creative industries, with a strong emphasis on youth and women empowerment.

The hybrid session brought together grantees from the first and second cohort, officials from the ministries of culture in mainland and Zanzibar, development partners, as well as UNESCO staff members from Dar es Salaam & Paris.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger