Na Marco Maduhu,SHINYANGA
HALMASHAURI ya wilaya ya Shinyanga,imefanya bonanza la michezo, kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi.
Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Oktoba 17,2024 katika Stendi ya Mabasi Salawe,ambalo limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga.
Dk.Kasanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo la michezo, amewasihi wananchi wa wilaya ya Shinyanga, kwamba waendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi, ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.
"Siku za kujiandikisha kwenye daftari la wakazi zimebaki 3 ambalo lilianza Oktoba 11 na litatamatika tarehe 20, na waombeni wananchi mjitokeze kujiandikisha ili mtumie haki yenu ya kikatiba kupiga kura na kuchagua viongozi wazuri watakao waletea maendeleo," amesema Dk.Kalekwa.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu,naye amewasisitiza wananchi kwa wale ambao bado hawajajiandikisha, kwamba wajiandikishe kwani siku siyo rafiki,ili wasije wakashindwa kupiga kura.
Uchaguzi huo wa serikali za mitaa ambao utafanyika Novemba 27 mwaka huu, ni kuchagua wenyeviti wa vijiji,vitongoji,mitaa pamoja na wajumbe.
Katika Bonanza hilo imefanyika michezo mbalimbali ikiwamo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na magunia na ngoma za kitamaduni.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga akizungumza kwenye bonanza hilo.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu akizungumza kwenye bonanza hilo.
Wananchi wakiendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakazi kwenye bonanza hilo.
Michezo mbalimbali ikiendelea kwenye bonanza hilo.
0 comments:
Post a Comment