Tuesday, 18 February 2025

SERIKALI KUENDELEA KUVUTIA WAWEKEZAJI WILAYANI SONGEA


Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Aviv Ltd inayojishughulisha na kilimo cha zao la kahawa katika kijiji cha Lipokela Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Hamza Kassim kushoto akiwaonyesha baadhi ya kampuni hiyo miche bora
Sehemu ya Shamba la Aviv Ltd lililopo katika kijiji cha Lipokela Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Aviv Ltd Hamza Kassim akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni.

Na Regina Ndumbaro - Malunde 1 blog Songea 

Serikali Wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaotaka kuwekeza na kushiriki shughuli za maendeleo wilayani humo. 

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Kapenjama Ndile, ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akitembelea shamba la kahawa la Aviv Tanzania Ltd lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 3,000 katika kijiji cha Lipokela.

Ndile amesema kuwa kampuni ya Aviv Ltd imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi tangu ilipoanza shughuli zake, ambapo mwaka jana pekee ililipa zaidi ya Shilingi milioni 700 kama mapato kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kutokana na mauzo ya kahawa, fedha zilizotumika kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.

Amebainisha kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali itaendelea kushirikiana na halmashauri zake kujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji, kuhakikisha hawakumbwi na vikwazo vinavyoweza kuathiri ulipaji wa mapato na kusababisha halmashauri kushindwa kujiendesha.

Ndile amesifu ubora wa kahawa inayozalishwa katika shamba la Aviv, akisema ina ladha bora zaidi kuliko kahawa kutoka mikoa mingine nchini, na kuongeza kuwa Wilaya ya Songea ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji wa kilimo kutokana na ardhi nzuri na mazingira yanayofaa kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Wilaya ya Songea, kwa mujibu wa Ndile, ni ghala kuu la hifadhi ya chakula nchini, hivyo akawahimiza wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo na uwekezaji. 

Amemtaja pia mwekezaji mwingine, kampuni ya Ndolela Farm katika Halmashauri ya Madaba, ambayo imepewa hekta 500 kwa kilimo cha mahindi na ngano inayotumika kama chakula na malighafi ya kutengeneza bia.

Meneja Uzalishaji wa Aviv Ltd, Hamza Kassim, amesema kuwa shamba hilo huajiri wafanyakazi kati ya 4,000 hadi 5,000 wakati wa msimu wa mavuno, hali inayochangia ajira kwa wananchi kutoka mikoa mbalimbali nchini na kuongeza mapato ya serikali kupitia halmashauri na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Baadhi ya wananchi waliopata ajira katika shamba hilo walisema limewasaidia kujikwamua kiuchumi. Yovitha Komba kutoka Ruvuma alieleza kuwa ajira aliyopata imemwezesha kusomesha watoto, kulipa michango na kujenga nyumba ya kuishi, huku akiitaka serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.

Rashid Mrope kutoka Masasi, Mkoa wa Mtwara, amesema anajivunia kufanya kazi katika Aviv Ltd kwani amepata fursa za kuboresha maisha yake na kujikwamua na umaskini kupitia ajira anayopata shambani hapo.
Share:

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTEKELEZA MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA NA KATEWAKA





......

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na Mwekezaji wa Mradi wa Makaa ya Mawe Ketawaka Kampuni ya MM Steel Resource Public Ltd( MMSR) kufikia makubaliano ndani ya wiki tatu ili utekelezaji wa Mradi huo uanze.

Vilevile, Waziri Jafo ameliagiza Shirika hilo kushirikiana na Wadau wake mbalimbali katika Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma na Katewaka kujenga majengo mawili katika Shule ya Msingi Nkomang'ombe iliyopo katika maeneo ya Miradi hiyo.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Mkoani Njombe katika Wilaya ya Ludewa yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi Mchuchuma na Ketawaka, Liganga na Maganga Matitu pamoja na kuongea na Wananchi wa maeneo hayo.

Akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Nkomang’ombe, Waziri Jafo amewahakikishia kuwa atashurukiana nao kuhakikisha Mtafi huo unaanza kutekrlrzwa ili kutumiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita, kuongeza ajira na Pato la Taifa kwa ujumla.

Awali Afisa Mradi wa NDC Bw. Wallu Kapaya akitoa Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Ketawaka amesema Mradi huo una tani milioni 100 za makaa ya mawe utakaapoqnza uchimbaji una uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.5 kwa mwaka na unatarajiwa kudumu kwa miaka 100 huku ukitoa ajira 1000 ambapo ajira za moja kwa moja 250

Naye Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo Bi Esther Mwaigomole akitoa Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Makaa ya Mawe ya Mchuchuma yaliyogunduliwa mwaka 1860. amesema Mradi huo unahifadhi tani milioni 426 za Makaa ya Mawe ambapo uzalishaji ukianza tani milioni tatu zitazalishwa kwa mwaka na Mradi utadumu kwa miaka 426 huku ukitoa ajira 33000.

Viongozi wa Mkoa wa Njombe, akiwemo Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw. Juma Sweda na Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga, wamesema kuwa kukamilika kwa miradi ya Mchumchuma na Ketawaka kutakuwa hatua kubwa katika kubadilisha uchumi wa wananchi wa Ludewa na maeneo jirani,.
Share:

Monday, 17 February 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 18,2025

Magazeti





Share:

WAZIRI MAVUNDE APIGA MARUFUKU WAGENI KUINGIA KWENYE LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO


▪️Awataka wenye Leseni kufuata taratibu za kisheria za msaada wa kiufundi

▪️Serikali kutunga kanuni za kuratibu wageni kwenye Leseni ndogo

▪️Awataka RMO kufanya ukaguzi katika maeneo yao

▪️Awaonya wachimbaji wanaoingiza wageni kinyemela



📍Morogoro

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amepiga marufuku raia wa  kigeni kuingia na kufanya shughuli kwenye leseni za uchimbaji mdogo; hii ni kufuatia changamoto zilizobainika katika uingiaji mikataba ya utoaji wa misaada ya kiufundi kati ya wamiliki wa leseni ndogo za uchimbaji madini na raia wa kigeni. 

Amesema hayo leo Februari 17, 2025 wakati akifungua Kikao Kazi cha kupokea maoni kutoka kwa wadau kuhusu mapendekezo ya kuandaa Rasimu ya Kanuni za Madini za Utoaji Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini za Mwaka 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Edema Hoteli Mkoani Morogoro.

Aidha, Waziri Mavunde ametoa wito kwa washiriki wote wa Kikao Kazi hicho kutoa maoni yao kwa uhuru na uwazi ili kusaidia upatikanaji wa Kanuni nzuri na inayotekelezeka kwa lengo la kuongeza tija katika mnyororo mzima wa shughuli za Sekta ya Madini nchini na kutekeleza sharti la kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini Sura Namba 123.

"Katika kipindi cha muda mfupi tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwenye Sekta ya Madini kutokana na utashi wa Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatamani kuona wachimbaji wadogo wanafikiwa, ambapo leo naagiza ofisi ya Kamishna kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kuhitimu kutoka hapo walipo na kuendelea mbele"

"Haiingii akilini, mgeni anakuja, anaingia kwenye leseni ya mchimbaji mdogo kupitia mkataba wa utoaji msaada wa kiufundi, wachimbaji wadogo hawanufaiki wala kuendelea zaidi kimatumizi ya teknolojia na mitaji, hili halikuwa lengo la Sheria katika kuweka sharti hilo ili kuendeleza wachimbaji wadogo", alibainisha Waziri Mavunde.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mavunde ametoa onyo kwa wachimbaji wadogo kutowakaribisha wageni bila kufuata utaratibu katika leseni za uchimbaji mdogo wa madini ambapo itapelekea kufutiwa leseni kwa atakaye kiuka agizo hilo na kutoa angalizo kwa Maafisa Madini Nchini kudhibiti uingiaji wa wageni bila kufuata taratibu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesema Kikao hicho kimelenga kupokea mapendekezo ya wadau kwa ajili ya kuandaa rasimu ya Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa ajili ya wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo ambapo Wizara iko huru na tayari kupokea maoni ya kila mdau.

Naye, Rais wa Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini Tanzania John Bina amempongeza Waziri Mavunde kwa uamuzi wa kuwashirikisha wadau wa Sekta ya Madini wakiwemo wachimbaji wadogo ili kuandaa rasimu ya Kanuni hizo kuliko kujifungia na kuandaa Wizara pekee.

Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Wachimbaji Wadogo kutoka mikoa yote nchini, vyama vya wachimbaji wadogo wanawake Tanzania na wafanyabiashara wa madini nchini.

Share:

Ngoma Mpya : KISIMA Ft. SHILANGILA - TENDA WEMA

Share:

Ngoma Mpya : KISIMA Ft. SHILANGILA - LUSALO

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger