Thursday, 24 October 2024

WANAHARAKATI WAOMBA JUHUDI ZIFANYIKE KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE VIONGOZI


Imebainika wanawake asilimia 2.1 pekee ndio walijitokeza  Katika kuwania  nafasi za uongozi wa vijiji  jambo ambalo limewaamsha wanaharakati kuona  umuhimu wa kuwekeza juhudi za ziada ili kuondokana na hali hiyo kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo na  usawa wa kijinsia.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 23,2024 na Afisa Idara ya Mafunzo TGNP Anna Sangai   kwenye semina za jinsia zinazofanyika kila Jumatano TGNP-MTANDAO Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Amesema  licha ya kutimia miaka 29 tangu mkutano wa Beijing ulipofanyika takwimu  bado zinaonesha hali sio nzuri hata katika nafasi za uongozi wa vijiji kwani wanawake ni Asilimia 2.1 pekee.

Aidha Sangai  ametoa Rai kwa wanawake waliowania nafasi za uongozi ambao kwa bahati mbaya hawatapita, wanatakiwa kutoa changamoto na vikwazo walivyopitia wakiwa wanagombea nafasi hizo.

Kwa upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia Nelson Munisi ameshauri kuwa mwanamke anapaswa  kutazamwa kwa jicho la kipekee Kama ilivyo katika nafasi za ubunge wa viti maalumu kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia Katika uongozi.
Share:

Wednesday, 23 October 2024

MZEE AFARIKI DUNIA AKIHONDOMOLA TENDO NA BINTI MDOGO HOTELINI

Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha kutatanisha cha mzee wa miaka 55, aliyepatikana amefariki dunia katika klabu moja iliyoko katika Kituo cha Biashara cha Shibuli, Eneo Bunge la Lurambi nchini Kenya.

Mudongo, ambaye ni mfanyakazi wa kawaida katika kituo hicho, aligunduliwa akiwa hana uhai ndani ya chumba chake saa chache baada ya kujumuika na mwanamke mdogo.

“Bado tunaendelea na uchunguzi wetu, ni kweli tulimkuta mwanamume huyo akiwa amefariki dunia, na kando yake kulikuwa na kondomu mbili zilizotumika, kuna tetesi za wananchi na wale wanaofanya kazi kwenye mgahawa huo kuwa mwanaume huyo alikuwa na mwanamke na akaondoka chumbani pekee yake.

 Baadaye, mfanyakazi wa mgahawa aligundua kuwa mwanaume huyo alikuwa amekufa,” afisa wa uchunguzi alisema. 

Je Elijah Mudongo alipatikana akiwa amefariki vipi? 

Mmiliki wa klabu hiyo, Velma Achema, alieleza kuwa Mudongo aliagiza chakula lakini akawataka wafanyakazi kusubiri amri yake kabla ya kukipeleka chumbani.

Wasiwasi uliongezeka wakati hakuna mawasiliano kutoka kwake hadi saa moja usiku, ambapo kifo chake kiligunduliwa. 

“Alikuja na kumwita mwanamke ambaye hatumjui, akaagiza chakula lakini akawaambia wahudumu wasubiri maelekezo yake, walipofika saa 7 usiku hawajamsikia, walimchunguza na kukuta amefariki dunia, kulikuwa na vitu vinavyofanana na dawa. kipande cha karatasi na vidhibiti mimba vilivyotumika," Achema alisema.

Wakazi wameeleza kukerwa na mazingira yaliyopelekea kifo cha Mudongo huku baadhi wakiwataka vijana kuepuka kujihusisha na wanaume wazee na kutafuta mahusiano na wanaume wa rika zao.

 Mwanamke huyo ambaye alionekana akitoka katika hoteli hiyo bado hajazuiliwa, na viongozi wanaendelea na msako wao wa kumtafuta.
Share:

TANZANIA YANG'ARA KIMATAIFA TUZO ZA UTALII



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Tanzania imepata tuzo za kimatifa za World Travel kwa mwaka 2024 katika sekta ya Utalii kutokana na juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania.

Tuzo hizo nne zimeendelea kuing’arisha Tanzania Kimatifa katika sekta ya utalii na kuwa Kivutio cha Utalii Afrika (African Leading Tourism Attraction 2024) – Mlima Kilimanjaro na Hifadhi Bora ya Taifa Afrika (Africa’s Leading National Park 2024) – Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea tuzo hizo leo October 22 Dodoma huku akitumia nafasi hiyo Amesema Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi makubwa katika utangazaji utalii kupitia Programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania na kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya utalii nchini.

Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Dkt Pindi amesema juhudi zilizofanywa na Dkt. Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa, Mhe. Dkt. Samia kupitia programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania zimeendelea kuing’arisha Tanzania katika sekta ya utalii kwa kupata Tuzo nne za kimataifa

Dkt. Pindi amesema juhudi hizo za Dkt. Samia zimechangia Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kunyakuwa tuzo nne za World Travel Awards kwa mwaka 2024.

Pia tuzo ya Kituo Bora cha Utalii Afrika (African’s Leading Tourism Destination) -Tanzania na Bodi Bora ya Utalii Afrika (African Leading Tourism Board 2024) – Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Dkt. Pindi amesema pia mawakala wa biashara za utalii wa hapa nchini nao wameshinda tuzo katika vipengele mbalimbali kutokana na juhudi zao za kutoa huduma bora katika sekta ya utalii.

Mawakala hao ni Gran Meliá Arusha, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire, Altezza Travel, Satguru Travel Tanzania, Skylink Travel & Tours na Gosheni Safaris.

“Niwapongeze mawakala hawa kwa tuzo walizopata kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika sekta ya utalii.”
Share:

Tuesday, 22 October 2024

DC KARATU AIPONGEZA CARMATEC KWA KUSAMBAZA MASHINE KWA WAKULIMA KARATU

 



Na Ferdinand Shayo ,Arusha.


Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba amekipongeza Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia vijijini (CAMARTEC) kwa kusambaza teknolojia na mashine mbalimbali za kulima ,kuvuna na kuchakata mazao pamoja na kuyaongezea thamani ili yaweze kupata bei nzuri katika masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuwakomboa wakulima.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo kihandisi cha Teknolojia za Kilimo kilichoanzishwa na CAMARTEC katika kijiji cha Gongali Wilayani Karatu ambapo amejionea zana mbali mbali ikiwemo mashine za Kupukuchua mahindi,maharage,alizeti na matrekta ,Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa kituo hicho kitawasaidia wakulima kulima kwa kisasa na kuchakata mazao yao kwa kutumia zana za kisasa.

Kolimba ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuiwezesha Camartec kufungua kituo kijijini hapo na kuwafikia wakulima wengi na kuongeza kuwa uhitaji wa mashine hizo bado ni mkubwa kwa wilaya hiyo yenye wakulima wengi zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa CARMATEC Mhandisi Godfrey Mwinama amesema wataendelea kufanya utafiti na kutengeneza mashine ambazo zitakua mkombozi kwa wakulima kwa kuwokolea muda na gharama lunwa walizokuwa wakitumia kutokana na teknolojia duni.

"Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr
Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha kuwasogezea wakulima wa vijijini mashine mbali mbali " Anaeleza Godfrey Mwinama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CARMATEC.

Kwa upande wao wakulima wakiwemo Rogati Israel na Musa Hussein wamesema kuwa mashine walizozipata kutoka CAMARTEC Zimewasaidia kupukuchua mahindi na maharage kwa muda mfupi bila kuharibu ubora wa mazao hayo.






Share:

WIZARA YA NISHATI KUJA NA MPANGO WA KUNADI VITALU VYA UTAFUTAJI WA GESI NA MAFUTA NCHINI



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulia Mafuta na Gesi Dkt James Mataragio akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Pili cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi PURA.
Mkurugenzi wa PURA Mhandisi Charles Jimmy na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la PURA akizungumza wakati wa kikao hicho

Na Oscar Assenga, TANGA.

WIZARA ya Nishati imesema kwamba wana mpango wa kunadi vitalu vya utafutaji wa Mafuta na Gesi asili nchini pamoja na kuingia makubaliano ya uzalishaji na makampuni ya nje.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulia Mafuta na Gesi Dkt James Mataragio Octoba 21 mwaka huu wakati wa Kikao cha Pili cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi PURA.

Ambapo alisema hiyo itakuwa ni raundi ya tano na zimeshafanyika raundi nne tokea mwaka 2000 na raundi ya 5 itafanyika mwaka kesho itayokwenda sambamba na mkutano wa Kimataifa wa East African Petroli Conference and Exibition ambao utajumuisha nchi zote za Jumuiya ya Africa Mashariki

Alisema kwamba mkutano huo unatazamiwa kufanyika Machi 5 mwaka Dar es Salaam na wanatarajia mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt Samia Suluhu kwa ajili ya kuzindua vitalu na watavinadi vitalu 24 ambavyo wanapanga kuvinadi huku wakiwakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuangalia vitalu.

Aidha alisema kwamba wameingia mkataba na kampuni ya TGS ambao wameingia mkataba wa kufanya masoko ya vitalu na Serikali imejipanga vizuri na kikubwa kuwa na uwazi na utayari na wizara imejipanga kushirikiana na Pura ambao ndio msimamizi wapo nao pamoja katika zoezi la kunadi vitalu hivyo.

“Tunategemea katika jitihada zinazofanywa sasa tunaanza kuitangaza nchi kwenye sekta ya mafuta na hivi karibu mtaona makapuni mengi yanakuja Tanzania na tuna miradi mikubwa ya kuchakata gesi unaofanyika Lindi ni miradi tunayoitangaza”Alisema

Alisema kwamba hiyo yote inaonyesha mazingira bora yaliyopo nchini ya uwekezaji kwa sababu mwekezaji anaposikia nchi ina mradi wa Dola Bilioni 42 ambao unataka kufanyika Tanzania anakuwa na imani kwamba sheria zetu,vivutio vyetu vya kifedha, taasisi zetu zinauwezo hivyo wawekezaji wakija nchini na kuwekeza uwekezaji wao utakuwa salama.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukinadi vitalu vyetu na kujitahidi kuhakikisha kunadi vitalu pamoja na kuingia makubaliano ya uzalishaji na makampuni ya nje mara ya mwisho tulinadi vitalu 2013 na kukaa muda mrefu bila ya kufanya hivyo kutokana na sababu mbalimbali ikwemo ni takwa ya kisheria”Alisema

Alisema kwa sababu njia ya shearingi ya mwaka 2013 ilikuwa haisomani na sheria ya mafuta ya mwaka 2015 na sasa walichokifanya kama wizara wamebadilisha mkataba wa mauzo wa mfumo wa uzalishaji ambao itasadia kwenda kujadili mikataba mbalimbali ya uwekezaji kwenye upande wa mafuta na itatoa vivutio vyingi itakayowasaidia kampuni za kimataifa za mafuta kuja kuwekeza Tanzania,

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi wa PURA Mhandisi Charles Jimmy na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la PURA alisema kwamba watanadi vitalu na ambacho kinachofanyika kwa mujibu wa sheria na wao wanasimamia kwa sasa Tanzania ukichukua eneo lake la kilomita za mradi 947,000 kiasi cha eneo la mraba 534,000 zinaonyesha viashiria vya kuwa na mafuta au gesi asilia.

Aidha alisema kati ya hizo ni 534,000 wana 162,000 ambazo tayari zimeshafanyiwa kazi sawa na asilimia 30 na vitalu 21 vitatoka bahari kuu na vitatu vitatu vitatoka upande wa Ziwa Tanganyika na watavitangaza na watu watatoa mapendekezo ya kuvifanyia kazi.

Alisema kwamba watazingitia vigezo vilivyowekwa pamoja na nchi itapata nini kutokana na mapendekezo yao na baadae watachagua aliyebora wampe vitalu kimoja, viwili au vitatu ili aendelee kufanya utafiti na wao watasimamia hizo tafiti .
Share:

Monday, 21 October 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 22, 2024

Share:

MSAADA WA TAASISI YA NVeP NA BARRICK WAENDELEA KUNUFAISHA TAASISI ZA KIJAMII NCHINI


Kaimu Meneja Mkuu Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Damian Brice­ Houseman,(kulia) akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe mfano wa hundi ya dola 10,000 zilizotolewa na taasisi ya taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Kaimu Meneja Mkuu Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Damian Brice­ Houseman,(kulia) akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe mfano wa hundi ya dola 10,000 zilizotolewa na taasisi ya taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe (katikati) akibadilishana mawazo na Maofisa Waandamizi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Wawakilishi wa vikundi vya kijamii vilivyopata msaada kutoka taasisi ya Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), wakiwa katika picha ya pamoja na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (katikati) baada ya kukabidhiwa hundi (dummy cheque) katika mgodi wa Bulyanhulu karibuni.

***Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa shule ya sekondari ya Bulangwa iliyopo mkoani Geita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kukuza taaluma. Hivi karibuni vikundi vya kijamii vya Enterprise and Rural Development Community Initiative, Sudama, na Jamii yetu Development & Relief Agency kila moja pia kilipata msaada huo ambao ulikabidhiwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini.

Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP, imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii mbalimbali zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 25 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto na utunzaji wa Mazingira.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa shule ya sekondari ya Bulangwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Kaimu Meneja wa Mgodi huo, Damian Brice Houseman, aliipongeza shule hiyo kwa kufanikiwa kupata msaada huu wakati wa awamu hii na kusema kuwa taasisi ya NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii kwendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mkuu wa shule ya sekondari ya Bulangwa, ameshukuru Barrick kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kuboresha miradi ya kuinua taaluma shuleni hapo na kupandisha ufaulu wa wanafunzi ili waweze kukabili changamoto mbalimbali kwa kutumia elimu bora wanayoipata.

Share:

KILA MWANAMKE ALINIACHA KISA NILIKUWA SINA NGUVU ILA SASA

Ukweli ni kwamba huku duniani kuna mikosi ya kila namna, mikosi ni mfululizo wa visa vibaya ambavyo vinaweza kuwa vinajirudia kila wakati na bila kujua sababu ni nini hasa.

Mathalani kuna mtu kila bishara anayofungua haiwezi kufikisha mwaka mmoja, mwingine kila gari analilonunua lazima liibiwe, mwingine kila mtoto anayempeleka shule anafeli.

Au kuna familia unakuta mabinti wanazalia nyumbani tu bila kuolewa, ukichunguza unakuja kugundua hata mama yao naye alizalia nyumbani na hapo watoto wanapoishi ni kwa Babu na Bibi yao.

Hiyo ndio mikosi yenyewe, kipindi ambacho jamii zetu zinaheshimu mila na tamaduni kabla ya kuathiriwa na utamaduni za magharibi zilizoletwa na utandawazi, jambo kama hilo likitokea lazima wazee wakae na wafanye jambo.

Ila sasa hiyo imekuwa ni ngumu, watu wanapata mikosi kila siku, wanaumia, wanarudi nyuma kimaendeleo na kiuchumi, hakuna anaweza kujua kipi kifanyike kwa sasa.

Hata hivyo, kuna hawa Dr Bokko, ni kiboko kabisa ya mikosi katika maisha, hawa ndio walioniondoa katika mkosi wa ndoa zangu kuvunjika.

Miaka ya nyuma kila mwanamke ambaye nilikuwa namuoa, baada ya miaka miwili, basi angechukua vitu vyake na kuondoka bila kusema sababu yoyote ile na mara moja angeolewa na mwanaume mwingine. 

Wanawawake wanne ambao niliwaoa waliondoka na kwenda kuolewa na watu wengine, na kibaya zaidi walikuwa wanaondoka bila hata kunizalia mtoto.

Ndipo nilipopata tiba kutoka kwa Dr Bokko na sasa mambo ni shwari kabisa, nimeoa na huu ni mwaka wa sita nipo kwenye ndoa na tumejaliwa kupata watoto wawili na mmoja tayari ameanza shule ya msingi.

Ninatoa wito kwa wenye shida au magonjwa, kusumbuliwa na mapenzi, ndoa, biashara, kukosa ujauzito n.k, basi wasisite kuwatembelea Dr Bokko, sio lazima usafiri hadi ofisini kwao, unaweza kuongea nao kwa njia ya simu na utasaidiwa kwa haraka. Piga simu +255618536050.

Mwisho.


Share:

MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA MKOMBOZI KWA MKULIMA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiangalia miche iliyopo katika kitalu cha kuotesha miche ya Kakao, Karafuu na Chikichi kilichopo katika kijiji cha Kichangani, Kata ya Mhonda, Tarafa ya Tuliani wilayani Mvomero.

........

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imetoa rai kwa wananchi kuutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kutunza na kuuza mazao yao kwa bei halisi ili kupata manufaa na kujenga uchumi kwa ujumla

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi hao na kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Viongozi wa Wilaya au Mkoa husika mara wanapoona watu wachache wenye lengo nia ovu yala kuharibu na kudhoofisha Mfumo huo ili kuuimarisha na kuuwezesha kufanya kazi kikamilifu.ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Hayo yamesemwa Oktoba 20, 2024 na Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika ( Mb) wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani Morogoro

Aidha amefafanua kuwa nia ya Serikali na Kamati hiyo ni kuhakikisha kuwa Mkulima anapata bei halisi na faida kutokana na Mazao yao kama vile zao la Kakao ambalo lililoongezeka bei kutoka Tsh 4,200 mwaka 2021 hadi Tsh 29,595 mwaka 2024

Vilevile, Mwenyekiti huyo imeielekeza Bodi ya Stakabadhi za Ghala (WRRB) kueneza Mfumo huo katika mikoa yote Nchini pamoja na kuongeza aina idadi ya nyingi za mazao yatakayohifadhiwamazao yanatotumia mfumo huo katika maghala kama vile Karafuu na mengineyo ili kuendelea kuwanufaisha Wakulima.

"Nawapongeza WRRB kwa kufanya kazi vizuri na nawataka muendelee kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuwawezesha Wakulima kupata thamani ya Mazao yao. Bodi hii ndio tegemeo katika kumnyanyua Mkulima"

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akijibu hoja mbalimbali za Wananchi wa Mvomero amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuwakomboa Wakulima kwa kuhakikisha kuwa wanaongeza tija kwenye uzalishaji kwenye eneo dogo, kuongeza thamani na kuwatafutia masoko ya mazao hayo.

Aidha, alitoa wito kwa Wakulima hao kuendelee kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kitumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa manufaa yao huku akiwaasa wasidanganyike kwa Madali wanaonunua mazao kwa bei ya chini bali wawe wavumilivu kwa muda wa siku tatu hadi tano wakisubiri fedha zao baada ya kuuza mazao kupitia Mfumo huo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewashauri wakulima kuutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuwa Mkoa wake unalima mazao mengi kujipanga kuongeza uzalishaji wa mazao mengi ya kibiashara hususani zao la Karafuu ambapo umepanga kugawa kila kaya kuwa na miche 40 ya karafuu ikiwa ni mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo Mkoani humo

Naye Naye Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Bw. Asangye Bangu amesema Bodi hiyo imepokea maelekezo wajumbe na ameahidi kuwa Bodi hiyo itaendelea kuusimamia Mfumo huo ili kuhakikisha kuwa unawanufaisha wakulima wa mazao yanayopita katika mfumo.

Nao Wananchi wa Mvomero kata ya Turiani wakiongea na Kamati hiyo wamekiri kuwa Mfumo huo ni mzuri na wamefanikiwa kuuza Kakao kwa bei ya tsh 29,000 na 17,000 kwa kilo mwaka 2024 wakati kabla ya kutumia Mfumo huo waliuza Kakao hiyo kwa Tsh 2500 na wameiomba Serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaodhoofisha Mfumo huo ili uendelee kuwawezesha kunufaika na bei za ushindani zilizoko sokoni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiangalia miche iliyopo katika kitalu cha kuotesha miche ya Kakao, Karafuu na Chikichi kilichopo katika kijiji cha Kichangani, Kata ya Mhonda, Tarafa ya Tuliani wilayani Mvomero.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akisalimiana na akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo walipowasili Ofisini kwake kwa ajili ya ziara Mkoani humo kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akijibu hoja mbalimbali za Wananchi wa Mvomero wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani humo.

Share:

Sunday, 20 October 2024

MUME WANGU ALIKUWA HAWEZI KAZI KITANDANI HADI NILIPOMPATIA DAWA HII

Jina langu ni Mama Jeni kutokea Geita, niliolewa mwaka 2019, mimi na mume wangu tunapenda sana ila kuna jambo fulani kipindi cha katikati karibia livunje ndoa yetu.

Nalo ni kwamba mume wangu ilikuwa anasusa kula chakula cha usiku, yaani kila nikitaka kumpa haki yake ya ndoa alikuwa anasema amechoka, mara hajisikiii, basi ni limradi tu asishiriki tendo hilo.

Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana na mashaka mengi, nilisema huyo atakuwa na mpango wa kando huko nje ambao unampatia mapenzi ya kutosha, hivyo akija kwangu anakuwa hana hamu tena.

Usiku mmoja niliamua kumuuliza kuhusu hilo, alikataa kabisa kuwa mpango wa kando, lakini nikamwambia anipatie haki yangu hakuwa tayari kufanya hivyo.

Ndipo kakachoka hali hiyo na kuamua kuchukua vitu vyangu na kurudi kwa wazazi wangu maana sikuona sababu ya kuendelea kuishi na mwanaume ambaye hanitumiziii mahitaji yangu ya kindoa.

Nilikaa kwa wazazi wangu miezi mitatu, ndipo mume wangu alikuja nyumbani kwetu kunibembeleza nirudi nyumbani, nilimkatalia kabisa na kusema siwezi hadi pale ambapo atakuwa ananitimizia haki yangu.

Katika mazungumzo yetu, ndipo akaniambia amekumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ila alikuwa anaona aibu kuniambia.

Nikamwambia kama ni hilo tu mbona ni jambo dogo sana, tunaweza kutafuta dawa na kufanikiwa bila ya tabu yoyote ile, ndipo tukawapata Dr Bokko ambao naweza kusema ndio wamekuja kuikoa ndoa yetu.

Rafiki yangu mmoja ndiye alinipatia namba za Dr Bokko ambazo ni +255618536050 na kuniambia kuwa hata mume wake aliwahi kukumbana na changamoto hiyo lakini Dr Bokko wakaweza kuwasaidia na sasa wanafurahia ndoa yao.

Baada ya kuwasiliana nao, waliweza kumtumia mume wangu dawa namna ambavyo anapaswa kutumia, basi alifuata maelekezo yale na baada ya muda alianza kurejea katika hali yake ya kawaida na sasa anakula chakula cha usiku vizuri tu.

Ninatoa wito kwa wenye shida au magonjwa, kusumbuliwa na mapenzi, ndoa, biashara, kukosa ujauzito n.k, basi wasisite kuwatembelea Dr Bokko, sio lazima usafiri hadi ofisini kwao, unaweza kuongea nao kwa njia ya simu na utasaidiwa kwa haraka.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger