Tuesday, 11 June 2024

VIONGOZI WA BODI ZA VYAMA WATAKIWA KUTAMBUA WAJIBU WAO KATIKA VYAMA




Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe, akizungumza wakati akifungua mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ya Wajumbe wa Vyama vya Ushirika vya Mbogamboga yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Mrajis Msaidizi wa (Uhamasishaji), Ibrahim Kadudu,akizungumza wakati wa mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ya Wajumbe wa Vyama vya Ushirika vya Mbogamboga yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe,(hayupo pichani ) wakati akifungua mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ya Wajumbe wa Vyama vya Ushirika vya Mbogamboga yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ya Wajumbe wa Vyama vya Ushirika vya Mbogamboga yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.

.............

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro, Jacqueline Senzighe, amewataka Viongozi wa bodi za Vyama vya Ushirika wa Mbogamboga kutambua wajibu wao katika Vyama na kutowaachia watendaji kuendesha Vyama hivyo.

Ameeleza kuwa Chama ni cha wanachama na si cha watendaji hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanakisimamia chama chao katika shughuli zote za utendaji.

"Ili kiwe chama bora ni lazima Viongozi wazingatie maadili ya uongozi kwani kiongozi ndiyo muonesha njia na kiongozi ndiyo anaweza kujenga au kubomoa chama chake akiwa hatokuwa na maadili," amesema Jacqueline.

Ameeleza hayo Leo tarehe 10/06/2024 wakati akifungua mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ya Wajumbe wa Vyama vya Ushirika vya Mbogamboga yaliyofanyika Mkoani humo.

Aidha, Mrajis Msaidizi amewataka viongozi hao kuzingatia Sheria zote za uendeshaji wa vyama watakazofundishwa ambazo ndiyo miongozo ya uendeshaji wa Vyama.

“Tume haijawaacha wakiwa, hivyo msiwe na hofu ya mtaendeshaje Vyama vyenu niwatoe wasiwasi, TCDC imetoa miongozo ambayo itawaongoza na ni vyema ikafuatwa ili mjenge hivyo vyama viwe imara,” amesema.

Naye Mrajis Msaidizi wa (Uhamasishaji), Ibrahim Kadudu, ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwanjengea uwezo Viongozi wa Vyama hi yo ili kuelewa kiundani dhana za Ushirika na kujua Vyama vya Mbogamboga vinaendeshwaje.

Mafunzo hayo yamehusisha taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Kilimo, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCu), Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI).

Share:

Breaking News : RAIS SAMIA AMTUMBUA YAHAYA NAWANDA UKUU WA MKOA SIMIYU, KIHONGOSI ABEBA MIKOBA

 

 Dk. Yahaya Nawanda


Share:

Monday, 10 June 2024

BEI ZA VOCHA ZA SIMU ZAPANDISHWA MIKOA 9 TANZANIA


Mikoa tisa imewasilisha malalamiko ya kupandishwa kiholela kwa bei za vocha za simu za mkononi.

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC), Mary Msuya iliyotolewa leo imesema hivi karibuni bei za vocha za mkononi zimepandishwa kinyemela ambapo vocha ya sh 500 inauzwa kati ya sh 550 hadi 600, vivyo hivyo vocha ya sh 1,000 kuuzwa kati ya sh 1,100, hadi 1,200 kinyume cha bei elekezi.

Ametajwa mikoa inayolalamika kuwa ni Dar es Salaam, Rukwa, Iringa, Ruvuma, Manyara, Lindi, Mbeya, Mtwara na Songwe.

Mary amesema katika kushughulikia changamoto hiyo, Baraza limeshauriana na watoa huduma za mawasiliano ya simu kufuatilia mawakala wao na kupiga marufuku upandishaji holela wa bei za vocha.

"Baraza limeshauri watoa huduma za mawasiliano ya simu kutoa taarifa kwa watumiaji kwa kuwataka kutonunua vocha kwa bei tofauti na inayoonekana kwenye vocha husika na utaratibu wa kutoa malalamiko wanapokutana na kadhia hiyo," amesema.

Ameshauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kununua vocha kwa kupitia simu zao za mkononi wakati changamoto hiyo ikitafutiwa ufumbuzi na kuendelea kutoa taarifa za kupanda bei kiholela katika maeneo mbalimbali ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na hali hiyo kukomeshwa.

Mary amesema, baraza linaendelea kufuatilia hali hiyo na kushauri hatua za kuchukua ili kuhakikisha watumiaji wa huduma za mawasiliano wanapata haki ya kupata huduma kwa bei halali na yenye ubora.

Imeandaliwa na Vicky Kimaro
Share:

TPDC YAHAMASISHA ULINZI NA USALAMA WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTAA WA ULONGONI A, DAR ES SALAAM




Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara, Mtaa wa Ulongoni A

Juni 8, 2024

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni Tanzu ya GASCO limeendea kuelimisha Umma juu ya ulinzi na usalama wa miundombinu ya bomba la gesi kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara. Elimu ya mara kwa mara imekuwa na matokeo chanya kwani ulinzi wa miundombinu ya gesi asilia umeendelea kuimarika hali inayopeleka miundombinu hiyo kuwa salama nyakati zote.

Katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Ulongoni A, sambamba na mambo mengine elimu ya ulinzi na usalama wa miundombinu ya bomba la gesi asilia ilitolewa. Aidha, Katika kuhakikisha miundombinu inakuwa salama ajenda ya ulinzi na usalama imekuwa ya kudumu kwenye Mitaa na Vijiji vyote vinavyopitiwa na miundombinu hiyo kuanzia Mtwara hadi Dar es salaam.

Dikson Kibala ambaye ni afisa ulinzi na usalama wa miundombinu ya bomba la gesi asilia alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Mtaa wa Ulongoni A katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za kiusalama pamoja na kushirikiana kukomesha shughuli zote za kibinadamu ndani ya Mkuza wa gesi asilia kama kuchimba mchanga/kokoto, ujenzi n.k.

"Tunapongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Mtaa wa Ulongozi A kwa kuimarisha ulinzi pamoja na kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na TPDC/GASCO kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na usafi wa Mkuza", aliongeza Kibala
Afisa Ulinzi na Usalama wa miundimbinu ya gesi asilia Ndg Dickson Kibala akitoa elimu ya ulinzi na usalama.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Mtaa wa Ulongoni A- Ndg Abdulrahim Munisi alipongeza jitihada zinazofanywa na TPDC kwenye kutoa elimu pamoja na kuinua huduma mbalimbali za kijamii kwenye mitaa inayopitiwa na midombinu ya bomba la gesi ikiwemo mtaa wa Ulongoni A.

"TPDC/GASCO mmekua wadau wa mfano kwenye kushirikiana na jamii, tunashukuru kwa kutupatia fedha za kujenga ofisi nzuri ya Mtaa tena ya kisasa ambayo kwa sasa imekamilika na inatumika kuhudumia wananchi, mtaa wetu utaendelea kutoa ushirikiano katika kulinda miundombinu ya bomba la gesi asilia", aliongea Mwenyekiti Munisi.

Kwa upande wake, Mhe Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mhe. Lucas Lutainurwa alitoa shukrani kwa uongozi wa TPDC/GASCO kwa kuendelea kuinua huduma za kijamii ikiwemo sekta ya elimu kwenye kata ya Gongo la mboto. Aidha alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia juhudi za serikali kwenye kuboresha huduma mbalimbali za kijamii kama Maji, Elimu na Afya.
Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Mhe Lutainurwa akiongea wakati wa mkutano na wanachi wa Mtaa wa Ulongoni A-Dar es salaam

"Mwaka 2022/2023 tulipokea Tsh 69,000,000 kutoka TPDC/GASCO kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Mzambarauni, ni jambo kubwa na la kujivunia kwani ujenzi wa Bweni ulikamilika na tayari linatumika", aliongea Lutainurwa.

#TPDC TUNAWEZESHA.



Share:

Sunday, 9 June 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 10, 2024

Share:

CRDB YAKABIDHI MADAWATI KIBONDO, MWENDELEZO WA KAMPENI YA KETI JIFUNZE


Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg Jumanne Wambura Wagana amekabidhi madawati 40 kwa shule ya msingi Kasebuzi Mkoani Kigoma ambapo madawati hayo yamepokelewa na mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh. Aggrey John Magwaza ikiwa ni mwendelezo wa benki hiyo ya CRDB katika kutekeleza sera yake ya uwekezaji kwa jamii na  kampeni ya KETI JIFUNZE inayolenga kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.

