Sunday, 13 April 2025

ABSA BANK TANZANIA YAZINDUA ‘AKAUNTI YA MZAWA’ – SULUHISHO LA KIBUNIFU KWA WATANZANIA WAISHIO UGHAIBUNI







Na Mwandishi Wetu

Absa Bank Tanzania imezindua rasmi Akaunti ya Mzawa, huduma kamili ya kibenki kwa Watanzania waishio, wanaofanya kazi na kusoma nje ya nchi.


Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kwa njia ya mseto (“phygital”) ambapo wadau muhimu walihudhuria ana kwa ana huku wengine wengi kutoka ughaibuni wakijiunga kwa njia ya mtandao.

Akaunti ya Mzawa imelenga kuondoa changamoto zilizodumu kwa muda mrefu zinazowakabili Watanzania waishio nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na ugumu wa kupata huduma za kifedha, changamoto za kufungua akaunti za fedha za kigeni, pamoja na upungufu wa taarifa za fursa na msaada wa mbali. Huduma hii inatoa upatikanaji wa kimataifa wa akaunti kwa sarafu tano (TZS, USD, GBP, EUR, na ZAR), kufanikisha miamala rahisi, fursa za uwekezaji, na huduma za bima kupitia Absa Bima.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni rasmi katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Cosato David Chumi alikiri mchango mkubwa wa diaspora pamoja na changamoto wanazokumbana nazo: “Diaspora yetu haijajitenga – imewekeza kwa dhati.

Lakini kwa bahati mbaya, hawapati fursa za kutosha kushiriki ipasavyo. Na sisi kama serikali tunasema tumewasikia. tunawaona. na tunachukua hatua. Chini ya uongozi wa . Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, serikali imepiga hatua kubwa kupitia huduma za ubalozi kwa njia ya kidijitali, majukwaa ya uwekezaji ughaibuni, na sasa kuhimiza mabenki kama Absa kuunda huduma mahsusi kwa diaspora.”

Naibu Waziri pia alipongeza Absa kwa kutoa suluhisho la wakati, jumuishi na lenye tija: “Akaunti ya Mzawa ya Absa inaleta pamoja kila kitu ambacho diaspora imekuwa ikikiomba. Kwa Watanzania wote waishio nje ya nchi, nawaambia: muda ni huu. Miundombinu inajengwa. Msaada unazidi kuongezeka. Tuchukue hatua sasa – tujenge nyumba, tufungue biashara, tuwekeze, na tujikite nyumbani Tanzania.”

Uzinduzi wa Akaunti ya Mzawa unaendeleza pia huduma ya awali ya Mkopo wa Nyumba kwa Diaspora kutoka Absa, ikiwapa Watanzania wa ughaibuni uwezo wa kudhibiti fedha zao huku wakiwekeza kwenye maendeleo ya muda mrefu nyumbani.

Kwa kuzingatia ahadi yake ya chapa, “Stori yako ina thamani’” na dhamira ya shirika “Kuiwezesha Afrika ya Kesho, pamoja, stori moja baada ya nyingine”, Absa Bank Tanzania inaendelea kutoa suluhisho bora zinazomlenga mteja, ili kuwaunganisha Watanzania wote na fursa zilizopo nyumbani – popote walipo duniani.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Idara ya Masuala ya Diaspora, inakadiriwa kuwa zaidi ya Watanzania 400,000 wanaishi nje ya nchi, wakiwa wengi wao wako Marekani, Uingereza, Kanada, Ulaya, Mashariki ya Kati, na kusini mwa Afrika. Mwaka 2022 pekee, Watanzania waishio ughaibuni walituma zaidi ya USD milioni 598 kurudi nyumbani, sawa na zaidi ya TSh trilioni 1.4, huku zaidi ya TSh bilioni 6.4 zikitumika kununua mali.










Share:

Saturday, 12 April 2025

TANZANIA YAPAA KIDIJITALI: YATAJWA MIONGONI MWA MATAIFA SALAMA ZAIDI MTANDAONI DUNIANI


Na Woinde Shizza , Arusha

Tanzania imeorodheshwa katika kundi la juu la nchi 46 duniani zilizofanikiwa kuwa na viwango bora vya usalama mtandaoni, hatua inayochangia kuvutia idadi kubwa ya wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Usalama Mtandaoni – Global Cybersecurity Index (GCI) kwa mwaka 2024, na imewasilishwa katika Jukwaa la Nne la Usalama Mtandaoni nchini Tanzania linalofanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika jukwaa hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT Commission), Dkt. Nkundwe Mwasaga, amesema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kujenga uchumi wa kidijitali na kuimarisha mifumo ya ulinzi wa kimtandao.

Aidha, Dkt. Mwasaga ameeleza kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa kituo cha kuchakata masuala ya usalama mtandaoni (Digital Technology Institute) huko Dodoma, ambacho kitaongeza ufanisi katika kulinda miundombinu ya kidijitali.
Kwa upande wake, mdau wa usalama mtandao Robert Karamagi amesema kwa sasa kuna maendeleo makubwa ya matumizi ya mifumo ya kidijitali, ikiwemo teknolojia ya akili bandia (AI), katika sekta za afya, elimu, biashara na sheria.
Naye mtaalamu wa usalama mtandaoni na uchunguzi wa makosa ya kimtandao, Yusuph Kileo, amesema mkutano huo ni muhimu kwani umewakutanisha wataalamu wa usalama wa mtandao kutoka ngazi ya kitaifa na kimataifa kujadili changamoto mbalimbali na kutafuta suluhu ya pamoja.

“Binafsi, katika jukwaa hili nitawasilisha mada mahususi kuhusu intelijensia ya uhalifu wa kimtandao, ambapo tutaangazia sababu mbalimbali zinazochochea ongezeko la uhalifu huu, na kwa pamoja kujadili mbinu za kukabiliana na changamoto hizo ambazo zinaathiri si tu wizi wa data na fedha, bali pia maeneo muhimu ya jamii,” alieleza Kileo.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa wa mwaka 2024, uhalifu wa kimtandao unagharimu dunia dola trilioni 10.5, kiasi ambacho ni hasara kubwa kwa uchumi wa dunia.

Jukwaa la Nne la Usalama Mtandaoni nchini Tanzania limewakutanisha wadau kutoka serikalini, sekta binafsi, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na washirika wa kimataifa.
Share:

DKT. YONAZI AKUTANA NA UJUMBE WA IFAD NA TIMU YA WATAALAM NA WATEKELEZAJI WA PROGRAMU YA AFDP



NA. MWANDISHI WETU - DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Sera,Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Majumuisho (wrap-up) cha Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Timu ya Wataalamu wanaotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) baada ya kukamilika kwa ziara ya kutembelea na kukagua maeneo yanayotekeleza programu hiyo.

Timu hiyo ya IFAD na wataalam ilitembelea maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa Programu ya AFDP kwa sekta za kilimo na uvuvi Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Aidha, timu hiyo ilitembelea pia Mradi wa Kuimarisha na Kuendeleza Upatikanaji wa Lishe kwa Wafugaji Wadogo wa Viumbe Maji na Wakulima wa Mwani (ARNSA).

Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Aprili, 2025 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alipongeza maendeleo mazuri ya utekelezaji program hiyo na kusema kazi zinazofanywa na mradi kwa sasa zinaonekana huku akiwasihi kuendelea kuimarisha mafanikio hayo na kuahidi kushirikiana na TAMISEMI kwa lengo la kuwafikia wanufaika wa program hii.

“Serikali kwa kushirikiana na IFAD itahakikisha inaleta matokeo chanya kwa kuzingatia mipango na mikakati inayotekelezwa na Program hii inawanufaisha walengwa,” Akisema Dkt. Yonazi

Aidha, akieleza umuhimu wa Mradi Mkurugenzi Mkaazi wa IFAD Nchini Bw. Sakphouseth Meng amelezea kuwa upo umuhimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa sehemu ya utekelezaji wa programu ili kuwafikia walengwa na kueleza umuhimu wa sekta binafsi kushirki katika Programu ili kuweza kuwafikia walengwa wengi zaidi na pia kuwa endelevu.

Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Nchini (IFAD) Bw. Sakphouseth Meng akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025


Share:

Friday, 11 April 2025

TGNP YARATIBU KIKAO CHA KUJADILI BAJETI INAYOZINGATIA USAWA WA KIJINSIA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

ASASI za Kiraia, Mashirika pamoja na wadau wanaojihusisha na utetezi wa wanawake wamesisitiza uhitaji wa serikali kuzingatia ujumuishaji na utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa vitendo katika bajeti ya kitaifa na kuhakikisha zinagusa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 11, 2025 Jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha kujadili bajeti ya mwaka 2025/26 inayojali usawa wa kijinsia, ikiwa ni sehemu ya tathmini ya mafanikio ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (TDV 2025) na maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 (TDV 2050) kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, wataalamu wa sera, na wawakilishi wa makundi ya wanawake, kikilenga kuchambua namna bajeti imekuwa chombo cha mabadiliko ya kijamii, hasa kwa wanawake. Taarifa zilitolewa kuonyesha kuwa ushiriki wa wanawake kwenye kazi za kipato umeongezeka kutoka asilimia 67 mwaka 2000 hadi asilimia 80.2 mwaka 2023 – mafanikio yanayoashiria nguvu ya bajeti jumuishi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Bi. Gema Akilimali alisema: “Bajeti yenye mtazamo wa kijinsia huanzia kwenye upangaji hadi utekelezaji wake. Ni muhimu wanawake na makundi maalum kushirikishwa kikamilifu katika hatua zote za mchakato huo.”

Aliongeza kuwa changamoto kubwa inabaki kuwa utoaji wa fedha halisi ikilinganishwa na makadirio. “Makadirio huwa makubwa, lakini fedha zinazotolewa ni ndogo. Kazi yetu ni kuhakikisha tunafuatilia matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha zinatumikia lengo lililokusudiwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, alisisitiza kuwa ili Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 iwe jumuishi, ni lazima misingi ya usawa wa kijinsia izingatiwe kuanzia sasa. “Tunapojadili bajeti na dira mpya, tunapaswa kujiuliza: Je, wanawake wana nafasi gani katika michakato ya maamuzi? Je, rasilimali zinaelekezwa kwa kuzingatia mahitaji ya wote?” alihoji.

Alisema TGNP itaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuhakikisha sauti za wanawake zinahesabiwa.

“Tunataka kuona wanawake wakiwa mstari wa mbele sio tu kama walengwa, bali kama wachangiaji wakuu wa maendeleo ya nchi,” aliongeza Liundi.

Mijadala ya kina pia iligusia mafanikio mengine kama vile kuongezeka kwa wanawake wanaojihusisha na taaluma za kihandisi, na uboreshwaji wa mifumo ya mikopo kupitia sheria za fedha za serikali za mitaa.

Hata hivyo, changamoto zimeendelea kujitokeza – hususan urasimu katika upatikanaji wa mikopo ya 4-4-2, umiliki duni wa ardhi kwa wanawake (asilimia 8 pekee), na ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu bajeti za jinsia.

Katika bajeti ya mwaka 2025/26 yenye thamani ya Sh trilioni 57.02, Serikali imeweka vipaumbele vya kukuza usawa wa kijinsia na kuwezesha makundi maalum.

Hata hivyo, TGNP imesisitiza kuwa kuna mapungufu katika kugharamia sekta muhimu kama viwanda, biashara na hifadhi ya jamii – maeneo ambayo ni nguzo za uchumi shindani na jumuishi.

Katika karatasi ya majadiliano iliyoandaliwa na mtaalamu wa sera za kijinsia, Makumba Mwemezi, inabainika kuwa licha ya hatua zilizopigwa kwenye sekta ya elimu, changamoto bado ni kubwa.

“Zaidi ya wanafunzi 148,000 waliripotiwa kuacha shule mwaka 2023 licha ya sera ya elimu bila malipo,” alisema, akisisitiza umuhimu wa ubora na ujumuishi katika elimu.

Kwa upande wa maji, alisema: “Upatikanaji wa maji safi vijijini umeongezeka kutoka asilimia 53 mwaka 2003 hadi asilimia 72 mwaka 2022. Hata hivyo, theluthi moja ya vyanzo vya maji havifanyi kazi ipasavyo.”

Mwemezi alipendekeza Tanzania iwe na Mpango Maalum wa Kitaifa wa Usawa wa Kijinsia (GEWE) badala ya kuacha masuala ya jinsia kuwa sehemu ya vipengele ndani ya sekta mbalimbali. “Hili ni muhimu kwa maendeleo endelevu,” alisisitiza.

Mapendekezo kutoka Wajibu Institute, kama yalivyowasilishwa na Karoli Kadenge, yanaitaka serikali kuhakikisha mgao na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo katika kipindi kilichosalia cha FYDP III. Kadenge alisema: “Serikali inapaswa kutathmini upya vipaumbele vya maendeleo na kuelekeza zaidi fedha katika huduma za kijamii kama afya, elimu na maji.”

Kikao hicho kimehitimishwa kwa wito wa kuhakikisha kwamba katika safari ya kuelekea TDV 2050, wanawake hawaachwi nyuma, bali wanakuwa sehemu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa usawa kamili.


Share:

MKE WAKE KASEMA NIKISHAJIFUNGUA ATAKUJA KUMCHUKUA MTOTO WAO....!

Naitwa Aisha kutokea Tarime, kuna mwanaume nilipata mimba yake ila yeye ana mke na mtoto mmoja, sasa kipindi naanza naye mahusiano akaniambia kabisa ana mke ila nikajua labda wamegombana nikabeba mimba mwezi huo huo. 

Alikuwa ananihudumia vizuri sana hadi mke wake aliporudi kwake, aliporudi akamwambia mke wake kuwa amenipa mimba, akampa na namba zangu za simu mke wake akanitafuta akaomba tukutane tuongee. 

Tulipokutana kaniuliza nina mpango gani na mume wake anajua nina mimba ila nimwambie mpango wangu, nikamwambia kuwa mume wake aliniambia ana mke lakini mimba imeingia bahati mbaya.

Akaniambia ndio yeye akiondoka mume wake anaruhusiwa kuwa na mwanamke yeyote huku nyuma na ndio sheria yao. Kwa hiyo mimi sio wa kwanza na nisijione special sana. Nikamwambia sina mpango nae simtaki. 

Akaniambia sawa kama sina mpango niache kuwasiliana naye, nikihitaji mahitaji, matumizi na kila kitu yeye atahakikisha napata na hata kujifungia nitajifungua vizuri tu na watalipa ila mtoto akimaliza kunyonya tu watamchukua, nikamwambia sawa. 

Wakati huo nilikuwa sina pesa na sina kazi, nilipopata huyu mwanaume nikajua maisha yatakuwa mepesi kidogo. Lakini nilipokuja kumtafuta akaniambia si nilishaonana na mke wake tukakubaliana nisimsumbue tena. 

Nilivumilia yote waliyonifanyia yeye na mke wake nikachoka, siku moja nimeamka nakuta navuja damu nikampigia mke wake. Akaja akanipeleka hospitali nikatibiwa lakini mimba imetoka. 

Nashukuru alinihudumia hadi nikapona ila baada ya wiki akaniambia mkataba wetu mimi na yeye umeisha niendelee na maisha yangu.  Hapo ndio mambo yakaanza kuwa magumu kwangu hadi ikabidi niende kwa Kiwanga Doctors huko Migori, Kenya. 

Yalikuwa magumu kwa maana kodi walikuwa wamenilipia, huduma nilikuwa napata kirahisi lakini ndio hivyo akaja kunimbia nimepona nijipambane bila hata kujua wapi ambapo nitaanzia. 

Hata hivyo nashukuru huko kwa Kiwanga Doctors nilifanyiwa dawa ya kupata kazi (job spells) ambayo ilinisaidia na sasa nimeajiriwa katika kampuni moja na mshahara wake ni mzuri sio haba.  Naweza kuendesha maisha yangu bila ya kumtegemea mtu yeyote. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana nao kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUWAONDOLEA WANANCHI KERO YA MAJI SINAI NA MANG’ULA


Mhandisi Vicent Bahemana (kulia) akiwa pamoja na Diwani wa kata ya Lilambo Exsaveri Iyobo wakati wa kukabidhi mabomba ya mradi wa maji Sinai na Mang’ula katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Mhandisi Vicent Bahemana kutoka kulia akizungumza na Mheshimiwa Diwani wa kata ya Lilambo Exsaveri Iyobo baada ya kukabidhi mabomba ya mradi wa maji Sinai na Mang’ula
Gari likiendelea na zoezi la kushusha mizigo ya mabomba Sinai kata ya Lilambo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Mhandisi Vicent Bahemana akizungumza na wananchi baada ya kukabidhi mabomba ya mradi wa maji katika mtaa wa Sinai na Mang’ula Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Wananchi wa mtaa wa Sinai na Mang’ula Kata ya Lilambo waliojitokeza kupokea mabomba ya mradi wa maji kutoka mamlaka ya maji safi na salama SOUWASA Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Na Regina Ndumbaro - Songea. 

Wananchi wa mtaa wa Sinai na Mang’ula Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa za kuleta maendeleo, hususan katika sekta ya maji. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao akiwemo Winfrida Gama na Renatus Sevelini wamesema wamekuwa wakikosa huduma ya maji kwa muda mrefu, hususan mashuleni, lakini sasa wanashuhudia mabadiliko makubwa na kuondokana na adha ya kubeba ndoo kichwani kwenda kutafuta maji mbali na makazi yao.

Kwa upande wake, Mhandisi Vincent Bahemana kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini na Mijini (SOUWASA) amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa maji katika maeneo hayo umegharimu shilingi bilioni 1.5. 

Mradi huo unahusisha ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 44.9, uchimbaji wa visima vya maji pamoja na ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200,000 za maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma endelevu.

Mhandisi Bahemana ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya mradi huo, amewasisitiza kuwa mafanikio ya mradi huo yanahitaji ushirikiano mzuri kati ya jamii na mafundi. 

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mafundi wanaotekeleza mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

Diwani wa Kata ya Lilambo, Mhe. Exsaveri Iyobo, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mhe. Damas Ndumbaro, kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi. 

Amesema hapo awali wananchi walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji, lakini sasa wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao, jambo ambalo limeleta faraja kubwa.

Wananchi wa mitaa ya Sinai na Mang’ula sasa wanafurahia matokeo ya juhudi za Serikali katika kuwapelekea huduma muhimu. 

Wametoa wito kwa wenzao kuendelea kulinda miundombinu hiyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo, huku wakisisitiza kuwa maendeleo yanapokuja, ni jukumu la kila mmoja kuyatunza.
Share:

TEA KUTUMIA MILIONI 300 KUKARABATI JENGO LA BODI YA MAKTABA PEMBA

Mratibu wa Bodi ya Maktaba Pemba Bw. Ahmed Hamis ( mwenye tisheti) akielekeza kitu kwa Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda, wakati wa ziara ya kukagua hali ya uchakavu wa jengo litakalofanyiwa ukarabati.


*********

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inaendelea na juhudi za kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji nchini kote. Katika jitihada hizo, TEA imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Bodi ya Maktaba lililopo kisiwani Pemba. 

Ukarabati huu unalenga kuimarisha miundombinu ya taasisi hiyo muhimu inayotoa huduma kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza katika ziara ya ukaguzi kisiwani Pemba, Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA, Bw. Masozi Nyirenda, alieleza kuwa fedha hizo tayari zimetolewa. 

Alibainisha kuwa ukarabati utaanza mara tu baada ya mkandarasi kusaini mkataba rasmi na kuwasilisha mpango kazi utakaoonesha hatua kwa hatua namna kazi hiyo itakavyotekelezwa hadi kukamilika kwa wakati.

Mradi huu wa ukarabati unatekelezwa kama sehemu ya majukumu ya TEA kama taasisi ya Muungano, ambayo kimsingi inahusika na utafutaji wa rasilimali kutoka kwa wadau mbalimbali ili kusaidia jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu. 

Kupitia miradi kama hii, TEA inalenga kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata mazingira bora ya kujifunzia bila kujali eneo analotoka.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Bodi ya Maktaba Pemba, Bw. Ahmed Hamis, jengo linalotarajiwa kukarabatiwa ni miongoni mwa majengo ya kihistoria yaliyojengwa kipindi cha ukoloni.

 Hata hivyo, tangu lijengwe, jengo hilo halijawahi kukarabatiwa, jambo lililosababisha uchakavu mkubwa wa jengo zima na miundombinu ya ndani, na hivyo kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bw. Hamis ameongeza kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutakuwa ni faraja kwa wakazi wa Wilaya jirani ambao hutegemea huduma za maktaba hiyo kwa ajili ya kusoma vitabu, hasa watoto wanaohitaji nyenzo za kielimu kama vile hadithi na historia za watu mashuhuri. 

Ukarabati huu unatarajiwa kuleta mwamko mpya wa elimu na kujifunza miongoni mwa wakazi wa Pemba.

Muonekano wa hali ya uchakavu katika jengo la Bodi ya Maktaba - Pemba ambalo litafanyiwa ukarabati kupitia TEA

Mratibu wa Bodi ya Maktaba Pemba Bw. Ahmed Hamis ( mwenye tisheti) akielekeza kitu kwa Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda, wakati wa ziara ya kukagua hali ya uchakavu wa jengo litakalofanyiwa ukarabati.

Muonekano wa hali ya uchakavu katika jengo la Bodi ya Maktaba - Pemba ambalo litafanyiwa ukarabati kupitia TEA


Ukaguzi wa jengo la Bodi ya Maktaba Pemba ukiendelea kuona hali halisi ya uchakavu kabla ya ukarabati kuanza.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger