Monday 5 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 6,2024

Share:

MBUNGE MTATURU AMWAGA VIFAA VYA UJENZI MANG'ONYI


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,amekabidhi mifuko 100 ya saruji na mtofali 1,000 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa maabara za sayansi katika Shule ya Msingi Mang'onyi Shanta ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka jana 2023.

Msaada huo ameukabidhi Agosti 4,2024,akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi,kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti 2024/2025 na kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji 2024.

Akikabidhi msaada huo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mohamed Khalid,Mtaturu amesema kukamilika kwa maabara hizi kutaondoa changamoto waliyokuwa wanaipata walimu kuwafundisha wanafunzi masomo ya sayansi kinadharia tu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya shule,Mkuu huyo wa shule Mwalimu Khalid amemshukuru mbunge kwa kuendelea kuwashika mkono muda wote.

"Tunaomba utufikishie shukrani zetu kwa Rais Dkt Samia Suluhu hasaan kwa kutuletea Milioni 37 za kujenga darasa moja na matundu 6 ya vyoo,tunamshukuru sana,ahsante sana pia ndugu yetu Mtaturu kwa kutimiza ahadi yako,".amesema.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe wake.

Share:

PROFESA ASSAD ATAKA USHIRIKIANO UJENZI WA HOSPITALI YA KIISLAMU TANGA

 

 










Na Oscar Assenga, TANGA

MDHIBITI  na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa zamani Profesa Mussa Assad amesema ni umuhimu kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Kiislamu Mkoani Tanga unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Profesa Assad aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Jijini Tanga wakati aliposhiriki kwenye Kongamano la tathimini ujenzi wa Hospitali ya Kiislamu Mkoa wa Tanga lililokwenda sambamba na kufanyika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wake huku akieleza ni ushirikiano ni lazima wawe wamoja katika kufanikisha hilo.

Harambee hiyo ilikwenda sambamba na uliokwenda sambamba na kukagua eneo la Ujenzi wa Hospitali hiyo lililopo Kata ya Masiwani, Kupanda miti ya Matunda pamoja na kuweka jiwe la Msingi.

Alisema kwa sababu jambo ambalo linafanyika ni la kuokoa maisha na ukiokoa maisha ya mtu mmoja utakuwa umeokoa maisha ya watu wote kwani hata vitabu vitakatifu vya Mungu (Quran) vimeandikwa hilo.

“Hata vitabu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu vinaeleza kumtibu mtu mmoja na kuyaokoa maisha yake ni sawa utakuwa umeuokoa umma nzima lakini tatizo ambalo analiona ni ajizi kwamba wanafikiria hawawezi leo kufanya jambo hilo labda wasubiri kesho itawezakena na mwisho miaka inapita anzeni sasa”Alisema.

“Hilo ni tatizo kubwa la ajizi hivyo tuondoe ajizi tulifanye kazi hi kwa ushirikiano mkubwa ili kuweza kutimiza malengo tuliojiwekea ya kuhakikisha ujenzi wa eneo hilo unaendelea “Alisema

“Leo nimefurahi kwa sababu kuna kazi kubwa imefanywa na amesikitika hatua zake zimekwenda taratibu mno na nimekuwa nikipita sana kwenye eneo hilo kila mwezi kwenda Tongoni na wala sijasikia kuwepo wa shughuli hizi pia kinachomsikitisha zaidi ni kumetolewa nondo 72 katika ujenzi huu”Alisema

Aidha alisema maana yake hawajali vitu vyao wenyewe hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wakifanya vitu hapo vilindwa ili kuepusha kuibiwa na wezi jambo ambalo litapelekea kuepukana na vitendo hivyo.

“Lakini niwasihi katika jambo hilo tuwe pamoja na kuongeza mshikamano ili kulifanikisha jambo hilo na mwakani mungu akipenda kutakuwa wamepandisha jengo pia tutaendelea kuona namna wadau mbalimbali wanaweza kuchangia kwenye ujenzi huu”Alisema

Kwa makadirio ya Fedha za ujenzi wa Hosptali hiyo unakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh.Bilioni 2.4 sio fedha ndogo hivyo ni lazima waone namna ya wao wenyewe wajipange wafanya juhudi kubwa za kuanza kazi hiyo na wao waanze wenyewe na wao watakaoona hivyo wanaweza kuona namna ya wadau wengine kuwaunga mkono.

“Lakini niwaambie kwamba Mwenyezi Mungu akijalia nikirudi Dar nitahamasisha wenzangu kuona namna nzuri ya kuliendelea jengo hlo lianze haraka sana kutokana na umuhimu mkubwa lilikokuwa nalo”Alisema

Alisema kwamba Mwenyezi Mungu amewajalia neema nyingi waislamu hivyo ni vema wajiulize wameifanyia nini hiyo neema ya umri wamekaa miaka miwili jengo hilo hivyo maana yake wamefanya ajizi na hawakufanya hima ya kutekeleza kazi hiyo.

“Jambo la muhimu ni kujikumbusha kwamba tumepewa neema ya umri siku zinavyokwenda tujipime namna gani tumefanya kazi hizo inshallah Mwenyezi Mungu ajalie tukae pamoja juhudi hizi ziendelezwe ili mwakani tusiwe na msingi tuwe tumepanda kama sio ghorofa moja itakuwa ghorofa mbili na hilo tutaliweza kama tutakuwa wamoja”Alisema

Awali akizungumza kuhusu mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali inayozingatia maadili ya Kiislamu Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Baraza la Waislamu Taifa (Bakwata) Sheikh Khamis Mataka alisema kwamba MwenyeziMungu atalipa nguvu jambo hilo ili litimie na uwezo huo wanao.

Alisema kwamba uwezo wa kulitimiza jambo hilo upo ndani yao wao wenyewe wakiondokana na matatizo na changamoto walizojiwekea wao wenyewe wataona namna suala hilo litakavyopata mafanikio.

Naye kwa upande wake Dkt Ally Fungo alisema kwamba mradi huo wa kimkakati umedhamiria kutatua tatizo la kimkakati kama halitatatuliwa litaadhidhiri dhamira ya jamii ya kiislamu kwa kwa maana hapo watakuwa na kituo cha afya cha kutoka tiba kinachzingtia maadili ya kiislamu ambayo ni ya kibinadamu.

Alisema kwamba hospitali hiyo haitakuwa ya waislamu pekee bali wote lakini haiwezekani wakina mama wakatibiwa na daktari mwanaume hiyo ni hospitali ya kimkakati kutatua kimkakati hospitali ya waislamu wenyewe kwa fedha zao wenyewe.

“Hospitali hii itakuwa na majengo sana kuanzia Jengo la Utawala ,Jengo la Madaktari,Wodi za Wakina Mama,Kina Baba ,Maabara,Mochwari ,na nyenginezo na gharama zake kwa awali tungetumia Bilioni 1.5 lakini kipindi kimepita miaka mitatu iliyopita”Alisema

Hata hivyo alisema kutokana na uchumi duniani kuadhirika hivyo sasa wamefanya ufuatiliaji vitu vimebadilika na bei ya vitu imeongezeka na hivyo watalazimika watumie bilioni 2.4 hilo sio jambo dogo ni kubwa hivyo watashirikiana na wadau wote kufanikisha hilo.

Share:

Sunday 4 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 5,2024


magazeti ya leo

















Share:

WMA YAELEZA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA YA KILIMO

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Vipimo (WMA) Albogast Kajungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala hiyo, wanaoshiriki katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima NaneNane (2024) yanayoendelea jijini Dodoma.WMA inatoa elimu kwa wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla kuhusu matumizi ya vipimo sahihi.

Veronica Simba na Paulus Oluochi – WMA


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Albogast Kajungu, amesema WMA ina mchango mkubwa katika sekta ya kilimo hususani katika mazao ya kimkakati ambayo ni korosho, ufuta, kahawa, tumbaku na pamba.

Amebainisha hayo Agosti 3, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo maarufu kama NaneNane yanayoendelea katika viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa kazi kubwa ya Wakala wa Vipimo katika sekta hiyo ndogo ya mazao ya kimkakati ni kuhakikisha Mizani zinazotumika katika ununuzi wa mazao hayo zinahakikiwa ili kujiridhisha kuwa ziko sahihi.

“Lengo ni kuhakikisha kwamba mkulima anapouza mazao yake anapata thamani ya pesa sawasawa na mazao aliyouza,” amefafanua Kajungu.

Akieleza zaidi, Mkurugenzi huyo wa Huduma za Ufundi amesema zoezi la kuhakiki Mizani hufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza huhusisha uhakiki wa mizani kabla ya msimu wa kila zao kuanza ilhali awamu ya pili huhusisha ukaguzi wa kushtukiza wakati wa msimu kwa kila zao ili kujiridhisha kama vipimo vilivyohakikiwa awali vinatumika kwa usahihi.

“Kwahivyo kabla ya msimu tunapita kuhakiki mizani zote zinazotumika kununulia mazao na wakati wa msimu tunapita kujiridhisha kama zinatumika kwa usahihi.”

Aidha, Kajungu ameeleza kuwa, mbali na zoezi la ukaguzi, Wakala wa Vipimo pia hutoa elimu kwa wakulima na wananchi kwa ujumla ili wafahamu sifa za mizani ya kununulia mazao iliyohakikiwa.

Ametaja mojawapo ya sifa za mizani iliyohakikiwa kuwa ni uwepo wa stika ya Wakala wa Vipimo inayoonesha tarehe ambayo mizani husika ilihakikiwa pamoja na tarehe ya mwisho ambayo stika hiyo itakuwa imekoma matumizi yake.

“Kwahiyo mwananchi akiiona ile stika inampa uhakika kuwa mizani hiyo imehakikiwa na Wakala wa Vipimo,” amesisitiza Kajungu.

Vilevile, akizungumzia kuhusu ufungashaji wa mazao ya shamba, ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria, kufungasha mazao ya shamba kwa uzito unaozidi kilo 100 unatafsiriwa kama lumbesa ambayo ni kosa kisheria.

Amesema, kumekuwa na mkanganyiko wa tafsiri ya neno lumbesa ambapo baadhi huitafsiri kama kufungasha mazao ya shamba kwa kuongeza kishungi, ambapo tafsiri hiyo siyo sahihi.

Kajungu ametoa wito kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kufahamu kwamba mazao yote ya shamba ni lazima yafungashwe kwa uzito unaokubalika kisheria ambao ni kilo 100.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria ya vipimo, Kajungu amesisitiza umuhimu wa kuwepo vituo vya kununulia mazao ambavyo ni rahisi kuweka mizani iliyohakikiwa na WMA ili itumike kwa wakulima kuhakiki mazao yao na kujiridhisha kwamba yamefungashwa katika uzito wa kilo 100 bila kuzidi ili kupata faida stahiki kwa pande zote mbili yaani muuzaji na mnunuzi.

Wataalamu wa Wakala wa Vipimo wanashiriki katika Maonesho ya NaneNane kitaifa jijini Dodoma na kikanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla.

Afisa Vipimo Mwandamizi kutoka Wakala wa Vipimo (WMA) akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhakiki dira za maji katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane (2024) yanayoendelea jijini Dodoma.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Veronica Simba akitoa elimu kuhusu matumizi ya vipimo sahihi katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo NaneNane (2024) yanaoendelea jijini Dodoma.

Share:

TBS YAKUTANA NA WAJASIRIAMALI NA KUWAHUDUMIA KWENYE MAONESHO NANENANE KANDA YA KUSINI


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewashauri wajasiriamali kuzingatia matakwa ya kisheria katika masuala ya afya,usalama na mazingira kwenye usindikizaji wa bidhaa mbalimbali kwa lengo la kuzalisha bidhaa bora na salama.

Akizungumza Agosti 03, 2024 katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi Meneja wa TBS, Kanda ya Kusini Mhandisi Said Mkwawa amesema TBS kama chombo. chenye dhamana ya kusimamia viwango vya kitaifa wameona ni vyema kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha zinazalishwa biidhaa bora ili kulinda afya ya mlaji.

Aidha Mhandisi Mkwawa ametoa rai kwa wajasiriamali kujitahidi kutengeeneza bidhaa ambazo zinakidhi matakwa ya viwango. vya. ubora ili kulinda afya ya watumiaji wa bidhaa. hizo na kuepuka kuzalisha bidhaa zilizo chini ya viwango kwani zinahatarisha afya,uchumi na usalama.

"Kamwe Shirika la Viwango haturuhusu iwe kutengeneza au kuingiza nchini bidhaa zote zenye viwango hafifu kwani zitaleta athari kiuchumi,kiafya na kiusalama kwa ujumla" amesema Mhandisi Mkwawa

Pamoja na hayo ameeleza kuwaTBS imekuwa na utaratibu wa kufanya kaguzi mara kwa mara kwenye maeneo ya uzalishaji ili kubaini makubaliano yao na mzalishaji kama bado yanazingatiwa. kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

TBS imekuwa ikuonesha nia yake ya dhati ya kuwainua wajasiriamali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora sambamba na kuwapatia alama ya ubora ambayo itawasaidia kukuza wigo wa soko lao nchini na kimataifa ambapo imekuwa ikiwahimiza kukagua bidhaa zao ili kujiridhisha kuhusu ubora wake ambapo itawapatia mwanya wa kupata ushauri jinsi ya kuboresha kunapokuwa na uhafifu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger