Wednesday, 4 September 2024

WAKANDARASI MIRADI YA UJENZI YA HEET UDOM WAASWA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka Wakandarasi walioshinda Zabuni ya Ujenzi wa Majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kuzingatia ubora katika ujenzi wa Majengo hayo na kukamilisha kwa wakati.

Hayo amesema , katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya uj enzi wa Majengo ya Madarasa na Maabara iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

"Sisi kama Mkoa tunachukulia UDOM kama Chuo cha pekee na ni Chuo ambacho tunajivunia, niwasisitize Wakandarasi kuwa mmejenga hoja kwenye makaratasi, mkaaminiwa, tuonyesheni kwa vitendo kuwa mnafaa kuaminiwa" Alisisitiza Senyamule

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Rwekaza Sympo Mukandala, amesema kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza ubora wa miundombinu ambao utapelekea mageuzi makubwa katika utoaji wa taaluma bora nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, amesema kutokana na ujenzi wa majengo hayo, UDOM itaongeza idadi ya wanafunzi ambao ni mpango wa muda mrefu wa serikali wa kuhakikisha UDOM inakuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi zaidi ya 40,000 kwa mwaka.

Akizungumzia Mratibu, Mratibu wa mradi huo UDOM ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina, amesema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na utakamilika mwaka 2026, kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Dunia.

Aidha, alieleza lengo la mradi huo ni kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kuwianisha mitaala na soko la ajira katika programu za kipaumbele katika taasisi za Elimu ya Juu, na kuboresha usimamizi wa mfumo wa Elimu ya Juu kwa ujumla.

Alieleza pia kuwa Mradi huu unatekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa UDOM ikiwa ni pamoja na kuanzisha kampasi mpya mkoa Njombe, kuboresha matumizi ya TEHAMA, kuhuisha mitaala inayozingatia mahitaji ya soko pamoja na kuongezea ujuzi wahadhiri kwa ngazi mbalimbali za masomo.

Utiaji saini wa Mikataba hiyo ulifanyika kati ya Chuo Kikuu cha Dodoma na M/S DEMATOCLASA REALHOPE JV MPONELA CONSTRUCTION AND COMPANY LTD ambayo itajenga jengo la madarasa katika Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi na M/S CHINA ENERGY ENGINEERING GROUP JIANGSU NO.1 ELECTRIC POWER CONSTRUCTION CO. LTD itakayojenga jengo la Maabara ya kisasa katika Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati.

Hafla hiyo ilihudhuria na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya UDOM wakiwemo Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini, Wajumbe wa Baraza la Chuo, Menejimenti ya Chuo, Viongozi wa kijiji cha Ng’hong’hona na Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi na Wanafunzi UDOM.
Share:

DAWA YA MATAPELI WA VIWANJA NA MBINU YA KUSHINDA KESI!

Jina langu ni Amosi kutokea Meru nchini Kenya, mwaka 2019 nilinunua kiwanja kwa ajili ya kuanza ujenzi baada ya kukusanya fedha zangu kwa miaka mingi sana.

Hii ilikuwa ni ndoto yangu ya miaka mingi kwamba siku moja nami nije kuwa na kwangu kisha kuanzisha familia yenye furaha.

Basi nilikutana na madalali na kuniambia kuna kiwanja kikubwa kinauzwa mahali na kipo katika eneo zuri hivyo naweza kuchangamkia fursa hiyo mara moja.

Nilienda kuona kiwanja hicho na kujidhirisha kweli ni kizuri, basi nilianza mchakato wa malipo mara moja ili asije akatokea mtu mwingine akakinunua kiwanja hicho.

Hatimaye nilifanikiwa kulipia na kupatiwa hati kuwa mimi ndiye mmiliki wa eneo hilo. Hapo moyo wangu ulitulia na kujua kilichobakia sasa ni hatua tu ya ujenzi ambao ulitarajia kuanza siku sio nyingi.

Cha kushangaza ni kwamba nilikuja kupata taarifa kuwa yule aliyeniuzia kile kiwanja ni mtu tapeli ambaye ameshatapeli watu wengi katika maeneo mengi nchini Kenya.

Ni mtu ambaye ana mtandao mrefu sana kiasi kwamba ni vigumu sana kumpata na hatia hata ukimfikisha mahakamani.

Kuna ndugu yangu aliniambia kuwa nikaonane na Dr Bokko atanisaidia kushinda kesi hiyo ya madai ambayo nilikuja kuifungua siku za mbeleni.

Nashukuru Dr Bokko alinifanyia tiba ya kweli na kunihahakikishia haki yangu itapatikana tena ndani ya muda mfupi tu. Basi nilifungua kesi ya utapeli mahakamani na shauri letu likaanza kusikilizwa.

Watu wengi walijua nitashindwa kesi hiyo maana mtu huyo ni tapeli aliyebobea. Lakini kwa nguvu ya dawa za Dr Bokko nilishinda kesi hiyo na kurudishiwa fedha zangu pamoja na gharama za kesi hiyo. Mpigie kwa namba+255618536050.

Mwisho.


Share:

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS XI JINPING WA CHINA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mkutano  na Rais wa China, Xi Jinping pamoja na ujumbe wake mapema leo katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing. 

Rais Samia  amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021. 

Kwa Mwaka huu wa 2024 Rais Samia na Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha  uhusiano wetu mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60.

Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.

Share:

CHADEMA WAMESHINDWA NA FALSAFA YA USTAHAMILIVU WA KISIASA


Na Mwandishi Wetu

MIONGONI mwa mataifa ya Kiafrika yaliyojenga misingi imara ya ustahamilivu ni Tanzania. Katika nyanja zote za kisiasa, kijamii na kiuchumi kuna funzo kubwa limeachwa na waasisi wa taifa hili.

Ndiyo maana panapotokea mtu au kikundi cha watu kikikosa ustahamilivu kwenye maeneo fulani si ajabu kuulizana mtu huyo anatokea wapi, hata kufikia kutilia shaka utaifa wake.

Haya ni mambo tuliyoshuhudia wazee wetu wakiyaishi. Si kitu cha paukwa pakawa au hadithi za kufikirika, ni kitu halisi.

Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Tanzania, Julius Nyerere katika mambo aliyoyapigia kelele kwenye miaka ya awali ya uhuru wa Tanganyika ni umoja na mshikamano.

Hizi ni tunu ambazo Watanzania hatuwezi kujiweka mbali nazo kwa namna yoyote ile.

Hakuna sababu ya kutoa maelezo marefu juu ya umuhimu wa umoja, ushirikiano na kustahamiliana ambavyo Mwalimu Nyerere alivipigania sana.

Kwa mfano akiwa jijini Rio De Janeiro nchini Brazil mnamo Juni, 1991 Mwalimu Nyerere alipata kusema: “Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe.”

Vilevile akiwa jijini Accra, Ghana mnamo Machi 6, 1997 alipata kusema: “Umoja hautatufanya kuwa tajiri, lakini unaweza kuwezesha kuiepusha Afrika na watu wa Afrika kutoheshimiwa na kudhalilishwa.”

Tubaki hapo kwenye maneno ya Mwalimu Julius Nyerere wakati tukitafakari kile ambacho Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kukifanya kwa Tanzania kupitia falsafa maarufu ya 4R. Ambayo inagusia mambo mtambuka juu ya maendeleo ya taifa lolote la Tanzania.

Maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reforms), Ustahamilivu (Resiliance) na Kujenga upya (Rebuilding).

Machi 8, 2023 ni tarehe ambayo haiwezi kutoka kwenye vichwa vya watu hasa wanaofuatilia siasa za Afrika, si Tanzania pekee. Hii ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuonekana katika mkutano wa chama kikuu cha upinzani nchini – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ilikuwa ni mkoani Kilimanjaro katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA), kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Ambapo waliomba Rais Samia awe mgeni rasmi, bila hiyana aliridhia.

Kwa mshangao mkubwa wachambuzi na wafuatiliaji wa siasa za Tanzania na ukanda huu wa Afrika Mashariki waliona hicho hakikuwa kitendo cha kawaida, lakini Rais Samia aliridhia na hakutaka kuwakilishwa alikwenda mwenyewe na kuhutubia.

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia aliwapa tumaini wanachama wa Chadema juu ya ujio wa Katiba Mpya lakini alisema kweli kuwa hilo si jambo mara moja, linahitaji mchakato wa muda mrefu.

Mengi aliyozungumza yalionekana kuwafurahisha wanawake hao wa Chadema (BAWACHA), kiasi cha kuamua kumpa tuzo ya kutambua mchango wake kwa kuboresha demokrasia nchini.

Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu alizungumza kauli yake maarufu katika mkutano huo: “Nimesimama hapa bila kuwa na hofu ya kukamatwa na Polisi wala kurushiwa mabomu, Mama pokea Baraka nyingi za Mungu. Mwenendo wako mwema, umeboresha demokrasia na haki nchini, maisha yetu ya awali katika serikali ya mtangulizi wako yalijaa hofu, kuwasiliana ilikuwa shida, kutengamana, kutekwa, kunyanyaswa, kuteswa na vilio.”

Hata hivyo, siku za hivi karibuni baada ya tukio lililotokea Mbeya baada ya mvutano wa Jeshi la Polisi na wafuasi wa Chadema, viongozi na wanachama wa chama hicho wamekuwa wakitangaza sifa mbaya za Rais Samia, bila kutoa maelezo ya kutosha. Haijulikani ndani ya mwaka mmoja ubaya huo ameutoa wapi.

Siasa ni ustahamilivu, kustahamiliana ndio sifa ya mwanasiasa yeyote mahiri. Hakuna mwanasiasa anayeendesha shughuli zake bila misukosuko wala kuvutana.

Katika falsafa ya Rais Samia (4R), ipo R moja inazungumzia Ustahamilivu (Resiliance).

Kwa dhati aliamua kuiweka R hii kwa sababu alijua mwanadamu ni mbinafsi, siku zote anapenda kuvutia kwake. Ndiyo sababu ya vita na vurugu zote duniani.

Ubinafsi unamfanya mwanasiasa siku zote aone yeye yuko sahihi na si vinginevyo. Chochote unachofanya lazima uangalie mustakabali mpana wa taifa.

Makosa yanafanywa na wanasiasa kwa kuamini kuwa wanafanya shughuli za kisiasa ili kujinufaisha kiuchumi, kujijenga kitaasisi lakini pia kuangalia namna gani wataendelea kupata faida za kichama kwa muda wote.

Wakati, sababu kubwa ya kuanzishwa vyama vya siasa ni kujua mustakabali wa nchi na wananchi wake. Hiki ndicho kitu cha kwanza kwa mwanasiasa wa kweli.

Zipo taarifa za kweli kutoka vyanzo vyetu kuwa BAWACHA wanajipanga kufanya maandamano makubwa nchini kushinikiza serikali kufuata kile wanachotaka, bila kuangalia mustakabali wa nchi na wale wanaowangoza.

Katika maandamano hayo ambayo inaaminika yatafanyika hivi karibuni, wanapanga kutangaza hadharani kumpokonya tuzo Rais Samia ambayo walimkabidhi katika mkutano wao wa Machi 8, 2023 mkoani Kilimanjaro.

Lengo ni kuionyesha dunia kuwa Rais Samia hakustahiki tuzo hiyo. Hii ni dhahiri kwanza; Chadema kupitia Bawacha hawajui thamani ya heshimwa waliyopewa na Rais Dk. Samia kuhudhuria kikao kile.

Pengine zaidi hawajui pia kuwa ndani ya chama chake (CCM), Rais Samia alitumia ushawishi wake kuwaelewesha wanachama wa chama hicho kikongwe barani Afrika (CCM), kuwa alichkusudia kukifanya kuhudhuria mkutano wa Bawacha si kitu kibaya katika siasa.

Kwa sababu siasa si uadui. Siasa si kuchukiana wala kupeana majina mabaya. Kukubali mwaliko ni ishara ya ukomavu na ustahamilivu wa kiwango cha kipekee. Ambacho kinataka kupongezwa badala ya kubezwa.

Hata hivyo, wanachodhamiria kukifanya Bawacha ni kujivua nguo. Baada ya Rais Samia kuamua kuwavika nguo wao wanazivua na kujiweka wazi kuonyesha namna gani si waungwana.

Ishara ya ubinafsi inawagubika Chadema katika hili. Wanaonyesha kwa kiwango gani hawana ngozi ngumu na pengine siasa si uwanja wao.

Kwa sababu kitendo cha kutaka wapate wao kila siku ni kuonyesha dhahiri hawana muda wa kusikiliza ya wengine, wanataka kuiaminisha jamii kuwa wao ndio watoto wa pekee wa Tanzania na wanachotaka kukifanya lazima wasikilizwe.
Share:

Tuesday, 3 September 2024

MBUNGE MTATURU ALISHUKURU KANISA,ACHANGIA SH MIL 11


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akizungumza wakati alipokuwa mgeni maalum katika hafla ya uzinduzi iliyofanyikia Kanisa la KKKT lililopo Ikungi.

......

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki Uzinduzi wa Jimbo la Ikungi KKKT na kuchangia vifaa vya ofisini vyenye thamani ya Shilingi Milioni 11.

Vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta,printa,Photocopy na samani za ofisi ikiwa ni maombi yaliyokuwemo kwenye risala iliyosomwa na Mkuu wa Jimbo Jipya la Ikungi Mch.Sara Msengi.

Aidha,amewakumbusha kuwa Mwaka huu 2024 ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali Za Mitaa,vijiji na Vitongoji hivyo kupitia jukwaa lao wawahimizw wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaona wanawafaa katika kuleta maendeleo.

Mtaturu ametoa salamu hizo ,alipoalikwa kama mgeni maalum katika hafla ya uzinduzi iliyofanyikia Kanisa la KKKT lililopo Ikungi.

"Nifikishe salamu za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenu kwa kuendelea kushirikiana na serikali kutoa huduma za kijamii kwenye sekta za Elimu na Afya,niwaombe muendelee na kazi ya kuliombea Taifa na kuwalea waumini kiroho ili waendelee kulina tunu ya amani,

"Nikupongeze Askofu wa Dayosisi ya Kati Dkt Syprian Yohana Hillint kwa kuendelea kuliongoza kanisa vizuri toka umechaguliwa na kusimikwa,hongera sana,"amepongeza

Akizungumzia uchaguzi unaokuja amewaomba waumini muda ukifika kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Uchaguzi wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura ili wapate sifa ya kupiga kura.

Akizungumza kwenye Ibada maalum ya uzinduzi wa jimbo la KKKT Ikungi Askofu Hilint amesema hilo ni Azimio la Halmashauri Kuu ya Dayosisi.

Amewahimiza waumini kushiriki kulijenga Jimbo jipya.

"Tunaendelea kuwaombea na kuwapatia msaada ili wafikiwe mtarajio yao,"amesema.
Share:

BLUE STAR LUXURY NDIYO HABARI YA MJINI!! MABASI MAPYAA TARIME - DAR

Blue Star Luxury ndiyo habari ya Mjini!! Mabasi mapya kisasa!! Safiri Nasi wakati wote wa safari zako Tarime - Bunda-Lamadi- Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma- Dar es salaam!! Wasiliana nasi DAR ES SALAAM 0747940519 , TARIME 0749664159


Share:

A DAYTIME OASIS WITH GORDON’S HOSTED BY EL-CASA: SUNSETS, SIPS, AND GROOVES AT LIVINGSTONE’S


As the evening sun set, the rooftop was curtained with a golden glow, which complimented the venue. There were twinkling blue lights and sunny yellow décor of photobooths and cocktail bars everywhere you looked, giving off major summer vibes and making everyone feel like they were living in a high-energy music video.

And don’t get me started on those cocktails! They were practically shouting “LOOK AT ME!”. The popsicle garnished green, yellow and red cocktails were so eye-catching! Whether you were in the mood for something sweet, tangy, or refreshingly cool, there was a cocktail that had your name on it.

Then the real magic happened as the sun set and the beats kicked in. The background music went from chill house vibes to a full-on summer soundtrack, with amapiano grooves that made your feet move whether you wanted them to or not. The DJ was on fire, spinning tracks that had everyone hitting the dance floor, and of course with your hosts being El-Casa, all the trendy socialites were there to show-off and looked the part.

It was one of those evenings where the vibe was so infectious, even the shyest of wallflowers couldn’t resist getting their groove on.

In short, the Gordon’s sundowners at Livingstone’s rooftop was a celebration of summer’s best—colorful, vibrant, and full of life. It was the kind of party that makes you forget about the world and just enjoy the moment. Here’s hoping for more nights like this one—where sunsets, sips, and summer beats come together to create the perfect evening, because, seriously, who wouldn’t want to do it all again?

If you weren’t at Livingstone’s rooftop for the Daytime Oasis last weekend, then you definitely missed out but YES you are in luck, because The El-Casa Boys are doing it all over again this month. YES! Let’s Bring BACK the DAY PARTIES with Gordon’s!
Share:

Monday, 2 September 2024

Video Mpya : GUDE GUDE - NKEMA MALAYA

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger