Friday, 31 January 2025
Thursday, 30 January 2025
ATCL YATANGAZA NAFASI 59 ZA AJIRA KWA WATANZANIA
Wednesday, 29 January 2025
ELIMU YA URAIA, UTAWALA BORA YAWAFIKIA NEWALA
WATUMISHI THBUB WATAKIWA KUTUMIA MIKUTANO YA BARAZA LA WAFANYAKAZI KUJADILI MAMBO YANAYOLETA TIJA
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wametakiwa kutumia mikutano ya Baraza la wafanyakazi kujadili mambo yanayoleta tija katika kuongeza ufanisi wa kazi.
Bi. Msemwa amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi ni sehemu sahihi ya kujadili, kushauri na kutoa mapendekezo juu ya njia sahihi ya kuongeza ufanisi wa kazi utakaosaidia kuweka mazingira mazuri kwa Wafanyakazi na Taasisi kwa ujumla.
“hivyo niwaombe wajumbe mtakaochaguliwa hakikisheni mnatumia vyema nafasi hiyo kwa kujadili yale yatakayokuwa na tija kwa watumishi wote.”amesema Bi.Msemwa
Naye, Mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Fraksed Mushi ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu THBUB, amesema kuwa kila mjumbe aliyechaguliwa anawajibu wa kutumia nafasi hiyo kushauri na kutoa maoni yatakayo saidia kujenga Mazingira bora kwa wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
“Tumieni Baraza hili katika kujadili mambo muhimu na kutoa mapendekezo sahihi juu ya kuboresha mazingira ya kazi, Idara na Vitengo ili kuongeza tija na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kuendeleza taasisi” amesema Bw. Mushi.
Jumla ya wajumbe tisa (9) walichaguliwa katika kikao hicho ambapo watatumikia nafasi hizo kwa muda wa miaka mitatu.



WANAHABARI KAGERA WANOLEWA DHIDI YA UGONJWA WA MURBURG
Tuesday, 28 January 2025
NI ZAMU YA TANDAHIMBA,WIZARA YA KATIBA NA SHERIA HAKUNA KULALA
MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATAKA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KUKAMILIKA OKTOBA 2025
TANESCO YAJITOKEZA KUTOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI BORA YA NISHATI YA UMEME KATIKA MKUTANO WA NISHATI AFRIKA
ORYX GAS YAWAKUTANA NA MAWAKALA MIKOA YOTE KUWEKA MIKAKATI YA 2025
THBUB YAENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA MISINGI YA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI KATA

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala (THBUB) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe.Mohamed Khamis Hamad,umetoa mafunzo kwa Watendaji Kata wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, leo Januari 27,2025 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Halmashauri hiyo.













































