Wednesday, 16 April 2025

AfCFTA KUKAMILISHA KANUNI ZA UASILI WA BIDHAA ZA NGUO NA MAVAZI 



Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo,akizungumza wakati akihutibia Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la AfCFTA uliofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) jijini Kinshasa





.......

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo (Mb.) ametoa rai kwa Wataalamu wa Eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA)kuhakikisha majadiliano kuhusu Kanuni za Uasili wa Bidhaa za Nguo na Mavazi yanakamilika ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa nguo na mavazi kuzalisha kwa wingi na kupunguza uagizaji wa nguo na mavazi ikiwemo nguo zilizotumika.

Aidha amesisitiza kuendelea kuzihamasisha nchi sita (6) Barani Afrika zilizosalia kukamilisha mchakato na kuridhia mkataba huo ulioridhiwa na Nchi 48 ili kuharakisha utekelezaji wa Mkataba huo na kuchochea maendeleo ya uwekezaji, viwanda, biashara na kuimarisha uchumi ndani ya Afrika.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la AfCFTA lililofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) jijini Kinshasa ambapo Tanzania imekuwa mwenyekiti kwa mwaka 2024 na kukabidhi Uenyekiti huo kwa Misri 2025

Aidha katika kipindi hicho cha Uenyekiti, Waziri Jafo amebainisha kuwa AfCFTA imefanikiwa kukamilisha Kiambatisho cha Itifaki ya Uwekezaji cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, Itifaki ya Biashara Mtandao, Kuridhia Kanuni za Mawaziri za kutoa upendeleo maalum wa soko kwa wafanyabiashara Wanawake na Vijana, Kuanzisha utaratibu wa mapitio ya utekelezaji wa Mkataba huo na Chombo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara.

Mpango wa kuhamasisha biashara ndani ya AfCFTA (GTI) unaotumiwa na Nchi Wanachama 39 umefanikiwa katika kuwawezesha wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo na kuongezeka kwa bidhaa kutoka kilimo hadi za viwandani kama vile kemikali, vifaa vya kieletroniki, betri na vigae. amesema Dkt Jafo.

Kwa Tanzania hadi Januari 2025 imefanikiwa kuwa na Jumla ya Makampuni 43 ambayo imeweza kuuza bidhaa zake katika nchi mbalimbali za Afrika kupitia Mkataba huo kwa kutumia cheti cha uasili wa bidhaa cha AfCFTA ambapo, jumla ya vyeti 226 vimeweza kutolewa kwa Kampuni hizo. Bidhaa ambazo zimeuzwa kwa wingi kupitia vyeti hivyo ni nyuzi za katani tani 6,150 kwenda nchi za Nigeria, Ghana, Morocco na Misri; Vioo (Float Glasses) tani 1,433 kwenda Misri; Mchele tani 433 kwenda Burkina Faso na Cote d’ivoire; na kahawa tani 273.3 kwenda nchini Algeria.

Mafanikio haya yamewezekana kutokana na juhudi za Serikali yetu inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wafanyabiashara wetu na sera za kimkakati zilizowekwa na serikali kwa kushirikiana na Sekretarieti ya AfCFTA.

Aidha, amebainisha kuwa AfCFTA imefanikiwa kuanzisha utaratibu wa kuwepo na Kampuni za Biashara (AfCFTA Trading Companies -ATC) ambao umesaidia kuanzisha makampuni ya biashara katika nchi za Kenya, Ghana, Misri na Rwanda na iko mbioni kukamilisha majadiliano ya ufunguaji wa Soko la Biashara ya bidhaa.




Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akisalimiana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) Aprili 15, 2025 mara alipowasili kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa 26 wa Eneo huru la Biashara Afrika wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa AfCFTA uliofanyika, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Kinshasa






Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo,akizungumza wakati akihutibia Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la AfCFTA uliofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) jijini Kinshasa
Share:

NILIVYOMBEBEA UJAUZITO NILIYEKUTANA NAYE FACEBOOK

Kuna mwanaume nilikutana naye mwaka 2016, wakati huo nilikuwa katika ndoa alitaka kunioa nikamjibu nishaolewa, basi alinisumbua sana tukaishia mimi ni mke wa mtu, basi bhna tukapotezeana kwa muda mrefu.

Ishukuriwe Facebook tukakutana tena 2021, basi tukaonana mnajua tena zile furaha za watu mliopotezana kwa muda mrefu, basi stori tukapiga nyingi tu na kunieleza yeye alioa baada ya kumwambia nimeolewa ila walishaana. 

Kipindi hicho na mimi nimeshaachana na mtu wangu, basi kila mmoja yuko single. Mara moja tukaanzisha mahusiano, nakuambia ndani ya muda mfupi tu mwanaume akanibadishia maisha, sio sana ila nashukuru akaonesha upendo vizuri. 

Yaani kanielewa sana, nikimuomba fedhha ananipa, hata kama ni biashara ananisaidia hadi sasa tuna miliki biashara kubwa tu ambayo imetuinua sana kimaisha hadi tumefanikiwa na kujenga nyumba mbili. 

Alionyesha kweli alikuwa ananihitaji maana alienda hadi kwetu kujitambulisha, kusema kweli mapenzi yalinoga hadi nikasema ningejua ningemkubalia ile mara ya kwanza ingawa nilikuwa mke wa mtu. 

Changamoto ilikuja pale ambapo alitaka nimzalie mtoto maana katika ndoa yake hakupata mtoto ingawa mimi tayari nilikuwa na wangu mmoja hivyo alikuwa na shauku kubwa sana ya kuwa na mtoto. 

Kila ambapo nilitarajia nitabeba ujauzito haikuwa hivyo, ndipo tukanza kwenda hukuo na kule kusaka suluhisho na mwisho wa siku tukaangukia katika mikono ya Kiwanga Doctors kutoka huko Migori nchini Kenya. 

Kiwanga Doctors alinifanyia kile ambacho kinajulikana kama pregnancy spell kisha kunipa baadhi ya dawa za kutumia nikiwa nyumbani.

Nilizitumia kama ambavyo alinielekeza na mwisho wa siku nilifanikiwa kupata mtoto na sasa nina wawili. 

Kama na wewe unapitia kitu kama hicho, ninakushauri kuwa fika au wasiliana na Kiwanga Doctors. Tiba zao zinafanya kazi haraka na wanaweza kukusaidia katika changamoto mbalimbali za kimaisha, kuanzia masuala ya uhusiano hadi matatizo ya kiafya. 

Wengine wengi wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma zao. Basi wasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao.

Share:

WANANCHI KYERWA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWALETEA MSAADA WA KISHERIA

Na Lydia Lugakila -Kyerwa

Wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera ya wilaya ya kyerwa wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogea karibu huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ijulikanayo kama Samia Legal Aid Campaign kwani imemulika migogoro mingi ikiwemo ya ndoa na ya ardhi.

Kauli hiyo imetolewa na  baadhi ya Wananchi katika kijiji cha kibimba kata ya Mabira waliojitokeza katika kampeini hiyo.

 Philbat France na Mathayo Bernard wemesema kuwa kuwepo kwa ujio wa kampeini hiyo katika ngazi ya vijijini inaenda kuwa mkombozi kwani familia nyingi zipo katika hali mbaya juu ya migogoro ikiwemo ya ndoa huku wakimtaja Rais Samia kuwa Mkombozi wao.

Aidha wameongeza kuwa familia nyingi zimekuwa na changamoto ya migogoro ya ndoa inayosababishwa na watoto wao wenyewe ambayo mwisho wa siku inasababisha migogoro ya ardhi mpaka kusababisha kufanyiana vitendo vibaya wakati mwingine, kwani asilimia kubwa ya waathirika katika mgogoro hiyo ni wanaume hasa pale wanapopigwa na wake zao .

Pia wamesema kupitia uelewa walioupata kutoka kwa Wataalam hao itasaidia kukuza malezi bora ya familia zao hasa kwa watoto na kuwa na uelewa juu ya mirathi katika familia zao.

Naye Getruda Mwiga kutoka dawati la jinsia na watoto ambaye naye ni miongoni mwa timu ya kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambapo amewasihi wazazi kudumisha malezi bora kwa watoto wao kwani hiyo itasaidia kuondoa changamoto hizo katika jamii.

“Malezi bora kwa watoto wetu ni muhimu pia kama familia tunatakiwa kusikiliza na unapopata changamoto usisite kutoa taarifa ili kupata msaada mfano kwa wakina Baba najua mnakutana na changamoto nyingi huko katika makazi yenu ila msiwe na aibu kutoa taarifa kwani itawasaidia kutojichukulia sheria mkononi”

Kwa upande wake afisa ardhi mwandamizi Bw. Bitabonwa Mkama amesema kila mwananchi anayo haki ya kumiliki ardhi kisheria bila kubagua jinsia na kupitia kampeini hiyo ya msaada wa kisheria itakuwa ni fursa kupata msaada zaidi.

Sambamba na hayo pia  Bitabonwa katika kutoa elimu hiyo ya msaada wa kisheria juu ya umiliki wa ardhi amekutana na changamoto ya kutokuwepo kwa mabaraza ya ardhi ya vijiji jambo linalopelekea migogoro mingi ya ardhi katika vijiji hivyo ambapo ameahidi jambo hilo kufanyiwa kazi kupitia kampeini hiyo.


Share:

RAIS SAMIA AMWAGA BILIONI 45 KUTATUA TATIZO LA MAJI JIJI LA DODOMA



Na Maandishi wetu Dodoma.

Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amesema Rais Dkt. Samia Suluh Hassan ameelekeza utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Tsh Bilioni 45 kutatua changamoto ya Maji Jijini Dodoma wakati ikisubiriwa utekelezaji wa Miradi ya kuleta maji kupitia Ziwa Victoria na mradi wa Bwawa la Farkwa.

Waziri Aweso ameyasema hayo wakati akishuhudia utiaji wa saini wa mkataba wa mradi wa kusambaza maji kupitia visima vya maji vya Nzuguni A wenye thamani ya Tsh 5bn unaotarajiwa kuwanufaisha watu 123,095.

“Mbunge wenu alileta maombi kwa Mh. Rais Samia juu ya uchimbwaji wa visima virefu wakati wa mkutano wa Mh. Rais pale Mpunguzi na sisi Wizara tukapata maelekezo ambayo tumeyafanyia kazi.

Tunamshukuru Mh. Rais Samia kwa kulivalia njuga suala la maji hapa Jijini Dodoma kwa kuelekeza utekelezaji wa miradi ya maji ya zaidi Tsh 45bn ambayo itasaidia sana kupunguza tatizo la mgao wa maji katika maeneo mbalimbali.

DUWASA inaendelea na utekelezaji wa miradi mingine kama vile Nala 3.8bn UDOM,(1.2bn), Mji wa Serikali (35.6bn), n.k. Aidha wizara ya maji kwa kushirikiana na taasisi

zake (DUWASA na RUWASA) imeunda timu zinazo endelea na Utafiti wa Maji chini ya Ardhi na Uchimbaji wa visima katika maeneo ya Mzakwe, Nzuguni, Kisasa, Nkuhungu,Miganga, Zuzu, Msalato na Ihumwa.

"Nipo hapa Jijini Dodoma na kesho naanza ziara maalum kukagua utekelezaji wa miradi hii ili wananchi wa Dodoma wapate maji ya uhakika”amesema Aweso

Kwa upande Wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma ambaye pia ni Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema utekelezaji wa mradi ya usambazaji wa maji utasaidia kupunguza adha ya mgao wa maji kwa wananchi wa maeneo ya nzuguni Nkuhungu,Miganga,Chidachi, Kisasa-Bwawani,Mwangaza, Ipagala, Ilazo, na Swaswa, Mpamaa na Njedengwa.

Awali akitoa taarifa yake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) Eng. Aron Joseph amesema Mradi huu unalenga kuhudumia wananchi wapatao 123,095 katika maeneo yaliyotajwa

Aidha Eng Aron amesema Kukamilika kwa mradi huu kutapelekea ongezeko la uzalishaji kutoka lita milioni 81 hadi 91 kwa siku sawa na ongezeko la 30% kutoka chanzo cha Nzuguni.





Share:

TUMIENI MIKOPO INAYOTOLEWA NA SERIKALI KUJIENDELEZA KIUCHUMI - NAIBU KATIBU MKUU MDEMU


Na WMJJWMM, Tarime - Mara

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu amewaasa wananchi kutumia mikopo inayotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi kwa maendeleo ya familia zao na jamii inayowazunguka.

Felister ameyasema hayo Aprili 15, 2025  kwenye mkutano na wakazi wa Kata ya Susuni, Bumera, Mwema na Sirari za Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. Mkutano huo ni muendelezo wa Kampeni ya Mageuzi ya Kifikra na Mtazamo wa kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo yao.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu, imetenga pesa kupitia mifuko mbalimbali ya uwezeshaji kiuchumi hivyo, amewasisitiza wananchi kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua kiuchumi.

" Nisisitize na wale wote ambao wamenufaika na mikopo  kuhakikisha mikopo hiyo imekuwa chachu kwao ya kupiga hatua za maendeleo na si vinginevyo" amesema Felister.

Aidha, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juliana Kibonde amesema Serikali imeanzisha mifuko mbalimbali iliyoanzishwa  ya kuwawezesha wananchi kupata mikopo yenye riba nafuu ikiwemo mfuko wa vijana, mfuko wa vikundi vya wafanyabishara, mfuko wa kundi la wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu na mfuko wa wanawake. 

"Mifuko yote hii imeletwa kwa ajili ya kuwasaidia  kuboresha na kuanzisha miradi mbalimbali, hakikisheni mnakidhi vigezo ikiwa pamoja na kuanzia vikundi ili muweze kunufaika na mikopo hii yenye riba nafuu" amesema Juliana


Mmoja wa mnufaika wa mikopo hiyo  Erick Odhiambo  amesema ametumia fursa ya mkutano huo kutoa hamasa kwa wananchi ya namna alivyonufaika na Mikopo inayotolewa na Serikali kwa masharti nafuu ili kuwa utia wananchi wenzake kupata mikopo hiyo na kuondokana na mikopo isiyo na tija inayowakandamiza.

"Mimi ni shahidi na mnufaika wa hii mikopo inatusaidia sana, awamu ya kwanza nilifanikiwa kupata mkopo wa shilingi milioni  tano (5 ), baada ya kukamilisha marejesho nikufuzu kuchukuwa  awamu ya pili kiasi cha shilingi milion sita (6) fedha ambazo zimenisaidia kulima, kujenga nyumba na kupanua biashara yangu ya ushonaji." ameeleza Odhiambo.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 16,202/

Magazeti ya leo



Share:

Tuesday, 15 April 2025

Breaking : TUZO ZA 'SAMIA KALAMU AWARDS' KUTOLEWA APRILI 29,2025 DODOMA!

 

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kimetangaza kufanyika kwa hafla ya utoaji tuzo za Samia Kalamu Awards tarehe 29 Aprili 2025 jijini Dodoma.

Tuzo hizo zinalenga kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo unaogusa maisha ya wananchi na kuzingatia weledi, uchambuzi na uwajibikaji.

 Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Makundi ya tuzo ni pamoja na: tuzo za kitaifa, tuzo kwa vyombo vya habari (TV, redio, magazeti na mitandao), na tuzo za kisekta kwa waandishi walioibua mada muhimu kama afya, elimu, mazingira, jinsia na uchumi.

Hafla hiyo itarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili wananchi waweze kufuatilia. Waandishi na vyombo vya habari wamehimizwa kushiriki kikamilifu kuhamasisha tukio hili la kihistoria.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger