Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha kutatanisha cha mzee wa miaka 55, aliyepatikana amefariki dunia katika klabu moja iliyoko katika Kituo cha Biashara cha Shibuli, Eneo Bunge la Lurambi nchini Kenya.
Mudongo, ambaye ni mfanyakazi wa kawaida katika kituo hicho, aligunduliwa akiwa hana uhai ndani ya chumba chake saa chache baada ya kujumuika na mwanamke mdogo.
“Bado tunaendelea na uchunguzi wetu, ni kweli tulimkuta mwanamume huyo akiwa amefariki dunia, na kando yake kulikuwa na kondomu mbili zilizotumika, kuna tetesi za wananchi na wale wanaofanya kazi kwenye mgahawa huo kuwa mwanaume huyo alikuwa na mwanamke na akaondoka chumbani pekee yake.
Baadaye, mfanyakazi wa mgahawa aligundua kuwa mwanaume huyo alikuwa amekufa,” afisa wa uchunguzi alisema.
Je Elijah Mudongo alipatikana akiwa amefariki vipi?
Mmiliki wa klabu hiyo, Velma Achema, alieleza kuwa Mudongo aliagiza chakula lakini akawataka wafanyakazi kusubiri amri yake kabla ya kukipeleka chumbani.
Wasiwasi uliongezeka wakati hakuna mawasiliano kutoka kwake hadi saa moja usiku, ambapo kifo chake kiligunduliwa.
“Alikuja na kumwita mwanamke ambaye hatumjui, akaagiza chakula lakini akawaambia wahudumu wasubiri maelekezo yake, walipofika saa 7 usiku hawajamsikia, walimchunguza na kukuta amefariki dunia, kulikuwa na vitu vinavyofanana na dawa. kipande cha karatasi na vidhibiti mimba vilivyotumika," Achema alisema.
Wakazi wameeleza kukerwa na mazingira yaliyopelekea kifo cha Mudongo huku baadhi wakiwataka vijana kuepuka kujihusisha na wanaume wazee na kutafuta mahusiano na wanaume wa rika zao.
Mwanamke huyo ambaye alionekana akitoka katika hoteli hiyo bado hajazuiliwa, na viongozi wanaendelea na msako wao wa kumtafuta.
0 comments:
Post a Comment