Friday, 18 April 2025

TASAC YAWAPIGA MSASA WADAU WA USAFIRI MAJINI MKOANI TANGA

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Wadau wa usafiri wa maji wametakiwa kufuata masharti na taratibu za kazi zao na kuwa na weledi ili kuepuka kudhoofisha ufanisi na kuingia kwenye migogoro baina yao.

Wito huo imetolewa na Mkurugenzi Udhibiti Huduma za Usafiri Majini Nelson Mlali wakati wa mafunzo mafupi ya Sheria za majini iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC).

Mlali amesema kumekuwa na tatizo la mgongano wa maslahi baina ya watoa huduma ambayo unawahusisha zaidi Mawakala wa Forodha dhidi ya Mawakala wa Meli lakini pia kuna tatizo la watoa huduma kutozingatia kanuni, masharti na taratibu zilizowekwa kuwaongoza.

"Pia kuna tatizo la ucheleweshwaji huduma zikiwemo mifumo, uwezo mdogo wa kiutendaji wa baadhi ya wadau, kutokana na matatizo haya tunajikuta tukiingia katika migogoro na gharama, hivyo kudhoofisha ufanisi na usafiri kwa njia ya maji " ,amesema.

Nitumie fursa hii kuwaomba, kufuatilia kwa umakini mjadala wa kikao hiki ili kwa pamoja tuweze kuboresha ufanisi, kupunguza migogoro na malalamiko katika sekta yetu ya usafiri kwa njia ya maji,

"Lakini pia naomba niwakumbushe kwamba, uwepo wa shehena, meli, bandari na maji pekee havitakuwa na tija kwetu iwapo hatutazingatia utii wa sheria na taratibu zilizowekwa kuongoza shuhuli zetu" ,amesisitiza.

Vilevile amesema mbali na hilo kuna utunzaji wa maji, ushiriki katika ulinzi na usalamanwa rasilimali zao na nchi kwa ujumla, pia ushirikiano katika kufanikisha taratibu mbalimbali zinaoongoza usafiri kwa njia ya maji.

"Uungaji mkono jitihada za serikali zinazolenga kuboresha mazingira ya usafiri kwa njia ya maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya usafiri wa ardhini,

"Ili kuziunganisha bandari zetu na masoko yake na jitahada za uboreshaji au ujenzi ili site kama Taifa tuweze kuneemeka na fursa zinazotokana na uchumi wa buluu" ,amesema.

Naye Ofisa Mfawidhi wa (TASAC) Mkoa wa Tanga Christopher Shalua amewataka wadau hao kuhakikisha wanazingatia afya na usalama kabla ya kutoa huduma za kupakua na kupakua mizigo kwenye Meli hususani zinazotoka nje.

Aidha Shalua aliwataka wadau hao kuhakikisha wanafuata Sheria na taratibu za nchi ikiwemo kuhusiaha lwseni zao ili waweze kupata ruhusa ya kufanya kazi zao bandarini wakati wote.

"Mawakala na wadau wote wanaotoa huduma za bandari lazima kuhakikisha kuwa vibali vyao vinahuishwa ili kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika utoaji wa huduma bandarini", amesema Shalua.








Share:

WAHITIMU WA MAFUNZO YA KUJITOLEA RUVU JKT WAHIMIZWA NIDHAMU

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.

*************

NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kutunza afya zao kwani wakiwa na afya njema watapata fursa nyingi zilizopo nchini ikiwemo kupata nafasi katika kada mbalimbali za ulinzi.

Amewaagiza wahitimu hao kujiepusha na matumizi ya vileo mbalimbali ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya kwani si sehemu ya maadili ya mafunzo ya kijeshi.

Tamko hilo amelitoa Aprili 17,2025 katika Kambi ya RUVU JKT 832 KJ alipokuwa akihitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT.

Amesema madhumuni ya mafunzo hayo ni kulea vijana wakitanzania katika maadili na kushiriki katika mafunzo ya ulinzi wa nchi pamoja na kukuza moyo wa kizalendo.

"Malengo makuu kwenye mafunzo haya ni pamoja na kuhakikisha vijana wanasifa nne kuu za msingi ambazo ni nidhamu, uaminifu, utiifu kwa viongozi na nchi yao, lakini pia kuwafanya kuwa hodari katika kazi, hali ambayo vijana hawa  ambao wamehitimu wanayo". Amesema Meja Jenerali Mabele.

Kwa upande wake, Brigedia Jenarali Aboubakar Charo, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amesema amethibitisha kuwa vijana hao wamepokea mafunzo hayo na wameiva kwani wamekuwa na ukakamavu, uzalendo, uhodari, uvumilivu na kujiamini.

Aidha Jenerali Charo amewataka vijana hao kuwa tayari kwaajili ya mafunzo ya stadi za kazi na maisha  katika kipindi cha miezi 20 ijayo.

Hata hivyo Jenerali Charo amewakumbusha wahitimu hao kukumbuka falsafa ya kazi iendelee ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta Maendeleo ya nchi.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akikagua gwaride wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mwakilishi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Brigedia Jenarali Aboubakar Charo akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT- Kanali Longinus Nyingo akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Kamanda wa Kikosi Ruvu JKT, Peter Mnyani akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akitoa zawadi kwa wahitimu wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT waliofanya vizuri katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akifurahi na wahitimu wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo hayo Aprili 17, 2025 Mlandizi mkoani Pwani.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

Thursday, 17 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 18,2025


Share:

SEKRETARIETI YA AJIRA YAPONGEZWA KWA KUFANYIA KAZI USHAURI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (katikati) akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (watatu kutoka kulia) akifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa usaili wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sang una wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Kamati yake iliyofanyika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.
Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Viongozi na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kamati yake katika ofisi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Omar Kombo akiwasilisha hoja wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyofanyika katika ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye akiwasilisha mada kuhusu TEHAMA ilivyoboresha mchakato wa ajira wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Katibu, Menejimenti ya Ajira, Bi. Somwana Manjenga akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu mchakato wa ajira wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakisikiliza maoni ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.


Na Veronica Mwafisi-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kuzingatia maoni na ushauri unaotolewa na kamati hiyo ili kuhakikisha mchakato wa ajira unafanyika kwa ufanisi mkubwa na uwazi wa hali ya juu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati yake wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza utendajikazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Mhagama ametolea mfano maoni ambayo Kamati yake iliyatoa kuhusu usaili kufanyika katika ngazi za mikoa badala ya kuwalazimu waombaji kazi wote kufika jijini Dodoma kumeleta matokeo chanya kwa waombaji kazi hao.

Vilevile Dkt. Mhagama amezungumzia matumizi ya mfumo wa Ajira Portal kwa waombaji kazi kuondokana na dhana tofauti ya upendeleo wa kupata ajira katika Utumishi wa Umma.

“Mfumo wa Ajira Portal umeondoa dhana ya kuwepo kwa upendeleo kwa waombaji kazi, ninaamini wengi wamepata ajira serikalini pasipo kupitia kwa mtu yeyote.” amesema Mhe. Dkt. Mhagama.

Kwa Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameishukuru Kamati hiyo kwa kutoa maoni na ushauri mara zote ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kutekeleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kikamilifu.

Aidha, Naibu Waziri Sangu amewaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuendelea kuwa Mabalozi wazuri wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma ili kuwahakikishia wananchi kuhusu uwazi wa namna ajira katika Utumishi wa Umma zinavyopatikana kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Sekretarieti hiyo wakati wa kuomba kazi.

Akielezea mafanikio baada ya kutumia mfumo wa Ajira Portal, Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye amesema, kupitia mifumo wameweza kuajiri Rasilimaliwatu yenye uwezo wa kufanya kazi na kutoa matokeo chanya pamoja na kuondoa hoja za kuajiri kwa dhana ya upendeleo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger