Mazishi ya mwili wa mwendeshaji na Mmiliki wa Mtandao wa MASWA YETU BLOG, Innocent Lugano Mbwaga maarufu Blogger Boy yamefanyika leo Jumatatu Desemba 11,2023 katika makaburi ya Roma Mjini Maswa Mkoani Simiyu.
Mazishi ya Innocent yamehudhuriwa na waombolezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi. Mariam Mwanzalima.
Innocent Mkazi wa Maswa Mkoani Simiyu ambaye alikuwa Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara alifariki dunia Desemba 8,2023 wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitali baada ya kupata ajali ya pikipiki aliyokuwa anaendesha Tandahimba Desemba 5,2023.
Mmiliki na Mkurugenzi wa Mtandao wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwa ameshikilia picha marehemu Innocent Mbwaga ' Blogger Boy'