 Akipokea Madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo  Mh. Aggrey John Magwaza ameishukuru Benki ya  CRDB kwa msaada huo mkubwa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano mkubwa zaidi kibiashara huku akiwasisitiza wazazi walimu na wanafunzi kuendelea kutumia Huduma za CRDB na kuwaasa wadau wengine kuiga mfano huo na kurudisha kwa jamii.

Share:

TANROADS, ZANROADS WAWEKA MPANGO KAZI WA MWAKA 2024/2025




Na Carlos Claudio, Dodoma.

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) wameweka mpangokazi wa kipindi cha mwaka mmoja, ambao utekelezaji wake utaanza kutumika rasmi mwaka wa fedha 2024/25.


Akizungumza na wakala wa barabara Zanzibar, wenyeviti wa bodi za ushauri, wawakilishi wa bodi ya ujenzi pamoja na kamati ya wataalam jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mha. Mohamed Besta amezungumza katika kikao hiko cha uwasilishaji wa mpango kazi wa utekelezaji wa Hati ya mashirikiano kati ya TANROADS na ZANROADS uliofanywa na Kamati ya Wataalam amesema mpango kazi huo utaanza kufanya kazi rasmi baada ya kusainiwa na uongozi wa juu wa pande zote mbili.

Mha. Besta amesema kuwa mpango kazi huo ni wa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024/25 hadi 2028/29 ambapo utakuwa unahuishwa kila mwaka, lakini kwa mwaka ujao wa fedha wataanza na vipengele vinne vya kuanzia kazi, ambavyo vimeainishwa kwenye rasimu hiyo, ambavyo ni kuandaa na kuendesha mafunzo, semina na warsha kwa ajili ya kujenga uelewa juu ya miongozo mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi katika shughuli za ujenzi wa barabara.

Amesema vipengele vingine ni pamoja na kuandaa na kuendesha vikao kazi vya kuandaa miongozo na taratibu za usimamizi na uendeshaji wa mizani, pia kuandaa mafunzo ya namna ya uendeshaji na utunzaji wa mizani kwa watumishi wa ZANROADS; na kutoa elimu kwa wadau wa usafirishaji kuhusu uanzishwaji na uendeshaji wa shughuli za mizani na umuhimu wake.

Mha. Besta amesema vipengele vingine ambavyo vitatekelezwa kwa kuanzia robo ya kwanza hadi ya nne ya mwaka wa fedha 2024/25 ni pamoja na kuandaa nyaraka za uanzishwaji wa kitengo cha Ushauri elekezi Zanzibar (ZANROADS Engineering Consulting Unit - ZECU) kuandaa na kuifanya ziara za mafunzo na kubadilishana uzoefu; Ufuatiliaji wa maendeleo ya uanzishwaji wa kitengo cha ZECU na kuratibu shughuli za kijamii ikiwemo mashindano na michezo mbalimbali kati ya taasisi hizo.

“Tunaamini utekelezaji wa mpango kazi huu kutasaidia kuimarisha uwezo wa utendaji wa taasisi zetu hizi, sisi tuna la kujifunza kwa wenzetu na wao wanalo la kujifunza kutoka kwetu,” amesema Mha. Besta.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa ZANROADS, Mha. Cosmas Masolwa amesema kutokana na mashirikiano hayo yataendelea kuleta na kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

Mha. Masolwa amesema,“ Ushirikiano huu naamini utadumu na pande zote mbili kila mmoja atanufaika kutokana na jambo jipya kutoka kwa mwenzake, ukiangalia wenzetu wapo mbele mfano sisi hatuna mzani wa magari huku kwetu Zanzibar na sasa mahoteli makubwa makubwa yanajengwa na magari mengi yanayoleta malighafi ya ujenzi yanakuja na mawe, mchanga hivyo ni rahisi kuharibu barabara zetu, hivyo tunaamini tutajifunza kutoka kwa wenzetu.”

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya ZANROADS, Msanifu Majengo Yasser de Costa amepongeza mashirikiano hayo yaliyochagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi na anaamini yatafanikiwa kunilingana na utekelezaji wa vipengele vilivyopo kila mwaka.


Sambamba na hayo TANROADS na ZANROADS wameandaa ziara ambapo Juni 10, 2024 watatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 9,2024













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger