Sunday, 11 May 2025
BREAKING NEWS: CHARLES HILARY AFARIKI DUNIA

Saturday, 10 May 2025
NDUMBARO AHAMASISHA UUNGWAJI MKONO KWA SONGEA UNITED KABLA YA MECHI DHIDI YA COSMO
Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa Damas Ndumbaro, ametoa kauli kuhusu mchezo wa kesho Jumapili tarehe 11 Mei 2025 kati ya Songea United na Cosmo Politan kutoka Dar es Salaam.
Waziri Ndumbaro amesisitiza umuhimu wa mchezo huo na kueleza kuwa Cosmo ni timu iliyowahi kushinda ubingwa mara mbili mbele ya vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa.Aidha, Waziri Ndumbaro ameisifu timu ya Songea United kwa kuonesha kiwango kizuri ilipocheza dhidi ya Yanga, licha ya kufungwa kwa bao moja kwa sifuri katika mchezo uliojaa ushindani mkali na tuhuma za upendeleo.
Amesema kiwango hicho kinaonesha kuwa Songea United ina uwezo mkubwa wa kushindana na timu kubwa nchini, hivyo inahitaji kuungwa mkono zaidi na jamii ya Songea.
Katika jitihada za kukuza na kuimarisha timu hiyo, Waziri Ndumbaro ametoa wito kwa wenyeviti wa mitaa kuanzisha matawi ya Songea United katika kila mtaa.
Ameeleza kuwa kuanzishwa kwa matawi hayo kutasaidia kuongeza wanachama, kukuza uchumi wa timu, na kuimarisha mshikamano wa mashabiki wa nyumbani kwa lengo la kuinua soka la Songea.
Waziri Ndumbaro amewataka wananchi wa Songea kuonesha uzalendo kwa kuvaa jezi za Songea United badala ya kuvaa jezi za timu zingine kama Simba na Yanga.
Amesisitiza kuwa mafanikio katika soka na maendeleo ya timu ya mkoa yanatokana na mshikamano, ushirikiano na kujitambua kama jamii inayojali maendeleo ya michezo kwao.
VIONGOZI 4,000 MANISPAA YA SONGEA WAPATIWA MAFUNZO YA KISHERIA

Waziri Ndumbaro ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mifumo ya utoaji haki kwa wananchi, huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mshikamano na imani ya wananchi kwa Serikali kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

MAREHEMU KAKATAA KUZIKWA NA KUIBUA TAFRANI MJINI
Friday, 9 May 2025
TET NA TANZANIA AI COMMUNITY KUSHIRIKIANA KUBORESHA UFUNDISHAJI KWA TEKNOLOJIA YA AI
TANZANIA UAE KUSHIRIKIANA KUWEZESHA ELIMU KIDIJITALI NCHINI
Thursday, 8 May 2025
TBS YATOA WITO KWA WAZALISHAJI WA NISHATI SAFI KUFUATA VIWANGO
WACHIMBAJI MADINI WAIPONGEZA REA KWA KUWAFIKISHIA UMEME
📌Ni kupitia Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati
📌Umeme umeleta ukombozi, uzalishaji madini waongezeka Geita
Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati, Viwanda vidogo na vya kati pamoja na maeneo ya kilimo umepokelewa kwa furaha na wananchi mkoani Geita mara baada ya kupata umeme wa uhakika katika migodi yao.
Hayo yamebainishwa na wachimbaji wadogo wa madini wakati wakizungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) mara baada ya kutembelea maeneo ya shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Magema katika ziara iliyolenga kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa mkoani Geita.
BARAZA LA HABARI KENYA LAVUTIWA NA MAIPAC, LAAHIDI KUSHIRIKIANA KUTOA MAFUNZO KWA WANAHABARI
Wednesday, 7 May 2025
WAKUU WA TAASISI ZA HABARI WASHUHUDIA UWASILISHAJI BAJETI YA HABARI
MKAGUZI WA USHIRIKA MKOA WA RUVUMA ATOA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UHASIBU KWA VYAMA VYA USHIRIKA MBINGA NA NYASA


































