Tuesday, 16 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 17, 2024

           
Share:

Monday, 15 April 2024

UWT IBADAKULI WAFANYA KONGAMANO LA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA MADARAKANI NA KUMPONGEZA KUFANYA KAZI KUBWA YA KUWALETEA MAENDELEO WATANZANIA

 


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga umefanya Kongamano la Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan Madarakani, kwa kumpongeza kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya ya kuwaletea Maendeleo Watanzania.

Kongamano hilo limefanyika leo Aprili 13, 2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Viwandani, ambalo lilitanguliwa na Maandamano,huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu, akimwakilisha Katibu wa CCM wa Mkoa huo Odilia Batimayo,Kongamano lililoandaliwa na Diwani wa Vitimaalum Tarafa ya Ibadakuli Mhe. Zuhura Waziri.
Ndulu akizungumza kwenye Kongamano hilo la UWT Tarafa ya Ibadakuli, amesema wanawake wanampongeza Rais Samia kwa kuwaheshimisha, kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya ya kuwatumikia Watanzania ndani ya Miaka Mitatu na kuwaletea Maendeleo.

Amesema Rais Samia aliichukua nchi kwenye kipindi kigumu cha kuondokewa na Hayati Rais John Magufuli, huku baadhi ya wananchi wakishindwa kumwamini kama ataweza kuongoza Nchi, lakini ndani ya miaka mitatu amewafuta machozi Watanzania na kuwaletea mapinduzi makubwa ya kimaendeleo, na kuonyesha kwamba wanawake wanaweza kushika nyazifa kubwa za uongozi.
“Ndani ya miaka mitatu Rais Samia ameleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwamo ya Afya, Elimu, Nishati na sasa hivi kuna Umeme kila kona hadi vijijini, Barabara zimejengwa, Maji yametapakaa kila mahali na kumtua ndoo kichwani Mwanamke,” amesema Ndulu.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Rehema Nhamanilo,amewataka wanawake kote nchini kwamba zawadi kubwa ambayo watampatia Rais Samia ni kumpigia kura nyingi za ushindi 2025, pamoja na kuwapigia kura wagombea wote wa CCM kuanzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu hadi uchaguzi Mkuu mwakani.
Naye Diwani wa Vitimaalum Tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri, amesema ameandaa Kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia kwa kushirikiana na viongozi wa UWT Kata ya Ibadakuli, kutokana na kazi kubwa ambayo wameifanya ya kuwaletea Maendeleo Watanzania ikiwamo Kata hiyo ya Ibadakuli.

Amesema hawana budi kumpongeza Mwanamke mwezao ambaye amekuwa chachu ya wanawake wengi kuaminiwa na kupata nafasi mbalimbali za uongozi na kufanya mambo makubwa, huku wakimwahidi kwamba katika Tarafa hiyo ya Ibadakuli wagombea wote wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa watapata ushindi mkubwa, pamoja na uchaguzi Mkuu mwakani.
Aidha, amewataka pia wanawake wenye sifa za uongozi kwamba wajitokeze kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali mwaka huu,ili washike nyazifa hizo na kuingia kwenye vikao vya maamuzi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.

Katika hatua nyingine Zuhura amewataka wanawake waendelee kupendana na pale wanapokwaruzana wasameheane, huku akiwakumbusha pia wasisahau malezi bora ya wototo wao wa jinsi zote wa kike na wakiume, pamoja na kuwapatia elimu kwa sawa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza kwenye Kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia kufikisha miaka mitatu Madarakani na kuwaletea Maendeleo Watanzania.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akiendelea kuzungumza kwenye Kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia kufikisha miaka mitatu Madarakani na kuwaletea Maendeleo Watanzania.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Sharifa Mdee akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ibadakuli Ester Komba akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kolandoto Zinila Kalwani akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Diwani wa Vitimaalum Tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu, akimpongeza Diwani wa Tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri kutokana na kuandaa Kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia pamoja na ujumbe Mzuri alioutoa.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Wanawake wakiendelea na Kongamano.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Kongamano la kumpongeza Rais Samia likiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akiwasili kwenye Kongamano hilo.
Wanawake wakiwa katika Maandamano kuelekea kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Wanawake wakiwa katika Maandamano kuelekea kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Wanawake wakiwa katika Maandamano kuelekea kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Share:

KAMATI YA WATAALAMU WA MASUALA YA HABARI ZANZIBAR YAONGEZA KASI UFUATILIAJI MAREKEBISHO SHERIA ZA HABARI


Kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO) imekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kufuatilia mchakato wa marekebisho ya sheria za habari ikiwemo sheria ya Utangazaji No. 7 ya 1997, ambayo ilifanyiwa marekebisho na sheria No. 1 ya 2010.

Katika vikao mbalimbali ZAMECO ilitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria hio kwa lengo la kupatikana sharia mpya na rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini.


Aidha mnamo tarehe 9/4/2024 ZAMECO wamefika katika afisi za Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar iliyopo Vuga kwa ajili ya kufuatilia hatua iliyofikiwa baada ya kupokea mapendekezo hayo mwezi wa Octoba mwaka 2023.


Mratibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa upande wa Zanzibar Shifaa Said ameeleza kuwa hatua hii ya ufuatiliaji imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mchakato wa kupata rasimu ya sharia ya Utangazaji unakwenda vizuri na hatimae sheria mpya itayokidhi vigezo vya kihabari ipatikane.


Kwa upande wake, Salim Said, mwandishi wa habari mkongwe amesisitiza kwamba vyombo vya habari havina nia mbaya na serikali, bali ni washirika muhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii hivyo jitihada za ZAMECO na wengine katika kuendeleza maboresho ya sheria ya Utangazaji zinachukuliwa kama sehemu ya ushirikiano mzuri kati ya vyombo vya habari na serikali.


“Vyombo vya habari havina uadui na Serikali, sisi ni washirika wazuri na wenye lengo jema kwa jamii na nchi kwa ujumla, kwa kuzingatia vyombo vya habari ni nguzo ya maendeleo ya uchumi” Alisema Salim Said.


Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria ndugu Mussa Kombo Bakari aliwapongeza ZAMECO kwa jitihada wanazozichukuwa kutafuta maendeleo ya tasnia ya habari na kubainisha kuwa mapendekezo waliyowasilisha yamepokelewa na kufanyiwa kazi.


“Tume imekwisha yapeleka mapendekezo hayo katika mamlaka husika na tunatumaini kwamba mapendekezo hayo yatachukuliwa kwa uzito unaostahili ili hatimaye rasimu ya mswaada wa sheria hio ipatikane , alieleza Katibu Mussa.


Nae mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa ametoa shukrani kwa katibu na wafanyakazi wote wa Tume kwa ushirikiano wao katika mchakato huu wa kupata sheria mpya huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kuhakikisha upatikanaji wa sheria mpya kwa maslahi ya Zanzibar na wazanzibari wote.


Ni takribani miaka 20 sasa wadau wa maswala ya habari Zanzibar wamekua wakipambania marekebisho ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu No. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka 1997 na Sheria ya Utangazaji No. 7  ya 1997 ambayo ilifanyiwa marekebisho na Sheria No. 1 ya 2010 , ambapo Oktoba mwaka jana Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar ilipokea mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya uatangazaji lengo ni kupata sheria huru iliyokua rafiki kwa tasnia ya habari na jamii kwa ujumla.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger