Wednesday, 13 March 2024

MBUNGE WA NGARA NDAISABA RUHOLO AJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA MIRADI NDANI YA MIAKA MITATU JIMBONI


Na Mariam Kagenda -Kagera

Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Ndaisaba Ruholo amesema katika kipindi cha miaka 3 wilaya hiyo imeweza kupata miradi mikubwa ya maendeleo tofauti na kipindi cha nyuma jambo ambalo linatakiwa kuwafanya wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa na imani na serikali yao.

Mhe. Ndaisaba Ruholo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Ngara amesema hayo wakati wa mikutano yake ya adhara ya kuzungumza na wananchi kuwaeleza yaliyofanyika katika kipindi cha miaka 3.

Amesema kuwa ahadi nyingi alizozitoa wakati akiomba ridhaa kwa wananchi hao hasa katika sekta ya elimu, afya, maji pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara ambazo zilikuwa hazipitiki na bado kuna miradi mikubwa ya maji na barabara inayoendelea kutekelezwa.


Amesema kuwa katika miradi inayoendelea kutekelezwa na iliyopo katika hatua za kuanza kwa ujenzi ni pamoja na ujenzi wa soko, serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa soko la kimkakati la Kabanga jambo ambalo lilikuwa ni moja kati ya ahadi alizowaahidi wananchi wa wilaya hiyo kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kabanga ,Hafidh Abdalla amesema kuwa mwaka 2020 waliahidi kuwatetea wananchi lakini kumekuwa na tatizo la migogoro ya ardhi bado ni changamoto kwani wananchi wanategemea kilimo na ufugaji hivyo watahakikisha wanawatetea wananchi kuhusiana na suala hilo.
Share:

23 WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Na Salvatory Ntandu _ Kahama

MAMLAKA ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) wamewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga watu 23 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Washitakiwa hao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya bangi, heroin na mirungi kinyume cha Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Sura 95 marejeo ya mwaka 2019 kifungu cha 15 A Kifungu kidogo (1) (2) na kifungu cha 17.

Akisoma Mashauri hayo 18 ya Jinai jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Christina Chovenye, wakili wa Serikali John Hamenya alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti katika mwezi Februari na Machi mwaka 2023 katika wilaya ya Kahama huku wakijua wazi kuwa biashara hiyo ni kosa kisheria.

Hamenya aliwataja watuhumiwa hao 23 ambao wamefikishwa mahakamani kuwa ni, Juma Lusangija (54), Mwajuma kavula(36), Tayson Mwita Marwa (23) Emmanuel Christopher (33), Amos Augustino 34, wakazi wa mtaa wa Mwime na Fred Bichuka(37) , Rojasi Daudi (18) wakazi wa mtaa wa Mhungula na Juma Merengo Merena (44) mkazi wa Kidete , Hassan ally Ngwenyau (27) mkazi wa Nyakato na Gerald Emmanuel (18) mkazi wa Nyasubi.

Wengine ni pamoja na Paulo Charles Wilson (25) Nyakato, Joseph Lugenzi, Zamoyoni Andrea (26) mkazi wa Nyashimbi , Kobelo Ntahondi(42) Mkazi wa Bukondamoyo, Raphael Masanja (37) mkazi Nyakato na Said Kayoka kayoka (27) mkazi wa Mhungula, Saidi mselem (22) mkazi wa Majengo, na Haitham salum Suleiman (31) mkazi wa Nyasubi.

Samwel Edward John (31) mkazi wa Malunga, Joseph Mussa lugenzi,(40) mkazi wa Malunga, Robert Elias Lameck (24) mkazi wa Mwitongo , Hillary salum nassoro(39) mkazi wa Malunga ,Richard Raphael mushi (30) mkazi wa Majengo, Izdory Nemes temba(23) mkazi wa Malunga, Kassim hamad amori(27) mkazi wa Nyasubi.

Watuhumiwa wote kwa pamoja walikana mashtaka yanayowakabili na mashauri yao yameahirishwa hadi Machi 14,15 na 26 mwaka huu kwa hatua ya kutajwa na kusikilizwa baada ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo, nafasi ya dhamana kwa watuhumiwa iko wazi kwa Watakaokidhi vigezo vya Mahakama.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 13, 2024

 

Magazetini leo
 
 
Share:

Tuesday, 12 March 2024

JAPAN YASHAURI MABORESHO KATIKA UCHUMI

 


 Balozi wa Japan nchini Yasushi Misawa akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa JATA jijini Dar es Salaam
                       ***********

BALOZI wa Japan nchini Yasushi Misawa amesema ili Tanzania kuendelea zaidi ihakikishe inaboresha maeneo ya kimkakati ikiwemo viwanda, afya, mazingira, elimu na sekta muhimu kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa shirikisho la watanzania wanufaika wa program za mafunzo ya JICA ( JATA,) Balozi wa Japan nchini Yasushi Misawa, amesema hatua ya maendeleo ambayo nchi nyingi za bara za Asia zimepitia ikiwemo Japani kukua kwa uchumi wa Nchi na jamii kwa ujumla kunatokana na uboreshaji wa miundombinu, sera za maendeleo ya viwanda, sekta ya rasilimali watu pamoja na mafunzo ya ufundi.

Aidha Balozi Yasushi, amesema kupitia Shirika la Maendeleo la Japan Tanzania(JICA ) wataendelea kutoa mafunzo ya ujuzi kwa Watanzania na kuwezesha miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi huku akidai kuendelea kufanikisha miradi kupitia wanafunzi waliowapa ufadhili ikiwemo mradi wa Hatua project.

“JICA imechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikijikita katika rasilimali watu na kumekuwa na fursa nyingi za mafunzo na miradi na siku ya leo ninafuraha kushiriki na kujua kutoka kwa wanachama wa JATA ambapo kuna miradi kama HATUA ulioanzishwa kutatua matatizo ya wananchi nah ii inaendana na mikakati yetu,”amesema.

Amesema tayari wadau kutoka Japan na serikali walijadili kuhusu changamoto za kiuchumi na kijamii ambapo wataweza kufanikiwa kutokana na ujuzi waliotoa na uzoefu walionao.

Katika hatua nyingine Misawa amesema, Uhusiano bora baina ya Tanzania na Japan umekuwa ukichangia maendeleo ya kijamii na uchumi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Hatua inayotekelezwa na wanachama wa JATA ambayo ina manufaa kwa watanzania kwa kuwa inalenga kutatua changamoto za kijamii ambayo ni moja ya mkakati wa JICA.

Pia ametumia wasaa huo katika kusherekea siku ya wanawake duniani kuwapongeza wanawake wa Tanzania kwa utendaji kazi uliotukuka na kueleza kuwa uhusiano wa ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Japan umelenga wanawake pia katika kuchukua nafasi sawa na wanaume.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA,) Ara Hitoshi amesema, JATA watumie fursa za jukwaa hilo kubadilishana ujuzi, uzoefu na maarifa kwa mafunzo waliyopata na hiyo ni pamoja na kujitolea ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Ameeleza kuwa uhusiano wa jukwaa hilo ni muhimu kwa JICA ambayo itaendelea kushirikiana na Tanzania kupitia Taasisi za Umma na sekta binafsi ili kuendelea kuleta matokeo chanya ya maendeleo.

" Uhusiano wa Tanzania na Japan ni imara na kupitia JICA imekuza ushirikiano huu na kupitia JATA tunaamini ujuzi mliopata kutoa mawazo, fursa na kwa jamii na kuleta matokeo yenye tija zaidi katika sekta sekta mbalimbali." Amesema.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Utumishi Leila Maviki amesema Serikali ya Tanzania inathamini jitihada za Serikali ya Japan katika kuchochea maendeleo ya Tanzania kupitia fursa za masomo na mafunzo yatolewao wa watanzania ikiwemo watumishi wa Umma ambao wamepata mafunzo kupitia JICA katika uga za afya, TEHAMA, sekta ya maji na kilimo.


Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa JATA Gregory Mlay amesema kuwa shirikisho hilo limewakusanya watanzania waliopata fursa ya kusoma nchini Japan ikiwemo waliopata kupitia ufadhili wa JICA umelenga kuendeleza uhusiano wa kimaendeleo, uhusiano, ushirikiano, kubadilishana uzoefu pamoja na kudumisha uhusiano na kuendelea kufanya kazi na JICA.

Mradi wa Hatua ulianza mwaka 2022 kwa miradi mitano ambayo miradi miwili ilitekelezwa mwaka 2022 na mitatu ilitekelezwa mwaka 2023 kwa lengo na kupata fursa ya kutumia Teknolojia waliyoipata Japan kwa manufaa ya Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwa JICA 1962 hadi mwaka 2022 jumla ya wanafunzi wa Kitanzania 147,863 wamepewa ufadhili wa masomo na shirika hilo katika nchi mbalimbali duniani.  
Balozi wa Japan nchini Yasushi Misawa (wa pili kulia) Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA, wa pili kushoto) wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa JATA Gregory Mlay na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Utumishi, Leila Maviki.

Share:

RAIS SAMIA ATEUA NA KUHAMISHA VIONGOZI... ANAMRINGI MACHA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger