Sunday, 11 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 11,2025





magazeti

Share:

BREAKING NEWS: CHARLES HILARY AFARIKI DUNIA


TANZIA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Charles pia aliwahi mtumishi mwandamizi wa Azam Media Limited kati ya mwaka 2015 na 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.
Share:

Saturday, 10 May 2025

NDUMBARO AHAMASISHA UUNGWAJI MKONO KWA SONGEA UNITED KABLA YA MECHI DHIDI YA COSMO

Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma 

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa Damas Ndumbaro, ametoa kauli kuhusu mchezo wa kesho Jumapili tarehe 11 Mei 2025 kati ya Songea United na Cosmo Politan kutoka Dar es Salaam. 

Waziri Ndumbaro amesisitiza umuhimu wa mchezo huo na kueleza kuwa Cosmo ni timu iliyowahi kushinda ubingwa mara mbili mbele ya vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa.

Aidha, Waziri Ndumbaro ameisifu timu ya Songea United kwa kuonesha kiwango kizuri ilipocheza dhidi ya Yanga, licha ya kufungwa kwa bao moja kwa sifuri katika mchezo uliojaa ushindani mkali na tuhuma za upendeleo. 

Amesema kiwango hicho kinaonesha kuwa Songea United ina uwezo mkubwa wa kushindana na timu kubwa nchini, hivyo inahitaji kuungwa mkono zaidi na jamii ya Songea.

Katika jitihada za kukuza na kuimarisha timu hiyo, Waziri Ndumbaro ametoa wito kwa wenyeviti wa mitaa kuanzisha matawi ya Songea United katika kila mtaa. 

Ameeleza kuwa kuanzishwa kwa matawi hayo kutasaidia kuongeza wanachama, kukuza uchumi wa timu, na kuimarisha mshikamano wa mashabiki wa nyumbani kwa lengo la kuinua soka la Songea.

 Waziri Ndumbaro amewataka wananchi wa Songea kuonesha uzalendo kwa kuvaa jezi za Songea United badala ya kuvaa jezi za timu zingine kama Simba na Yanga. 

Amesisitiza kuwa mafanikio katika soka na maendeleo ya timu ya mkoa yanatokana na mshikamano, ushirikiano na kujitambua kama jamii inayojali maendeleo ya michezo kwao.

Share:

VIONGOZI 4,000 MANISPAA YA SONGEA WAPATIWA MAFUNZO YA KISHERIA


Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma

Takribani viongozi zaidi ya 4,000 wa ngazi ya mashina katika Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, wamepatiwa mafunzo ya kisheria kwa kipindi cha siku tatu kuanzia tarehe 10 Mei 2025.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana Songea Mjini na yamehusisha mabalozi wa nyumba kumi, wajumbe wa mashina pamoja na watendaji wake.

Lengo la mafunzo hayo ni pamoja na kutoa elimu ya utawala bora, uraia, mbinu mbadala za utatuzi wa migogoro, mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia pamoja na elimu ya uchaguzi.

Akifungua rasmi mafunzo hayo, Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ameambatana na timu nzima ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (Samia Legal Aid).
Waziri Ndumbaro ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mifumo ya utoaji haki kwa wananchi, huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mshikamano na imani ya wananchi kwa Serikali kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, Mhe. Ndumbaro ameeleza kuwa msaada wa kisheria uliotolewa kwa wananchi wa Songea ni sehemu ya shukrani kwa ukarimu mkubwa waliouonesha kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni Mkoani Ruvuma.

Amesema kuwa ziara hiyo siyo tu imeleta heshima kwa mkoa huo, bali pia imechochea Serikali kuendelea kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi zikiwemo barabara, vituo vya afya na huduma za elimu.

Katika kuhitimisha Waziri Ndumbaro ametoa wito kwa wananchi wote waliojiandikisha kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa kupiga kura, akisisitiza kuwa hiyo ni njia mojawapo ya kulinda na kudumisha demokrasia na maendeleo ya taifa.

Amesisitiza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika jamii.



Share:

MAREHEMU KAKATAA KUZIKWA NA KUIBUA TAFRANI MJINI



Mji mdogo wa Kisii nchini Kenya ulijikuta katika majonzi na mshangao huku mwili wa Fetty Moraa, anayedaiwa kuuawa na mumewe, ukikataa kuzikwa hadi pale Kiwanga Doctors ambao ni wabobezi wa tiba asilia walipoingilia kati suala hilo.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwaka 2021 na kuibua mshtuko kwa jamii, mamlaka za eneo hilo zilichukua hatua haraka za kumkamata mume wa Moraa ambaye ni mshukiwa mkuu wa uhalifu huo wa kutisha.

Walakini, kilichofuata ni hali ambayo sio ya kawaida iliyoacha gumzo katika eneo hilo, hali hiyo ni kwamba mwili huo uligoma kuzikwa jambo ambalo liliwaacha katika sintofahamu waombolezaji.
Share:

Friday, 9 May 2025

TET NA TANZANIA AI COMMUNITY KUSHIRIKIANA KUBORESHA UFUNDISHAJI KWA TEKNOLOJIA YA AI


TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imepanga kufanya mafunzo ya kukuza uwezo kwa wakuza mitaala na walimu nchini kwa kutumia Akili Mnemba (AI) ili kukuza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.

Hayo yamebainishwa leo Mei 9, 2025 Jijini Dar es Salaam, wakati TET wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitatu na Taasisi ya Tanzania AI Community kwa lengo la kuingiza matumizi ya AI katika ufundishaji na ujifunzaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema jukumu lao kubwa itakuwa ni kuhakikisha kwamba wadau hao wa teknolojia wanapata karikulam, silabasi na vitabu ili waweze kuwasaidia kuweza kutumia AI katika ufundishaji na ujifunzaji.

"Haya ni mapinduzi makubwa kwa hatua zinazoendelea kupigwa, kwa sasa duniani kuna maendeleo makubwa sana katika sayansi na teknolojia, kwahiyo matumizi ya AI katika ufundishaji na ujifunzaji yatampunguzia sana mzigo mwalimu," amesema Dkt. Aneth

Amesema lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanawafiki walimu wote nchini wanaoweza kutumia teknolojia hiyo katika jirahisisha ufundishaji na ujifunzaji, na kwamba katika mtaa mpya wataingiza kipengele cha kutumia AI katika ifundishaji na ujifinzaji.

Aidha Dkt. Aneth ameishukuru Taasisi ya Tanzania AI Community kwa kuwa tayari kushirikiana na TET, hivyo wapo tayari kutimiza majukumu yao kama TET kuhakikisha wanaendana na teknolojia iliyopo kwa sasa/

Naye, Mkurugenzi wa Tanzania AI Community, Essa Mohamedal, amesema wamefurahi kushirikiana na Taasisi ya Elimu kwakuwa wataweza kuwaongezea uwezo walimu wote nchini na kuwafanya watekeleze vizuri zaidi majukumu yao.

"Tuko hapa kwaajili ya kuwapatia walimu zana muhimu zitakazowasaidia kufundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi, na tunafurahisana kushirikiana na TET katika kuhakikisha AI inatumika kuleta mapinduzi ya elimu nchini," amesema Mohamedal.

Share:

TANZANIA UAE KUSHIRIKIANA KUWEZESHA ELIMU KIDIJITALI NCHINI


Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesaini makubalino na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ya kushirikiana katika Teknolojia ya Shule Kidijitali.

Makubaliano hayo yamesainiwa tarehe 8 Mei Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo na Dkt Waleed Ali Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Shule Kidijitali ya UAE.

Utiaji saini makubaliabo hayo umeshuhudiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Balozi wa UAE Nchini Balozi Khalifa Abdulrahman Mohamed Abdulrahman Al Marzouqi
Share:

Thursday, 8 May 2025

TBS YATOA WITO KWA WAZALISHAJI WA NISHATI SAFI KUFUATA VIWANGO

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WADAU mbalimbali wa tasnia ya kutengeneza nishati safi za kupikia nchini wameshauriwa wanapokuwa kwenye mchakato wa kutengeneza nishati hizo kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kupata viwango vya kutengeneza nishati hizo.

Wito huo ulitolewa na Afisa Viwango wa TBS, Mhandisi Mohamed Kaila, wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika kongamano la siku tatu la nishati safi ya kupikia kwa nchi za Afrika Mashariki lililofanyika jijini Arusha wiki hii.

Alisema TBS ina maabara na vifaa vya kupima vifaa vya nishati safi za kupikia, hivyo jukumu lao ni kuhakikisha vifaa vyote vinavyoingia kutoka nje na vinavyozalishwa nchini vinakuwa vinakidhi viwango vya nishati safi ya kupikia, kwani shirika hilo lina wataalam wa kutosha na kila siku wanapima vifaa hivyo .

Aidha, alisema TBS inathibitisha ubora kwa wazalishaji wa ndani wanaozalisha bidhaa za nishati safi za kupikia na kwamba wakishamthibitisha anakuwa amepata leseni ya ubora kuwa anaweza kuuza ndani na nje ya nchi bila tatizo lolote.

"Kwa hiyo tunatoa wito kwa wazalishaji wa ndani wanaozalisha nishati safi za kupikia na wale wanaoagiza kutoka nje ya nchi kufika TBS ili kuhudumiwa katika suala zima la viwango vya nishati safi pamoja na uthibati," alisema Kaila na kuongeza;

"Kwa hiyo nishati safi ya kupikia bila TBS kutakuwa hakuna nishati safi ya kupikia nchi hii, kwa hiyo tunawashauri wadau wakati wakiwa kwenye tasinia nzima ya nishati safi ya kupikia kukaa na sisi kupata huduma zao za kutengeneza viwango .

Alisema TBS ndiyo wenye jukumu mama la kutengeneza viwango ili kuhakikisha nishati safi ya kupikia inakuwa kweli nishati safi ya kupikia.

Alisema katika kutekeleza jukumu lao hilo kuna vitu vya msingi wanaviangalia ambapo kitu cha kwanza ni usalama wa nishati safi za kupikia lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wnakuwa na uhakika kuwa vifaa hivyo viko salama.

Aidha, Kaila alisema pia wanaangalia suala la afya ili kumlinda mpishi , kwani wakati wa kupika kuna vitu vinaweza vikatokea kama moshi endapo nishati inayotumika si safi.

"Kwa hiyo kwetu sisi ili kufika kwenye nishati safi ya kupikia TBS tunaangalia suala hilo kwa umakini sana ili kulinda mtumiaji wa hiyo nishati," alisema Kaila.

Alitaja jambo lingine kuwa ni kuhakikisha wanatunza mazingira, hivyo wakati wa kutengeneza viwango vya hizo nishati, TBS wanahakikisha mazingira yanatuzwa..

Kwa mujibu wa Kaila jambo lingine wanaloangalia TBS ni uimara, kwani hawataki mtu anunue jiko leo baada ya miezi mitatu liwe limeharibika.

Pia Kaila, alisema jambo lingine wanaloangalia ni ufanisi wa nishati safi za kupikia ukoje, hivyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara , Wizara ya Nishati pamoja na wadau wa kitaifa na nje kama UNDP wameshirikiana kuweka viwango ili kupata nishati safi za kupikia .

Alisema kulingana na majukumu ya TBS kama hawatafanya vizuri kama wanavyoendelea kufanya vizuri hiyo nishati safi ya kupikia haitakuwa nishati ya kupikia.

Naye Afisa Afisa Viwango Spiradson Kagaba, alisema wakati tunaelekea kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia wanatakiwa kuhakikisha hakuna kinachoharibika,kwa maana ya kuhakikisha mtumiaji anakuwa salama na mazingira yanakuwa salama.

"Lakini pia mtumiaji aweze kupata kitu ambacho kiko kwa mujibu wa viwango," alisema Kagaba.

Alisema mojawapo ya matakwa ya viwango ni mzalishaji aseme ni kwa namna gani yale majiko yanafaa, anaweza kuja akasema ufanisi wake ni asilimia 90 kama TBS haijasimama ikamwambia yule mtu ni asilimia 80 ni rahisi sana huyo mtu kudanganya.

"Kwa hiyo sisi TBS tunaingia kuangalia yule mtu aliyetuambia ni la asilimia 80 ni asilimia 80 kweli anachosema mzalishaji," alisema.

Alifafanua kwamba TBS imefanya mambo mengi imeandaa viwango ili vitumike kuwalinda watu na kwamba wana viwango vya teknolojia zote kama ilivyotajwa kwenye mkakati.
Share:

WACHIMBAJI MADINI WAIPONGEZA REA KWA KUWAFIKISHIA UMEME

 

📌Ni kupitia Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati

📌Umeme umeleta ukombozi, uzalishaji madini waongezeka Geita

Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati, Viwanda vidogo na vya kati pamoja na maeneo ya kilimo umepokelewa kwa furaha na wananchi mkoani Geita mara baada ya kupata umeme wa uhakika katika migodi yao.

Hayo yamebainishwa na wachimbaji wadogo wa madini wakati wakizungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) mara baada ya kutembelea maeneo ya shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Magema katika ziara iliyolenga kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa mkoani Geita.

Share:

BARAZA LA HABARI KENYA LAVUTIWA NA MAIPAC, LAAHIDI KUSHIRIKIANA KUTOA MAFUNZO KWA WANAHABARI


Mkurugenzi mtendaji MAIPAC,Mussa Juma akimkabidhi Mkurugenzi wa mafunzo na Maendeleo wa baraza la habari Kenya Victor Bwire kitabu cha maarifa ya asili katika uhifadhi wa mazingira kilichoandaliwa na MAIPAC ambacho kinasambazwa bure
Mwandishi wetu,maipac

Baraza la Habari la Kenya(KMC),limetembelea Ofisi za Taasisi ya wanahabari ya usaidizi wa jamii za pembezoni(MAIPAC) jijini Arusha na kuvutiwa na kazi za Taasisi hiyo na kuahidi kushirikiana kuwajengea uwezo wanahabari juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Matumizi sahihi ya akili mnemba(AI).

Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo wa baraza hilo,Victor Bwire akizumgumza na watendaji wa MAIPAC baada ya kupata taarifa za utendaji wa shirika hilo,licha ya kupongeza ameahidi baraza hilo kushirikiana na MAIPAC kuwajengea uwezo wanahabari.

"Kuna waandishi wa habari wa Kenya pia wanafanyakazi na hizi jamii za pembezoni hivyo tutawaunganisha na wanachama wa MAIPAC kupata mafunzo zaidi ya juu ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya AI kwa sababu mazingira yanafanana",amesema.

Bwire amesema, jamii za pembezoni za Tanzania na Kenya zinaendelea kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kwa wanahabari ni muhimu kusaidia jamii hizo kuwapa elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kuweza kuhimili mabadiliko hayo.

"Nawapongeza sana MAIPAC kwa miradi yenu ,nyie kama wanahabari mnafanyakazi nzuri sana katika jamii hizi katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi,miradi ya kurekodi maarifa ya asili lakini pia miradi ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto",amesema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC Mussa Juma amesema taasisi ya MAIPAC inaundwa na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali Tanzania ambao wamekuwa wakiandika masuala ya mazingira na katika jamii za pembezoni.

Juma amesema , MAIPAC imekuwa na miradi kadhaa ikiwepo kurekodi maarifa ya asili kwa jamii za pembezoni katika uhifadhi wa mazingira,misitu na vyanzo vya maji.

"Lakini pia tumekuwa na mradi wa kusaidia jamii kutunza vyanzo vya maji,mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto",amesema

Amesema miradi hiyo,inafadhiliwa na taasisi kadhaa ikiwepo mfuko wa mazingira duniani(GEF) kupitia programu ya miradi midogo ambayo inaratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) Tanzania na ofisi ya makamu wa Rais Mazingira na shirika la kimataifa la Cultural Survival.

Hata hivyo amesema kwa wanahabari wanachama wa MAIPAC wanahitaji sana mafunzo juu ya masuala mabadiliko ya tabia nchi,masuala ya akili mnemba na masuala ya biashara ya hewa ya ukaa na taratibu zake.

Katika ziara hiyo, Bwire ameambatana na viongozi wengine wa MAIPAC, Stella Kaaria Meneja wa utafutaji fedha na mahusiano,Careen Mang'eni na Evaes Teddy.
Share:

Wednesday, 7 May 2025

WAKUU WA TAASISI ZA HABARI WASHUHUDIA UWASILISHAJI BAJETI YA HABARI

 Wakuu wa  Taasisi za Kihabari nchini kwenye picha ya Pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma na  Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Greson Msigwa baada ya uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya habari, utamaduni, Sanaa na Michezo  Bungeni Leo Jijini Dodoma. 

Wakuu hao ni pamoja na Katibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),  Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Misa Tanzania {Misa Tz), Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Wafanyakazi Waandishi wa Habari Nchini (Jowuta) na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri TEF, Caren-Tausi Mbowe pamoja na  Mhariri Mkuu mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah.

Share:

MKAGUZI WA USHIRIKA MKOA WA RUVUMA ATOA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UHASIBU KWA VYAMA VYA USHIRIKA MBINGA NA NYASA


Mkaguzi wa Ushirika Jackson Sinde akitoa Mafunzo ya Usimamizi na Uhasibu kwa Vyama vya Ushirika Mbinga na Nyasa katika ukumbi wa Mbicu Hotel Wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma
Wajumbe wakiwa kwenye mafunzo
Wajumbe wakiwa kwenye mafunzo

Na Regina Ndumbaro Mbinga-Ruvuma 

Katika juhudi za kuimarisha usimamizi wa fedha na uwajibikaji ndani ya vyama vya ushirika, Mkaguzi wa Ushirika Mkoa wa Ruvuma, Bw. Jackson Sinde kutoka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma(COASCO)ameendesha mafunzo kwa watendaji na wajumbe wa bodi wa vyama vya ushirika katika halmashauri za Mbinga Mji, Mbinga Vijijini na Nyasa. 

Mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu juu ya taratibu za uhasibu, umuhimu wa ukaguzi wa hesabu, na wajibu wa bodi katika kulinda mali za vyama kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya ushirika.

 Mafunzo hayo yamefanyika kwa watendaji wa vyama ambapo wamekumbushwa umuhimu wa kuzingatia taratibu za uhasibu kwa uwazi na usawa katika miamala ya kifedha. 

Vilevile, wameelekezwa namna bora ya kujiandaa kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu unaofanywa na COASCO na kuhamasishwa kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza uwezo wao wa kutekeleza majukumu ya kila siku kwa ufanisi.

Tarehe 07 Mei 2025, mafunzo hayo yameendelea katika ukumbi wa Mbicu Hotel ambapo yamewahusisha wajumbe wa bodi waliopata mwongozo wa kusimamia kwa karibu utendaji wa watendaji, kuhakikisha taarifa za kifedha zinaandaliwa kwa wakati na kwa usahihi, na kuhakikisha zoezi la ukaguzi linafanyika kwa mujibu wa ratiba. 

Pia wamesisitizwa kuwajibika kwa kuhakikisha vyama vyao vinafuata miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa ushirika.

Hata hivyo, changamoto kubwa iliyobainika ni kuwepo kwa vyama takribani 30 kutoka halmashauri hizo tatu ambavyo bado havijawasilisha taarifa za fedha na nyaraka muhimu kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu, licha ya kutakiwa kufanya hivyo hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2024. 

Hili imeonyesha hitaji la kuimarisha uwajibikaji zaidi na kufuatilia utekelezaji wa wajibu wa vyama hivyo kwa karibu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger