Wednesday, 7 May 2025

POLISI POLISI WAZIONDOA HOFU ASASI ZA KIRAIA USALAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU


Nihifadhi Abdulla

JESHI LA POLISI ZANZIBAR limezitoa hofu Asasi za Kiraia zinazoendelea kusimamia haki za Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ZNZ ambapo limesema litaendelea kuhakikishia Haki, Ulinzi na Usalama kwa makundi hayo katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu Mwaka huu 2025 zinalindwa kikamilifu.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Khamis Kombo Khamis alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa Asasi za Kiraia zinazotetea haki za Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu zilizofika katika Afisi kuu za Jeshi hilo Ziwani Wilaya ya Mjini Unguja katika kikao maalum cha kujadili mustakbali wa ulinzi na usalama wa makundi hayo wakati wa Uchaguzi.


Aidha Kamishna Khamis ameziasa asasi hizo kufikia pia wadau na taasisi nyengine muhimu nchini ili kwenda sambamba na azma hiyo.


Alizitaja taasisi nyengine kuwa ni pamoja na Vyama vya Siasa, Vikosi vyengine vya Ulinzi na Tume ya Uchaguzi. Alieleza pia kuna haja ya kuwaelimisha wananchi jinsi ya kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa sheria ili kujiweka katika hali ya usalama.


Kamishna amesisitiza pia kuwa Jeshi la polisi lina utaratibu mzuri wa kuwawajibisha maafisa wake pindi wakienda kinyume na utaratibu wa kazi.


Wakizungumza katika kikao wana Asasi hao wameliomba Jeshi hilo kuendelea kuwa msimamizi namba moja wa amani wakati wa uchaguzi sambamba na kuwalinda Wanawake pamoja na Watu wenye Ulemavu ili waweze kuwa salama na kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia kama wapiga kura, wagombea na mawakala.


Walisema mwaka 2020 baadhi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu walipatwa na kadhia ya uvunjifu wa haki zao kutoka kwa Vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini kama wagombea na mawakala na hivyo kujenga hofu kuhusu ushiriki wao kwa mwaka 2025.


Asasi hizo zimeahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa makundi hayo na kufatilia ushiriki wao katika kipindi hicho cha Uchaguzi Mkuu.


Kikao hicho kilichofanyika Mei 2 huko katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo zimewakutanisha Wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia Zanzibar zinazotetea, kulinda na kusimamia haki za Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu zikiwemo Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya inayoshughulika na Changamoto za Vijana Zanzibar (ZAFAYCO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ).
Share:

MHE. CHATANDA AMPONGEZA RAIS KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI


Na Mwandishi Wetu..

Mwenyekiti wa UWT- CCM Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 25 inayotekelezwa wilayani Rufiji na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Mbali na kumpongeza Mhe. Rais Samia, pia amempongeza Mbunge wa Rufiji kwa kusimamia utekelezaji wake ambapo amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na ina tija kubwa kwa wananchi.
"Hapa naomba niungane na watanzania wote kumpongeza Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya nchi nzima, na hapa leo Rufiji tunashuhudia kazi nzuri ambayo imetekelezwa kupitia miradi hii" amesisitiza Mhe Chatanda

Mhe Chatanda ambaye yupo kwenye ziara ya siku mbili katika jimbo la Rufiji amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Mbambe linalojengwa kwa urefu wa mita 81 na ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha barabara kuu ya kilomita 3 itakayogharimu bilioni 24.1.
Mkataba wa daraja hilo ulisainiwa na Wakala wa Barabara Tanzania na Mkandarasi M/S Nyanza Road Works Ltd ya Mwanza ambapo kazi hiyo inatarajia kukamilika katika kipindi Cha miezi 6 kuanzia sasa.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa daraja hilo Mhe. Mchengerwa alifafanua kuwa mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii wilayani Rufiji maeneo jirani.
Rashid Salum Mkazi wa Ikwiriri amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambapo amesema kukamilika kwake kutakuwa msaada mkubwa kutokana na adha kubwa walihokuwa wakipata hapo awali.

Aidha, Mhe. Chatanda ameshuhudia utiaji saini wab mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Mloka, Mbinju Mvuleni na Ndundutawa ambapo pia ameshuhudia zoezi la kupewa mabati 45 na Mhe. Mbunge vijana wa bodaboda wa kijiji cha Mloka ili kuezekea eneo la kuegesha bodaboda zao.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Rufiji Mhandisi Alkam Omari pamoja na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali katika kuwapatia wananchi maji safi na salama, mahitaji ya maji yamezidi kuongezeka ambapo amesema mradi huu unakwenda kuwa suluhisho.


Share:

Tuesday, 6 May 2025

TEHAMA KUBORESHA ELIMU KWA MAFUNZO YA WALIMU


TEHAMA ni nyenzo muhimu katika sekta ya elimu, kwa kutambua hilo Serikali imewezesha mafunzo kwa walimu ili kuongeza maarifa na kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji ngazi mbalimbali za elimu.

Ameeleza hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Aprili 06, 2025 akizungumza na Clouds TV kuhusu maandalizi ya Kongamano la eLearning Africa 2025 kuanzia tarehe 7 hadi 9 Mei, 2025 JNICC jijini Dar es Salaam.

‘’matumizi ya TEHAMA yanatumika kikamilifu katika sekta ya elimu, walimu wote wamefundishwa namna ya kutumia teknolojia katika kufundisha, lengo letu ni kuhakikisha wana maarifa na mbinu za kidijiti zinazochagiza ujifunzaji’’ Alisema Prof. Nombo.

Amesema kongamano hilo linatoa fursa mbalimbali kwa nchi, ikiwa ni pamoja na maonesho ya bunifu na teknolojia zikiwemo zilizobuniwa na vijana wa kitanzania zinazolenga kutoa suluhu za kidijiti na kielimu.
Share:

AMREF TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA MKUNGA DUNIANI 2025



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akipewa maelezo katika banda la Amref Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza na wananchi, wageni na wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Wananchi na wageni mbalimbali wakipata maelezo katika banda la Amref Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Shinyanga.
Wageni na wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akiwa katika picha ya pamoja na wageni na wadau wa maendeleo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Watumishi wa Shirika la Amref Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Shinyanga.

****
Katika kuadhimisha Siku ya Mkunga Duniani kitaifa iliyofanyika mkoani Shinyanga, Shirika la Amref Health Africa Tanzania limeeleza mafanikio makubwa ya Mradi wa Thamini Uzazi Salama, unaolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa wanawake na watoto wachanga kupitia uwezeshaji wa wakunga na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Zimamoto, Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana wa Amref Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa alisema:

 “Mradi huu unafadhiliwa na Global Affairs Canada (GAC) na unasimamiwa na UNFPA. Unalenga kuongeza upatikanaji wa wakunga wenye ujuzi na kuboresha huduma katika vituo vya afya, taasisi za mafunzo na kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii”.

Dkt. Mkuwa aliongeza kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, mradi huo umefanikiwa kuwafikia watu 17,167 kupitia uhamasishaji wa afya ya uzazi, jinsia na ukatili wa kijinsia (GBV), kutoa mafunzo kwa waelimishaji rika wa kiume 142, na kuimarisha uwezo wa wasimamizi 112 wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHW) kupitia jukwaa la LEAP.

 “Mradi pia umewezesha CHW 112 kwa kuwapatia simu za mkononi, kuwawezesha viongozi wa jamii 424 kuhusu jinsia na haki za afya ya uzazi, na kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za usimamizi wa vituo vya afya na wakuu wa vituo 518 kuhusu bajeti na mipango ya afya,” alieleza zaidi Dkt. Mkuwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, aliishukuru Serikali kwa kuimarisha miundombinu ya afya mkoani humo, akisema:

Kati ya mwaka 2015/2016, asilimia 66 ya wanawake walijifungulia katika vituo vya afya. Kwa sasa idadi imeongezeka hadi asilimia 85. Hii ni hatua kubwa kuelekea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.”

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania, Dkt. Beatrice Milike, alisisitiza mchango wa wakunga nchini.

Wakunga hutoa asilimia 90 ya huduma za afya ya uzazi nchini. Ikiwa watawezeshwa kwa mafunzo na vifaa, wanaweza kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa zaidi ya asilimia 87,” alisema Dkt. Milike.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Mkunga ni Nguzo Muhimu katika Kila Janga”, ikionyesha umuhimu wa wakunga hasa katika nyakati za dharura kama vile majanga ya kiafya na kijamii.

Mradi wa Thamini Uzazi Salama umeendelea kuwa mfano bora wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika ya kimataifa na jamii katika kuhakikisha uzazi salama na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika kwa mama na mtoto nchini Tanzania.
Share:

MATHIAS CANAL ASHINDA TUZO YA SAMIA KALAMU AWARDS, WAZIRI ULEGA AMPA SHAVU MBELE YA RAIS SAMIA









Na Dotto Kwilasa,DAR




Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal ameshinda Tuzo mbili za SAMIA KALAMU AWARDS sekta ya Ujenzi na chombo bora cha mtandaoni.




Pamoja na zawadi ya Cheti, Ngao, Tsh Milioni 10, lakini pia Mathias Canal amezawadiwa safari ya kwenda nchini Japani pamoja na kufanya kazi ya kusafiri nchi nzima kueleza kwenye vyombo vya habari mafanikio na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.







Tuzo hizo zimetolewa leo tarehe 5 Mei 2025 katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan








Tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari watanzania kwa lengo la kuhamasisha, kuhimiza na kukuza wigo wa uchakataji, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari.






Tuzo hizi zitahusisha maudhui yaliyochapishwa kupitia magazeti, redio, televisheni, majukwaa ya mtandaoni pamoja na tuzo kwenda kwa vyombo vya habari. Tuzo hizi zinahusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari 01 hadi Oktoba 26, 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Mhe Abdalah Ulega, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa pamoja na zawadi ya Tuzo pia Waziri Ulega amempa zawadi ya kufanya kazi katika wizara hiyo hivyo akaripoti Wizarani kwa ajili ya kuanza kazi.


Aidha, utoaji wa tuzo hizi umelenga kuchochea uandishi wa makala zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi kuhusu maendeleo ya nchi, uwajibikaji, uzalendo na kujenga chapa na taswira ya nchi.







Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 6,2025





Magazetini leo
   

Share:

Monday, 5 May 2025

KAMHONGA MKE WANGU SH5.7 MILIONI LAKINI HAJAAMBULIA KITU


Jina langu ni Frey, tumeishi na mke wangu Tuma kwa miaka 12 ndani ya ndoa yetu, naweza kusema kati ya wanaume duniani ambao wamefaidi matunda ya ndoa mimi ni mmoja wapo.

Nasema hivyo kwa sababu tangu nimemuoa huyu mke wangu sikumbuki kama kuna siku tumewahi kugombana au kununiana ndani ya nyumba, muda wote kwetu sisi ni upendo tu.

Pia mke wangu ni nzuri sana kisura na kiumbo, ni vidume wengi sana mtaani na sehemu mbalimbali vimekuwa vikimmezea mate, kila anapokatiza lazima watu wageuke kumtazama hata wanawake wenzake hufanya hivyo.
Share:

SHINYANGA WENYEJI MAADHIMISHO SIKU YA MKUNGA DUNIANI KITAIFA







Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MAADHIMISHO ya Siku ya Mkunga Duniani Kitaifa yanafanyika mkoani Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Seif Shekalaghe.

Maadhimisho hayo yameanza leo Mei 4,2025 na yatahitimishwa kesho Mei 5 na yanafanyika katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga.

Rais wa Chama Cha Wakunga wa Tanzania (TAMA)Dk. Beatrice Mwilike, akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu wameamua kuyafanyia mkoani Shinyanga, ili kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi juu ya masuala ya afya ya uzazi, na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

“Maadhimisho ya siku ya ukunga duniani kitaifa hapa nchini Tanzania, mwaka huu tumeamua kuyafanyia hapa mkoani Shinyanga,na Mgeni Rasmi atakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Seif Shekalaghe,”amesema Dk Mwilike.


Aidha,amesema katika maadhimisho hayo, elimu mbalimbali zitatolewa bure kwa wananchi, yakiwamo masuala ya afya ya uzazi,pia kutakuwa na huduma ya utoaji wa damu salama ili kuchangia benki ya damu,na hata kuokoa wazazi wakati wa kujifungua.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo,wajitokeze kwa wingi kwenye maadhimisho hayo ya siku ya ukunga dunian mkoani humo ili wapate elimu mbalimbali bure za masuala ya afya na afya ya uzazi.


Kauli Mbiu katika maadhimisho ya siku ya ukunga duniani mwaka huu inasema”Mkunga ni Nguzo Muhimu katika kila Janga.”
Share:

Sunday, 4 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 5,2025




Magazetini



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger