Tuesday, 25 March 2025

WANAWAKE 3000 DODOMA KUNUFAIKA NA KOZI MBALIMBALI KUTOKA VETA




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewahimiza wakina mama wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanajifunza kwa makini na kuwa tayari kupokea mafunzo watakayopatiwa na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwani yatawasaida kwenda kuajiliwa na kuwa watumishi bora.

Senyamule ameyasema hayo leo Machi 24,2025 Jijini Dodoma wakati akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya wanawake hao na kuongeza kuwa watakuwa watumishi bora kwasababu wametoka kwenye mafunzo ya VETA yenye ujuzi na utaalamu wa ufundi wanaoufanyia kazi.

"Mimi nina imani kuwa mafunzo haya yatakwenda kuleta mapinduzi katika sekta ya huduma hizo mnazojiajili ndani ya mkoa wa Dodoma, hivyo nitoe pongezi kwa Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwani anafanya kazi nzuri sana na ndiye amefanikisha hili kwa juhudi zake anazozifanya,"amesema.

Aidha amesema kuwa wanawake wengi hawana ujuzi ndiyo maana hata kujiajili ili watoe huduma mbalimbali imekuwa changamoto pia hawana mitaji jambo linalopelekea wakipewa tenda za kazi kutatamani kukimbia.

"Unaweza ukampa tenda akasema napata wapi mtaji wa kutoa hiyo tenda, lakini bado kuna suala la nidhamu ya kazi yeye anajua pia akipata kazi anaifanyaje,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore amesema katika mafunzo wanayoyatoa eneo waliloliwekea mkazo ni kuhakikisha wanawake wanaodahiliwa katika vyuo vya ufundi stadi wanaongezeka hadi kufikia 45% .

"Sasa hivi tunapata changamoto tuko 27% kunamuda tunakuwa hapo tunafika 35% lakini lengo letu tunataka tufike 45% wawe ni wanawake na kuweza kufikia haya tunayo mafunzo mbalimbali ambayo tunahitaji tuweze kuyafanya ili kuhakikisha sasa eneo hili la kufikia asilimia hizo tunazifikia,"amesema.

Awali Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha amesema dhumuni la kuandaa mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi wanawake wa Mkoa wa Dodoma ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii yao pamoja na familia zao na hivyo kuleta tija kwa taifa.

"Lengo ni kuwafikia wanawake wa Mkoa wa Dodoma wapatao 3000 na hivyo utaratibu utakuwa kwa hawamu na kwa kuanza tutaanza na wanawake 250 watakapomaliza watakuja wengine 250 mpaka tuweze kufikia idadi yetu ya mwisho tuliyoilenga,"amesema.

Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi amesema wamefurahia fursa hiyo na wako tayari kujifunza hivyo wanaamini kupitia mafunzo hayo wataenda kuwa bora, wajuzi na kuongeza kipato na hali ya wanwake kuonekana ombaomba inakwenda kuondoka.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Mkuu ww Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Wanawake wa kikundi cha wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi chao.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.



Picha ya pamoja ya washiriki wa ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.
Share:

Monday, 24 March 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 25,2025



Magazeti
Share:

WASIRA, ASKOFU BAGONZA WAKUTANA, WATETA KARAGWE



Na Mwandishi Wetu,Bukoba

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, wamekutana na kuzungumza wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.

Wasira na Dk. Bagonza wamekutana jana wilayani Ngara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara mkoani Kagera.




Share:

Video Mpya : NG'WANA KALANGA - ICHOLA

 

Share:

"HAIWEZEKANI ANIFANYIE HIVI HALAFU ANIACHE", MDADA ASIMULIA

Jina langu ni Aisha kutoka nchini Kenya, kipindi cha nyuma nilikuwa kwenye uhusiano na kijana mtanashati kweli kweli, kila mwanamke mwenye afya njema, basi ni lazima angevutiwa naye kimahaba.

Kijana huyu aitwaye, Abdallah alikuwa akifanya kazi ya kuongoza watalii katika maeneo mbalimbali hapa Tanga, aliwahi kuniambia kuwa utanashati wake ndio uliofanikisha kupata kazi hiyo yenye fedha nyingi.

Kijana huyo katika mchezo wa kitanda hakuwa mchovu hata kidogo kwani alikuwa bingwa kila wakati tulipokuwa na mchuano, alijua kunichanganya sana kwa penzi lake tamu ajabu, alijua kunipa raha kusema kweli hadi nikawa sijielewi kwake.

Hata hivyo, siku zilipozidi kwenda mambo yalianza kubadilika kwani Abdallah hata alianza kutorudi nyumbani kama iliyokuwa kawaida yake kila wikendi kitu ambacho kilininyima raha kabisa.

Suala hili lilianza kunitia wasiwasi kwani sikuamini pendo langu kwake lingeelekezwa kwingine, nilikumbwa na msongo wa mawazo kwani alikuwa ndiye mpenzi wangu wa kwanza kuwahi kumpata katika ujana wangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu.

Kuna siku alinitembelea na niliopomuliza mbona tabia zake zilikuwa zimeanza kubadilika alisema kuwa kila kitu kilikuwa shwari, hivyo niendelee kumwambini kama mpenzi wake, basi nilikubaliana naye kishingo upande.

Ila akilini nilijua kwamba alikuwa akinificha ukweli wa mambo, pia nilifahamu kuwa alikuwa keshapata mpango wa kando jambo lililonikasirisha kwani urembo wangu huu ulikuwa kwa ajili yake.

Jinsi muda ulivyokuwa ukisonga ndivyo mambo yalikuwa yanakuwa hata mabaya zaidi kwani wakati mwingine hata alisusia kunipa mapenzi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Nilifahamu kwamba alikuwa amepata mpenzi mwingine na hapo uhusiano wetu yakaisha kwa wakati ule huku nikiachwa mpweke bila kujua nini cha kufanya maishani, tayari kashanitoa bikira halafu ananiacha.

Basi nilibaki nimesononeka tu, baada ya siku kadhaa nilikumbana na tovuti ya Kiwanga Doctors nilipokuwa katika hali ya kusoma vitu mtandaoni.

Nilifuatilia kila kitu kilichoendelea kwenye tovuti ile na hapo nikaona kuwa Kiwanga Doctors alikuwa na uwezo wa kunisaidia kumrudisha mpenzi wangu. 

Nilifunga safari hadi kwenye ofisi za Kiwanga Doctors huko Migori, Kenya kwa ajili ya usaidizi, alinishughulikia kupitia utaalam wake wa miaka mingi (get back your ex lover) na kunihakikishia kuwa mambo yatakuwa sawa.

Kisha nikarejea nyumbani, baada ya siku chache Abdallah alinipigia simu kwamba alitaka tukutane. Siku iliyofuata nilienda kwake, nilipofika alinipokea vizuri na kuniomba msamaha pamoja na kunipa zawadi.

Tangu siku hiyo uhusiano wetu umekuwa imara kwani mwishowe tulifunga ndoa ya kifahari na kuwa mke na mume na sasa tuna familia ya watoto wawili wa kiume.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

Sunday, 23 March 2025

TAIFA GAS , UMOJA WA MAMA LISHE TANZANIA WAUNGA MKONO NISHATI SAFI YA DKT. SAMIA


Baadhi ya akina mama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania (UMALITA) kulia wakipika futari kwa kutumia majiko ya gesi wakati wa hafla ya kusoma dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan na watoto yatima wakati wa futari iliyoandaliwa na umoja huo kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam kwa udhamini wa Taifa Gas
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania wamekusanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma dua ya kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwafuturisha watoto wa yatima ikiwa ni sehemu ya sadaka kwenye mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Masoko wa Taifa Gas, Anthony Martin kwenye shughuli ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na futari kwa ajili ya watoto yatima

***
Umoja wa Mama Lishe Tanzania (UMALITA) umesoma dua ya kumwombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kumpongeza katika juhudi zake za kuhamasisha watanzania na matumizi ni nishati safi kwa ajili ya kupikia ili kuokoa mazingira.

Akizungumza jana kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Umoja huo , Jane Nyanda amesema kwamba umoja huo unaunga mkono kampeni ya Rais Dkt. Samia Suluhu ya kampeni ya nishati safi.

“Tumekusanyika hapa kwa mambo mawili kwa ajili ya kumwombea Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake hizo za kampeni ya nishati safi kwa sababu sie mama lishe kampeni hii inatugusa moja kwa moja kwenye shughuli zetu za kila siku,”

“Ukizingatia sisi ni mama lishe tunapaswa kuzungumza suala la nishati safi ili kuendelea kulinda mazingira lakini pamoja hayo pia tunaipongeza kampuni ya Taifa Gas kwa kutuunga mkono kwenye shughuli yetu hii,” amesema Bi. Nyanda.

Amesema kampuni ya nishati ya Taifa Gas ni wadau wakubwa wa mama lishe Tanzania na kampuni hiyo pia ni wawezeshaji wakubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi hapa nchini.

Bi. Nyanda ameongeza kwamba mitungi ya Taifa Gas ni mizuri kwa ubora, ufungaji na ujazo wa gesi na ni salama kwa matumizi ya nyumbani , kwenye sehemu ya biashara na makazini.

Amefafanua kwamba shughuli hiyo ya dua ilikwenda sambamba na kuwafuturisha watoto yatima kwa kupikia mitungi ya Taifa Gas na njia moja wapo ya kuhamasisha watanzania waendelee kutumia nishati safi hata kwenye vituo ya watoto yatima.
Share:

Saturday, 22 March 2025

ACHENI MIGOGORO NDANI YA CHAMA, CHAPENI KAZI – ODDO MWISHO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akizungumza na wananchi na wanachama Kata ya Namiungo Wilayani Tunduru

Na Regina Ndumbaro  - Tunduru .

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amewataka viongozi wa chama hicho kuacha migogoro na badala yake waelekeze juhudi zao katika kuwahudumia wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Tarafa ya Nakapanya, Wilaya ya Tunduru, Oddo amesisitiza umuhimu wa mshikamano ndani ya chama ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi.

Ziara hiyo ilihusisha mazungumzo na wanachama wa CCM kutoka kata nane, ambapo aliwataka viongozi wa chama kuwaelimisha wanachama kuhusu umoja na ushirikiano kwa ajili ya ustawi wa chama na wananchi.

Katika hotuba yake, Oddo Mwisho ametoa rai kwa viongozi wa chama kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi.

Amewakumbusha wenyeviti wa vijiji na mitaa kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa mujibu wa taratibu, huku akisisitiza kuwa madiwani wana wajibu wa kusimamia mikutano hiyo.

Aidha, amewataka viongozi wa kata kuwahimiza watendaji wa vijiji kufanya mikutano na kuhakikisha haki na sheria vinafuatwa katika uongozi.

Pamoja na kuhimiza mshikamano ndani ya chama, Oddo Mwisho ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa katika kuboresha miundombinu, huduma za afya, maji, na umeme.

Ameeleza kuwa serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, akitolea mfano ujenzi wa madarasa, madawati, na vyoo safi katika shule za msingi, kama vile Shule ya Msingi Ligoma.

Pia amewahimiza wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia na kuzilinda kura zake katika uchaguzi ujao.

Katika mkutano huo, wananchi wamepata nafasi ya kueleza changamoto zao, miongoni mwao Yasin Omar aliuliza kuhusu ubovu wa barabara ya Mindu-Ngapa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma amejibu kuwa watawasiliana na mamlaka husika, ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ili kuhakikisha barabara hiyo inafanyiwa matengenezo.

Aidha, Ausi Mohamed ameuliza kuhusu changamoto ya mikopo kwa wananchi, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Hairu Musa, ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa mikopo hiyo, lakini amesisitiza kuwa elimu zaidi inahitajika kwa wananchi ili waweze kunufaika na fursa hiyo.

Oddo Mwisho amewataka wanachama wa CCM kufikiria maendeleo badala ya kugombania nafasi za uongozi kwa sasa.

Amesisitiza kuwa huu si wakati wa malumbano, bali ni kipindi cha kujenga mshikamano na kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika jamii.

Pia amewahakikishia wananchi kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa suluhisho kwa wakati.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akizungumza na wananchi na wanachama Kata ya Nakapanya Wilayani Tunduru

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger