Tuesday, 17 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 17,2024

 

Magazeti ya leo
 
 
Share:

Monday, 16 December 2024

Video Mpya : OMKAYA ELIZA Ff. NG'WANA KANG'WA - NGOSHA KE


Hii hapa video mpya Omkaya Eliza Ft. Ng'wana Kang'wa inaitwa Ngosha Ke
Share:

WATHAMINI WAPATIWA MAFUNZO UANDAAJI VITALU VYA THAMANI YA ARDHI

Mratibu wa Mafunzo ya Wathamini na Warasimu Ramani ambaye ni Mthamini kutoka Ofisi ya Mthamni Mkuu wa Serikali Bw. Baraka Mollel akizungumza wakati wa utoaji mafunzo ya uandaaji vitalu vya thamani ya ardhi mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Disemba 2024.

*******************

Na Munir Shemweta, KILIMANJARO

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini (LTIP) imetoa mafunzo kwa Wathamini na Warasimu Ramani kwa ajili ya zoezi la Uandaaji Vitalu vya Thamani ya Ardhi (Valuation Block)

Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 16 Disemba 2024 na yanahusisha wataalamu wa fani ya Uthamini na Urasimu Ramani kutoka ofisi ya Kamishna wa Ardhi mkoa wa Kilimanjaro pamoja na halmashauri zote za mkoa huo.

Mratibu wa Mafunzo hayo ambaye ni Mthamini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Bw. Baraka Mollel amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha na kuwafundisha wathamini na warasimu ramani ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa kipindi hiki ambacho Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaboresha mifumo yake na kuwa ya kidigitali.

Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yanawafundisha wathamini na warasimu ramani namna ya kuandaa Vitalu vya Thamani ya Ardhi (Valution Block) ili kusaidia utekelezaji wa shughuli za uthamini kama vile Rehani, Uhamishaji Milki na Uthamani kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya serikali.

"Uandaaji Vitalu vya Thamani kwa Wathamini na Warasimu Ramani utajumuishwa kwenye mfumo wa e-ardhi utakaowezesha ukilaji tozo mbalimbali ikiwemo kodi ya ardhi na tozo nyingine zitokanazo na thamani" amesema Bw. Mollel.

Ametaja faida ya Vitalu vya Thamani ya Ardhi (Valutaion Block) kuwa, ni kuiwezesha wizara katika makusanyo ya kodi ya ardhi, miamala mbalimbali ya uthamini pamoja na tozo nyingine kama vile tozo ya mbele hivyo wanatoa mafunzo namna ya kuandaa vitalu na kuwaelekeza namna ya kuunganisha katika mfumo wa e-ardhi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kilimanjaro Bi. Rehema Jato ameishukuru Wizara Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuona umuhimu wa kuupa mkoa wake kipaumbele cha kupata mafunzo hayo aliyoyaeleza kuwa ni muhimu sana kwa wathamini na warasimu ramani katika mkoa huo.

‘’Tunajua kuwa mafunzo haya yataenda mikoa yote lakini angalau sisi Kilimanjaro tumekuwa watu wa mwanzo mwanzo hivyo tuyatumie mafunzo haya katika kuongeza ujuzi na hatimaye kufikia malengo’’ amesema Rehema

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza matumizi ya mifumo ya kidigitali (e-ardhi) ambapo hivi karibuni Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Ardhi aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanatumia mifumo ya teknolojia katika yale maeneo ambayo mfumo huo umeanza kutumika.

Mfumo wa e-Ardhi umeanza kutumika kwenye maeneo mbalimbali nchini kama vile Dodoma, Arusha, Tabora katika halmashauri ya Nzega, Pwani halmashauri ya Chalinze pamoja na manispaa ya Shinyanga na Kahama zilizopo mkoa wa Shinyanga.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kilimanjaro Bi. Rehema Jato akifungua mafunzo ya uandaaji vitalu vya thamani ya ardhi kwa wathamini na warasimu ramani mkoa wa Kilimanjaro tarehe 16 Disemba 2024.
Sehemu ya washiri wa mafunzo ya uandaaji vitalu vya thamani ya ardhi kwa wathamini na warasimu ramani yanyoendelea mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Disemba 2024.
Mkufunzi wa mafunzo ya uandaaji vitalu vya thamani ya ardhi kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Bi. Odeta Vianey Nyarubaji akitoa mafunzo kwa wathamini na warasimu ramani yanyoendelea mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Disemba 2024.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kilimanjaro Bi. Rehema Jato (wa nne kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wathamini na warasimu ramani wanaopata mafunzo ya uandaaji vitalu vya thamani ya ardhi mkoani Kilimanjaro tarehe 16 Disemba 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

FAINALI ZA CRDB BANK SUPA CUP 2024 ZAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI ARUSHA



Jumamosi tarehe 14 Desemba 2024, jijini Arusha, Benki ya CRDB ilihitimisha fainali za CRDB Bank Supa Cup 2024, mashindano yaliyojumuisha michezo ya soka na netiboli, kwa timu zilizoundwa na wafanyakazi wa benki hiyo, yakiwa ni mashindano yenye mbwembwe na ushindani wa hali ya juu. Timu mbalimbali kutoka kanda tofauti za Tanzania zilishiriki katika fainali hizo ambazo zilileta burudani, mshikamano, na ushindani mkubwa.

Fainali hizo zilihudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Frank Mmbando, pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki ya CRDB. Viongozi hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi wa CRDB Bank Congo, Jessica Nyachiro, Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Bruce Mwile, Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa.
Matokeo ya Soka

Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu, timu ya Ulipo Tupo FC kutoka Kanda ya Ziwa iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Boom Advance FC kutoka Kanda ya Kaskazini.

Fainali kubwa ya soka ilishuhudia timu ya iMbeju FC kutoka Kanda ya Pwani ikiibuka kidedea kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Al Barakah FC kutoka Kanda ya Magharibi. Ushindi huu umeifanya iMbeju FC kutwaa ubingwa wa CRDB Bank Supa Cup 2024.

Matokeo ya Netiboli

Kwa upande wa netiboli, nafasi ya tatu ilichukuliwa na Lipa Hapa Queens kutoka Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuwashinda Popote Inatiki Queens kutoka Kanda ya Kati kwa alama 50-45.

Fainali ya netiboli iliwaweka uso kwa uso iMbeju Queens kutoka Kanda ya Pwani na Ulipo Tupo Queens kutoka Kanda ya Ziwa. iMbeju Queens walifanikiwa kushinda kwa alama 45-39, na hivyo kutwaa ubingwa wa netiboli.

Zawadi na Tuzo

Mashindano haya yalihitimishwa kwa utoaji wa tuzo mbalimbali kwa washindi wa michezo yote, huku fedha taslimu, medali, na vikombe vikikabidhiwa kwa washindi kama ifuatavyo:
Soka

Mshindi wa Kwanza: iMbeju FC – TZS 13,000,000/=
Mshindi wa Pili: Al Barakah FC – TZS 9,000,000/=
Mshindi wa Tatu: Ulipo Tupo FC – TZS 6,000,000/=

Netiboli

Mshindi wa Kwanza: iMbeju Queens – TZS 9,000,000/=
Mshindi wa Pili: Ulipo Tupo Queens – TZS 6,000,000/=
Mshindi wa Tatu: Lipa Hapa Queens – TZS 4,000,000/=
Tuzo Binafsi za Soka


Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP): Godwin Edward Junye (iMbeju FC) – TZS 500,000/=
Mfungaji Bora: Abdallah Magoe (Ulipo Tupo FC) – TZS 500,000/=
Kipa Bora: Abbas Wadi Makame (iMbeju FC) – TZS 300,000/=
Mchezaji Bora wa Mechi ya Fainali: Stanislaus John Masaswe (iMbeju FC) – TZS 300,000/=

Tuzo Binafsi za Netiboli


Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP): Ikutungangisya Richard (Ulipo Tupo Queens) – TZS 500,000/=
Mfungaji Bora: Saada Ally Juma (Lipa Hapa Queens) – TZS 500,000/=
Mchezaji Bora wa Mechi ya Fainali: Tumaini Ndosi (iMbeju Queens) – TZS 300,000/=
Akizungumza katika fainali hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema kuwa benki hiyo imeweka mikakati na sera mbalimbali za kuongeza chachu kwa wafanyakazi wake, na michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuhakikisha wanajenga umoja, afya njema, na furaha miongoni mwao.

"Mashindano ya CRDB Bank Supa Cup ni zaidi ya michezo; ni jukwaa la mshikamano, mawasiliano, na afya bora kwa wafanyakazi wetu. Tunajivunia kuona mshindano haya yakiendelea kuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Benki yetu," alisema Nsekela.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa, alisisitiza umuhimu wa mashindano hayo katika kuongeza mshikamano miongoni mwa wafanyakazi. "Michezo huchangia kwa asilimia kubwa kuwaleta watu pamoja, na kupitia Supa Cup tumeweza kuona mshikamano wa kipekee kati ya wafanyakazi wetu kutoka kanda mbalimbali," alisema Rutasingwa.

Mashindano ya CRDB Bank Supa Cup 2024 yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa, huku timu ya iMbeju kutoka Kanda ya Pwani iking'ara kwa kushinda vikombe vyote vya soka na netiboli. Shangwe na matarajio yameanza kuandaliwa kwa mashindano ya mwaka 2025, huku wafanyakazi na mashabiki wakiisubiri kwa hamu kubwa msimu ujao wa burudani.

Share:

Sunday, 15 December 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 16, 2024

Share:

TANZANIA BADO TUPO VIZURI KULIKO NCHI YOYOTE DUNIANI- JAJI MSTAAFU MWAIMU


MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Tawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema haki za binadamu Tanzania bado tupo vizuri kuliko nchi yeyote duniani.

Hayo ameyabainisha leo Desemba,14 2024 jijini Dar es Salaam, Jaji Mwaimu wakati wa Wanafanya maadhimisho ya haki za binadamu duaniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Desemba, 10 na yenye Kauli mbiu ya; Haki zetu, maisha yetu, sasa na baadae.

Amesema hakuna nchi duniani inaweza kusema kwamba inazingatia haki za binadamu kwa asilimia 100 ili wanazidiana kwa viwango.

"Tanzania hatuko vibaya tupo vizuri pamoja na changamoto ambazo tunazo bado Tanzania tutafanya vizuri, kwa mfano maeneo ya habari kuna malalamiko ndio watu hawapati fursa ya habari pengine maafisa wanapokwenda katika ofisi unakuta hawapo hawapati taarifa stahiki lakini serikali imetoa maelekezo kila wizara au taasisi lazima iwe na wasemaji kwa sasa Serikali iliweka utaratibu huu," amesema Jaji Mwaimu.

Amesema huwa wanaadhimisha haki za binadamu duniani yanatokana na tamko la dunia kuhusu haki za binadamu lilotolewa mwaka 1948 lililenga katika kuratibisha haki mbalimbali za binadamu.

Amesema Lengo la maadhimisho haya ni Kutafakari kwa pamoja kauli mbiu ya mwaka huu kwa kushirikiana na wadau na wageni mbalimbali waliohudhuria.

Ameeleza kuwa wataendelea kuhamasisha haki za binadamu na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi watajadili kuwa kila binadamu anahaki za msingi na haki za binadamu hazi gawanyiki ila zinategemeana.

Ameongeza kuwa kuimarisha mifumo ya utoaji haki na kulinda haki za makundi maalum watoto, walemavu na wengineo na wote wanakumbusha kulinda haki zao.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Tawala Bora, Patiance Mtwina amesema kila mwaka huadhimisha siku ya haki za binadamu kwa kusikiliza hoja mbalimbali, kutatua changamoto na kupokea malalamiko ya wananchi ili kuweza kuwasaidia.

"Tumekuwa kwa siku tatu katika Wilaya ya Temeke kwaajili ya wananchi wa Temeke ambapo tulipokea shida za migogoro ya ardhi tunafanyia kazi wananchi wengi wana migogoro ya ardhi," amesema.

Ametaja baadhi malalamiko waliopokea ni pamoja na mirathi imekuwa tatizo kwa wananchi, faida za bima wanapopata ajali, mafao na wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuifikia Tume hiyo.

Kwa upande wake, Mwanasheri wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Richard Shumbusho, amesema ni muhimu haki za binadamu nchini zilindwe haki si ya mtu mmoja ni jamii nzima.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger