Sunday 8 September 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 8,2024

Share:

Saturday 7 September 2024

MAONESHO YA UWINDAJI WA KITALII ABU DHABI KUZAA MATUNDA:TAWA




Wawekezaji waonesha nia kuwekeza kwenye biashara ya uwindaji wa kitalii na hoteli nchini.
Na. Mwandishi wetu, Abu Dhabi.

Maonesho ya Kimataifa ya Uwindaji wa Kitalii yanayojulikana kwa Jina la "Abu Dhabi International Hunting and Equestrian Exhibition - ADIHEX 2024" yamezaa matunda kufuatia idadi kubwa ya wawekezaji waliohudhuria katika maonesho hayo yaliyoanza tarehe 31 Agosti hadi 08 Septemba, 2024 kuonesha nia ya kuwekeza nchini.

Miongoni mwa mafanikio ya maonesho hayo ni mazungumzo mahsusi yaliyofanywa baina ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA Mabula Misungwi Nyanda na wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza kwenye biashara ya uwindaji wa kitalii, ujenzi wa hoteli za kulala watalii ndani ya Hifadhi na uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA) mazungumzo yaliyoongozwa na Kaimu Balozi wa Tanzania katika nchi za umoja wa falme za kiarabu Bw. Hangi L. Mgaka.

Bw. Hangi Mgaka ameipongeza TAWA kwa ushiriki wake kwenye maonesho hayo ambayo kwasasa ni mara ya tatu tangu Taasisi hiyo ianze kushiriki mwaka 2022, maonesho yanayotajwa kukutanisha zaidi ya washiriki 170,000 Kila mwaka.

Aidha katika kufikia masoko makubwa katika nchi za Mashariki na Kati, Kaimu Balozi huyo amesisitiza kuwa TAWA iendelee kushiriki makongamano mbalimbali yanayofanyika katika falme za kiarabu ikiwa ni pamoja na nchi za Saudi Arabia na Bahrain.

Vilevile ametoa wito kwa Kampuni za uwindaji wa Kitalii kutoka Tanzania kushiriki maonesho hayo ili kupata wageni watakaokuja nchini kwa shughuli za uwindaji wa kitalii na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

TAWA inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji kwenye maeneo inayoyasimamia ikiwemo uwindaji wa kitalii na utalii wa picha na maeneo ya uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA).
Share:

RAIS WA KENYA ATANGAZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA VIFO VYA WANAFUNZI 17


Baadhi ya waombolezaji baada ya ajali ya moto


Nchi ya kenya imetangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kutokana na vifo vya wanafunzi 17 wa shule ya msingi ya Hillside Endarasha kufariki katika ajali ya moto iliyotokea katika shule hiyo.

Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombolezo ya kitaifa yatakayoambatana na bendera ya nchi hiyo pamoja na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitapepea nusu mlingoti katika Ikulu, vituo vyote vya kidiplomasia vya Kenya pamoja na ofisi zote za umma kuanzia Jumatatu, Septemba 9, 2024, hadi Jumatano, Septemba 11 .

Awali baada ya kuripotiwa kutokea kwa tukio hilo Rais Ruto alitoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto wao, huku akiwaombea majeruhi kupona kwa haraka.

Aidha Rais Ruto ameagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na watakaobainika kuhusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo, tayari timu ya uchunguzi imeshafika katika eneo hilo na inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo ili hatua zingine ziweze kufuatwa.

Wakati akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Dk Resila Onyango alisema tukio hilo pia limesababisha majeraha kwa watoto 14 ambao wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 7,2024

Share:

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA 21 YA WAHANDISI TANZANIA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya 21 ya Wahandisi Tanzania  kwa kutoa elimu kwa wahandisi kuhusu uwepo mashine bora na za kisasa katika maabara ya TBS ambazo wanaweza katika miradi yao kuhakiki bidhaa katika miradi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 6, 2024 katika Maonesho hayo ambayo yamefanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wahandisi TBS, Mhandisi Mohammed Kaila amesema TBS limefanya uwekazaji mkubwa katika swala la mashine za  kupima ubora wa bidhaa.

Amesema uwekezaji uliofanywa na  TBS kwenye suala la mashine, kuna Hydrostatic Test Pessure Machine ambazo zinaweza kupima mabomba kuanzia kipenyo cha milimita 12 mpaka ya milimita 800 na mashine hiyo ni miongoni kwa mashine 5 tu zinazopatikana Afrika.

Aidha amesema miongoni mwa mashine zilizopo TBS pia kuna mashine nyingine ya kupima Solar katika mazingira yoyote bila kuzingatia uwepo wa jua tu na ni mashine pekee inayoweza kufanya hivyo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kato.

Pamoja na hayo Mhandisi Kaila amewataka wahandisi pamoja na wakandarasi kutembelea banda la Shirika hilo katika maonesho hayo ili waweze kupata elimu ya viwango na kuweza kutoa huduma zenye viwango na bora katika miradi yao kwa jumla. 

Ameeleza namna walivyojipanga katika kutoa elimu mbalimbali huku akiwataka wahandisi wote watumie Viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Share:

MUONEKANO MPYA SERENGETI BEER

Serengeti Premium Lite

*************

Serengeti Breweries Limited imezindua muonekano mpya na maridadi kwa chapa zake pendwa, ikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Premium Lite, na Serengeti Premium Lemon.

 Mabadiliko haya yanalenga kusherehekea urithi wa kitanzania na ubora ambao Watanzania wameuzoea, huku ikiwavutia kizazi kipya cha wapenzi wa bia.
Serengeti Premium Lemon
Serengeti Premium Lager 

Share:

Friday 6 September 2024

DAWASA KUSHIRIKIANA NA JAMII KUBORESHA MIFUMO USAFI WA MAZINGIRA BUGURUNI

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imepanga kuanza mkakati jumuishi na wakazi wa Buguruni kisiwani, katika Wilaya ya Ilala katika utunzaji wa miundombinu ya Usafi wa Mazingira ili kumaliza changamoto ya utiririshaji majitaka katika makazi ya watu.

Akizungumzia alipotembelea na kukagua mfumo rahisi wa uondoshaji majitaka katika Makazi uliotekelezwa katika eneo hilo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire ameeleza kuwa jamii inaposhirikishwa katika usimamizi na uendeshaji wa miradi ya kijamii kama hii huleta mafanikio makubwa.

"Kila penye mafanikio huja na changamoto, changamoto ya mradi huu tumeitambua na wakati tunaendelea na mipango mikubwa ya uboreshaji tumeona tuanze kwa kushirikisha jamii husika kwanza kwa kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya mfumo lakini pili uendeshaji wa mradi ni lazima jamii hii ihusike katika uendeshaji na utunzaji wa mradi huu"ameeleza Mhandisi Bwire.

Mhandisi Bwire ameongeza kuwa kwa kuwatumia Wananchi wazawa wa eneo husika katika utunzaji na uendeshaji wa mradi ni dhahiri kutatoa chachu ya elimu kwa jamii m juu ya matumizi sahihi ya mfumo wa uondoshaji majitaka katika makazi.

Nae Diwani wa Kata ya Buguruni Mheshimiwa Bussolo Pazi amemshukuru Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA kwa kufika eneo la Buguruni kisiwani na kujionea changamoto inayowakabili akiamini kuwa changamoto ya uchafuzi wa Mazingira inakwenda kumalizika katika Kata hiyo.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amefanya ziara ya kukagua mfumo rahisi wa uondoshaji Majitaka eneo la Buguruni kisiwani kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Edward Mpogolo aliyotoa mapema wiki hii kumtaka afike na kuangalia namna bora ya DAWASA kuimarisha mifumo hiyo ili kutunza afya za Wakazi.



Share:

MONGELLA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA SHINYANGA

Naibu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili mkoani hapo kwa ziara ya chama ya siku saba leo, tarehe 6 Septemba 2024.
 Mongella ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Pamoja na kutia saini kitabu cha wageni, Ndugu Mongella pia amepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama 2020-2024 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa.


Share:

KAMPENI YA KISHERIA YA MAMA SAMIA YALETA HAMASA KWA WANANCHI KUJUA UMUHIMU WA SHERIA


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza na moja wa mteja mara baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Mteja ,uzinduzi huo umefanyika katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

WIZARA ya Katiba na Sheria imezindua Kituo cha Huduma kwa Mteja huku Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign), imetajwa kuleta hamasa kubwa kwa wananchi kuwasilisha malalamiko na hoja za kisheria zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema kuwa serikali imeanzisha kituo hicho baada ya kubaini wananchi wamekuwa wakiwasilisha malalamiko mengi kwa njia ya barua na wengine wakitumia gharama kubwa kusafiri kuyapeleka wizarani Dodoma.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo ambayo hadi sasa imefika mikoa ya Dodoma, Manyara, Singida, Simiyu, Shinyanga, Ruvuma na Njombe imechochea kuanzishwa kwa kituo hicho.

Amesema kituo hicho ni muendelezo wa kampeni hiyo ambayo hivi karibuni itaendelea kwenye mikoa iliyosalia ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Kituo hichi ni utekelezaji wa falsafa ya R nne za Rais Samia Suluhu Hassan ambazo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya, kupitia falsafa hizi wizara inawezesha utatuzi wa migogor, inatoa elimu na msaada wa kisheria,”amesema Prof.Kabudi

Amebainisha kuwa serikali iliamua kuanzisha kituo hicho ambapo mwananchi anaweza kuwasilisha hoja yake kupitia namba ya simu 0262160360.

“Hii imesaidia kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za usafiri kuja kuwasilisha malalamiko yao wizarani, kwasasa wananchi walio maeneo ya mbali sasa wana uwezo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya simu kwenye kituo hichi na kufanyiwa kazi bila kufika wizarani,”amesema

Ameeleza kuwa takwimu za mwezi Februari hadi Agosti 31, 2024, malalamiko 499 yamesajiliwa na kati ya hayo 410 sawa na asilimia 82 yamefanyiwa kazi kikamilifu na 89 yapo hatua mbalimbali ya kutafutiwa ufumbuzi.

Aidha amesema wananchi wanakabiliwa na kero nyingi na kuanzishwa kwa kituo hicho ni dhamira ya serikali kutumia njia rahisi za kiteknolojia kuwafikia wananchi ili kutatuliwa kero zao kwa wakati.

“Wizara inampango wa kuongeza muda wa kutoa huduma uwe saa 24 na siku saba kwa wiki, niwashukuru wadau wa maendeleo FCDO kwa kufanikisha uwepo wa kituo hichi kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali,”amesema

Hata hivyo ameviomba vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa jamii uwepo wa kituo hicho ili wananchi wawasilishe malalamiko yao yafanyiwe kazi.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara hiyo,Bi. Jane Lyimo, amesema uwapo wa kituo ni mikakati ya kukabiliana na rushwa kupitia program inatotekelezwa na wizara hiyo inayosimamiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu kupitia ufadhili wa serikali ya Uingereza.

Amesema kutokana na umuhimu wa kituo hicho ni muhimu taasisi za serikali kushirikiana na Wizara ili kutatua hoja za kisheria na kurahisisha mchakato wa kumhudumia mwananchi.


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Jane Lyimo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.


SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani),akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza na moja wa mteja mara baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Mteja ,uzinduzi huo umefanyika katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.



WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
Share:

Wednesday 4 September 2024

WAZEE NCHINI WALAANI VITENDO VYA UKATILI VINAVYOENDELEA


CHAMA Cha Wazee Wanaume Nchini kinasikitishwa na kulaani vitendo vya ukatili vinayoendelea kufanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu, katika maeneo mbalimbali.

Kiongozi mkuu wa chama hicho Tadei Mchena amesema vitendo vinayoendelea havipaswi kabisa kufanywa na binadamu wenye akili timamu na wengine wakiwa ni watu wa makamo na wazee.

Mchena ametoa kauli hiyo kufuatia tukio la Septemba 2 mwaka huu katika Kijiji cha Kifuni, kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo, Wenseslaus Olomi, miaka (50) alikuwa akimbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 6.

"Kama chama cha wazee tunaendelea kulaani sana na kunakemea vikali kwa matukio haya yanayoendelea nchini, ukatili huu haukubaliki, tunaiomba serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia na kupitia upya Sheria hii ya ubakaji na ulawiti kwa watoto,

"Ikiwezekana Sheria itamke bayana ikibainika mtu anyongwe kabisa ili iwe fundisho la Wazee na watu wote wenye tabia hii mbaya ambayo inakithiri kila kukicha, watu hawa wasioogopa hata hofu ya Mungu", amesema Mchena.

Imeelezwa kwamba Olomi baada ya kukutwa akifanya kitendo cha ubakaji, alichukua hatua ya kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger