Sunday, 24 March 2024

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA NA WENYE MAHITAJI MAALUM GEITA

Katika mwendelezo wa utamaduni wa Benki ya CRDB kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan imejumuika na wateja pamoja na makundi  yenye uhitaji maalum katika futari waliyoandaa.

Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB imefanyika Ijumaa Machi 22,2024 katika ukumbi wa Otonde  mkoani Geita ambapo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Said Juma Mkumba alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela huku  Menejimenti ya Benki  ya CRDB iliwakilishwa na  Mkurugenzi wa Rasimali Watu Godfrey Rutasingwa. 

Benki ya CRDB pia imekabidhi vitu mbalimbali kwa vituo vya watu wenye mahitaji maalum vitakavyowasaidia kukamilisha funga yao  katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Benki ya CRDB ambayo mwaka 2021 ilianzisha dirisha la huduma za kibenki ambazo zimefuata misingi ya dini ya kiislamu maarufu kama Al Barakah Banking, imekuwa na utaratibu kila mwaka wakati wa Ramadhan kushiriki Futari na wateja wake na kutoa Sadaka ya vyakula kwa watu wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi wa rasilimali watu Godfrey Rutasingwa  akitoa salamu za benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ndugu Jumanne Wambura Wagana akitoa salamu za ufunguzi
Shekhe mkuu wa mkoa wa Geita Alhaj Shekhe Alhad Kabanju akitoa salamu na pongezi kwa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Chato  Mh. Said Mkumba akitoa salamu kwa niaba ya mgeni wa heshima mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Sophia Jongo aliye mbele na akina mama wa Mkoa wa Geita wakati wa Iftar.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 24, 2024


Share:

Saturday, 23 March 2024

TANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUTATUA VIKWAZO VYA KIBIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano (waliosimama) wakikabidhiana Hati za Makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru baina ya Kenya na Tanzania wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya .

Wanaoshuhudia wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza,waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na uwekezaji, viwanda biashara wa nchi zote mbili, Katibu Mkuu wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya.

............

Tanzania na Kenya zimekubaliana kuendelea kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru kwa kuwa na Mpango wa pamoja wa kuwianisha tozo, ada , ushuru, ada na sheria au taratibu zinazoathiri biasharabaina ya pande hizi mbilmasharti mengine yanayoathiri biashara pamoja na kuwezesha ufanyaji biashara mpakani kwa saa 24 ili kukuza biashara baina ya nchi hizo kila siku, kila mwezi na kila mwaka.

Aidha, amebainisha kuwa Nchi hizo zimekubaliana kuhakikisha kuwa .Sheria za Tanzania hazizuii wafanyabiashara wa Kenya kufanya biashara Tanzania na Sheria za Kenya hazizuii wafanyabiashara wa Tanzania kufanya biashara nchini Kenya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano baada ya kusaini na kukabidhiana Tamko la Pamoja la Makubaliano ( Communique) wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024

Akifafanua zaidi kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini , Mhe Byabato amesema Mkutano huo ulitambua kuwa katika siku 30 zilizopita, baadhi ya vikwazo visivyo vya kiushuru vimeondolea ili kukuza biashara na uchumi baina ya nchi hizo kwa kasi na kuimarisha uhusiano na Kenya ambayo ni Mshirika muhimu wa kibiashara wa Tanzania.

Amesema vikwazo hivyo ni pamoja na kuruhusu kuondolewa kwa zuio la kuingiza chai nchini kutoka Kenya, kuondolewa kwa zuio la kuingiza pombe aina ya Konyagi kwenda nchini Kenya, kuondolewa kwa zuio la kusafirisha mbao kwenda Kenya kupitia mpaka wa Horohoro uliokuwa umezuliwa na Shirika la Viwango nchini Kenya

Naye Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano amesema Kenya iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kukuza biashara na uchumi pamoja na kuimarisha umoja wa wananchi wa nchi zote mbili

Aidha amebainisha kuwa Nchi hizo mbili zimekubaliana kushughulikia baadhi ya vikwazo kwa njia za kiutendaji na mamlaka mbalimbali kutoka pande zote mbili na kuimatisha utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa makubaliano na kubadilishana taarifa kuhusu maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo.

Mkutano huo wa nane ni utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto yaliyolenga kuondoa vikwazo vyote vinavyoathiri biashara ili kuimarisha uhusiano wa biashara

Aidha, Mkutano huu wa nane ulilenga kushughulikia vkiwazo vilivyobaki katika Mkutano wa Saba wa Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika tarehe 9-12 Machi 2022 huko Zanzibar na unatarajiwa kufanyika Julai 2024 ukilenga kupunguza au kuondoa kabisa vikwazo vilivyobaki ili kukuza biashara na uchumi wa nchi zotw mbili.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano (waliosimama) wakikabidhiana Hati za Makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru baina ya Kenya na Tanzania wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024.

Wanaoshuhudia wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza,waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na uwekezaji, viwanda biashara wa nchi zote mbili, Katibu Mkuu wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akiwa na Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano (waliokaa) wakisaini Hati za Makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru baina ya Kenya na Tanzania wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024.

Wanaoshuhudia wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza,waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na uwekezaji, viwanda biashara wa nchi zote mbili, Katibu Mkuu wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 23,2024

 

Share:

Friday, 22 March 2024

NILIVYOJIKUTA NIMEFUNGUA BIASHARA BILA KUPENDA KISA MAPENZI!


Jina langu naitwa Ndaroka kutokea Mwanza nchini Tanzania, wakati naanza mwaka wa kwanza nilimpa mimba mpenzi wangu, nilikuwa naye toka nikiwa kidato cha tano, bahati mbaya alifeli akaishia hapo hapo.

Aliniambia mimba ni yangu na nilikubali nikaanza kuilea ile mimba, japo tulisumbuana sana kwenye pesa za matumizi kwa sababu sikua na pesa za kutosha kila kitu kwa wakati huo.

Chuki kwangu ikazidi balaa, sikuiweka moyoni niliamini ni mimba inamsumbua, baada ya muda alienda kwao kujifungua mkoa mwingine, na akajifungua mtoto wa kiume.

Baada ya siku tatu akaniambia mtoto amefariki na baada ya hapo hakupokea simu zangu tena wala za mama yangu. Mama yangu alilia sana kwa sababu nilimtambulishwa kwake na alimpenda sana.

Tayari tulishanunua vitu kibao vya kwake na vya mtoto, kuna namna niliamini huu ni mchezo nimechezewa ila nilikaza maisha yakaendelea, nikasonga na maisha mapya.

Baadae nikapata mwanamke mwingine na tulipendana sana japo shida yake ilikua ni wivu mwingi, alitaka kuchunguza kila kitu katika maisha yangu hadi watu ambao nawasiliana nao.

Siku moja akaja ghetto mi nikamuacha humo sababu nilikua nawahi kipindi, yeye akajiongeza kufanya usafi. Eenh bwana enh si akakuta vile vitu tulivyonunua na mama kwa ajili ya mtoto vipo chini ya uvungu.

Ile narudi nakuta mtu kanuna, nikamuuliza shida nini mama, akawaka sana kuhusu vile vitu ikabisi nitafute namna ya kujitetea nikamwambia kwa sasa nahitaji kufungua biashara hasa hasa ya vitu vya kike so hizi ni sample.

Basi akafurahi kweli kusikia hivyo na akanipongeza akaahidi kuwa nami kwenye safari yangu ya maendeleo, hapo moyoni nawaza nitaanzia wapi wakati sihawahi hata kufanya biashara ya kuuza pipi.

Kila siku akawa ananikumbusha kuhusu ile biashara hadi nikajikuta nafungua ili mradi nitunze lile penzi, changamoto ikatokea ile biashara ikawa haifanyi vizuri kabisa, nikawa natoa fedha tu ila hakuna ambacho naingiza.

Mpenzi wangu akaja na wazo kuwa anamfahamu mtu anaitwa Kiwanga Doctors ambao ni wataalam wa tiba asilia, akaniambia kuwa wanaweza kutusaidia kukukuza biashara yetu.

Basi akatafuta namba yao katika mitandao hadi akaipata, tuliwasiliana nao kwa namba (+254 769 404965) na wakatufanyia dawa ya kuvuta wateja na kweli tumefanikiwa.

Nimeifanya tangu namaliza chuo hadi leo na nikazidi kuamini ule msemo “everything happens for a reason”.

Kiufupi bado sijapata kazi ila nina kipato na nimeridhika sana na hii biashara. Nashukuru mpenzi wangu ulikuja kwangu ukawa baraka, umeniokoa na wivu wako wewe barafu wa moyo wangu.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA NA KUFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA DAWASA YETU


Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma imekagua na kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la DAWASA Yetu lililogharimu shilingi bilioni 48.9 na linatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mradi wa jengo hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deus Sangu amesema kuwa Kamati imejionea utekelezaji mzuri wa mradi huu wa ujenzi wa jengo kwa ufanisi na kwa ubora.

Amesema kuwa kupitia jengo hili, DAWASA ambayo ni Mamlaka kubwa nchini ya maji litasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya Majisafi kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.

Mhe. Sangu ameipongeza Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia umuhimu wa kazi kubwa waliyonayo DAWASA ya kuhudumia majimbo 16 ya uchaguzi na mikoa minne ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, baadhi ya maeneo ya Morogoro na Tanga, na kuamua kutoa fedha za kujenga jengo hili la kisasa.

"Niipongeze Serikali kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwenye utekelezaji wa mradi huu," ameeleza Mhe Sangu.

Ameongeza kwa kuipongeza DAWASA kwa kuongeza ubunifu kwa kufunga mifumo ya kufuatilia upotevu wa maji na miundombinu ya maji kwenye maeneo ya huduma, na hii imekuwa ni changamoto kubwa kwenye Mamlaka nyingi kunakosababishwa na kutokuwa na mifumo sahihi ya kufuatilia upotevu wa maji. Hivyo hatua hii ya DAWASA ni mfano wa kuigwa.

Amebainisha kuwa Kamati imewasihi DAWASA kuongeza nguvu na kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 37 ya sasaa mpaka kiwango kinachopendekezwa kimataifa cha asilimia 20 ili kuboresha huduma kwa wananchi wote.

Mbali na hapo Mwenyekiti wa Kamati ameipongeza Mamlaka kwa kuweza kuongeza wigo wa utoaji wa huduma kutoka wateja laki 2 mpaka wateja 432000 ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Ndugu Laston Msongole ameishukuru Kamati ya Bunge kwa kutembelea mradi huu na kujionea maendeleo ya jengo letu na hatua ilipofikia.

"Wamejionea na wameridhika na kazi iliyofanyika pamoja na kuona thamani ya fedha iliyowekweza imeleta tija, tunawaahidi kukamilisha sehemu iliyobaki ndani ya wakati," ameeleza Ndugu Msongole.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger