Saturday, 25 January 2025

Picha : RC MACHA AZINDUA WIKI YA SHERIA SHINYANGA, APONGEZA MAHAKAMA KWA UFANISI

Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mcheza ngoma akicheza na nyoka wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga - Picha na Marco Maduhu na Kadama Malunde

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amezindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga na kuipongeza Mahakama kwa ufanisi wake katika kusikiliza mashauri kwa wakati na kutoa haki kwa wananchi.

Macha amezindua maadhimisho hayo leo, Januari 25, 2025, katika viwanja vya Zimamoto, vilivyopo eneo la Nguzonane, Manispaa ya Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo, Macha amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya sheria, kujua kazi za Mahakama, na namna ya kufungua mashauri ili waweze kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha.

“Maadhimisho haya ya Wiki ya Sheria ni muhimu sana kwa wananchi, kwani kuna watu wengi wanashindwa kupata haki zao kutokana na kutokujua sheria. Hivyo, ni vyema wakajitokeza kwa wingi kwenye vibanda na wapate elimu ya sheria, namna ya kufungua mashauri mahakamani, pamoja na kujua kazi za Mawakili,” amesema Macha.

Pia, Macha ameipongeza Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga kwa kasi kubwa ya kusikiliza mashauri.

 Amesema kuwa mwaka jana (2024) hakuna viporo vya mashauri na kwamba mashauri yote yalikuwa yamesikilizwa kwa wakati.

 Ameisihi Mahakama iendelee na kasi hiyo ya ufanisi mwaka huu (2025).

Katika hatua nyingine, Macha amezungumzia Mahakama za Mwanzo na kusema kuwa kuna haja ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa mashauri katika ngazi hizo ili wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia uadilifu, weledi na uwajibikaji.

Macha amewataka wananchi kutii maamuzi ya Mahakama. 

Amesema ikiwa wananchi hawajaridhika na maamuzi hayo, wanapaswa kukata rufaa na kwenda ngazi za juu zaidi.

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali, ameeleza kuwa katika Wiki ya Sheria, elimu ya sheria itatolewa bure kwa wananchi kupitia vibanda mbalimbali vilivyopo viwanja vya Zimamoto na maeneo ya mikusanyiko, magereza, mashuleni na vyuo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali.

Amesema maadhimisho hayo yatakuwa na bonanza la michezo mbalimbali, ambalo litafanyika jijini Mwanza tarehe 1 Februari, huku kilele cha Wiki ya Sheria kikifanyika tarehe 3 Februari katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Aidha, maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria yanaashiria mwanzo wa shughuli za Mahakama kwa mwaka mpya, baada ya kumalizika kwa likizo ya Mahakama, ambayo huanza tarehe 15 Desemba na kumalizika tarehe 31 Januari kila mwaka.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka huu inasema: “Tanzania 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo, Januari 25, 2025, katika viwanja vya Zimamoto, vilivyopo eneo la Nguzonane, Manispaa ya Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akimpa zawadi mwanafunzi aliyeimba vizuri wimbo wa Afrika Mashariki wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Sehemu ya meza kuu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Sehemu ya meza kuu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mcheza ngoma akicheza na nyoka wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mcheza ngoma akicheza na nyoka wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mcheza ngoma akicheza na nyoka wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Wadau waki kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Wadau waki kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Wadau waki kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Wadau waki kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Matembezi ya Km 6  yakiendelea Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Mazoezi yakiendelea baada ya Matembezi ya Km 6  wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga




Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga

Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu
Share:

KARATU WAHAMASISHWA KUSAJILI VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA


Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Diego, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Renatus Lucas, akitoa ufafanuzi kuhusu akiba baada ya kuwagawia vipeperushi kuhusu akiba, baada ya kuhitimisha programu ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa wilaya ya Karatu ambapo Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilitoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Diego, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akifafanua kuhusu umuhimu wa kuzingatia mikataba ya mkopo, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Diego, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Mratibu Huduma Ndogo za Fedha Wilaya ya Karatu Bw. Joshua Mwamsojo, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbulumbulu, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Ofisi ya Tarafa ya Mbulumbulu, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Msajili wa Vikundi vya Huduma Ndogo za Fedha Wilaya ya Karatu, Bw. Richard Motta, akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Mbulumbulu kuhusu utaratibu wa upatikanaji wa mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Ofisi ya Tarafa ya Mbulumbulu, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha. 

Baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Mbulumbulu, wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Diego, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Karatu, Arusha)


Na. Saidina Msangi, WF, Karatu, Arusha.


Serikali imetoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa vikundi vya huduma ndogo vya fedha vinavyojulikana kama VICOBA vinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2028 ili kuweza kujikwamua kiuchumi, kupata mikopo katika Taasisi za Fedha na kuondokana na changamoto ya kiutendaji.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi za Wizara ya Fedha na watoa huduma za Fedha kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha zilizo rasmi katika ukumbi wa Ofisi ya Tarafa ya Mbulumbulu, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Bw. Kibakaya alisema kuwa vikundi vya huduma ndogo za fedha vinavyotumiwa na wananchi katika maeneo mengi mjini na vijijini ni muhimu kusajili ili kuweza kutambulika kisheria na kupata fursa mbalimbali katika Halmashauri na Taasisi za Fedha.

‘‘Usajili wa vikundi vya huduma ndogo za fedha ni muhimu sana na unafanyika kwa njia ya mfumo ambapo mwana kikundi anaweza kujisajili mwenyewe bila kwenda Ofisi ya Halmashauri. mfumo unaotumika unaitwa "WEZESHA PORTAL" pia Halmashauri zote Nchini wapo Waratibu wa Huduma Ndogo za Fedha ambao watawasajili kupitia Mfumo huo” alisema Bw. Kibakaya.

Alisisitiza kuwa usajili wa vikundi vya huduma ndogo za fedha utawawezesha pia kunufaika na mikopo ya halmashauri ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali ambayo imeanza kutolewa ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Naye Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, amesisitiza wananchi kusoma mikataba ya mikopo ili kujua masharti ya mikataba na utekelezaji wake na kuwa na uhakika wa urejeshaji wa mkopo ili kuepuka migogoro na watoa huduma.

Aidha, alisisitiza wananchi kuzingatia kiwango cha mkopo wanachopokea kilingane na kiwango kilichoandikwa katika mkataba, kufahamu riba ya mkopo, aina ya urejeshaji na kufahamu adhabu ya kuchelewesha kurejesha mkopo kabla ya kusaini mkataba.

‘Ni muhimu kuhakikisha mkataba una kipengele kinachotoa fursa ya majadiliano juu ya marekebisho ya masharti ya mkataba ikiwemo kuongezewa muda wa marejesho ili kumpatia nafuu ya marejesho tofauti na awali endapo mkopaji atapata changamoto itakayosababisha kushindwa kurejesha mkopo kwa wakati,’ alisisitiza Bw. Myonga.

Kwa upande wake Mratibu Huduma Ndogo za Fedha Wilaya ya Karatu, Bw. Joshua Mwamsojo, alisema kuwa mafunzo hayo yatawezesha wananchi kufuata Sheria na taratibu za namna ya ukopaji, ili kuepukana na mikopo isiyo rasmi.

‘‘Naipongeza Serikali kwa mafunzo haya na nitoe rai mafunzo haya yawe endelevu ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kusaidia kuondokana na changamoto za fedha. Natoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Karatu waepuke kukopa katika taasisi zisizo rasmi, watumie elimu waliyoipata katika kupanga matumizi ya fedha wanazopata na nina Imani yatawasaidia kujikwamua kiuchumi dhidi ya umaskini’ alisisitiza Bw.Mwamsojo.

Maeneo yaliyofikiwa katika Wilaya ya Karatu ni pamoja na Kata ya Karatu Mjini, Tarafa ya Endabash (Kata ya Kansay, Kata ya Buger na Kata ya Endabash), Tarafa ya Eyasi (Kata ya Mang’ola na Baray) na Tarafa ya Mbulumbulu (Kata ya Rhotia na kata ya Mbulumbulu) ambapo baada ya kuhitimisha programu timu hiyo inaendelea na programu katika Wilaya za Ngorongoro na Longido.
Share:

Friday, 24 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 25, 2025

Share:

THBUB KUTUMIA NJIA MBALIMBALI KUIFIKIA JAMII


   

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Khamis amesema Tume inaendelea kutuma njia mbalimbali  za kutoa elimu ya haki za binadamu  na misingi ya utawala bora ili wananchi waweze kutambua haki na wajibu wao.

Hayo ameyasema Januari 23, 2025 wakati akitoa elimu hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika  Kata ya  Kinampanda, Wilaya ya Ilamba Mkoani Singida.

Akitoa elimu kuhusu haki za binadamu na utawala bora, Mhe. Mohamed amesema kuwa Serikali ina dhamira nzuri ya kukuza na kulinda haki za binadamu kwa kuanzisha Ofisi ya THBUB yenye dhamana ya kuendeleza dhamira hiyo kwa kutekeleza  majukumu yake ambayo yameainishwa katika  Katiba ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania ya Mwaka 1977.

"Ibara ya 12 mpaka ya 24 ya Katiba ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania imeainisha haki mbalimbali ambazo ukizivunja Sheria inachukua mkondo wake" amesema Mhe. Mohamed 

Aidha, Mhe. Mohamed ametoa wito kwa jamii kutimiza wajibu wao ili wasikinzane na Sheria.

“Haki inaenda na Wajibu, ni wajibu wa kila mmoja kutii Sheria zilizowekwa” amesisitiza Mhe. Mohamed. 

Kwa upande wao,   wakazi wa  Kata ya Kinampanda waiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuendelea kutoa elimu juu ya Haki za Binadamu  na misingi ya Utawala Bora.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bw. Samson Mpanda amesema  kuwa wananchi wengi hawajui haki zao kama vile haki ya kujieleza na kutoa maoni, haki ya kumiliki mali na haki nyingine.

"Utakuta mtu anakamatwa anapokwonywa mali  kutokana na kutojua haki zake" amesema Bw. Mpanda


Share:

Thursday, 23 January 2025

PROF. MBARAWA AHIMIZA UJENZI WA HARAKA KIWANJA CHA NDEGE KIGOMA

Na Mwandishi Wetu, KIGOMA.

Waziri wa Uchukuzi Prof.  wa kiwanja cha Ndege Kigoma kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kinakamilika kwa wakati kutokana na kuchelewa kulikosababishwa na sababu mbalimbali. 

Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana alipotembelea kwa lengo la kukagua mradi huo wa upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa viwanja vinne ambapo viwanja vingine ni Tabora,Shinyanga na Sumbawanga vyote vikigharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 46.6.

" Wananchi wa Kigoma wamesubiri maboresho ya kiwanja hiki kwa muda mrefu hivyo tumsukume mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kazi imalizike haraka iwezekanavyo," Amesema Mbarawa.

Pamoja na hayo Prof. Mbarawa amemuagiza mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) kusimamia ubora katika ujenzi wa kiwanja hicho pamoja na kuharakisha uagizaji wa vifaa vya kukamilisha ujenzi wa jengo la abiria ili kutokwamisha kasi ya ujenzi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema wameupokea mradi huo kwa furaha na shauku kubwa na kuahidi kutoa ushirikiano kadri unatakavyohitajika kusaidia mradi kukamilika na kuanza kutumika.

Aidha Mhandisi wa Mradi kutoka Tanroads Donatus Binemungu amesema kwa siku za karibuni hali ya mvua imekuwa kikwazo cha kasi ya ujenzi huku akieleza kuwa ujenzi wa jengo la abiria umefikia asilimia 50 na ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege ukiwa kwenye hatua nzuri zaidi.

Share:

Breaking : TAZAMA HAPA 23 Thu Jan MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024

Share:

KARIBU KATIKA USIKU WA WADAU SHINYANGA 2025 MSIMU WA 3


📢 Fursa Adimu kwa Wadau wa Maendeleo!

Karibu kwenye tukio la kipekee ambalo limekusudiwa kusherehekea michango ya kipekee ya wadau wenye maono ya kuinua maendeleo ya Shinyanga. Tukio hili litakusanya viongozi, wadau wa kibiashara, na wanajamii wa kada mbalimbali kwa lengo la kujenga ushirikiano wenye matokeo chanya.

📅 Tarehe: Jumamosi, 01 Februari 2025

📍 Mahali: Ukumbi wa Makindo, Shinyanga

⏰ Muda: Saa 12:00 jioni – Saa 6:00 usiku


🎯 KILELE CHA TUKIO:


1. Tuzo za Kipekee: Tunatoa heshima kwa wadau walioleta mchango wa dhati katika maendeleo ya Shinyanga.


2. Mtandao wa Kibiashara: Nafasi ya kujenga mahusiano yenye thamani kwa ukuaji wa kibiashara na kijamii.


3. Ushereheshaji wa Hali ya Juu: Chakula na vinywaji maalum vitakuwepo ili kukamilisha ladha ya tukio hili.


3. Burudani za Kisasa: Onyesho la wasanii wa ngazi za juu litapamba jukwaa la tukio kwa heshima yako.

💰 VIWANGO VYA KIINGILIO:

🎟️ VIP Single: TZS 50,000

🎟️ VVIP Single: TZS 100,000

🎟️ Meza ya VVIP (Watu 5): TZS 500,000

🎟️ Meza ya VVIP (Watu 12): TZS 1,000,000

📞 JINSI YA KUKATA TIKETI:

Hakikisha nafasi yako sasa!

Wasiliana nasi kupitia: 0756 254 146 au 0622 891 972

🌟 Jiunge nasi!

Ushiriki wako ni muhimu katika kuhamasisha maendeleo na mshikamano wa Shinyanga. Usiku huu sio tu burudani bali pia ni hatua thabiti kuelekea mustakabali wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

#Shinyanga2025 #WadauShupavu #MshikamanoNaMaendeleo

Share:

Wednesday, 22 January 2025

NOTI MPYA ZA FEDHA KUANZA KUTUMIKA FEBRUARI 1,2025 TANZANIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi elfu moja, kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, Noti ambazo zitaanza kutumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, kuanzia tarehe Mosi Februari, 2025.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi elfu moja, kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, Noti ambazo zitaanza kutumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, kuanzia tarehe Mosi Februari, 2025.

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasazinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.


Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.  
Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu. 

Share:

MATOGORO YAVUTIA WATALII, SERIKALI YAIMARISHA MIUNDOMBINU


Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Songea wakiwa katika Bustani za Msitu huo ya Matogoro

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanal Ahmed Abbas katikati Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Kapenjama Ndile na Kushoto ni Mhifadhi wa Msitu Asili wa Matogoro Musa Kitivo


Na Regina Ndumbaro Ruvuma.


Jumla ya watalii 871 wa ndani na 9 kutoka mataifa ya kigeni wametembelea msitu wa hifadhi ya asili wa Matogoro uliopo kata ya Ndilimalitembo, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, na kuchangia zaidi ya shilingi 1,472,390 katika mwaka wa fedha 2024/2025. 


Taarifa hiyo imetolewa na Mhifadhi wa Msitu huo, Mussa Kitivo, alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, aliyetembelea msitu huo jana.


Kwa mujibu wa Kitivo, mwaka wa fedha 2023/2024 uliwashuhudia watalii 2,341 wa ndani na 30 wa nje wakitembelea msitu huo, huku mapato ya shilingi 5,467,000 yakikusanywa kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). 


Amebainisha kuwa mwaka 2021/2022 TFS ilipokea shilingi 394,135,000 kutoka mpango wa maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya vumbi yenye urefu wa kilometa 9.


Kitivo ameeleza kuwa kazi nyingine zilizokamilika ni ujenzi wa njia ndogo ya miguu yenye urefu wa kilometa 4.3, kuboresha lango kuu la kuingia msituni, na kuimarisha vivutio mbalimbali. Vivutio hivyo ni pamoja na miinuko mikubwa inayotoa mwonekano mzuri wa mji wa Songea na vijiji vyake, chanzo cha Mto Ruvuma wenye urefu wa kilometa 800, na vyanzo vingine vya maji vinavyotegemewa na wakazi wa Songea kwa matumizi ya kila siku.


“Msitu wa Matogoro una vivutio vya kipekee, ikiwemo mapango yanayotumika kwa tiba za jadi na matambiko, pamoja na wanyama kama swala, digidigi, nyani, simba, na ndege mbalimbali. Aidha, hali ya hewa ya msitu huu ni tofauti na maeneo mengine ndani ya Ruvuma,” amesema Kitivo.


Kitivo ameongeza kuwa mkakati wa TFS kwa sasa ni kutafuta mwekezaji atakayejenga hoteli ya kitalii kwenye eneo la milima (viewpoint), kuongeza idadi ya watalii kufikia 5,000 mwaka huu, na kuboresha miundombinu ya msitu kwa kuweka choo cha kudumu, jiko la kisasa, na vifaa vya michezo kwa watoto. Pia, TFS inapanga kuanzisha utalii wa kuruka na parachuti kutoka viewpoint ya pili.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, amewapongeza wakala wa TFS kwa juhudi kubwa katika uhifadhi wa msitu wa Matogoro na vivutio vingine vya utalii mkoani humo. Ametoa wito kwa wakazi wa Ruvuma na kanda ya kusini kwa ujumla kutembelea vivutio vya utalii ili kujifunza na kuhamasisha uchumi wa ndani.


Kwa upande wake, Kamanda wa TFS Kanda ya Kusini, Manyise Mpokigwa, amesema Ruvuma ina misitu minne ya asili inayotumika kwa utalii, ikiwemo msitu wa Mwambesi wilayani Tunduru. Amebainisha kuwa Matogoro pia una utalii mpya wa ikolojia ambao umeanza kuvutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ndilimalitembo, Magnus Nyoni, amesema tangu msitu huo ulipohifadhiwa rasmi, wananchi wamefaidika kwa ajira, kuuza bidhaa kwa watalii, na kuongeza fursa za kipato. Ameipongeza serikali kwa juhudi zake za kuimarisha hifadhi hiyo, akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na TFS katika kulinda urithi huo wa asili.
Share:

Breaking! TUNDU LISSU MWENYEKITI MPYA WA CHADEMA!! MBOWE AKUBALI YAISHE!


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Katika hatua inayovutia na kuibua hisia mchanganyiko, Tundu Lissu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akimshinda mtangulizi wake, Freeman Mbowe aliyekuwa anatetea nafasi yake katika uchaguzi wa kihistoria uliofanyika Januari 21,2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

 Uchaguzi huu unafunga ukurasa wa miaka 21 ya uongozi wa Mbowe, ambaye ameiongoza CHADEMA kwa kipindi kirefu na aliyejizolea umaarufu mkubwa kama nguzo kuu ya upinzani nchini Tanzania.

Lissu, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kurejea kutoka uhamishoni na kuwa kiongozi shupavu katika upinzani, ameongoza kampeni ya kushinda nafasi hiyo. 

Hata hivyo, Mbowe amekubali matokeo kwa heshima, akimpongeza Lissu na kusema anajiandaa kuunga mkono uongozi wake mpya.

Licha ya matokeo ya jumla kutotangazwa baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza wajumbe wa mkutano mkuu matokeo yatatangazwa baadaye, lakini ukumbini shangwe limetawala. 

 Msingi wa shangwe hilo ni kura za nafasi ya uenyekiti zimemalizika kuhesabiwa na mawakala wa Lissu kwa namna moja au nyingine wamepenyeza matokeo ya awali. 

 Katika ukurasa wake wa Mtandao kijamii wa X, Mbowe ameandika ujumbe wa kukubali kushindwa akiweka na picha aliyopiga na Lissu na kuandika: 

 "Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya Uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama", ameandika Freeman Mbowe

Kuchaguliwa kwa Lissu kunakuja wakati muhimu kwa CHADEMA, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. 

Lissu anaonekana kama kiongozi mwenye mvuto na msimamo mkali dhidi ya utawala wa sasa, na chama kinatarajia kuimarika zaidi chini ya uongozi wake.

Kwa upande wa Mbowe, kumaliza kwa uongozi wake ni ishara ya demokrasia ndani ya CHADEMA, ambapo mabadiliko ya kisiasa yanapatikana kwa njia ya amani na heshima.

Share:

Tuesday, 21 January 2025

Wimbo Mpya : MJUKUU WA MWANAMALONDE - BHOLOGI

Share:

Video Mpya : ROBO LITA - CHANGAMOTO

 

Share:

🔴 Live : MKUTANO MKUU WA CHADEMA

 

Share:

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO 2 ZA KIMATAIFA ZA MWAJIRI BORA - 'TOP EMPLOYER'

 

Dar es Salaam, Januari 20, 2025 - Benki ya CRDB imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kutunukiwa tuzo 2 za Mwajiri Bora (Top Employer) na taasisi ya kimataifa ya Top Employers Institute. Ushindi huu unaiweka Benki ya CRDB katika nafasi ya Dar es Salaam, Januari 20, 2025 - Benki ya CRDB imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kutunukiwa tuzo 2 za Mwajiri Bora (Top Employer) na taasisi ya kimataifa ya Top Employers Institute. Ushindi huu unaiweka Benki ya CRDB katika nafasi ya kipekee kama moja ya waajiri bora barani Afrika, ikitambua jitihada zake za kujenga mazingira bora ya kazi yanayochochea ubunifu, ustawi wa wafanyakazi, na maendeleo ya kitaaluma.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa, alisema tuzo hizo zinadhihirisha juhudi za dhati za kuboresha maisha ya wafanyakazi wake ndani na nje ya kazi.

“Tuzo hii ni ishara ya wazi kwamba Benki ya CRDB inajali na kuthamini wafanyakazi wake, ikiwapa mazingira bora yanayowezesha mafanikio yao binafsi na ya kitaaluma. Huu ni ushindi wa pamoja, si wa benki pekee bali pia ni wa familia nzima ikiwamo wateja na wadau wote wa Benki ya CRDB,” amesema.

Tuzo ya Top Employer inatolewa baada ya tathmini ya kina ya viwango vya usimamizi wa rasilimali watu, ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika maendeleo ya kitaaluma, usawa wa kijinsia, programu za afya na ustawi wa wafanyakazi, na utamaduni wa uwazi na mshikamano. Katika maeneo haya, Benki ya CRDB imeonyesha ubora wa kipekee, ikiwasaidia wafanyakazi wake kufanikisha ndoto zao za kitaaluma huku wakichangia ukuaji wa Benki hiyo kwa kasi.

Tuzo za Top Employer ni mwendelezo wa Benki ya CRDB kutambuliwa kimataifa ambapo katika mwaka 2024 pekee, Benki hiyo ilikusanya tuzo zaidi ya 50 za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Benki Bora Tanzania, huduma bora kwa wateja, ubora wa huduma za kidijitali, na ufanisi wa mikakati ya maendeleo endelevu. Tuzo ya Top Employer ni nyongeza ya heshima inayodhihirisha dhamira ya benki hiyo ya kuimarisha rasilimali watu kama msingi wa mafanikio yake.

Rutasingwa alibainisha kuwa Benki ya CRDB inajipanga kuimarisha nafasi yake kama kinara wa usimamizi wa vipaji barani Afrika. “Tunajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko yanayoangazia wafanyakazi kama rasilimali muhimu. Maendeleo endelevu ya benki yetu hayawezekani bila jitihada za kila mfanyakazi,” aliongeza.

Rutasingwa alitoa wito kwa wafanyakazi wa benki hiyo kuendelea kuonyesha moyo wa ushirikiano na ubunifu, akisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja. “Benki ya CRDB si tu sehemu ya kazi – ni familia inayowekeza katika ndoto na ustawi wa kila mmoja wetu. Ushindi huu unathibitisha dhamira yetu ya kuweka viwango vipya vya ubora,” alisema.

Kupitia tuzo hizo za Top Employer, Rutasingwa amewahakikishia wadau, wateja, na washirika wa Benki hiyo kuwa itaendelea kuwekeza katika ubora wa wafanyakazi wake, lakini pia katika huduma na bidhaa ili kukuza ustawi wa watu wake na jamii kwa ujumla.

Share:

Monday, 20 January 2025

RC MACHA KUZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA SHINYANGA JANUARI 25


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza na waandishi wa habari - Picha na Malunde

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga yatazinduliwa rasmi Januari 25 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha. Utoaji wa elimu ya sheria katika maadhimisho hayo utatumika utaratibu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa leo Januari 20, 2025 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Amesema siku ya Sheria huashiria mwanzo wa kuanza kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka mpya husika baada ya kumalizika kwa likizo ya Mahakama inayoanza kila tarehe 15 Desemba na kumalizika Januari 31 ya mwaka unaofuata, ili kuanza rasmi utendaji kazi wa utoaji haki.

Amesema uzinduzi rasmi wa Wiki ya Sheria katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga utafanyika Januari 25 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika viwanja vya Zimamoto, Manispaa ya Shinyanga, na itahitimishwa rasmi Februari 1 katika Viwanja vya Mahakama Kuu.

“Kwa kuzingatia kuwa maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanafanyika siku za kazi, ambapo wananchi wengi watakuwa katika shughuli za utafutaji wa kipato, utoaji wa elimu kwa mwaka huu umelenga kuwafuata wananchi karibu zaidi na maeneo yao wanayofanyia kazi, tofauti na ilivyokuwa hapo awali,” amesema Jaji Mfawidhi Mahimbali.

“Elimu hii ya kisheria tutaitoa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kwa kutumia magari maalumu yatakayokuwa yanahama kutoka eneo moja kwenda jingine. Pia, tutaongeza wigo wa utoaji elimu kwenye maeneo ya shule za msingi, sekondari na vyuo,” ameongeza Mahimbali.

Amesema ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia watu wengi zaidi, watatumia pia vyombo vya habari kupitia luninga, redio na mitandao ya kijamii.

Amesema katika maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria, pamoja na mambo mengine, elimu hiyo itachagizwa pia na Tamasha kubwa la bonanza la michezo kwa Watumishi wa Mahakama katika ukanda huo.

Pia, amesema katika Wiki ya Sheria, kauli mbiu itakayokuwa ikijadiliwa ni “Tanzania 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”

Amesema kauli mbiu hiyo inawasaidia kutumia mkakati na utekelezaji wa maboresho ya Mahakama, hasa wanapoiendea dira mpya ya matumaini ya mafanikio 2050, ya uchumi wa kiwango cha kati ngazi ya juu. Na kwamba wao Mahakama wamejipanga kufanikisha mpango huo na watakuwa watekelezaji wakuu wa Dira hiyo ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 hadi 2050.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza na waandishi wa habari - Picha na Malunde
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza na waandishi wa habari
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza na waandishi wa habari
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger