Wednesday, 19 June 2024
MAONESHO YA UJASIRIAMALI NA UVUMBUZI IAA 2024
Uongozi wa IAA kupitia idara ya usimamizi wa biashara umeandaa maonesho ya ujasiriamali (Grand Entrepreneurship & Innovation Exhibition) yanayofanyika chuoni hapa na kushirikisha wanafunzi kuonesha ujuzi, na vipaji walivyonavyo pamoja na maandiko yao ya biashara.
Akimwakilisha Mkuu wa Chuo katika Maonesho hayo Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Epaphra Manamba amesema uongozi wa Chuo umekuwa ukiandaa Maonesho haya katika kutekeleza sera ya elimu ya Taifa, jambo ambalo limepelekea kuwapa wanafunzi ujuzi na maarifa ya kupambana na soko la ajira wanapomaliza masomo yao.
Prof Manamba ameongeza kuwa kama Chuo wanahakikisha kuwa wanafunzi wanafikia malengo ambayo Chuo, wazazi na wanafaunzi wenyewe wamejiwekea, hivyo kupitia Maonesho haya wanathibitisha jambo hilo kutokana na vitu vinavyooneshwa na wanafunzi wao kwa vitendo.
“Kama mwanafunzi hakikisha ubunifu uwe ndio kitu cha kuzingatia ukiwa chuoni, na ili uwe na wazo zuri katika ujasiriamali ni lazima uangalie wapi kuna mapungufu kwenye soko ili uje na kitu kimpya” amesema Prof. Manamba
Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Usimamizi wa Biashara na Manunuzi IAA, Dkt. Grace Idinga amewataka wanafunzi kuhakikisha chochote walichokipata kupitia masomo yao na Maonesho hayo, wahakikishe wanakifanyia kazi kwani mtaani nafasi hii inapatikana kwa gharama
Naye Afisa Biashara wa Jiji la Arusha Bw. Dominick William amewaasa wanafunzi kuwa ni vyema wakaendelea kuwa wabunifu, kuwa na uvumilivu kupenda wanachokifanya na kuwa wenye kujifunza kila siku ili kuongeza thamani na kukomaa Zaidi katika sekta ya ujasiriamali.
Maonesho haya yanatarajiwa kufanyika kwa takribani siku nne kuanzia tarehe 18 mpaka 21 mwaka 2024.
Tuesday, 18 June 2024
MBUNGE UMMY AUNGANA NA TAASISI YA SHITTA KUTOA SADAKA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUCHINJA
MBUNGE wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Mkoani Tanga (SHITTA) kutoa sadaka kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kusherehekea sikukuu ya Eid Al_Adha kwa ajili ya kuchinja.
Akiwa Hospitalini hapo Mbunge Ummy alionyesha furaha yake kutambulishwa shirikisho hilo ambalo linaziunganisha Taasisi za dini ya kiislamu katika mkoa wa Tanga huku akiwatoa wito kwa taasisi nyengine kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa wahitaji ikiwemo wagonjwa.
"Kwa kweli nimefurahi sana kushirikiana na Taasisi hii,wakati mwingine mimi kama mbunge napata shida kuzungumza na taasisi moja moja ,lakini kama nataka kukutana na taasisi za kiislamu naweza kuitafuta SHITTA ambayo inaweza kuniletea taasisi zote",Alisema mbunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu.
MALUNDE 1 BLOG INAKUTAKIA KHERI YA EID AL ADHA!
Monday, 17 June 2024
BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI
CCM TANGA YATAJA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA UDIWANI, UBUNGE TANGA 2025
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kuwa vigezo ambavyo vitatumika kuwapata wagombea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na ule Mkuu wa Wabunge na Madiwani wa mwakani 2025 kwamba ni wale ambao wanashiriki kwenye vikao kuanzia ngazi ya mashina.
Vigezo hivyo vilitangazwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati aliposhiriki kwenye mkutano wa Shina namba 5 Mtaa wa Majengo Kata ya Pangani Mashariki ambapo pamoja na mambo mengine alihamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.
Katika mkutano huo wa Shina namba 5 Mwenyekiti huyo aligawa viti 100 ikiwa ni kuhakikisha wanakuwa na uchumi imara ambao utawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika shina hilo
Alisema kwamba wanahitaji wapate viongozi ngazi ya serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Ubunge na Madiwani ambao wanakiheshimu chama cha Mapinduzi.
Alisema kwamba tafsiri ya kukiheshimu chama hicho ni kuhudhuria mikutano ya mashina yako na waanapokuwa hawaudhurii maanake bado haujaonyesha kukithamini na kukipenda chama cha mapinduzi.
“Niwaambie kwamba sio hiari ni suala la lazima viongozi wa ngazi za mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa wilaya, Kata na Mitaa na Vitongoji kuhudhuria kwenye mikutano ya mashina na kwa sasa atakayechukua fomu na kujaza na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano wakati hajafanya hivyo tutafuatulia maana mikutasari ipo”Alisema
“Sio suala la Hiari ni lazima kuhakikisha viongozi wa ngazi za wilaya wahudhurie mikutano ya shine lake ,Mwenyekiti wa Kata, Mbunge,Diwani hilo ni jambo la msingi linahimizwa kwenye chama chetu lazima wahudhurie kufanya hivyo ndio kukitendea haki chama chetu ujumbe huo ni kwa viongozi wote wa mkoa wa Tanga kwa sababu ndi anadhama nao na wote”Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha alisema kwamba suala la viongozi hao kuhudhuria kwenye mikutano hiyo ya mashina yao sio suala la hiari ni suala la lazima na mtakumbuka wakati najaza fomu kwenye uchaguzi wa chama 2022 ile fomu inavipengelea vingi miongoni mwao ilitaka ueleza vikao ambavyo ulivyoshiriki vya CCM kwa nafasi yako.
“Kwa maana lazima ueleze mikutano ya shina umehudhuria mara ngani kwa maana vikao vya matawi na mikutano mashina umehudhuria mara ngapi hilo ni suala la lazima na mara nyingi tumekuwa tukifanya mazoea kuona jambo la kawaida kawaida”Alisema
“Niwahakikishie uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na Mkuu wa Mwakani 2025 wa uchaguzi wa kumchagua Rais, Ubunge na Madiwani kipaumbele cha kwanza cha watakaopewa kwenye kugombea ni wale wote ambao wanashiriki vikao na mikutano ya matawi na mashina ya CCM”Alisema
Aidha alisema kwamba atakayejaza fomu na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano na hajawahi kufanya hivyo watafuatilia maana mikutasari ipo kwa nafasi hiyo nyeti wanayotaka kumpa huyo mtu wanajua lazima akakiheshimu chama hivyo lazima wapate kumbukumbu zake kwa usahihi na kwa uhakika.
“Kwa hivyo wale wote wanaotarajia kugombea nafasi kwenye chama chao kwenye kura za maoni wajue kama kwenye mashina yao hawakuheshimu vikao vya mashina waliviona havina maana yoyote balozi balozi maana balozi kazi tuliomuachia ni kusuluhusha ndoa za watu”Alisema Mwenyekiti.
SERIS FOUNDATION YATOA MSAADA WA VIFAA KWA WATOTO WACHANGA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Awali akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali hiyo, Ofisa Muuguzi kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Sinkamba ameishukuru taasisi ya SERIS kwa vifaa hivyo, huku akiendelea kuomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia mahitaji muhimu.
‘’Kwa msaada huu tunashukuru SERIS Foundation utaenda kusaidia watoto wetu wadogo hapa Amana kwani wapo wazazi wanaokuja na mahitaji yao ni madogo hivyo vinaenda kuwagusa.
Pia vifaa tiba hivi, vinaenda kuwa msaada kwa wazazi wengine watakaokuwa wanaendelea kufika hapa kitibiwa.’’ Amesema Sinkamba.
Aidha, Sinkamba amesema kuwa usiku wa kuamkia leo Juni 16, jumla ya Watoto 22 wamezaliwa, ambapo kati ya hao watoto 11 wamezaliwa kawaida na watoto 11 wamezaliwa kwa upasuaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SERIS Foundation, CPA. Deborah Wami amewashukuru uongozi wa Amana kwa kuwapokea na kuahidi kuendeleza mashirikiano katika kuhakikisha wanawafikia watoto Wachanga, katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.
“Leo siku ya Mtoto wa Afrika wana SERIS Foundation tumetembelea watoto wachanga katika hospitali ya Amana ambapo ni mojawapo ya malengo yetu katika kufikia watoto wachanga wenye umri wa sifuri hadi miezi mitatu.
Kwa mujibu wa UNICEF inayoonesha kuwa kwa wastani watoto milioni 2.1 huzaliwa kila mwaka hapa nchini, kati ya watoto hao wanaozaliwa wakiwa wazima wapo na wengine huzaliwa wakiwa na shida mbalimbali ikiwemo upumuaji na shida zingine ambazo zinawasumbua sana watoto wachanga, hivyo SERIS tumejikita katika upande huu.’’ Amesema CPA.Deborah Wami.
Na kuongeza kuwa, wameona vyema kutupia jicho watoto hao ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali huku gharama zao za matibabu kuwa kubwa kulingana na ukubwa wa tatizo lakini pia watoto hawa kutokana na mfumo wa bima nchini, baadhi ya watoto hawa hupata bima kwa kuchelewa kidogo na wengine kutopata kabisa.
“SERIS Foundation inatoa wito kwa jamii na Taasisi zingine nchini kuangalia watoto wachanga na matatizo ya kiafya wanayokutana nayo ili kuweza kuokoa maisha ya watoto hawa.
Vifo vya watoto wachanga hutokea ndani ya wiki nne baada ya kuzaliwa na Vifo vingi hutokea ndani ya wiki ya kwanza baada ya mtoto kuzaliwa
Hivyo SERIS Foundation imejikita kwa watoto hawa kuangalia namna ya kuwawezesha kuokoa maisha yao.’’ Amemalizia CPA. Deborah Wami.
Katika tukio hilo, wameweza kuchangia 'Baby diapers for new babies' na Fetoscope daipa za watoto pamoja na vifaa tiba vya kumpima mama mapigo ya moyo ya mtoto kabla ya kujifungua.
Aidha, amesema SERIS Foundation wamejikita katika mambo mbalimbali ya kijamii na maendeleo kwa ujumla ikiwemo masuala maji, afya, elimu na mengine.
‘’SERIS pia tunafanya kazi na Wahandisi na Wakandarasi Vijana ambao wamemaliza katika vyuo mbalimbali na hawajui wafanye nini, sisi tunawaunganisha na kuona namna ya kuwaonesha fursa na kupata kuona wenzao nini wanafanya ili kuwasogezea soko la ajira.’’ Amesema CPA. Deborah Wami.
Amemalizia pia kwa kueleza kuwa:"SERIS Foundation Inafanya haya katika kuchangia kufikia Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 sambamba na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hii ni katika maendeleo endelevu ya nchi ikiwa katika kupunguza vifo vya watoto wachanga." Amemalizia CPA. Deborah Wami.