Tuesday, 28 May 2024

JK KINARA UTAFUTAJI FEDHA ZA KUIMARISHA ELIMU AFRIKA


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (GPE) ameshiriki Mkutano wa Mwaka 2024 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB 2024 Annual Meeting) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 26 – 28 Mei, 2024.

Ametumia fursa ya kushiriki Mkutano huo kuzungumza na vongozi mbalimbali, hususan kutoka sekta za kifedha, sekta binafsi na washirika wa kimaendeleo kuhusu umuhimu wa kuongeza ufadhili wa kifedha ili kuimarisha mpango wa utoaji chakula kwa wanafunzi wakiwa mashuleni pamoja na kuhamasisha ubunifu wa mbinu mpya za kufadhili elimu ya juu, elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Taasisi ya GPE ambayo Rais Mstaafu Kikwete ni Mwenyekiti wa Bodi imejikita katika kujenga ubia na wadau mbalimbali wa kimataifa na ndiyo Taasisi kinara duniani inayohamasisha jitihada za kuzisaidia nchi zaidi ya 76 kuimarisha mifumo yao ya elimu ili kutoa elimu bora zaidi kwa watoto wa kike na wa kiume, hususan wale wanaotoka katika mazingira duni, wenye ulemavu na wanaoathiriwa na majanga kama vile vita na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wa Afrika, GPE ina miradi inayozunufaisha nchi 40, ikiwemo Tanzania. Tangu mwaka 2016 hadi sasa, Taasisi ya GPE imetoa msaada wa zaidi ya shilingi bilioni 250 za Kitanzania kufadhili programu hiyo ya utoaji wa chakula mashuleni katika nchi inapofanya shuhuli zake.

Katika Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Rais Mstaafu Kikwete alieleza umuhimu wa washiriki kufikiria mbinu mpya za kupata fedha zitakazotumika kugharamia programu za kutoa chakula mashuleni kwani ukweli ni kwamba licha ya jitihada kubwa inayofanyika na nchi nyingi za kipato cha chini na kati katika kuimarisha programu hiyo, bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kuelemewa na madeni.

Akaeleza kuwa programu ambayo ni moja ya mikakati muhimu ya kielimu inayoongeza mahudhurio ya watoto mashuleni na kukuza uelewa wa wanafunzi inasaidia pia katika kukabiliana na tatizo la udumavu na unyafuzi linalolikabili bara la Afrika.

Aidha, aliwakumbusha washiriki kuwa msingi wa bara la Afrika na Dunia kufikia malengo waliyojiwekea kama vile lengo la Umoja wa Afrika la Ajenda 2063 (Afrika Tunayoitaka) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ni kuwekeza katika elimu ili kuwaandaa watoto na kuwajengea uwezo wa kupambana, kuishi na kustawi katika mazingira mapya ya karne ya 21.

Mkutano huo unaofanyika kila mwaka ulihudhuriwa na Mawaziri wa Fedha na wa Elimu kutoka nchi mbalimbali duniani, viongozi kutoka Umoja wa Afrika na Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika, wawakilishi wa mashirika ya kimaendeleo kama vile Rockefeller Foundation, Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) pamoja na viongozi wa sekta binafsi kutoka barani Afrika.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 28, 2024

Share:

Monday, 27 May 2024

OFISI YA WAZIRI MKUU YASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU TANGA

 

Na Mwandishi Wetu. 

Ofisi ya waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeshiriki Maadhimisho ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yaliyoanza tarehe 25 hadi  31Mei, 2024 mkoani Tanga yenye Kauli isemayo; "Elimu, Ujuzi, Ubunifu na Teknolojia kichocheo cha Maendeleo kwa Uchumi Shindani.

Maafisa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi hiyo wanaendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa nchini hususan kwa wanafunzi na watu mbalimbali  wanaofika na kutembelea Banda la ofisi hiyo katika Maadhimisho hayo.

Aidha pamoja na hao wapo maafisa kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) iliyo chini ya  Ofisi ya Waziri Mkuu kwa pamoja wameendelea na uelimishaji umma kuhusu matumizi sahihi ya mbegu na faida za zao la mwani, katika Maadhimisho hayo Tanga.



Share:

POLISI SHINYANGA WAKAMATA PIKIPIKI 16, DAWA ZILIZOISHA MUDA, ALIYEMTAJA MTU MCHAWI ATUPWA JELA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata pikipiki 16 za wizi na zisizo na kadi, viroba 25 vya madawa ya kulevya aina ya Mirungi, Tv 01, Mzani 01, Redio 01, pombe ya moshi lita 20 pamoja na pakti 86 za dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 27,2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema vitu hivyo vimekamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja kuanzia Aprili 17, 2024 mpaka Mei 27, 2024 kufuatia Ushirikiana wa Jeshi la Polisi na Jamii katika kubaini na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako pamoja na Operesheni mbalimbali.

Katika kipindi hicho pia Jumla ya kes 15 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya kuvunja nyumba usiku na kuiba mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01 na kesi moja ya kumtaja mtu mchawi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.

"Kesi 01 ya kupatikana na bhangi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 03, kesi 01 ya kuvunja duka usiku na kuiba mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje miezi 12, kesi 01 ya kupatikana na madawa ya kulevya mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 02, kesi 01 ya kutorosha mtoto mshtakiwa ameamriwa kulipa faini tsh 50,000/=, kesi 01 ya kupatikana na mirungi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 02 jela.

Kesi 05 za wizi washtakiwa wamehukumiwa kifungo kati ya miezi 03 hadi miaka 03 jela, kesi 01 ya kujeruhi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha mwaka 01, kesi 01 ya shambulio la kudhuru mwili mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01, kesi 01 ya kutishia kuua kwa silaha panga mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01",amesema Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kikosi cha Usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 6320 ya Usalama Barabarani ambapo makosa ya magari ni 4847 na makosa ya bajaji na pikipiki ni1473 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.
Muonekano sehemu ya dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha pikipiki zilizokamatwa


Share:

ZINAHITAJIKA JUHUDI NA NGUVU YA PAMOJA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO YA UHAMIAJI HARAMU - CHIEF CHARUMBIRA

Mhe. Chifu Fortune Charumbira


Na Moshi Ndugulile

Rais wa Bunge la Afrika Chief Fortune Charumbira amesema Bunge hilo lina wajibu mkubwa wa kukuza na kuimarisha misingi ya haki za binaadamu, demokrasia na utawala bora , uwazi pamoja na uwajibikaji katika Nchi wanachama barani Afrika,hasa katika hatua za kushughulikia uhamiaji.

Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uhamiaji wa Euro-Afrika Mjini Benghazi Nchini Libya ambapo ametaka kuweka umadhubuti kuhakikisha kunakuwa na uhamiaji wenye manufaa kwa pande zote kupitia sera na mipango baina ya maeneo husika.

Chief Charumbira ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine Mkutano huo umelenga kujadili na kuangalia namna bora ya kutatua changamoto ya uhamiaji kuvuka na kuingia Italia na Malta kupitia Libya, ili kuondokana na athari za uhamiaji haramu,hivyo kukuza zaidi Amani,usalama, utulivu, ushirikiano na maendeleo barani Afrika.

Ameeleza zaidi kuwa hatua hiyo imelenga kukabiliana uhamiaji haramu ambao umekuwa ukisababisha athari kwa raia ambao wanafanya biashara halali.

“Kwa kuzingatia ukweli kwamba, hivi karibuni, Libya ilikuwa sehemu kuu ya kuondoka wahamiaji kuelekea bara la Ulaya,na kwamba tangu wakati huo Tunisia imeipiku Libya kwa zaidi ya asilimia 62% ya watu zaidi ya 150 000 waliovuka Katika eneo la Mediterranean kwa kutumia usafiri wa boti mwaka 2023”.

“Njia ya kati ya Mediterania (njia ya kutoka Algeria, misri, Libya na Tunisia hadi Italia na malta) imerekodi angalau vifo 3 na kupotea kwa watu 129 mnamo mwaka 2023,” ameeleza Chief Charumbira.

Ametaka kukomeswa kwa matumizi ya silaha na badala yake kuimarisha ushirikiano ,umoja na mshikamano wa kidiplomasia baina ya Ulaya na Afrika kwa mstakabali mwema wa Amani na usalama.

Ametaka kuwepo ushirikiano zaidi baina ya bara la Afrika na Ulaya katika hatua zote za kukabiliana na suala hilo,huku akiutaja umaskini kama chanzo cha uhamiaji haramu ambapo ameomba juhudi zaidi zitakazowezesha kuondoa hali hiyo.

Kongamano hilo limeanza Mei 25,2024 na litahitimishwa Mei 27,2024 kufikiwa kwa maazimio kuhusu uhamiaji.

Share:

Sunday, 26 May 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 27, 2024

Share:

KASEKENYA AIPA TANROADS WIKI MOJA MALINYI KUFIKIKA




Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro kuhakikisha anarudisha Mawasiliano ya barabara kati ya wilaya ya Ifakara na Malinyi katika kijiji cha Misegese, mkoani humo ili kuruhusu magari kupita mara baada ya daraja la Mto Fulua kuharibika kutokana na mafuriko.

Kasekenya ametoa agizo hilo Mei 25, 2024 wakati alipowasili wilayani Malinyi mkoani humo kukagua miundombinu ya barabara na madaraja iliyoathiriwa na mvua za El-Nino ambapo amesisitiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka kurekebisha miundombinu hiyo ambayo ni kiungo muhimu kwa wilaya hizo mbili.

"Nakupa wiki moja, hakikisha hadi kufikia Jumamosi ijayo magari yawe yanapita hapa, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hili pamoja na kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami", amesema Kasekenya.

Aidha, Kasekenya amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha za matengenezo ya dharura katika miundombinu iliyoathiriwa na mafuriko ili kurejesha mawasiliano katika maeneo hayo.

Kadhalika, Kasekenya ametoa rai kwa wananchi kutokufanya shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo karibu na mito kwani hali hiyo huathiri mabadiliko ya tabia nchi na kusabisha mito kuhama na hivyo kuharibu miundombinu ambayo hujengwa kwa gharama kubwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba, ameipongeza TANRAODS Mkoa wa Morogoro kwa kuendelea kukarabati na kuweka Makalvati katika daraja la mto Fulua ili kurejesha mawasiliano katika eneo hilo ambalo liliathiriwa na mvua za El-Nino zilizonyesha mwaka huu.

Ameeleza kuwa kwa sasa magari hayawezi kupita kutoka Njia panda kwenda Malinyi Mjini kutokana na maji kukata barabara kwa mita 100 hivyo uongozi wa wilaya kwa kushirikiana na wananchi wamejenga daraja la muda ambalo linaruhusu kupitisha watumiaji wa njia ya miguu, baiskeli na pikipiki tu.

Naye, Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Alinanuswe Kyamba amemhakishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa tayari wamejipanga na wameanza kurejesha mawasiliano kuanzia eneo la Lupilo na kusisitiza kuwa wataendelea na kasi zaidi ili kurejesha mawasiliano eneo hilo ndani ya muda walioagizwa.

*Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi*

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger